Wenye akili timamu tujadiri hili, yanayoendea simba na yanga ni utani au chuki?

kambale mnene

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
271
197
Utani wa simba na yanga ulijengwa kwenye misingi ya ushindani toka huko nyuma hasa uwezo wa uwanjani.

Leo utani umetoka kwenye misingi yake badala yake imekuwa mashambulizi ya mtu na mtu au kundi na mtu.
Imefika mahali chuki imekuwa kubwa hata huku mitaani.

Imefika mahali timu fulani ikikutwa na kadhia fulani au kiongozi wa timu fulani,watu wanatukanana hovyo.
Vijana wanawatukana wazee utadhani kwao hakuna wazee.

HALI HII IKIACHWA IENDELEE HUKO MBELE ITAKUWA NA MADHARA MAKUBWA KWA TAIFA.
Leo hii Haji Manara anatukanwa pande zote,mitandaoni mpk mitaani.
Je huu ni utani?

Tunajua tff imeoza haitamaniki na ndiyo chanzo cha matatizo ya mpira wetu,haiwezi kukemea timu yoyote.

JE WIZARA YENYE DHAMANA NA SOKA LETU HAIONI HAYA?

weusi wenzetu huko ulaya wakiitwa nyani sisi tunalalamika,lakini Mara kadhaa tumeona mamlaka zao zikitoa adhabu kwa timu husika ili mashabiki zao wasiendelee kubagua rangi za binaadam wenzao.

Sakata la manara kufungia,anakula matusi ya nguoni,ana baguliwa na kuitwa majina mengi mabaya kutokana na ulemavu wake,je huu ni utani wa mpira?

Serikali ipo tu!
Moja ya sheria za jamii forum ni kutomshambulia mtu bali kumjibu hoja.

LEO WAPENZI WA SIMBA WANAMKASHIFU HAJI NA KUMTUSI VIBAYA VIBAYA, MAADIMIN MPO KIMYA TU WALA HAMCHUKUI HATUA!!!!

Mfano huyu gentermycine,kwa siku anaanzisha nyuzi nyingi za kumkashifu na kumtusi Haji,lakini kesho na kesho kutwa utamkuta yupo tu humu anatembea na nyuzi zake.
MAADIMIN
Mmelala,macho hayaoni,fahamu hazifanyi kazi au?
Mpk leo hakuna tusi linalothibitishwa waziwazi kuwa Haji kamtukana Karia.

Wasemaji wanamung'unya maneno tu,wanashindwa kuyakaza,lakini wanasimba hawaoni haya wanamchafua haji,kisa alitoka kwao.
HUU NDIYO MPIRA WETU ULIPOFIKIA!!

Haji anafamilia na wazazi pia,mmejiuliza wanajisikiaje mnapomkashifu kwa kumwita sokwe mwekundu? Admin mnawaacha tu! Serikali inaacha tu!
 
Hivi unajua Haji Manara amechangia kwa asilimia kubwa huu uhasama uliopo? Alianza wakati yuko Simba kuwatukana washabiki wa Yanga kuwa ni hamnazo (wapumbavu) ila Baba yake Mzee Sunday Manara na Mzee JK. Aliwahi kumkejeli Makamu Mwenyekiti wa Yanga Kwa kumuita kilo 800 kutokana na maumbile yake. Na baada ya kufukuzwa Simba kwa utovu huo wa nidhamu ndiyo Yanga wakamdaka na jujumu lake likawa kuwatukana viongozi wa Simba na kuikashifu club ya Simba kila alilopata jukwaa la kuongea.

Nakushangaa wewe kumtetea huyu chanzo cha matatizo na kuona yeye ndiye anaonewa. Hatuwezi kupata ufumbuzi wa tatizo kwa kukwepa kujua chanzo chake.
 
Utani wa Simba Sc na Yanga ulikuwa ni mzuri na wenye kuhamasisha upendo, mpaka pale ambapo kulikuja kuibuka the so called wasemaji ambao waliamini katika uhasama.

Hapa nawazungumzia JERRY,MANARA, ZAKAZAKAZI, huyo mmoja kwasasa katulia ila huyu mwingine ndiye kurusi haswaa. Jaribu kufikiria mpira ungekuwa unasemewa na watu aina ya NUGAZ, BUMBULI, AHMEDY ALLY na wengineo.
 
