Yanayojiri Bungeni Dodoma: Ijumaa, January 30

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Ijumaa, January 30

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
Habari wakuu,

Tuwe pamoja kutoka bunge la Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dodoma, aliekalia kiti leo ni Mheshimiwa Zungu
===========================

HATI ZA KUWASILISHA MEZANI
Mwenyekiti kamati ya miundominu: Amewasilisha ripoti ya mwaka

Mwenyekiti Nishati na madini: Nawasilisha taarifa ya kamati ya nishati na madini kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa mwaka 2014

MASWALI
Kasikila: Serikali ina mpango gani wa kujenga hospitali katika wilaya mpya Kalambo

Majaliwa(Jibu): Ili kuanza ujenzi wa hospitali, serikali imeshatenga eneo na halmashauri imeshapanga kutenga milioni 100 katika mwaka ujao wa fedha

Kasikila: Kituo cha afya Matai kimeteuliwa kuwa hospitali ya wilaya lakini hakina uwezo, ni lini serikali inapanga kuwapa wananchi wa Matai hizo Milioni 100, watu wanapeleka wagonjwa Sumbawanga, lini serikali inajenga hospitali ya wilaya.

Majaliwa(Jibu):
Ni kweli halmashauri inahitaji hospitali yenye uwezo lakini kwa sasa, wizara tunaangalia mahitaji muhimu kwanza, tutahakikisha hospitali itoe huduma kwa haraka. Wote rufaa zao ni hospitali ya mkoa, ni kwa sababu sehemu husika huduma bado hazikuwa tayari, tunawashirikisha pia CHF

Suzan: Dhana ya upandishwaji hadhi hospitali, zinapandishishwa bila huduma yoyote kuongezwa, dhana hii maana yake nini?
Jibu:
Dhana hii ni kwanza kutokana na mahitaji ya eneo husika ya rufaa zake lakini inaenda sambamba na uboreshaji na mipango yake inatakiwa iandaliwe. ofisi ya mkoa lazima iweke mahitaji yake.

Nassari: Mpango wa vituo vya afya umekuwa mgumu kutekelezeka kutokana na kutopeleka watumishi na vifaa
Jibu: Utumishi wameshaomba kibali cha kuajiri, mchakato ukikamilika tutapeleka watumishi


Kilufi(Mbarali): Ni lini maslahi ya madiwani yataboreshwa?
Jibu: Serikali imekua ikiboresha maslahi yao na limekua likijaliwa mara kwa mara serikali, serikali imeshafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuongeza posho.

Nyongeza: Madiwani maeneo wanayotawala ni makubwa sana, serikali iko tayari kuwakopesha vyombo vya usafiri kama pikipiki?
Jibu: Tuliwahi kuwasiliana na wakurugenzi wote waangalie ni jinsi gani watawawezesha kuwakopesha vyombo vya usafiri, baadhi ya halmashauri zimetekeleza.

Leizer: Halmashauri vyanzo vyao vidogo, kwanini serikali isichukue jukumu hilo tena kwa kuwakopesha magari?
Jibu: Naomba nilichukue hilo.

Nyangwine: Watanzania wengi wanapenda soga kuliko kufaya kazi, serikali ina mpango gani?
Jibu: Kila mtu anao wajibu wa kujituma kwa kazi halali, serikali imetunga sera mbalimbali kuhusu umuhimu wa kufanya kazi. Naomba waheshiwa wabunge tushirikiane wananchi watii sheria bila shuruti.

Mbasa: Seikali ina mpango gani wa kukarabati uwanja wa Biharamulo?
Jibu: Matengezo ya barabara yanafanyika kila wakati, namuahidi itaendelea kufanya matengenezo kiwanja cha Biharamulo

Swali:
:Uwanja wa Arusha ndege kubwa haziwezi kutua na hamna taa, lini serikali itakarabati?
Jibu: Serikali ina ufahamu umuhimu ya uwanja huo na kufunga taa, urefu wa uwanja ule una limitation. Mpango upo wa kujenga jengo zuri la abiria na kufunga taa.

