Yanayojiri Kombe la Mapinduzi Zanzibar: Simba na Taifa Jang'ombe

Yanayojiri Kombe la Mapinduzi Zanzibar: Simba na Taifa Jang'ombe

Bila kushusha thamani ya ushindi wa mikia, Taifa Jang'ombe walikuwa wamechoka baada ya kucheza mechi siku mbili mfulilizo bila kupumzika. Waandaji waliangalie hilo mwakani. Ndiyo maana timu za nje zimeanza kutoweka taratibu.
 
celebration kubwa ni kufanikiwa kuwekeza na hawa vijana wanaelekea kuwa nguzo ya timu

  1. Manyika
  2. Isihaka
  3. Miraji Adam
  4. Gallasi
  5. Mkude
  6. seseme
  7. Hajib
  8. Ndemla
hawa wote ni matunda ya kuwekeza

cc Yeboyebo

Halafu zisingekuwa siasa za viongozi wetu wale madogo wangekuwa wameshakomaa tayari na pengine tungehitaji wageni hata wawili tu. Nakumbuka kulikuwa na majina mengine kama Frank Sekule, Rashid Mkoko, Ramadhan Kipalamoto, Marcel, Abuu Hashim pamoja na Edward Christopher na Chanongo na yule Khatib mwingine. Hawa wangelelewa kimaadili lazima wangekuwa loyal kwa club kama walivyokuwa kina Giggs, Scholes, Gary na Phil Neville kwa Man U au pale Barcelona jinsi wachezaji walivyo loyal kwa club.
 
Wamekimbia wametuacha wenyewe.Yaan natamani nusu fainali tukutane na vibonde wetu.ambao timu nzima imejaa mababu a.k.a simba B.

Hivi baada ya mechi mliendelea kushangilia eeh!

Usiku uliopita naamini mmeutumia vizuri sana kushangilia, ulikuwa ni usiku wa kuangalia sana katika kombe hili la Mapinduzi 2015 kwani usiku wa mechi ijayo hamtaonekana tena hapa jukwaani. Kajifunzeni maana ya maneno hayo!
 
Halafu zisingekuwa siasa za viongozi wetu wale madogo wangekuwa wameshakomaa tayari na pengine tungehitaji wageni hata wawili tu. Nakumbuka kulikuwa na majina mengine kama Frank Sekule, Rashid Mkoko, Ramadhan Kipalamoto, Marcel, Abuu Hashim pamoja na Edward Christopher na Chanongo na yule Khatib mwingine. Hawa wangelelewa kimaadili lazima wangekuwa royal kwa club kama walivyokuwa kina Giggs, Scholes, Gary na Phil Neville kwa Man U au pale Barcelona jinsi wachezaji walivyo royal kwa club.

Lugha za watu hizi!!!!!!!!!!!

loyal adj.
1 faithful and true.
2 personally devoted to a sovereign, government, leader, friend, partner, etc.
3 expressing or showing loyalty o the loyal toast to the Queen.
loyally adverb.
[16c: from French loial, from Latin legalis legal.]

royal adj.
1 relating to or suitable for a king or queen.
2 (sometimes Royal) under the patronage or in the service of the monarch o Royal Geographical Society.
3 belonging to the monarch.
4 related to the monarch.
5 regal; magnificent.
6 larger or of better quality, etc than usual.
7 naut situated immediately above the top-gallant.

Source: Chambers 21st Century Dictionary.
 
R na L ni janga la kanda ya ziwa.
 
Halafu zisingekuwa siasa za viongozi wetu wale madogo wangekuwa wameshakomaa tayari na pengine tungehitaji wageni hata wawili tu. Nakumbuka kulikuwa na majina mengine kama Frank Sekule, Rashid Mkoko, Ramadhan Kipalamoto, Marcel, Abuu Hashim pamoja na Edward Christopher na Chanongo na yule Khatib mwingine. Hawa wangelelewa kimaadili lazima wangekuwa royal kwa club kama walivyokuwa kina Giggs, Scholes, Gary na Phil Neville kwa Man U au pale Barcelona jinsi wachezaji walivyo royal kwa club.

