Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Lula wa Ndali Mwananzela
Toleo la 239 (RAIA MWEMA)
16 May 2012
KUNA msemo kwenye kitabu cha Mhubiri kuwa ‘hakuna kipya chini ya jua', kwamba lile ambalo linatokea limewahi kutokea na lile ambalo tunadhani ni jipya kumbe tayari ni la zamani.
Msemo huu kwa kweli huwa unataka kuwakumbusha watu kuwa waangalifu wanapoona mambo ambayo wanadhania ni mapya na wakayachangamkia, kumbe ni mambo yale yale.
Sasa hivi bila ya shaka yoyote hakuna chama kinachoonyesha kupendwa sana kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Watu wanapozungumzia siasa za Tanzania hawawezi kuzungumzia bila kugusia CHADEMA na baadhi ya vitendo ambavyo watu wameona vikifanywa dhidi ya viongozi wa CHADEMA na wanachama wake vimewafanya hata watu ambao walikuwa hawakipendi kuanza kukiangalia kwa huruma.
Lakini wapo ambao kwa kweli kabisa wanakipenda kutoka katika mioyo yao na wako tayari kufanya lolote ili kuona kinakubalika zaidi na hatimaye kinashika madaraka.
Nilikuwa nafikiria – kwa mara zaidi ya 1000 – juu ya wimbi la wanachama wa CCM ambao wamekuwa wakiamua kukikimbia chama hicho na kujiunga na CHADEMA kiasi cha kufanya waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kuwabembeleza vijana jimboni mwake kuwa wasikimbie kwani chama bado kinawajali. Wapo pia wengine ambao wanaweza kuwa wanaona jambo hilo hilo na sasa imebidi CCM iamue kujipanga vizuri zaidi kukabiliana na changamoto hizi.
Tunapoangalia CCM baada ya kikao chake cha Dodoma ni wazi kiko katika majaribio ya namna mbalimbali za kukabili changamoto hizo na wao wanaelewa hatari iliyopo mbele yao zaidi kwani kushuka kwao ni kupanda kwa CHADEMA.
Lakini tukiwa tumefunika vichwa vyetu kwa vilemba vya shangwe tunaweza kujikuta tunashindwa kuona hatari ambayo ipo na ambayo si ngeni, hatari ambayo tayari imewahi kuwapo humu humu Tanzania.
KUSOMA ZAIDI MFANANO WA AJABU KATI YA CDM NA TANU