Rage: Serikali imetumia pesa nyingi kukarabati viwanja vya ndege lakini ndege hamna, ni lini ATCL itaweza kupata ndege ili tupate huduma?
Jibu: Hilo ni swala la kibiashara ndege kwenda au kutokwenda hata ATCL ingenguwepo.

Rukia: Serikali imafanya uchunguzi wa faida na hasara kwenye zao la tumbaku
Jibu: Ni zao linalochangia pato la taifa ikiwemo ajira, zao la tumbaku linaongoza kwa kuleta fedha za kigeni katika mazao ya kilimo, serikali inafahamu athari za kimazingira na za kiafya. Kumwkuwepo na taarifa kuwa matumizi ya bidhaa za tumbuku inaleta magonjwa ya mapafu na saratani, tahadhari hutolewa ili kulinda afya sawa, serikali inapendekeza mazao mbadala badala ya tumbaku.

Rukia: Kwa kua serikali inaelewa athari ikiwemo saratani ya mapafu ocean road, haioni umuhimu wa afya za watanzania kuliko mapato
Jibu:
Tunawaelimisha watumiaji madhara

Zitto: Wakulima wa tumbaku wamekuwa na shida ya kudhulumiwa pesa zao na hamna hatua zilizochukuliwa
Jibu: Nikiri serikali inatambua upotevu wa pesa Tabora, wizara ilichukua hatua ikiwemo kutuma wakaguzi na taarifa imeshakabidhiwa polisi. Tususbiri hatua

Swali: Umeme Mpanda vijijini umekuwa mgumu kutekelezwa, lini mradi wa REA unatekelezwa kwani umesimama muda mrefu?
Jibu: Sijaridhika na miradi ya umeme vijijini, nimehakikishiwa pesa zimeshakwenda REA


UTAMBULISHO NA MATANGAZO

Asumpta Mshana:
Asante mheshimiwa mwenyekiti, napongeza wilaya ya Misenyi kwa kupata hati safi miaka mitano. Naanza na REA, katika kila lita moja, Tshs 50 inaenda REA, nawapongeza lakini kuna tatizo lipo siku hizi, hizi fedha zinashindwa kwenda REA na miradi mingi kushindikana. Kuna nguzo tu lakini watu hawafanyi kazi, baada ya ufuatiliaji imebainika fedha haziendi. Watu wanasubiri umeme, waziri akija atueleze lini atarejesha hizo fedha. Tatizo hili lipo kwenye barabara pia. Waziri atusaidie kuelewa hizo fedha zimeenda wapi na lini atazipeleka.

Pia kuna tatizo la matumizi mabaya ya fedha. Sababu kubwa ni sheria ya manunuzi, ni vyema ikaletwa bungeni na kuibadili kwani inatoa mwanya mkubwa sana wa matumizi mabaya ya fedha. Lini serikali italeta utaratibu mpya, katika maeneo mengi hii sheria ni kiini macho. Kuna watu wanalipwa mishahara hewa, inakuwaje malipo hewa. Kwanini tusiweke kipengele kwenye hati safi kuhusu mishahara hewa. Kama tunafanya sensa na inventories, kwanini tusifanye kwa wakurugenzi wana watu wangapi wanaofanya kazi. Yanatokea kwa sababu tumeamua kuweka kamlango kadogo ka kutokea. Njia ya kulipa moja kwa moja kutoka hazina imepunguza ama kuongeza.