Umenena vyema Mkuu.. ila tunatakiwa tuwalinde hawa waliobaki nao wasije "choropoka".
 
"huyu goran ni bingwa sana wa kusoma mbinu za timu pinzani, na anapenda mpira wa kasi na kuanzisha mashambulizi kutokea pembeni" Dany Mrwanda akimzungumzia kocha wake wa zamani Goran Kopunovic.

Nimeamini maneno ya Mrwanda, maana 2nd half alipoingia Ajibu wenyewe tunajua kipi kilitokea. #NinakumbukaKitambo
 
Heshima kwako mkuu MM....Lakini mkuu nadhani unajua kwa simba hata iwe mbaya vipi...yanga haina uwezo wa kutufunga

Kuna kipande kidogo cha ukweli, bahati mbaya katika Mapinduzi 2015 Simba atatolewa nusu fainali hivyo hatakutana na Yanga, tutakutana ligi kuu bara.
 
Halafu zisingekuwa siasa za viongozi wetu wale madogo wangekuwa wameshakomaa tayari na pengine tungehitaji wageni hata wawili tu. Nakumbuka kulikuwa na majina mengine kama Frank Sekule, Rashid Mkoko, Ramadhan Kipalamoto, Marcel, Abuu Hashim pamoja na Edward Christopher na Chanongo na yule Khatib mwingine. Hawa wangelelewa kimaadili lazima wangekuwa royal kwa club kama walivyokuwa kina Giggs, Scholes, Gary na Phil Neville kwa Man U au pale Barcelona jinsi wachezaji walivyo royal kwa club.

Kila nikiitazama Simba ya leo nakosa tumaini na naamini kuwa kweli Tanzania aliyeturoga ameshakufa. Ndio maana baada ya muda mrefu naanza kukubaliana na mdau mmoja aliyesema Tanzania hakuna mpira ila KABUMBU.

Simba leo hii ilipaswa kuwa timu bora sio tu Afrika Mashariki bali hata ukanda wote wa mashariki kati na kusini. Kuanzia mwaka 2012, wengi wa wajuzi wa mikakati kukuza soka waliitazama Simba B kuwa ni uwekezaji sahihi katika kutengezeneza timu ya muda mrefu iliyokaa pamoja na kuzoeana kiasi cha kuleta ile maana halisi ya kitu kinachoitwa 'timu'.

Wakiwa pamoja vijana hawa walionyesha uwezo mkubwa wa kucheza soka tamu la pasi, kasi na umiliki wa mpira wa kiwango cha juu, kitu ambacho ni nadra sana kwa timu za Tz tangu kutoweka kwa timu kama Ushirika ya Moshi na Pamba ya Mwanza. Vijana walikuwa wamezoeana na kuwa kama ndugu kitu ambacho ni muhimu sana ktk kujenga mfumo sahihi wa timu ya soka au mchezo mwingine wowote.

Tatizo likaanza kwa viongozi wa Simba kuanza kutoboa jahazi la vijana hawa kwa kuanza kuwabebesha majukumu mazito ya timu ya wakubwa kabla umri wao ukiwa bado. Mbaya zaidi wakaanza kuwapachika haraka haraka kwenye timu ya vikongwe waliokuwa tayari wamepoteza morali, na maono katika career zao za soka. Vijana wakashindwa kuendana na uchezaji wa wakongwe wa kubutua, kupania, n.k na ndio taratibu viwango vyao vikaanza kushuka huku pressure ikizidi. Hapa ndipo alipopotelea Edward Christopher, Chanongo, na hata Messi

Mabadiliko ya walimu, wenye falsafa na mifumo tofauti na hata mabadiliko ya viongozi yakazidi kupigia msumari wa mwisho kwenye jitihada na maono mazuri ya Simba B. Kazi nzuri ambayo Simba waliianzisha ikauawa na Simba hao hao. Kuibuka kwa walimu kama Logarusic ambaye falsafa yake ni Big Results Now kukazidi kuwachanganya vijana kiasi cha kupoteza hata kule kujiamini kwao.

