Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Trh 15 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima kwa sura ya 1 & 6

Watanzania wenzangu nimesikitishwa sana na mambo yanayoendelea bungeni

Lugha inayotumika kwa wajumbe si ya staha kabisa, malengo hasa ya kujadili rasimu ya jaji warioba siyaoni? na sissiemu kwa makusudi kabisa nadiliki kusema wametupotezea tena pesa zetu nyingi (Gharama za zaidi ya milioni 100 zilizotumika na wakina jaji warioba)

Tujikumbushe kidogo,

Mara baada ya uchaguzi mkuu wa uraisi 2010, sisisemu hawakuwa na ajenda kabisa ya kuandika katiba mpya, mara tu baada ya kelele toka upinzani ndipo jk akalishilikilia bango lakini mawaziri wake wakubwa kama Jaji werema na mama serilina kombani na wakina chikawe wakasema hakuna haja ya katiba mpya. Kwa kweli tungejua ni heli tusingepoteza hizo fedha na muda tungeacha tu, kwa sababu sasa hivi bungeni ni dhahiri shairi kuwa Sisiemu wote wa zanzibar na bara wanataka hali inendelee kama ilivyo yaani serikali mbili.

Sasa najiuliza kwanini jk alikurupuka kutuingiza gharama za hizi katiba mpya wakati hata yeye mwenyewe amaeonyesha kutoiunga mkono rasimu hii ya katiba, na sasa sisiemu wote wanashikiria suala lile lile la serikali mbili kama jinsi lilivyo SASA Liendelee,

Wanakataa hata suala la uwazi na uwajibikaji kuwa moja wapo ya tunu za taifa, leo nchi zinazoendelea zote hii ni silaha muhimu katika kuleta maendeleo, sasa hutaji uwazi na uwajibikaji unataka nini??

Sioni dalili za kusikilizana hata kwa wazazibar wenyewe, tayari wanatofautiana kwa itikadi za kichama, sasa najiuliza kelele zao hasa huko nyuma ni zipi kama wanaona huu muuondo unafaa, kwanini walikubali kutoa maoni?? mbona wanaserikali ya mseto?? mbona tayari wanaserikali ya nchi yao yenye mamlaka kamili, Tanganyika iko wapi??

Maana sielewi huu Muuungano ambao nchi mmoja inaishi na kuonekana (Zanzibar) wakati Tanganyika haionekani, halafu tunasema serikali mbili ziendelee??

NAJIULIZA KAMA HAWAKUWA TAYARI KWA MABADILIKO?? KWANINI WAMERUHUSU TUPOTEZE MUDA NA MAMILIONI YA SHILINGI HATA SASA BUNGE LA KATIBA LINAKULA ZAIDI YA MILIONI 180 KWA SIKU, WAKATI HAWAKO TAYARI KUKUBALIANA NA MAONI YA WANANCHI.. NI HATARI SANA HII.

WATOTO HAWANA MADAWATI, SASA MIUNDO MBINU IMEHARIBIKA ZAIDI, MAJI SHIDA, AJIRA SASA NI MAJANGA, NA KWA HARI HII TUTENGEMEE MATATTIZO ZAIDI YA HUDUMA ZA KIJAMII KUYUMBA KWA SABABU PESA NYINGI ZINATUMIKA KATIKA KATIBA HII, AMBAYO SISIEMU TAYARI WAMEONYESHA KUKATAA MAPENDEKEZO YA TUME WALIYOIPA MAMALAKA WENYEWE NA KULETA MAONI YA WANANCHI.

WATANZANIA TUNA PESA KIASI GANI HATA TUZICHEZEE KAISI HIKI??
 
Punde utamsikia sheni naye akiunga mkono serikali 3, kwa nini wanawachukia wenye asili ya kiarabu kwani Karume alikuwa na asili gani na watoto wake wana asili gani na je mmoja wao ajawa rais wa zanzibar ?
 
