Yanayojiri baada ya MNYIKA (MB) kufika Polisi Singida!

[h=6]Nimefika Singida kuitikia mwito wa Polisi kutoa maelezo kuhusu mkutano nilioalikwa Iramba kwa nafasi yangu ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.

Nimekutana na RPC, amesema kwamba nisubiri mpaka saa 10:30 alasiri ndiyo nikutane nao kwa kuwa kwa sasa kuna kikosi cha upelelezi toka Dar Es Salaam kimekwenda eneo la tukio. Nimemuuliza RPC maswali mawili;

1. Wameniita kutoa maelezo kama mtuhumiwa au shahidi?
Amenijibu kuwa ni mahojiano ya kawaida.

2. Kwanini mpaka sasa watuhumiwa 12 waliofunguliwa jalada NDG/RB/190/2012 kwa kurusha mawe kwenye mwanzo wa mkutano wakati Bwana Waitara akitoa hotuba ya utangulizi huku polisi wakiachia hali hiyo. Baada ya kufungua jalada na polisi wa juu kupigiwa simu kuwa kuna njama kati ya Polisi na CCM hali ilitulia, Waitara akamaliza hotuba yake, Dkt Kitila akasalimia name nikahutubia kwa amani na kwenda kwenye mkutano mwingine. Mauaji yalitokea baadae mbali na tulipohutubia.

John John MNYIKA,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
18 Julai, 2012
[/h]
 
Njia ya mafanikio hainyooki hata siku zote lazima kona na speed hamps zinakuwepo, ila waTz tuko nyuma yake
 
hizi ni comments kwenye hiyo post ya mnyika huko facebook

-Sasa mwigulu ulimshindwa bungeni ukamfuata mpka jimbon kwake kufanya mauaji mkaenda na sera yenu ya Vua Uhai,Vaa sanda wana Iramba magharibi wanamkubali mbunge wao vilivyo hakuna kitila mkumbo wala nani

-subiri wacha papara watu wafanye kazi yao kama wewe unavyo fanya kazi zako akuna aliye juu ya sheria

-kwan wewe wasi wasi wako nini kama sio muhusika? Acha uoga mtoto wa kiume wewe.subiri sheria ifuate mkondo wake kupost fb hayo maele yako haitakusaidia
 
.acha wasi wasi mnyika tulizana chombo cha dola kifanye kazi yake syo kuja kulalama fb sawa....polis watalifikisha mahakamani nawe utalijibu huku syo fb..
 
utakoma mnyika,kiherehere chako,kilichokupeleka huko nini? ndo maana Mabumba alikueleza unawa....! eti hukuwepo.ptuuuu!
 
Pumba zenu wanasiasa-uchwara,
wewe kuhojiwa tu unalalama,
Je, aliyekufa?
Shirikiana Dola kubaini wahalifu.
 
MUNGU AWE NAWE, NA OLE WAO WADAI WE MTUHUMIWA PATACHMBIKA

nilikupigia kura, nililinda kura zako siku tatu, USIOGOPE WALA USIHOFIE SISI TUKO NYUMA YAKO
 
Sasa na wewe unawashwa nini hasa, umejoin juzi juzi tu inaelekea kwa sababu maalum maana uharo umezidi posts mia ktk thread hii !! Kama nawe umetumwa na akina Mwigulu, basi nenda wakajifaidishe vizuri.

Hukulazimishwa usome fb yake na ametoa taarifa tu !! Acheni hizo za kuleta, kama umezidiwa basi omba next mkutano wa uzazi wa mpango nawe upelekwe ukiandamana na naniii !!

Cameron anawafurahia sana...:alien:

utakoma mnyika,kiherehere chako,kilichokupeleka huko nini? ndo maana Mabumba alikueleza unawa....! eti hukuwepo.ptuuuu!
 
mnyika tupo nyuma yako nguvu ya umma,na mungu twakuombea usiku na mchana akulinde,likitokea baya juu yake nch haitakuwa ktk utawala bora.
 
Kuua aue Mwigulu halafu polisi wa ccm wanamkamata Mnyika!! Hii dhuluma ndio itakayoipelekea nchi hii kutotawalika; ccm acheni siasa za majitaka!!

Nchi inatawalika tena vizuri sana, na wahalifu wanashughulikiwa ipasavyo.
 
Pumba zenu wanasiasa-uchwara,
wewe kuhojiwa tu unalalama,
Je, aliyekufa?
Shirikiana Dola kubaini wahalifu.

Dola ipi wakati inasemekana polisi walikuwa pale mwanzo mwisho.
Na mnyika alikuwa mbele akihutubia.

Unataka kulidahalilisha jeshi la polisi kuwa ni dhaifu na lililala wakati wakuangalia usalama mkutanoni.
Hiji akilini. upuuuzi mtupu!
 
Back
Top Bottom