Hiki tunachokiona leo vijana kama Ibrahim Hajibu wakiendelea kujikakamua ni kama 40% ya uwezo wao halisi kama timu kama wangeendelea kukomazwa pamoja kimwili kihisia (kujiamini) na morali.
 
Kuna kipande kidogo cha ukweli, bahati mbaya katika Mapinduzi 2015 Simba atatolewa nusu fainali hivyo hatakutana na Yanga, tutakutana ligi kuu bara.

Amini usiamini mkuu...kwa simba hii hii unayoiona ni dhaifu itafika fainali na itachukua kikombe

Ninyi ombeni mkutane na Azam

Mkikutana na Mtibwa ndio mwisho wenu
 
Amini usiamini mkuu...kwa simba hii hii unayoiona ni dhaifu itafika fainali na itachukua kikombe

Ninyi ombeni mkutane na Azam

Mkikutana na Mtibwa ndio mwisho wenu

Mkuu sisi yeyote atayekatisha mbele yetu, imekula kwake including Simba.
 
Mkuu sisi yeyote atayekatisha mbele yetu, imekula kwake including Simba.

Duh...huo ujasiri wa kuifunga simba mnautoa wapi mkuu?

Cha kushangaza tukiwafunga mnasingizia ushirikina

Na ni kwa nini ni Yanga tu hua wanalalamikia ushirikina?

Inaonekana wao ndio mbinu zao ndio maana wanadhani kila timu inafanya hivyo.
 
Yanga ndiyo tageti la wachawi katika soka:

'DOUGLAS Muhani, beki wa zamani aliyepata kuchezea klabu kadhaa za Tanzania pamoja timu ya taifa, Taifa Stars, anakumbuka siku ambayo yeye na wachezaji wenzake walipokesha makaburini wakiroga ili kupata ushindi. Hii ilikuwa ni mechi ya Ligi ya Taifa Tanzania katika kituo cha Mwanza mwaka 1978, wakati akiichezea Sigara (sasa Moro United) na mechi hiyo ilikuwa inaikutanisha timu yake na Yanga. Tuliambiwa na mtaalamu wetu kutoka Tanga kwamba lazima tufanye ndumba kwa sababu mechi ingekuwa ngumu. Mganga wetu, ambaye tulikuwa naye tangu mwanzo wa mechi zetu, alituambia kwamba tungeshinda, lakini mwenzetu mmoja angedondoka uwanjani Tuliamriwa kutomgusa wala kumsogelea, kwa sababu kufanya hivyo kungemaanisha kwamba angepoteza maisha," anakumbuka. Na kweli, kabla hatujafunga bao, mchezaji mwenzetu, John Mlebo, alianguka na kuzimia. Tulimtazama tu mpaka alipochukuliwa kwenye machela. Tulifunga bao, na wakati tulipodhani tumeshinda, Omar Hussein akaisawazishia Yanga zikiwa zimesalia dakika nane tu."

Source: Imani za uchawi zinavyoangamiza soka, nini kifanyike kwa sasa? - Fikra PevuFikra Pevu
 
Bila kushusha thamani ya ushindi wa mikia, Taifa Jang'ombe walikuwa wamechoka baada ya kucheza mechi siku mbili mfulilizo bila kupumzika. Waandaji waliangalie hilo mwakani. Ndiyo maana timu za nje zimeanza kutoweka taratibu.
tatizo mnasahu haraka sana
 
mtaa wa tumbo sio siasa, wakisajili wana chao cha juu
Halafu zisingekuwa siasa za viongozi wetu wale madogo wangekuwa wameshakomaa tayari na pengine tungehitaji wageni hata wawili tu. Nakumbuka kulikuwa na majina mengine kama Frank Sekule, Rashid Mkoko, Ramadhan Kipalamoto, Marcel, Abuu Hashim pamoja na Edward Christopher na Chanongo na yule Khatib mwingine. Hawa wangelelewa kimaadili lazima wangekuwa royal kwa club kama walivyokuwa kina Giggs, Scholes, Gary na Phil Neville kwa Man U au pale Barcelona jinsi wachezaji walivyo royal kwa club.
 
ulitaka tuhuzunike?

Back
Top Bottom