Dovutwa anasema:
Alama za taifa zitakua Wimbo wa taifa, nembo ya taifa na bendera. Dora haimtambui Mungu kwa hiyo iyo wimbo wa taifa itolewe kwenye alama ya taifa. dhana ya Kuomba Mungu asaidie inamaana Dola inasilikiliza wanaMungu tu wakati taifa hili halifungamani na dini. Nami ntasimama ntapigana kuhakikisha Katiba inamtambua Mungu.

Kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine. sera ya tanu iliruhusu wazee watoto na walemavu kunyonya. nataka iwe kutegemeana sio kunyonyana.

Watu wqanaoamini serikali tatu mpaka sasa wameshindwa kutuonesha jinsi watakavyo tatua matatizo tulio nayo. watu wa serikali tatu wameshindwa kujenga hoja. Namlaumu sana Mbowe. Chadema wana wana serikali za majimbo lakini wanashindwa kufafanua vizuri.

Natoa shukrani za pekee za rais kwa kulidhia hii ijadiliwe na kusimamia elimu za kata. namshukuru pia Lowasa aliye mshauri Rais
 
Dovutwa ni kichaa watu wanajadiri muundo wa muungano yeye anamsifia Kikwete na Lowasa kwa shule za kata.

Huyu ni bure kabisa.
 
MBILINYI anazungumza mambo ya msingi sana. Vizuri sana hii ni kwa Resima watubie ma kuwapa wananchi wanachotaka.
 
Hapana hakumsaliti "Abdul" Jumbe, alimsaliti Aboud Jumbe.

Badili umekosea, na uombe moderator abadili jina uliloweka.

Dah! vijana wa Kitanzania mnasikitisha sana IQ zenu, hata aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Muungano hamumjui jina lake? mnasikitisha sana.

Halafu watu kama wewe ndiyo wabishi ikija historia ya Tanzania na Tanganyika mnakuwa wabishi ajabu, mnajifanya mnajuwa kila kitu kumbe hata huyu aliye hai bado hamumjuwi.

Pole sana.

Kuna mmoja alinambia Dr. Shein alipokea kijiti cha urais toka kwa Abeid Aman Karume. Tena akiwa serious kabisa.
 
Kwa ujinga wa wanaccm na uroho wa madaraka tayari kwa kadiri mjadala unavyoendelea ulionzaq kugusa upemba na uunguja , kupata theluthi 2 kwa zanzibari wasahau


Mkuu nakubaliana na wewe, kuhusu Wazanzibar muungano na Tanganyika si tatizo, tatizo ni Upemba na Uzanzibari. Kwao serikari mbili si tatizo tatizo ni kama Mpemba hastaili kutawala tokana na asili yake.
 
maige kasema suala la serikali ya muungano kuisaidia znz, mbona hiyo ya muungano haisaidii bara?kasema znz inafaidika zaidi maana ina barabara za lami wilaya zote na umeme kuwaka wilaya zote angali tz bara pwani umeme hakuna.
 
Huyu si ndiye yule aliyegombea urais akasema kura zake wampe kikwete ? mmesahau mara hii, hao ukisikia kura za urais kapata ujue kalamu ilitua kwa bahati mbaya tu
 
Sugu: wenzetu tulikuwa wote mkiti wao alipohubiria wameingia mitini meli inazama basi tikiseni miguu tujue mko hai...
 
Unaoga nje!!!!!?????

Hahahaaaaaa... niko bafuni. Any way ameshauri hili swala la katiba lisifanywe la vyama vya sasa bali liwe la wananchi kwa sababu vyama vinapita, mfano leo wanatawala ccm wanataka serikali mbili je wakiingia chadema au cuf itakuwaje??? Kashauli iitishwe kura ya maoni tuwaulize wananchi ili kusiwe na Chama chochote cha siasa kitakachojinasibu kuwa huu muundo ni wetu
 
Back
Top Bottom