Uzi wako usituulize sisi.. unaemtetea huyo Haji ndo muasisi wa upuuzi wote huu..huyu haji ndo kaleta uhasama akisaidiwa na tff ambao wamemlea kwa muda mrefu.. ingewezekana huyu jamaa angepigwa ban ya maisha kabisa ili tuondokane na ombwe lake..
 
Hapo ndio tatizo la wadau wengi napoliona

Kilichotokea juzi ni matokeo ya matukio mengi ambayo aliyafanya na mkayayamazia kimya

Kama unaona ameonewa kwasababu kapigwa faini ebu jaribu kufikiria yule aliyefungiwa miaka mitano kwa kupost tangazo la TFF

Huyo unayemtetea kuwa ana familia inayomtegemea kumbuka ndio huyo huyo alikuwa akimshinikiza majizo amfukuze kazi Jemedari Saidi bila kujari familia yake itakula wapi
 
Ina maana hujui huu uhasama umeletwa na huyo ‘The so called Buggati’? Mbona lipo wazi sana hilo mzee.!
Ingekuwa sio kuchekeana na kuleta siasa, Manara alitakiwa asijihusishe na soka la Tanzania maisha yake yote.
Ametengeneza ‘Damage’ kubwa sana katika soka letu huku yeye akifanikiwa kimaisha kwa ‘ Upumbavu’ alioupandikiza.
 
Utani wa Simba Sc na Yanga ulikuwa ni mzuri na wenye kuhamasisha upendo, mpaka pale ambapo kulikuja kuibuka the so called wasemaji ambao waliamini katika uhasama.

Hapa nawazungumzia JERRY,MANARA, ZAKAZAKAZI, huyo mmoja kwasasa katulia ila huyu mwingine ndiye kurusi haswaa. Jaribu kufikiria mpira ungekuwa unasemewa na watu aina ya NUGAZ, BUMBULI, AHMEDY ALLY na wengineo.
Huyo Bumbuli pia ana hamnazo,
 
Mkuu umesema hakuna maneno yaliyothibitika kuwa alimtukana Raisi wa TFF Uko serious???? Hivi " unanifatilia Sana wewe leo ni Mara ya tatu sikuogopi Na huna Cha kunifanyia naweza kukufanya kitu chochote Na Wala huna Cha kunifanya " mwisho wa nukuu.

Mkuu hayo tu amemtishia Hilo ni jinai ilitakiwa aende polisi pengne hizo siku mbili Raisi wa TFF angezulika au kupiga hata Na vibaka au majambazi ni Nani angekuwa suspect namba moja? Jibu ni manara.

Kingne Kama Hana hatia Na hakuwa ametenda kosa ni kwa Nini aliomba msamaha??
 
Hapo ndio tatizo la wadau wengi napoliona

Kilichotokea juzi ni matokeo ya matukio mengi ambayo aliyafanya na mkayayamazia kimya

Kama unaona ameonewa kwasababu kapigwa faini ebu jaribu kufikiria yule aliyefungiwa miaka mitano kwa kupost tangazo la TFF

Huyo unayemtetea kuwa ana familia inayomtegemea kumbuka ndio huyo huyo alikuwa akimshinikiza majizo amfukuze kazi Jemedari Saidi bila kujari familia yake itakula wapi
Fact
 
Sasa hv Kuna chuki hakuna utani tena.. Yanga alishinda vikombe vyote vya ndani basi Simba anateseka kama kakatwa kidole
 
Hapo ndio tatizo la wadau wengi napoliona

Kilichotokea juzi ni matokeo ya matukio mengi ambayo aliyafanya na mkayayamazia kimya

Kama unaona ameonewa kwasababu kapigwa faini ebu jaribu kufikiria yule aliyefungiwa miaka mitano kwa kupost tangazo la TFF

