Yanga mnaivimbia TFF kisa kanuni imekiukwa. Mmejipanga kuzifuata kanuni zote au ni mihemko tu?

TFF inaendesha Mambo yake kwa kuzingatia kanuni na sheria. Ni sawa.

Lakini ni mara nyingi sana TFF imekuwa ikifumbia macho makosa mengi ya ukiukwaji wa kanuni na sheria zake yanayofanywa na vilabu vyetu, vikiwemo Yanga na Simba.

Ni muktadha huo wa kubebana na kuchukuliana ndiyo TFF iliutumia kusukuma mbele kwa masaa mawili mpambano wa watani wa jadi, Simba na Yqnga.

Kitendo cha Yanga kuikaba koo TFF kinamaliza enzi za kuchukuliana na kubebana. Yanga inaiambia TFF kwamba Sasa izifuate kanuni zake kwa 100%. Hapa naona atakayeumia ni Yanga, maana TFF wameshikilia mpini.
Huyo Msomali atashindwa uchaguzi ujao na TFF mpya itapatikana, TFF ya sasa haina maslahi yoyote kwa Yanga. Tena wawaambie watu namna ya kurudisha viingilio vyao.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Wakati Yanga SC wanang'ang'ana na saa 24 kupewa taarifa. TFF wanaweza kuchomoa kwa hicho kifungu cha tatu. Wakisema walichoelezwa na upande wa Serikali kilikuwa ni cha dharura na msingi.

Wakati huo, si kila kilicho cha dharura na msingi kwa TFF, ni lazima kiwe hivyo kwa Yanga SC.

Kuna upenyo wa ki-mamlaka TFF wanaweza kuutumia na kulingana na kwamba wao si kisiwa, bado wanahitaji kufanya kazi vyema na Serikali.

Ukisoma sheria na kanuni tusipende kuutumia mstari mmoja, baadaye ndo tunabwagwa kirahisi sana.

Huwezi kugomea jambo la Serikali, hasa pale unaendesha mambo yako chini ya mwanvuli wake, uwanja wao na ulinzi ni wao. Ili uendeshe hiyo michezo unahitaji ushiriki wa Serkali kwa njia moja au nyingine.

Wakikwambia tuna dharura ya chochote kwa tukio linaloenda kutokea hapo uwanjani huwezi kuvimba ukaendelea kwani huwezi kujibeba kivyakovyako.

Mengine tunabaki ni ushabiki na ukereketwa tu.

View attachment 1778287
Hapo kinachoongelewa ni kuhairisha mchezo na sio mda wa mchezo boss
 
Suala ni uelewa si ushabiki.
TFF haiwezi ku-survive peke yake kamwe mambo inayofanya bado yanaihitaji serikali, ni mtambuka.

Usione mpira unachezwa kirahisi, kuna mambo ya ulinzi na usalama. Kwa mfano siku umepanga mechi ukaambiwa tuna tukio jingine linalohitaji wana usalama, utavimba tuu na kusema hatuingiliwi na serikali? Siku unataka kuutumia uwanja ukaambiwa kuna shughuli ya serikali au chama kwa viwanja vya vyama utavimba tuu na kusema FIFA inasema .....

Serikali imewapa TFF sababu zao, wao walitakiwa kujitathmini na kutoa maamzi kama sababu zinakidhi. Hakuna aliyekamatwa huko TFF na kushinikizwa akubali hoja ya serikali.

Suala la msingi ni je hili la jana kulikuwa na udharura na mhimu?

Kuna mambo si ya kwako moja kwa moja kama yakitokea mfano: tishio la kiusalama, utasubiri uambiwe kuna taarifa ya kuwepo kwa mabomu ndo ukubali kuahirisha mpira?

Tujitathimini?
Kwenye ile barua waliyotoa jana TFF hiyo sababu iliwekwa? Kuwa muelewa ndugu,Fifa inaruhusu serikali kuingilia kama kutakuwa na usalama mdogo yaani polisi au mamlakani ya hali ya hewa wakitangaza kutatokea na hali mbaya.
Sasa barua ya hao TFF ilisema sababu ya kusogeza mchezo mbele kwa masaa mawili?
Saa 11 usalama ulikuwa mdogo uwanjani? Je Yanga na Simba ziliambiwa sababu hiyo?
Hali ya hewa ilikuwa mbaya saa11? Je Yanga na simba waliambiwa?

TFF imeshikwa pabaya safari hii na yanga, kama wanauwezo wawapige faini yanga kwa kutotii maagizo yao ya hovyo. Kisha Yanga wapeleke malalamiko yao FIFA ndipo utaelewa
 
Yanga hawajaigomea tff wameigomea serikali bahati mbaya yao wamefanya uamuzi kwa kukurupuka wakidhani wanawakomoa TFF. tnaenda kuona gsm wakiyumbishwa mpaka waombe poo.
Serikali na mpira wa miguu wapi na wapi? Kama wao wababe wakipokea pointi yanga na mengineyo kama wanauwezo huo
 
Kwenye ile barua waliyotoa jana TFF hiyo sababu iliwekwa? Kuwa muelewa ndugu,Fifa inaruhusu serikali kuingilia kama kutakuwa na usalama mdogo yaani polisi au mamlakani ya hali ya hewa wakitangaza kutatokea na hali mbaya.
Sasa barua ya hao TFF ilisema sababu ya kusogeza mchezo mbele kwa masaa mawili?
Saa 11 usalama ulikuwa mdogo uwanjani? Je Yanga na Simba ziliambiwa sababu hiyo?
Hali ya hewa ilikuwa mbaya saa11? Je Yanga na simba waliambiwa?

TFF imeshikwa pabaya safari hii na yanga, kama wanauwezo wawapige faini yanga kwa kutotii maagizo yao ya hovyo. Kisha Yanga wapeleke malalamiko yao FIFA ndipo utaelewa
Kanuni imesema timu iambiwe sababu ya kuahilisha mchezo?

Kanuni imeipa TFF kutafsiri sababu kama ni dharura na msingi siyo timu na TFF.

Serikali haikutoa maamuzi na haijaingilia mchezo bali ilitoa taarifa kwa TFF na TFF walifanya maamuzi baada ya kutafakari yaliyotoka serikalini. TFF hawajashinikizwa na yeyote na hapo unaiingizaje suala la katazo la FIFA la serikali kutoingilia michezo?

Mbona mechi ya jana ya Namungo ilisogezwa na wakacheza? Mbona mechi ya jana ya Yanga princess ilisogezwa na wakacheza?

Ukweli ni kuwa watu hawakusoma vifungu kwa ujumuishi.
 
Back
Top Bottom