Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Amon anawaasa wabunge kutohubiri ubaguzi wa kikabila na aina nyingine ya ubaguzi. Hata humu JF nami napinga kabisa ubaguzi wa wazi unaooneshwa na huyu Kayoka
 
Amon Mpanju anasema;
Yanapotokea mafuriko kama haya walemavu tunataabika. yanapotokea mabomu walemavu tunataabika.

Sijapendezwa na kauri ya viongozi wanaosema kwamba kama serikali tatu haziruhusiwi tupo tayari kwa lolote. mimi ni mwenyekiti wa walemavu nina wafuasi pia, kuna wakulima wana wafuasi pia. Watanzania wenzangu hatunabudi kuwasusa watu wa namna hii. nawaomba sana vijana tusiwaunge mkono.

Jusa alinambia anapuuza taarifa na mimi ananipuuza. maneno haya yaliwaumiza walemavu. Tusimguse Mungu machoni kwani hakuna aliye amua kuwa mlemavu.

ibara ya nne kuna mapendekezo yameletwa nami nayaunga mkono. ligha ya alama na lugha ya alama amguso itakua ni ligha ya alama kwa watu wasio ona. haya mabadiliko nayaunga mkono.

Nashangaa sana wanaanza kuhoji na kubeza uhalali wa huu muungano hasa tundu lisu. huu muungano sio wa wanasheria ,huu muungano unatambulika hadi UN. huu muungano una matatizo lakini tunaweza kuyatatua kwa kupitia muundo wa serikali mbili. uanasheria wenu usiwe kero.

Tuache kupotosha watanzania. serikali tatu ni kaburi la Muungano. tuache kuhubiri ubaguzi la sivyo zanzibar watagawana mikoba na huku bara tatagawana mikoba. Tuache kuwapa nafasi wazandiki na wanafiki wa nchi hii. wanasema wana watu wakati hawana watu kalenga na chalinze ilionesha
 
Unazungumzia Chadema au Tundu Lissu? Kama ni mfuatiliaji mzuri ungeweza kuona mipasho wanayotoa Chadema na matusi juu, sasa wakijibiwa ndio iwe nongwa?....haifai bwana jino kwa jino.

Watanzania woooote wanajua kuwa ccm hawana hoja zaidi ya ujanja ujanja na uhun uhun na mipasho.
 
Walemavu wanadeka sana aisee,wanatumia vibaya ulemavu wao,kwamba wao wasichalenjiwe,hawa wametumwa,inajulikana ivo
Ni kweli alipuuzwa si kwa ajili ya macho yake, bali kwa hoja na ndio kinachofanyika
bungeni watu hupuuziana kwa hoja, hata mimi nampuuza sana Mpanju kwa hoja zake
kwani anawakilisha walemavu lakini anajitoa akili na kuwa kama mwakilishi wa CCM.
 
Baada ya huyu msemaji wa sasa atafuatiwa na mheshimiwa Kisasi kisha mheshimiwa Jussa.
 
Kaongea vizuri lkn mwisho kajionyesha kabisa hayupo bungeni kuwakilisha walemavu bali yupo kuiwqkilisha ccm sasa kalenga na chalinze kwa uwakiloshi wake vinahusika na nn
 
Ujinga huu hakika ni aibu kwa JF

hata kama unachongea kwa moderators ukweli ndo huo.
Hebu msikie hoja zake huyo mpanju.
Ina maana na yeye anashindwa kuelewa hesebu ndogo kama hii hapa:
x + y = xy
badala ya kusema hii


x + y = xy + y.

Where as
x - tanganyika
y- zanzibar
xy- Tanzania
 
Nimemsikia mama Kabaka akisema kuwa jinsia ni tunu ya Taifa. Hoja yake kaijenga kwa kuwauliza wanaume kwamba wangejisikiaje kama wangekuwepo wanaume peke yao ndani ya bunge. Akaendelea kuwaulizia wangefurahi kama wangekuwa peke yao. Mmmmmmhh mimi nimebaki macho pima

HUYU mama na watu wengi kwenye Bunge la katiba hawawezi kutafautisha kati ya "JINSI" na "JINSIA". Huyu mama alochosema ni 'jinsi' na siyo 'jinsia'. Jinsi ni ya kibaolojia (a-kike au a-kiume), jinsia ni mfumo wa maisha kati ya binadamu aghalabu ukiegemea zaidi kiuchumi-jamii, utamaduni, dini nk. Unyanyasaji wa Kijinsia unawezekana hata kati ya jinsi moja kama vile wanawake au ndani ya wanaume.
 
Kisasi anasema;
Naunga mkono maoni ya walio wengi.
------------------------------------------------

ngoja ninywe maji kwanza
 
Huyu kipofu ameamua kapisa kuweka hazarani mahaba ya ccm.
Amemaliza kwa kusema salamu za Kalenga na Chalinze ziwafikie..........


Na mimi namwambia Mungu hufanya jambo kwa makusudi/habahatishi, hivyo alimjua kabla ya kumuumba.
 
Back
Top Bottom