Huyo unayemtetea kuwa ana familia inayomtegemea kumbuka ndio huyo huyo alikuwa akimshinikiza majizo amfukuze kazi Jemedari Saidi bila kujari familia yake itakula wapi
Naomba nikujibu kistaarabu maana Leo umejitendea haki kama binadamu. Mleta mada hoja yake kubwa ni mashambulizi yanayohusiama na Hali ya kimaumbile ya Manara. Kitendo cha Manara binafsi huko nyuma kuwahi kutumia kauli za ovyo dhidi ya watu wengine hakuhalalishi watu wengine kumkashifu kilema chake. Wewe sijakusikia ukimuita majina ya kudhalilisha ambayo naogopa hata kuyarudia, lakini wapo mashabiki wa Simba humu kazi Yao ni hiyo na wewe unawajua. Hakuna sababu ya kudhalilisha watu kimaumbile Kwa sababu ya utani wa soka. Hata Haji alipokuwa anatoa maneno ya ovyo Wenye busara tulikemea lakini akaungwa mkono na kundi linaloshabikia ujinga ilimradi anayesema Yuko upande wao. Sisi tusio na upande tunakwazika na maneno ya ovyo yanayodhalilisha ubinadamu na tunawaomba Mods wachukue hatua Kali.
La pili umeongelea adhabu za TFF dhidi ya Mwandishi na pia kuna mdau ameongea kuhusu kocha wa Mbeya Kwanza. Mimi ni miongoni mwa watu wa awali kuona kichaa hicho cha adhabu na kukemea. Kosa la Mwandishi lilikuwa na ukubwa gani wa kufungiwa miaka 5 na Kocha akafhngiwa miaka 5 utadhani wamefanya kosa la Mauaji bila kukusudia? Hao wanasheria waliojazana kwenye Kamati ya Maadili hawaoni nchi nyingine za Ulaya zinavyoshughulika na nodhamu ya watu wapo michezoni. Hivi Morino angekuwa Kocha wa Biashara si angeshafungiwa maisha Kwa makosa yake ya mara Kwa mara?
Makosa ya kwenye michezo ni ya kawaida Sana na hayana madhara Makubwa maana mengi yanasababishwa na mihemko ya matokeo ambayo huisha baada ya watu kukubali kupokea matokeo.
Watu wa Usalama barabarani waliona vyanzo vya ajali mara nyingine ni out of control ya ubinadamu wakaweka adhabu kulingana na ubinadamu isipokuwa uzembe unapotawala, lakini Leo soka imewekewa adhabu ya kifo. Kocha anayefundisha kuinua vipaji anafungiwa kutojihusisha na soka miaka 5 bila kujali gharama za kumkosa na kukosa utaalamu wake.
Ifike mahali tukatae adhabu za kikandamizaji ambazo hazina manufaa Kwa soka letu.
 
we mwenyewe nawe ndio wale wale huna lolote ungekuwa na busara usingemtaja Gentamycin kama umemtolea mfano ungatafuta wote wenye maudhui kama yake mfano Demigod yeye kila siku maneno ya dharau kwa Simba hata juzi anasema goli la sako Simba wamenunua huyu mbona hujamtaja humu Jamii forum anavyoichafua Simba au hujamuona au na ww unachuki na Gentamycin?
Ili ungekuwa fair ungewataja wote wanaoleta kuchafuana humu lkn ukimtaja mtu mmoja peke yake na wengine wapo hujatendea haki jukwaa nawe tunakuweka katika kundi hilo la ushabiki maandazi
 
You nailed it.
 
Naomba nikujibu kistaarabu maana Leo umejitendea haki kama binadamu. Mleta mada hoja yake kubwa ni mashambulizi yanayohusiama na Hali ya kimaumbile ya Manara. Kitendo cha Manara binafsi huko nyuma kuwahi kutumia kauli za ovyo dhidi ya watu wengine hakuhalalishi watu wengine kumkashifu kilema chake. Wewe sijakusikia ukimuita majina ya kudhalilisha ambayo naogopa hata kuyarudia, lakini wapo mashabiki wa Simba humu kazi Yao ni hiyo na wewe unawajua. Hakuna sababu ya kudhalilisha watu kimaumbile Kwa sababu ya utani wa soka. Hata Haji alipokuwa anatoa maneno ya ovyo Wenye busara tulikemea lakini akaungwa mkono na kundi linaloshabikia ujinga ilimradi anayesema Yuko upande wao. Sisi tusio na upande tunakwazika na maneno ya ovyo yanayodhalilisha ubinadamu na tunawaomba Mods wachukue hatua Kali.
La pili umeongelea adhabu za TFF dhidi ya Mwandishi na pia kuna mdau ameongea kuhusu kocha wa Mbeya Kwanza. Mimi ni miongoni mwa watu wa awali kuona kichaa hicho cha adhabu na kukemea. Kosa la Mwandishi lilikuwa na ukubwa gani wa kufungiwa miaka 5 na Kocha akafhngiwa miaka 5 utadhani wamefanya kosa la Mauaji bila kukusudia? Hao wanasheria waliojazana kwenye Kamati ya Maadili hawaoni nchi nyingine za Ulaya zinavyoshughulika na nodhamu ya watu wapo michezoni. Hivi Morino angekuwa Kocha wa Biashara si angeshafungiwa maisha Kwa makosa yake ya mara Kwa mara?
Makosa ya kwenye michezo ni ya kawaida Sana na hayana madhara Makubwa maana mengi yanasababishwa na mihemko ya matokeo ambayo huisha baada ya watu kukubali kupokea matokeo.
Watu wa Usalama barabarani waliona vyanzo vya ajali mara nyingine ni out of control ya ubinadamu wakaweka adhabu kulingana na ubinadamu isipokuwa uzembe unapotawala, lakini Leo soka imewekewa adhabu ya kifo. Kocha anayefundisha kuinua vipaji anafungiwa kutojihusisha na soka miaka 5 bila kujali gharama za kumkosa na kukosa utaalamu wake.
Ifike mahali tukatae adhabu za kikandamizaji ambazo hazina manufaa Kwa soka letu.
Ni kweli mimi sio muumini wa kuponda udhaifu wa mtu eidha race au weakness yeyote ile

Watu tumetofautiana kihisia, kuna vitu ambavyo kwako vinaweza vikawa vidogo lakini vitu hivyo hivyo kwa mwingine vinaweza kuzuia gumzo.

Kumbuka huyo manara alishawahi dhihaki weakness ya mtu kumwambia mwakalebela ana kilo 800 kwasababu tu ya unene wake.

Kwa kipindi kile hakuna mtu aliyejitokeza kukemea hilo, hata kwa nyinyi mnao jinasibu kutokuwa na upande lakini hamkuwahi kukemea mlilichukulia poa

Ahmedy ally kila siku anaambiwa anabana pua kwasababu tu ya uongeaji wake. Lini ushawahi kujitokeza kukemea?

Au hao wanaolalamikia haji kudhihakiwa race yake ulishawahi ona wakionesha kutofurahishwa na kauli hiyo?

Mwisho ni kwamba kila mtu aplay role yake, unaweza kuwa msemaji bila kutumia lugha za kejeli zinazogusa moja kwa moja udhaifu wa mtu. Kwasababu nao hao watu watafika hatua wataangalia sehemu gani ambayo wewe una udhaifu halafu watajua watumie vipi udhaifu huo kutengeneza vijembe ambavyo vitakuuma.
 
You nailed it.
Huyu ndio wale wale hana analojua kwanini amtaje Gentamycin peke yake ni bora asingemtaja uzi wake ungekuwa bora sana ila kitendo cha kumtaja Genta peke yake na kumuacha mtu kama Demi hatuwezi kumuelewa hata kidogo yaan kashaharibu uzi wake maana tunamuona naye anachuki kwa Genta halafu anataka kuelimisha watu hana ajualo
 
