Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumamosi, Tarehe 12 Aprili 2014 - Uwasilishaji wa Taarifa za Kamati

KAKA HAWA WAHUNI MWISHO WAO UMEFIKA HATA NAO WASIPO RUSHWA cc tumeshapata, CCM NA WANACHAMA WAO NI ISHARA YA LAANA KWA HILI TAIFA.
Napenda kutoa wito kwa vituo hivyo viwili kurudia hotuba mh.Tundu Lissu alioitoa bungeni ambayo kwa bahati mbaya ilikatika kwa kile kilichielezwa na TBC 1 kuwa kimetokana matatizo ya kiufundi na si vinginevyo.

Ukweli wa maelezo ya TBC wanaujua wenyewe kwani mwenendo wao ni wa mashaka.

Nawaomba wamiliki wa vituo hivyo muwe wazalendo na kuweka mbele maslahi ya taifa.

Mods naomba msiunganishe huu uzi kwani mh.Lissu alikuwa anafanya kile kinachoitwa "kukata mzizi wa fitina" kwa faida ya umma hasa kuhusu uhalali wa hati ya muungano.
 
Chabruma umepoteza credibility hapa jamvini ya kuripoti yanayojiri bungeni wewe ni mnafki mkubwa sawa na Mwakyembe na Shivji, usitie puwa yako hapa jumatatu tutapeana wenyewe updates kupitia vyanzo mbadala.
Mnafki mkubwa wewe.

Chabruma njoo ujibu hoja hii ili jamii itakayosoma bandiko hili ipambanue ukweli ni upi.
 
Last edited by a moderator:
TBC1 imemkata Tundu lissu akitoa elimu ya muungano,sasa hii ni mwanzo tu sasa je tutafika?
 
Safi kumbe shivji ni penguin anayosema sasa sio yale aliyokuwa anayaamini hapo zamani upro wake unamatatizo inatakiwa tuombe mwongozo ili tufanye uchunguzi wa huo upro, huwezi pro mzima ukawa kigeugeu vitabu vitatu vyote unazungumzia serikali tatu, kanusha kwanza vile sio vitabu vyako.
Hongera Kingwala kwa kumwita Shivji na mwakyembe ni penguin hawajui kuchambua data kwa lakini hizo ndizo zilizowapa Dr. na Pro
 
nakumbuka kusoma kwenye history kuhusu mfalme chabruma wa kule kusini,Nasikia alipigana na wareno,chabruma alikua shujaa lakini wareno walimzidi nguvu,ilibidi akimbilie msumbiji.

Shujaa chabruma alivuka mto ruvuma bila kulowana map*mb*.

mmh hiyo historia yako nayo!! bila kulowana...??? basi inawezekana hata chabruma wetu kashavuka mpaka wa dodoma anakaribia singida dakika hii, basi uyu atavuka bonde la sekenke kuelekea shinyanga bila ya kulowana ma...hapana, bila ya kuvuja jasho!!
 
kwa kodi ninayolipa naweza hata kulipa wafanyakzai wa serikali wawili kila mwezi, hatuwezi kuendelea kuchangia ruzuku ili icho kichaneli kioneshe ushenzi, tunataka kodi iende sawa, acheni uhuni!!
Kwahiyo maagizo ya viongozi wako kugomea kuangalia TBCCM umeyapuuza?
 
Kuna hotuba za kujenga na kuna hotuba za kubomoa,, sasa kwa wanaoipenda Tanzania wao wenyewe wapime maana zote zinavutia kusikiliza lkn zina matokeo na athali tofauti zikitafsiriwa.
 
Mkuu skype heshima yako!
mimi naomba kama unaweza uirushe clip ya Tundu lisu alipokuwa anaongea saa hizi!ni muhimu sana tuipate kwasababu kumbe tulikuwa tunadanganywa kuhusu muungano!


