Yanayojiri mkutano wa taifa vijana, Dodoma...!

hao vijana wa ccm wengi wao ni watoto wa vigogo, baadhi yao ni walala hoi ila wapo hapo ili wawe mafisadi na wengine ni wajinga aka mangumbaru
 
Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi..,Chama tawala na Chama Imara Tanzania amaliza hotuba yake kwa kuwaambia kuwa anaamini kuwa "RAIS WA TANZANIA MWAKA 2025 YUPO KWENYE UKUMBI HUU LEO HII"

Na hivi sasa anaelekea nje ya Ukumbi ambapo atapiga picha ya pamoja na wageni waalikwa kwa ajili ya ukumbusho na kisha ataendelea na majukumu yake mengine ya kuijenga na kiimarisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

RED: Kikwete huwa anawazia URAIS tu, na sasa anawaza USHINDI tu, siyo kuwahudumia wananchi kwa kutumia KODI ZAO. Anawaambia UVCCM wawazie urais tu 2025. Kuna tatizo hapa.

Rais Kikwete, kiongozi wa dola, mwenyekiti wa CCM, analalamika tu kuwa uchaguzi wa UWT ya CCM ulijaa rushwa.
 
Nadhani baada ya kumaliza hiyo speech yake sasa anaelekea kwenye vimada vyake vya UDOM ili kujivinjari!
 
Kushinda tu?.....Kushinda kivipi?......Na vipi kuwahudumia wananchi? Ndio maana alitoaahadi 100 za uwongo
Inashangaza sana. Hata juzi kwenye hotuba yake wakati akifunga uchaguzi wa UWT alisema hilohilo, kuwa lengo la CCM ni kushinda. Inashangaza kuwa hajaongelea wajibu wa chama tawala kuhakikisha kinaunda serikali ambayo iyawatumikia wananchi. Au labda kwa sababu ni uchaguzi wa chama ndio maana amezungumzia hayo na kuacha jukumu kubwa wananchi wanalolitarajia
 
Mara nyingi nimekuwa nasema Takukuru wana tumia kodi zetu vibaya na wanastahili kushtakiwa. Sioni umuhimu wa hii taasisi. Kama Amiri jeshi mkuu anaruhusu wapokee rushwa ni nani atakamata watoaji wakati tayari boss wao amesharuhusu? Tuombe Mungu Ccm iondoke madarakani mapema coz sijui wanatupeleka wapi hawa jamaa. Uongozi wa kununua ni HATARI kuliko ukimwi.
 
huo mkutano pekee una wajumbe wapatao 1300.achilia mbali wale waliopo ngazi za chini ambao wanaishia kwenye matawi kata na mashina.wewe peke ako ndio uko huko lakini vijana wenye akili timamu wapo ccm
mngejua
 
Huo mnada wao haujaisha tu? Wasiwatafutie watu lawama bure,hakuna kijana yeyote mwenye akili atakayeshawishika kujiunga na hicho chama.
 
Kwa style hii naona upinzani utapwaya baada ya uchaguzi mkuu 2015.Tunahitaji CCM kiwe chama kizuri kutukosoa baada ya uchaguzi mkuu lakini naona matumaini yanafutika.Labda CUF ijiimarishe au wafanye allince ya upinzani na CCM baada ya uchaguzi mkuu ili waunde kambi imara
 
Kwa style hii naona upinzani utapwaya baada ya uchaguzi mkuu 2015.Tunahitaji CCM kiwe chama kizuri kutukosoa baada ya uchaguzi mkuu lakini naona matumaini yanafutika.Labda CUF ijiimarishe au wafanye allince ya upinzani na CCM baada ya uchaguzi mkuu ili waunde kambi imara
Well said
 
Mheshimiwa Rais atoa hotuba kali kwa vijana ambayo inalenga kuwajenga na kuwataka wafanye tathmini ya kutosha kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa ngazi ya Taifa ya Jumuiya hiyo ya Vijana.

Alianza kwa kuwakumbusha Ibara ya 5 ya katiba ya chama cha mapinduzi ambayo inaeleza MALENGO NA MADHUMUNI ya CCM.,ambapo imeelezwa kwenye ibara hiyo kuwa madhumuni ya CCM ni "kushinda katika uchaguzi wa serikali kuu na Mitaa"

Lakini pia akaeleza kuwa CCM kinategemea Jumuiya yake hii kufanya kazi ya siasa miongoni mwa vijana wa TANZANIA na kuwashawishi wakubali kuwa wanachama na wapenzi wa CCM. Akasisitiza kuwa matumaini makubwa ya msingi kuliko yote ya Chama Cha Mapinduzi ni kuona jumuiya yake hii inakuwa MKOMBOZI wa vijana.

Akawataka wahakikishe kuwa wanapata Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na viongozi wengine ambao wataongoza vyema,watakaoongoza juhudi za kuendeleza, kutetea na kulinda maslahi ya CCM. Viongozi wanaoijua na kuipenda jumuiya ya Vijana.

Na pia akawataka baada ya uchaguzi wajipange kutimiza wajibu wao kwa jumuiya yao na Chama kwa Ujumla..,

HOTUBA INAENDELEA....

mbona unapotosha umma? Ni vijana gani hao wa Taifa?
 
Back
Top Bottom