Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,264
Aliwahi kusema aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CHADEMA-2005 Ndugu Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA katika mikutano ya kampeni za kuwania urais kipindi hicho. Sina nukuu sahihi bali alisema kuwa, anahitajika 'kichaa' mmoja ambaye atawasha njiti kwenye hizi nyasi kavu (hali tete ya kiujumla ya bongo), na wale wanaoishi Mbezi na Masaki wataungana na wenzao wa ubungo kuelekea kwenye makambi huko Kibaha. Hiyo ni lugha ya fumbo tu ila hali kwa sasa inajionyesha. Mengi kachokonoa na 'mapapa' wanaanza kusikia joto la kikaangio. Waanza kubwabwaja. Hii itaenda hadi kauli ya hayati Nyerere itakapotimia. Kwamba, ili upinzani wa dhati utokee ni lazima CCM igawanyike. Tunasubiri kushuhudia mengi katika kipindi hiki cha uongozi wa aina yake