Nilikuwa naangalia Bunge linaloendelea mjini Dodoma,mbuge wangu wa Jimbo la Bukene,hata simfahamu jina lake kamili,namfahamu kama Zedi,anasimama kwa kuanza,"...naunga hoja kwa asilimia mia...". Sasa mwisho wa siku anasema bajeti hiyo(katika wizara ya maji) haitatosha sawasawa kwani kwenye jimbo langu kuna maeneo mengi yenye shida na maji.Sasa hapa,Mnyika alipopata fursa ya kuzungumza akauliza swali,kama anasema anaunga mkono kwa asilimia mia,halafu mwisho wa siku unasema haitoshi,unaunga mkono nini?
Mzalendo wangu ndo aliposimama(Lissu) akaja na shuhuda nyeti kwamba bajeti ya maji ipo kwa upendeleo mkubwa sana,maeneo ya wakubwa,mfano,kata anayotoka waziri wa maji,Bw.Magembe imetengewa bilion 1.6 wakati kata moja ya singida imepangiwa milion 100 tu(maelezo haya yalikuwa katika maandishi hotuba ya waziri wa maji,ambayo Lissu aliitumia kama rejea[reference] mbele ya waziri mwenyewe).
Hapa ndipo najifunza kumbe Lipumba hakukosea kuwaita MA-INTERAHAMWE maana yamejaa upendeleo,unafiki na uzuzu.
SOURCE;Bungeni asubuhi,nilikuwa naangalia kwa Luninga