Yanayojiri Kombe la Mapinduzi Zanzibar: Simba na Taifa Jang'ombe

Yanayojiri Kombe la Mapinduzi Zanzibar: Simba na Taifa Jang'ombe

Kuna kipande kidogo cha ukweli, bahati mbaya katika Mapinduzi 2015 Simba atatolewa nusu fainali hivyo hatakutana na Yanga, tutakutana ligi kuu bara.
basi farijianeni kwa maneno hayo
 
simba inakua kwa kushuka
Kila nikiitazama Simba ya leo nakosa tumaini na naamini kuwa kweli Tanzania aliyeturoga ameshakufa. Ndio maana baada ya muda mrefu naanza kukubaliana na mdau mmoja aliyesema Tanzania hakuna mpira ila KABUMBU.

Simba leo hii ilipaswa kuwa timu bora sio tu Afrika Mashariki bali hata ukanda wote wa mashariki kati na kusini. Kuanzia mwaka 2012, wengi wa wajuzi wa mikakati kukuza soka waliitazama Simba B kuwa ni uwekezaji sahihi katika kutengezeneza timu ya muda mrefu iliyokaa pamoja na kuzoeana kiasi cha kuleta ile maana halisi ya kitu kinachoitwa 'timu'.

Wakiwa pamoja vijana hawa walionyesha uwezo mkubwa wa kucheza soka tamu la pasi, kasi na umiliki wa mpira wa kiwango cha juu, kitu ambacho ni nadra sana kwa timu za Tz tangu kutoweka kwa timu kama Ushirika ya Moshi na Pamba ya Mwanza. Vijana walikuwa wamezoeana na kuwa kama ndugu kitu ambacho ni muhimu sana ktk kujenga mfumo sahihi wa timu ya soka au mchezo mwingine wowote.

Tatizo likaanza kwa viongozi wa Simba kuanza kutoboa jahazi la vijana hawa kwa kuanza kuwabebesha majukumu mazito ya timu ya wakubwa kabla umri wao ukiwa bado. Mbaya zaidi wakaanza kuwapachika haraka haraka kwenye timu ya vikongwe waliokuwa tayari wamepoteza morali, na maono katika career zao za soka. Vijana wakashindwa kuendana na uchezaji wa wakongwe wa kubutua, kupania, n.k na ndio taratibu viwango vyao vikaanza kushuka huku pressure ikizidi. Hapa ndipo alipopotelea Edward Christopher, Chanongo, na hata Messi

Mabadiliko ya walimu, wenye falsafa na mifumo tofauti na hata mabadiliko ya viongozi yakazidi kupigia msumari wa mwisho kwenye jitihada na maono mazuri ya Simba B. Kazi nzuri ambayo Simba waliianzisha ikauawa na Simba hao hao. Kuibuka kwa walimu kama Logarusic ambaye falsafa yake ni Big Results Now kukazidi kuwachanganya vijana kiasi cha kupoteza hata kule kujiamini kwao.

Hiki tunachokiona leo vijana kama Ibrahim Hajibu wakiendelea kujikakamua ni kama 40% ya uwezo wao halisi kama timu kama wangeendelea kukomazwa pamoja kimwili kihisia (kujiamini) na morali.
 
mtaa wa tumbo sio siasa, wakisajili wana chao cha juu

Mkuu ndo siasa zenyewe bin ujanja ujanja bin umjini mjini bin dili dili bin kupiga hela bin kupiga cha juu bin uchafu wote usiofaa kwa maendeleo ya soka.
 
Mkuu ndo siasa zenyewe bin ujanja ujanja bin umjini mjini bin dili dili bin kupiga hela bin kupiga cha juu bin uchafu wote usiofaa kwa maendeleo ya soka.
sawa au pia bin propaganda
 
celebration kubwa ni kufanikiwa kuwekeza na hawa vijana wanaelekea kuwa nguzo ya timu

  1. Manyika
  2. Isihaka
  3. Miraji Adam
  4. Gallasi
  5. Mkude
  6. seseme
  7. Hajib
  8. Ndemla
hawa wote ni matunda ya kuwekeza

cc Yeboyebo

Miraji Adam tulibadilishana na Mtibwa tukapewa H. Kessy
 
Halafu zisingekuwa siasa za viongozi wetu wale madogo wangekuwa wameshakomaa tayari na pengine tungehitaji wageni hata wawili tu. Nakumbuka kulikuwa na majina mengine kama Frank Sekule, Rashid Mkoko, Ramadhan Kipalamoto, Marcel, Abuu Hashim pamoja na Edward Christopher na Chanongo na yule Khatib mwingine. Hawa wangelelewa kimaadili lazima wangekuwa loyal kwa club kama walivyokuwa kina Giggs, Scholes, Gary na Phil Neville kwa Man U au pale Barcelona jinsi wachezaji walivyo loyal kwa club.

Mbona unataka kuniliza mkuu? Mimi hawa madogo niliwashudia KIRUMBA kwenye kombe la Ba
nc ABC niliwambia niliokuwa nao kuwa hiyo ndo ilikuwa timu sio hawa mafather. Kwa upande mwingine ushabiki wa kibongo ni wa kijinga make kama wangepandisha wote afu tukafungwa ungeona jinsi watu wangetokwa povu.Jamani wako wapi Marcel, Mkoko, Kipalamoto na Sekule?
 
Mbona unataka kuniliza mkuu? Mimi hawa madogo niliwashudia KIRUMBA kwenye kombe la Ba
nc ABC niliwambia niliokuwa nao kuwa hiyo ndo ilikuwa timu sio hawa mafather. Kwa upande mwingine ushabiki wa kibongo ni wa kijinga make kama wangepandisha wote afu tukafungwa ungeona jinsi watu wangetokwa povu.Jamani wako wapi Marcel, Mkoko, Kipalamoto na Sekule?
Wale madogo sijui waliishia wapi huenda wako timu za daraja la kwanza, sijawasikia muda mrefu.
 
Back
Top Bottom