Hakuna yamini ya damu kati ya mtu na mpenzi wake, mara nyingi yamini inafanyika kati ya mtu na rafiki yake walioshibana sana ili kuwafanya wawe ndugu wa damu, ndo maana wanachanjia yamini ya damu, sasa itakuwaje ule yamini ya damu na mpenzi wako, si mtakuwa tayari ndugu wa damu ? Sasa mtaoanaje tena mmeshakuwa ndugu wa damu ? Waliokula yamini ya damu hawaoani tena kwani hao tayari ni ndugu wa damu, na yamini ya damu huwa haivunjwi.