Lema: Ghetto ni chumba kimoja ambacho wanakaa vijana wengi na mara nyingi hakina utaratibu maalumu, baada ya kupitia taarifa hizi, nchi yangu ni ghetto. Taarifa ya bajeti, nchi haina fedha mfano miradi ya maji ni asilimia 16 tu ndo pesa iliyotolewa. Serikali inayoshindwa hata kuchuma fedha kupitia huduma ya maji. Unashangaa unapoona ma-model wanaanza kufatilia kuwa rais wa nchi, kwenye uchukuzi serikali imetoa asilimia 17 pekee. Yametolewa mapendekezo ya vyanzo mbadala vya kupata fedha. General tyre inahitaji bilioni 20 iweze kufufuliwa, serikali inashindwa kufufua kiwanda kwa pesa ambazo wabunge huwa wanachangiwa humu ndani na bado ndoa zinaweza kushindikana. Mawaziri wanashinda Instagram, FB na mitandao ya JamiiForums na kupiga picha za kung'aa alafu wanafikiri wanaweza kuongoza nchi hii kwa sababu kwenye vikao vyenu mnajadili mambo ambayo hayana kina cha mawazo. Ukiweza kutengeza mkakati wa kibiashara, hata kiwanda cha general tyre kinaweza kisifikie mahitaji.

Serikali inakusanya bilioni 150 kwenye madini, ukienda Arusha hizi pesa wanazo vijana ambao wako mtaani, serikali ndio inakusanya sekta nzima. Leo waziri anaenda kutangaza utalii nje, anaenda na aunt Ezekiel. Hata kama nchi itakusanya trilioni mbili kwa mwezi lakini wizi usipoachwa nchi haiwezi kubadilika. Taarifa ya PAC, ATCL imefikaje hapa, pesa iliyotumika kukodi ndege miezi sita, nusu yake ingeweza kufufua kiwanda cha general tyre. Jengo la VIP Airport ungenipa bilioni mbili, ningerudisha chenji ya milioni 500, bilioni 9-12 zimetoka wapi. Ndo mana hata jana wakati Chikawe anashambuliwa. Leo jeshi la polisi Chagonja haamini kama rais ameshafanya uteuzi, wanafanya sabotage, hata hii kituo kuvamiwa na silaha kuibiwa. Halmashauri ya Arusha mjini wamejaa wajanja wajanja, mishahara hewa inaenda wapi.

Nyie mkitawala kwa wema, sisi lengo letu sio kushika dola. Lengo ni kuona maisha yetu yanabadilika. Nyie mkiharibu, mnaharibu Tanzania.

Kwa hali ilivyo sasa, kama Mungu anaendelea kushusha vitabu, angeongeza amri ya kumi na moja, usiwe CCM. Kwa hali hii mnaweza mkakuta siku moja mmeharibu hii nchi.

Bulaya: Nakushukuru mwenyekiti kwa kunipa nafasi, Nianze na kitu cha kwanza na Asumpta amekiongelea. Bunge linatunga sheria na kama viongozi tunapaswa kuonyesha mfano. Pesa hazitakiwa kutumika kwa matumize mengine kwa mujibu wa sheria, waziri umevunja sheria, hupaswi kupewa hata heshima ya kujiuzuru, unafukuzwa mahakamani.

Fedha zimewekwa kwa ajili kutatua matatizo ya watanzania wasitumie koroboi, mngechukua hata fedha za chai kuliko kuchua zilizozungushiwa uzio. Jana waziri anasema TPA wametumia bilioni 9 kulipana mishahara na safari bila idhini alafu jibu jepesi, eti walikua hawana ufahamu wa kisheria. Mifuko ya hifadhi ina hali mbaya, trilioni 1.8 serikali inadaiwa, alafu mnasema mtaunda kikosi kazi, tunafatilia na hiki kitakua cha kumi, sijui hivyo tisa havijajua serikali inadaiwa kiasi gani.

Jengo la VIP limejengwa kwa bilioni 12, warudishe bilioni 9. Kuna mishahara hewa, watu wanajituma kujikwamua basi hizo pesa zitengwe wapewe vijana na kina mama. Lazima wawe panyarodi, kila taarifa ni shida ya wizi. Tunaomba wezetu wabaneni hawa ambao ndio watendaji. Nakushukuru muheshimiwa mwenyekiti.

