Yamenikuta mwenzenu naombeni ushauri

Yamenikuta mwenzenu naombeni ushauri

mwajei

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
129
Reaction score
38
Habari za leo wana JF.

Mimi ni mama wa mtoto mmoja, nimeajiriwa.

Tatizo ambalo ninalo ni kuhusu mpangaji mwanzangu (ke) kaambiwa natoka kimapenzi na hawara yake lakini ukweli huyo hawara yake hata salamu hatusalimiani, sasa ananikosesha raha na maneno maneno yako. Nimeshindwa kuvumilia nikamwambia mwenye nyumba amwite na amwite na aliyemwambia kaniona mimi na hawara yake lakini amekuwa mkali kama pili pili anasisitiza ni kweli na huyo mwanaume anakujaga kwangu. Note: Naishi na wadogo zangu wakiume 2 na vyumba ni viwili.

Sasa nimeshindwa kumwelewa anataka nini au nimweleze vipi anielewe maana mi si mtu wa maneno na ni short temper nahisi akiendelea kuniletea mdomo nitakuwa na keshi ya kujibu.

Hekima zenu zinahitajika.

Ahsanteni.
Mama S.
 
Pole sana hiyo nifitna kubwa mungu akuepushe nahizo balaa dada yangu Ila usikae kimya tafuta suluhu haraka iwezekanavo
 
maneno yangekuwa yanaua basi marehemu tungekuwa wengi. kama ukweli unao kwamba hufanyi hivyo na umemwambia ila haelewi sioni haja ya kusumbua akili yako tena.
fanya yako, muda wa kumsikiliza mpuuzi usiupate.
 
Mlipoti mapema kunakohusika kama akiendelea maana huo ni udhalilishaji
 
Pole mkuu...nenda katoe taarifa polisi kbs uwe na RB itakusaidia siku hayo maneno yakivuka mipaka

Pili,kodi ikiisha hama hapo maana kukishakuwa na mifarakano na mpangaji amani inapotea hata mtt atakosa raha.
 
Mh, pole hayo yalishawahi kunikuta, tena bora wewe maneno matupu mimi nilishikiwa hadi kisu. Ila mwisho wa siku yule dada alinipigia magoti na kuniomba msamaha.
We mnyamazie, zizuie hasira zako maana kukaa kimya ni jibu la mjinga ila ukiona hakomi mchukue kweli huyo bwana ake lolz.
 
just achana nae huyo hana akili ... as long as maneno hayang'ati usijali do your life tu ndo jmbo la msingi..
 
Am telling you, kitu inaitwa wanawake nawekaga mbali mnooo.

Wengine ni limbukeni hawaaaa.
 
Ahsanteni kwa ushauri. Nitaufanyia kazi.

Mbekeche: Sina tabia ya kubadili wanaume najiheshimu sana na naheshimu familia yangu siwezi waonyesha wadogo zangu picha mbaya ila kinachomchanganya anaona maisha yangu tofauti na yake. Mi nafanya kazi ila yeye sijui anajishughulisha na nini pia kipindi cha nyuma tulikuwa tunasalimiana vzr akawa ananiambia tutoke twende Disco nikawa namkatalia. Sa sijui alichofikiria.

Pili huyo mwanaume ni mume wa Mtu alikuwa mpangaji hapo hapo nilipo sa sijui kwa vile ye kamchukulia mwenzake anadhani na mm nitamchukua.
 
Habari za leo wana JF.

Mimi ni mama wa mtoto mmoja, nimeajiriwa.

Tatizo ambalo ninalo ni kuhusu mpangaji mwanzangu (ke) kaambiwa natoka kimapenzi na hawara yake lakini ukweli huyo hawara yake hata salamu hatusalimiani, sasa ananikosesha raha na maneno maneno yako. Nimeshindwa kuvumilia nikamwambia mwenye nyumba amwite na amwite na aliyemwambia kaniona mimi na hawara yake lakini amekuwa mkali kama pili pili anasisitiza ni kweli na huyo mwanaume anakujaga kwangu. Note: Naishi na wadogo zangu wakiume 2 na vyumba ni viwili.

Sasa nimeshindwa kumwelewa anataka nini au nimweleze vipi anielewe maana mi si mtu wa maneno na ni short temper nahisi akiendelea kuniletea mdomo nitakuwa na keshi ya kujibu.

Hekima zenu zinahitajika.

Ahsanteni.
Mama S.

Acha kumsikiliza ni kumpuuzia tu
 
pole sana jamani ni bora ukae kimya tu mwache Mungu akutetee kwa hayo makusudi anayokusingizia kwani huyo analo litafuta kwako na anataka kugomvi au maneno wewe nyamaza ikishindikana nenda kwa mwenyekti au mjumbe wa serikali za mitaa ukamweleze hicho kisa chote uenda akaitwa na kujirekebishia hapo. ANA MATATIZO kuwa nae makini
 
Pole sana mkuu..
Busara ni kumpuuza tu, wewe endelea na mambo yako acha kusikiliza maneno yake. Ukikaa kimya kila mtu atajua huyo jirani anamatatizo. Usikuze hayo mambo ni yakawaida sana kwenye nyumba za kupanga hasa kukiwa na wanawake wengi.
 
hilo ndo likusumbue akili?
mwambie akuondolee ujinga wake
asikuchoshe

anawehuka kwa ajili ya hawara? angekua mume si angefunga mtaa
 
kama ana maneno mengi sana yasiyo na maana kamripoti serikali ya mtaa au kwa mjumbe wa nyumba kumi hao ndio wahusika wa matatizo ya wapangaji...!
 
just achana nae huyo hana akili ... as long as maneno hayang'ati usijali do your life tu ndo jmbo la msingi..

.we miss chagga. wewe!!! maneno hayang'ati eeh?..kumbuka Mungu aliumba mbingu na nchi kwa neno, na nakuhakikishia ukiambiwa maneno mabayaaaa/mabovuuuuu tena kutoka kwa mtu wa karibu waweza tamani dunia ipasuke na kukumeza, huyu mpangaji dawa ni apelekwe vyombo husika vinginevyo mwajei atakuwa na kesi ya kujibu siku si nyingi.
 
wakati mwingine usimpomfatilia mtu inamuuma, jaribu kumpuuza
 
Back
Top Bottom