Yanayofanywa na CHADEMA leo ni mapya au ni yale yale ya TANU?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,930
Lula wa Ndali Mwananzela

Toleo la 239 (RAIA MWEMA)

16 May 2012

KUNA msemo kwenye kitabu cha Mhubiri kuwa ‘hakuna kipya chini ya jua', kwamba lile ambalo linatokea limewahi kutokea na lile ambalo tunadhani ni jipya kumbe tayari ni la zamani.

Msemo huu kwa kweli huwa unataka kuwakumbusha watu kuwa waangalifu wanapoona mambo ambayo wanadhania ni mapya na wakayachangamkia, kumbe ni mambo yale yale.
Sasa hivi bila ya shaka yoyote hakuna chama kinachoonyesha kupendwa sana kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Watu wanapozungumzia siasa za Tanzania hawawezi kuzungumzia bila kugusia CHADEMA na baadhi ya vitendo ambavyo watu wameona vikifanywa dhidi ya viongozi wa CHADEMA na wanachama wake vimewafanya hata watu ambao walikuwa hawakipendi kuanza kukiangalia kwa huruma.
Lakini wapo ambao kwa kweli kabisa wanakipenda kutoka katika mioyo yao na wako tayari kufanya lolote ili kuona kinakubalika zaidi na hatimaye kinashika madaraka.


Nilikuwa nafikiria – kwa mara zaidi ya 1000 – juu ya wimbi la wanachama wa CCM ambao wamekuwa wakiamua kukikimbia chama hicho na kujiunga na CHADEMA kiasi cha kufanya waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kuwabembeleza vijana jimboni mwake kuwa wasikimbie kwani chama bado kinawajali. Wapo pia wengine ambao wanaweza kuwa wanaona jambo hilo hilo na sasa imebidi CCM iamue kujipanga vizuri zaidi kukabiliana na changamoto hizi.


Tunapoangalia CCM baada ya kikao chake cha Dodoma ni wazi kiko katika majaribio ya namna mbalimbali za kukabili changamoto hizo na wao wanaelewa hatari iliyopo mbele yao zaidi kwani kushuka kwao ni kupanda kwa CHADEMA.

Lakini tukiwa tumefunika vichwa vyetu kwa vilemba vya shangwe tunaweza kujikuta tunashindwa kuona hatari ambayo ipo na ambayo si ngeni, hatari ambayo tayari imewahi kuwapo humu humu Tanzania.

KUSOMA ZAIDI MFANANO WA AJABU KATI YA CDM NA TANU
 
Kwani TANU ilikuwa inakimbiliwa na wanachama kama CHADEMA? na hao wanachama walikuwa wanatoka wapi?

Au ni kutuchanganya? Hii habari ni haielewiki unaweza kuifafanua?
 
AHSANTE KAKA CHADEMA INASIMAMIA UKWELI AMBAO SI TANU TU ILIUSIMAMIA HATA MITUME NA MANABII WALISIMAMIA UKWELI NA HAPO NDIPO WALIPOPATA WAUMINI.
kwa maana nyingine unapopoteza ukweli na kubaki katika uongo unapotea na atakayeanza na ukweli atakuwa kazaliwa upya.
CCM SIKU ZOTE IMEKUWA IKISIMAMIA UONGO,WAKATI TULIPOKUWA TUNASOMA WALIKUWA WANAJENGA JENGO LA CHIMWAGA MCHORO WALICHUKUWA KOREA KAMA SI CHINA KILA WAKATI WALIKUWA WANAWEKA JENGO LA MCHORO HUO KATIKA GAZETI LA UHURU NA KILA SIKU TUKILIONA TULIKUWA TUNAHASIKA KUCHANGIA KLUMBE TULIKUWA TUNACHANGIA MATUMBO YAO.
SASA HIVI KILA WANACHOZUNGUMZA CHADEMA KINAONEKANA KAMA KIPYA KWA SABABU BLANKETI WALILOKUWA WAMETUWEKEA USONI LIMESHATOKA.
 
Ni sawa na kipindi cha TANU,Lula kanena

Historia hii inatakiwa kuisaidia CHADEMA kusahihisha makosa ambayo CCM walifanya na wanaendelea kufanya
 
ukweli ni kwamba CDM ni chama ambacho kimeonesha kuwa kipo kwaajili yakukomboa tabaka watu ambao wametupwa na kusahauliwa na ccm na ndo maana inadhidi kupata wafuasi kutokana na kuwajali walalaho
 
Ni nakala mzuri sana. Tena Lula ametoa somo zuri hata kwa tabia iliyojengeka JF ya wafurukutwa wa CDM hawapendi chama kukosolewa, kupingwa etc. Ninanukuu.
"Ninachosema kwa ufupi ni kuwa tunaposhabikia CHADEMA sasa hivi na CHADEMA wanapojiona wanapendwa na kukubaliwa zaidi wasije kujidanganya hata kidogo kuwa wanastahili zaidi na kuwa basi asiulizwe, wasikosolewe, wasipingwe na hata kukataliwa".
 
If it ain't broke, don't fix it!

It worked for TANU and it may well work for CDM after all the country needs to revive some of the founding principles. i.e nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko, nitaitumikia nchi yangu kwa moyo wangu wote, binadamu wote ni sawa etc.
 
Kwani TANU ilikuwa inakimbiliwa na wanachama kama CHADEMA? na hao wanachama walikuwa wanatoka wapi?

Kwani unafikiria kulikuwa na chama kimoja tu cha siasa katika Tanganyika? na unafikiri wote wanaokimbilia CDM leo wote ni wanachama wa vyama vingine?
 
Peopleeez Power, si mchezo chadema tumaini letu jipya.EHEE MAULANA ENDELEA KUWAPA MARADHI YA MPASUKO HAWA WEZI WA HAKI YA WTZ sisiem wafe kabisa.
 
TANU ilikuwa inapigania uhuru kutoka kwa wazungu wakati CHADEMA inataka kuwakomboa WATZ kutoka ukoloni wa CCM katika kizazi ambacho kiko well informed kuliko kile cha enzi ya TANU
 
Chadema is larger than LIFE itself. Tanu is history Chadema is the future of this country!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom