Yanayopasa na yasiyopaswa kutendeka katika ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanayopasa na yasiyopaswa kutendeka katika ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Rapunzel, Jul 26, 2012.

 1. Rapunzel

  Rapunzel JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,089
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  NDOA ni tamu ndugu yangu asikwambie mtu, kosa ni pale wanandoa au mwanandoa mmoja anapofanya ngono nje ya ndoa, kujali sana ushauri wa watu wengine wa nje wakiwemo ndugu na wazazi au marafiki badala ya kumsikiliza na kumjali mke au mumewe, kumdharau mwenzi wake na kufanya mambo mengine ya kipuuzi kama haya.
  Je katika ndoa yako mama yako ndio mshauri mkuu? Baba yako ndio mshauri mkuu? Kama jibu ndiyo fahamu kuwa hauna akili. Ndoa yoyote, watu wake wanategemea kwa asilimia 100 ushauri wa mama zao au baba zao, ni sawa na kwamba imekufa.
  Ndoa yoyote ambayo mume anategemea ushauri wa mama yake, ni dalili kwamba mwanaume huyo ni pumbavu na kamwe hataweza kuendesha ndoa yake. Nafahamu kuwa wanaume wengi hawana muda wa kuingilia ndoa za watoto wao, wenye matatizo makubwa kwa asilimia kubwa ni wanawake, huwa wanapenda kuwaendesha watoto wao wa kiume.
  Je ndoa yako ikoje? Vitabu vitakatifu vimeeleza wazi kuhusiana na suala la ndoa kwamba wanandoa wanapaswa kujiendeshea mambo yao…kwa mfano katika Biblia inasema (Utawaacha baba na mama yako, .... mtakuwa mwili mmoja
  Ni muhimu wanandoa kupendana, kuthaminiana na kuheshimu mipango yao waliyojiwekea kabla ya ndoa kwamba utawaacha baba na mama yako na mtakuwa pamoja na huyo mwanamke ambaye leo unamtukana na kumnyanyasa au huyo mwanaume ambaye leo unamuona hana thamani hata ya kutembea nawe mitaani, wa thamani ni mama yako na baba yako.
  Kuna wanaume ukiwaangalia wanaonekana ni wenye hekima, lakini hawana akili kwa maana kuwa wanawasikiliza zaidi dada zao, mama zao na baba zao au majirani na watu wengine, kuliko kukaa na wake zao na kujadiliana nao.
  Ndugu yangu kuwa na mama au baba ni mfumo wa kawaida katika maisha, hata inzi ana baba na mama, hata kuku ana baba na mama, ni ujinga kukubali ndoa yako kuyumbishwa na kitu chochote. Kuna wazazi wengine hawana hekima, nafikiri tutakubaliana katika hili kwamba kuwa mzazi haina maana kwamba tayari umehitimu shahada ya ushauri, kwa maana hiyo ni lazima uwe makini na mzazi pia. Lakini pia kila aina ya ushauri unaopewa, ni lazima uutafakari.
  Kilichoelezwa kwenye vitabu vitakatifu ni kwamba tunapaswa kuwaheshimu wazazi, kwa maana ya kwamba tuwasaidie, tusiwadharau, au kuwatesa kwa namna yoyote, sio kuwakubalia kila kitu hata kama tunakiona hakifai.
  Kuna wanaume wana nyumba ndogo, mama zao wanajua na wanaona ni sawa, wala hawawaonyi, labda ni kwa sababu hao wanawake wa nje wana fedha zaidi ya mke au wanamsaidia. Ndio nasema ni lazima katika maisha tuangalie kwa makini namna ambavyo tunaishi.
  Mume imara anayefaa ni yule ambaye hayumbishwi na kitu chochote, kama wewe mwanamke una mume ambaye yuko karibu sana na mama yake, kiasi kwamba halali bila kumuomba ushauri kama ampeleke mtoto shule ipi au afanye lipi, pole ndugu yangu, endelea kuomba Mungu, usikate tamaa.

  NI MAKOSA MAKUBWA; Kutoa siri za tendo la ndoa au mambo yafanyikayo kitandani kwa watu wengine.
  NI MUHIMU KUFANYIKA; Ni vizuri kumtumia mke au mume ujumbe mzuri wa mapenzi.
  Kuoga mume na mke pamoja au kuogeshana: Je mara ya mwisho ni lini kuoga na mke au mumeo? Kutooga na mwenzi wako ni kosa kubwa.

  KULIKONI UNAHEMA KWA SAUTI, UNAPIGA MAKELELE KAMA UNACHINJWA BILA HAYA?; Ni vizuri wanandoa kuwa na hekima, ni lazima kujizuia namna ya kutotoa mihemo au makelele ya juu, kwa sababu unaweza kusababisha hata wasiotaka kufanya matendo haya nao kushindwa kujizuia.
  Ni kweli kwamba watu wamekuwa wakifurahia tendo kwa staili tofauti wengine kwa kufumba macho, wengine kwa kulia, wengine kwa kuhema, wengine kwa kutukana matusi makubwa, wengine kwa kusifiana viungo, sura na mambo mengine kama haya, lakini ni vizuri kuwa na hekima (fanya vitu kwa umakini).
  Sio wanawake tu, kuna wanaume nao huwa wanapiga makelele, ndio nasema kwa vyovyote itakavyokuwa, unapaswa kuangalia uko katika mazingira gani na nini cha kufanya ili usiwe kero kwa wengine.
  Ni kweli baadhi ya wadada ni matapeli tu, wanalia kinafiki ili wawaibie wanaume. Ukiona hivyo kuwa mwangalifu sana, jua unajengewa mazingira ya kuibiwa ndugu yangu maana kuna wengine wanafanya mapenzi kama biashara. Utaligundua hili hasa pale anapoanza kukueleza matatizo, eeeh kodi ya chumba imekwisha, aaah sina vocha (ukimtumia vocha unaishia kubipiwa au kutumia ujumbe, kesho anaomba nyingine, ukiuliza unaaambiwa aaah wewe bahiri sana)
  kwa leo naishia hapo.
   
 2. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ukisikiliza ushauri wa mzazi wako huna akili? duh, hii ni mpya
   
 3. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Umesema vyema, hata katika mahusiano ya kawaida sio kila ushauri unaopewa unafaa, ushauri mwingine lazima uuchuje na kuchanganya na za kwako ili ufanye maamuzi sahihi..hata kama umepewa ushauri na mzazi sio lazima ucopy na kupaste mzazi sio malaika nae ana mapungufu yake.
   
 4. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  samari jaman wengine wagonjwa:israel:
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  hii manual imekuwa verified na nani? Usije ukatulisha kasa.
   
 6. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ushauri mzuri, ingawa hautafaa ktk situation zote.
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kongosho Nafikiri ametoa maoni yake tu usiogope!!!
   
 8. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ndio maana mpaka kwenye kiSwahili kuna usemi 'adui wa mwanamke..ni mwanamke'...umeshawahi kujiuliza kwa nini hakuna usemi adui ya mwanaume ni mwanaume?

  Duniani mpaka sasa (japo si lazima ndio ukweli) lakini 'kujiamini' inaonekana ni personality ya 'kiume'...kutoogopa, kutobabaishwa..kwa mwanaume kutoogoapa ni sifa, wakati kwa mwanamke kuogopa ni sifa (chukulia tu mfano nyumbani aruke mende...kama dume litakimbia likiscream ni aibu kubwa, lakini mwanamke akifanya hivyo..ni sifa, na mwanaume atatoka aliko aje kuua huyo mende huku akijiona 'shujaa' ajabu..its just a cockroach, nothing to be hero about!)

  Ugomvi na wakwe ni hulka ya wanawake...mke na mama wa mume...wote kwa hulka yao ya kuwa wanawake. Ukikuta mume anagombana na baba mkwe, ujue kuna jambo...kwa wenzetu hawa hata lisiwepo...mwanaume akioa ikapita siku hajapiga simu kwa mamaye basi atalaumiwa MKE..na mwanaume huyu huyu akimjali mama yake basi MKE atalia wivu. Mashindano ya nani anajaliwa zaidi ni hulka ya wanawake. Ukisiliza nyimbo za taarab nyingi walizoimba wanawake ni mashindano tuu nani anapendwa zaidi na mwanaume!

  It is VERY WRONG wanawake mnaposhambulia wanaume kuwa 'weak' eti kisa kamsikiliza au kamjali mama yake...au mama kumshambulia mwanaye wa kiume kisa anaonekana kumjali sana mkewe...weakness hapo si ya mwanaume, ni yenu wenyewe na wivu wenu kati ya mwanamke na mwanamke kuhusu nani anatakiwahapendwe zaidi! Rarely a man will be the cause. Na kwa kweli watupa wakati mgumu sana...usiombee kuwa katika situation mkeo anaoneana wivu na mamayo...under no circumstance what-so-ever...huwezi kuwaridhisha wote!
   
 9. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Dah! Hili nalo neno
  Hivi anayefanya verification ya Manuals za mapenzi ya Ndoa ni nani tena?
  Tumtafute aipige hii mhuri kisha iwe legal kwa matumizi ya ndoa zote
   
 10. Rapunzel

  Rapunzel JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,089
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mzazi nae ana mapungufu yake katika ushauri c lazima ufuatishe kila unachoambiwa na mzazi wako katika masuala ya ndoa
   
 11. Rapunzel

  Rapunzel JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,089
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  dont be afraid kongosho just my opinion
   
 12. Rapunzel

  Rapunzel JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,089
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  najua hii mada inawasuta wengi sana kiasi ya kwamba mtu anadhani nimetupa dongo kwake jamani
  simjuhi mtu yoyote humu kama unafikiri nakufahamu utakuwa umekosea sana, inakuwaje wewe mwanaume mama yako mzazi akutawale pka chakula ukale kwa mama yako kila siku kisa nini?, nguo zako mama yako ndio akufulie, ukitoka kazini upite kwa mama yako kwanza usipopita mama yako anakuja juu kitu kidogo unakimbilia kwa mama, what heack of all this?
   
 13. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  "Naksh, Naksh, Nak... - A-a-hsanteeeeeeeeee"
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mh sidhani kama ni zote...ndoa tamu chache sana siku hizi
   
Loading...