Mkuu! Uko Dunia gani Mkuu? Huu Muungano unashida sn ni kwamba ukweli uzibwa kwa Nguvu zote Lkn Ktk hili swala kuna kero nyingi mno!
 
TBC radio na televison ya taifa kimsingi zilitakiwa kuwa pengine mstari wa mbele kuliko chombo chochote cha habari katika nchi yetu. Inasikitisha sana kuona imeamua kuwatupa wananchi wanaokatwa kodi kuendesha chombo chao ili kupata habari zote muhimu bila chenga, na TBC kuamua kujiunga na mafisadi, wanyonjaji na mibaka uchumi wa taifa letu kuficha ukweli kuhusu swala la muungano na hati ya muungano. Dhambi hiyo ya kukata matanagazo wakati wa hutuba ya Tindu Lissu ili mje na sababu kuwa mlipata itilafu iliyo nje ya uwezo wenu, mjue tu Tanzania ya leo, kizazi hiki si kile cha kudanganywa kitoto kwa namna hiyo.

Kwa kua mmeshindwa kutetea wanyonge, kuhabalisha ukweli na kuzingatia maadili yenu ya vyombo vya habari Historia itawahukumu na dhambi hiyo haitawacha salama. Na sasa mumeamsha moto waa kila mtanzania kufuatilia kwa makini na kujua kiundani kuhusu hati ya muungano kama ipo au ni porojo tu mmetuaminisha kwa miaka 50. Lazima wananchi waelewe na nihaki yao kupata taarifa na ikiwezekana copy zisambazwe ili kizazi kijacho 100 years later wasidanganywe kama kizazi chetu.

"A day is coming soon when no stone will remain unturned"
 
Tundu Lissu hiyo hotuba tunaihitaji sana ikibidi ujirekodi upya kabisa uiweke YouTube ili watu wengi waipate...itasaidia sana kuwafungua vichwa waTanganyika walio wangu.

Atawekwa kizuizini kwa kosa la UHAINI, ni ile kinga ya Bunge inamlinda Lissu

Huwajui ccm nini wewe
 
Last edited by a moderator:
Anaedai muungano ulindwe kwa gharama zote sawa lakini kabla hatujafika huko leteni kwanza hati ya Muungano tujue tunalinda nini
 
Hili bunge nafikiri liahirishwe tu maana hakuna chochote kipya wanachofanya zaidi ya kurudia yaleyale tu....bora tubaki tulivyo kuliko ubabaishaji huu......
 
Mlimo hao ccm na vaibaraka wao ni ishara ya laana kwa taifa hili ila namshukuru mungu kwamba mwisho wao umefika,
 
Huu ni upuuzi watz uwoga ndio umaskini wetu tunazidi kuishi kweny maisha magumu wakati kuna watu hawataki tujue mambo yanayoendelea ili tuchambue mbivu na mbichi ,,,hii ni mbinu iliyopangwa makusudi kuhakikisha ccm wanafanya km walivyokusudia, Amkeni watanganyika tudai nchi yetu hata kwa mabavu
 
Kwa kweli TBC wanachotufanyia si haki kabisa!!... Wakumbuke kuwa mishahara yao inatokana na kodi zetu leo wanatunyima fursa ya kupata Habari....

Je kuna umuhimu wa kuendelea na hiki kituo kuitwa Televisheni ya Taifa?

Tusiwalaumu sana TBC, wanapokea tu maagizo. Wa kushughulika nao ni hao wanaotoa maagizo. Kwa wenye akili timamu wanajua maagizo yanakotoka
 
Ukiukaji wa haki za binadamu umezidi kutawala sekta zote, vyombo vyote vya habari pamoja na majukwaa yote ya kijamii. Raia hana tena uhuru wala haki ya kutoa na/ kupata habari au maoni!!

Raia tuko katika giza nene na hatuna msaada wa wapi tutolee/ kupokelee habari!
 
Back
Top Bottom