Mnyaa: Fedha ambayo haikupelekwa kijijini kama ilivyokusudiwa ya REA, sote tunakubaliana tozo hii ni kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini, kwa kuangalia taarifa, bilioni 180.7 zimekusanywa na zilizofika ni bilioni 144 na bilioni 36 hazikufika. Tukisimama hapa tunaambiwa tunalalamika mno, mafuta yote yanaagizwa in bulk, pesa yote inakusanywa hapa hapa, ndo maana Znz mafuta yanauzwa 2200 kama hapa yakiuzwa 2000. Znz wanalipia na hii ni dhuluma kwa sababu kule haziendi ilhali pia kule vijiji vipo. Tangu mwaka 2008 hajienda shilingi moja, kwanini tunatozwa sote na haki ya ZNZ haiendi. Mfumo wa serikali mbili haufai, bora serikali tatu. REA kuna 3% kwa watumiaji wote wa umeme na ZNZ yote inatumia umeme huku na inakatwa na ZNZ haipelekwi. Kwanini tusipate waziri wa fedha, naomba ulishughulikie.

ATCL, kamati ya PAC imebainisha tatizo ni mikataba mibovu. Tuliomba mikataba mikubwa kupitiwa, wachangiaji wote wanasema tunaibiwa. Bunge tuisaidie TAKUKURU wote waliohusika na hii mikataba wafikishwe mahakamani.

Christina: Nawapongeza wananchi na wapiga kura wa mkoa wa Singinda wanaounga mkono vyama vya upinzani katika serikali za mitaa, hakuna kulala mpaka kieleweke. Miradi karibu yote haikupelekewa fedha, serikali imesimama. TRA mpaka kufika Nov wamekusanya kwa asilimia 90 lakini kwenye matumizi haionekani kama hizi fedha zimeenda.

Shekifu: Napongeza wote waliohusika kutoa taarifa hizi, nimshukuru pia CAG. Tunayajua yote kwa sababu kuna ukaguzi, Uk wa 8 inaonekana kabisa kuna juhudi ya kuufahamisha umma ya kinachotokea.
 
Ze Comedy Originale !!! Long time niliacha kuangalia TV wakati napiga kazi ... KIbajaji, Nchambi, Asumpta, Kiroboto, Ngeleja, Wassira, Pinda, Ghasia et al ni zaidi ya Burudani kwa jinsi wanavyo ibemenda CCM ...
 
Mh. Lema akichangia hoja za kamati amesema kuwa Tanzania watu wanatafuna hela kiholela.Pia amewalipua mawaziri kuwa wanaenda kwenye vikao kupiga picha na kutwa wanashinda kwenye mitandao kama vile Jamiiforums, Facebook na Instagram wakifikiri kuwa Tanzania itapiga hatua bila kufanya bidii.Pia amemlipua Waziri wa Maliasili na utalii kuwa anashinda nje wakati wizara inafifia.
 
Hivi kwa nini kila anapochangia Lema anainama na kushikilia meza? Halafu haangalii mtu yeyote? Anaona aibu gani? Na kuinama kwake kunamkumbusha nini?
 
Lema aache siasa za kihuni kwani na i hajui kuwa wameshindwa kulishika jeshi la polisi sasa wanatafuta kutengeneza ufa ili wapate pakuingilia.
 
Nondo za Kamanda Lema Bungeni leo, "Kama Libya na Somalia wangekuwa wanatawala hapa na wakaviona hivi vitabu vilivyojaa mahesabu ya wizi, nyie viongozi wote mngekuwa kaburini!"
Ova
 
Uzi ukishaingiliwa na msalani, lizaboni na mchalo mtamu hata kama ulikuwa wa maana unapoieza hadhi yake, jamaa wamejitoa ufahamu hadi lumumba wanajuta kuwaajiri
 
Toka auze lile Trekta la wana Arusha nimegundua LEMA akili yake sio nzuri.
 
hivi TV na radio zingine
hawaruhusiwi kuonyesha
bunge zaidi ya TBC? (
 
Hakika. Wana Arusha wamechoka kuongozwa na jambazi

Jambazi mamayako............... mbona usiwaseme wezi wanaokwapua fedha zetu bila huruma?

Kikwete ameiharibu nchi hii imekuwa kama Gheto!
 
Back
Top Bottom