Naomba nikujibu kistaarabu maana Leo umejitendea haki kama binadamu. Mleta mada hoja yake kubwa ni mashambulizi yanayohusiama na Hali ya kimaumbile ya Manara. Kitendo cha Manara binafsi huko nyuma kuwahi kutumia kauli za ovyo dhidi ya watu wengine hakuhalalishi watu wengine kumkashifu kilema chake. Wewe sijakusikia ukimuita majina ya kudhalilisha ambayo naogopa hata kuyarudia, lakini wapo mashabiki wa Simba humu kazi Yao ni hiyo na wewe unawajua. Hakuna sababu ya kudhalilisha watu kimaumbile Kwa sababu ya utani wa soka. Hata Haji alipokuwa anatoa maneno ya ovyo Wenye busara tulikemea lakini akaungwa mkono na kundi linaloshabikia ujinga ilimradi anayesema Yuko upande wao. Sisi tusio na upande tunakwazika na maneno ya ovyo yanayodhalilisha ubinadamu na tunawaomba Mods wachukue hatua Kali.
La pili umeongelea adhabu za TFF dhidi ya Mwandishi na pia kuna mdau ameongea kuhusu kocha wa Mbeya Kwanza. Mimi ni miongoni mwa watu wa awali kuona kichaa hicho cha adhabu na kukemea. Kosa la Mwandishi lilikuwa na ukubwa gani wa kufungiwa miaka 5 na Kocha akafhngiwa miaka 5 utadhani wamefanya kosa la Mauaji bila kukusudia? Hao wanasheria waliojazana kwenye Kamati ya Maadili hawaoni nchi nyingine za Ulaya zinavyoshughulika na nodhamu ya watu wapo michezoni. Hivi Morino angekuwa Kocha wa Biashara si angeshafungiwa maisha Kwa makosa yake ya mara Kwa mara?
Makosa ya kwenye michezo ni ya kawaida Sana na hayana madhara Makubwa maana mengi yanasababishwa na mihemko ya matokeo ambayo huisha baada ya watu kukubali kupokea matokeo.
Watu wa Usalama barabarani waliona vyanzo vya ajali mara nyingine ni out of control ya ubinadamu wakaweka adhabu kulingana na ubinadamu isipokuwa uzembe unapotawala, lakini Leo soka imewekewa adhabu ya kifo. Kocha anayefundisha kuinua vipaji anafungiwa kutojihusisha na soka miaka 5 bila kujali gharama za kumkosa na kukosa utaalamu wake.
Ifike mahali tukatae adhabu za kikandamizaji ambazo hazina manufaa Kwa soka letu.
Msome hapa shafii dauda

Kuna vitu havipo sawa kwenye mpira kisa Usimba na Uyanga, kuna muda tunataka kubadili nyeupe kuwa nyeusi kisa Usimba na Uyanga, this is not fair.

Nalitazama sakata la Haji Manara na hukumu ya miaka miwili namna watu wengi wanavyopinga hukumu na kuipa presha kubwa sana TFF, hiyo haipo sawa.

Mlikuwa wapi wakati Mbwana Makata anapigwa miaka mitano, Lwitiko wa Mbeya anachukua miaka 10, kuna yule Kiongozi wa Biashara United kafungiwa maisha na hata Mimi nimepigwa miaka mitano.

Haji sio exceptional ni Mwanafamilia ya mpira kama ilivyo kwa wengine, anapopewa hukumu kwa mujibu wa kanuni haipaswi kuonekana ameonewa, kumbuka hata Mimi nilifungiwa kisa tu MAKALA tena ya mtandaoni, why not Haji dhidi ya Rais wa TFF?

Tunaupa taswira gani mpira wetu? Tunamaanisha kosa likifanywa na vigogo wa Kariakoo it means linapaswa kufumbiwa macho? Jibu ni HAPANA, binafsi ni muumini wa utawala wa sheria.

Kila kitu kipo wazi sana, kama Haji hajaridhishwa na hukumu anapaswa kukata rufaa, ni haki yake! Sioni mantiki ya press na kusigana bila sababu, ni kuonesha mnataka kuwa juu ya mfumo.

Sioni sababu ya mvutano, Haji na Yanga wana vitu viwili tu vya kufanya kwasasa, kukata rufaa kama hawajaridhika au kukaa kimya ili Haji atumikie adhabu yake, nje na hapo ni kuunajisi mpira wa miguu na kupoteza sifa nzuri tunayoanza kuijenga

Nawaelewa nyote kuwa mnaamini kwenye haki na sheria, lakini kuna utaratibu wake, napenda sana kumuona Ndugu yangu Haji kwenye mpira ila kuna utaratibu wake nae anafahamu, basi muufuate

Tunapocodify na kuweka mifumo ituongoze ni kwakuwa tunafahamu sie ni Binadamu na huwa tunakosea, hatuwezi kwenda bila mfumo na sio kwa ubaya, inapokuja sheria haipaswi kuwa Simba wala Yanga bali SHERIA

DIGALA
 
Back
Top Bottom