Yamenikuta: Mchumba wangu amezaa angali bikra

Yamenikuta: Mchumba wangu amezaa angali bikra

Mmhhh, wamekuingizia wajanja. Ni bora angekuwa na imani kwa Mungu wa Mbinguni, lakini ana imani ya dini tuu, sijui. Ni dini gani hiyo....mizimu ama???

Mi nadhani huyo anaamini Mungu wa wanyoni! hukoo Kenya sio bure
 
Wanajamvi habari zenu. Mimi nina mchumba wangu ambaye ni mkristo mwenye imani sana na dini yake. Mtaratibu, mpole, na ana heshima sana. Katika mahusiano yetu hatujawahi kufanya mapenzi mpaka tutakapofunga harusi na pia ni bikra. Nilipata safari kwa mda nimerudi nimemkuta amejifungua mtoto wa kiume. Nimeshangaa namuuliza kulikoni, anadai mimba hiyo alipewa na malaika.

Nimemwamini ila nikamuambia kama ndivyo basi huyu mtoto atakuwa nabii hivyo amsimamishe ili atembee juu ya maji kama Yesu, akaniambia amefunuliwa ndotoni kuwa mtoto huyo ataanza kufanya maajabu atakapofikisha miaka mitano.

Hapa nimeanza kupata shaka naombeni ushauri!

Huyo atakuwa bikira maria, unaweza kuta ndio ujio wa yesu ohooooo
 
Hee, hongera sana, mtoto wa pili atakuwa mungu mweusi kama yule wa Kenya bila shaka
 
Wapelekee bongo movie waichezee filamu!!
 
Yesu ndo amerudi nn!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
hii hadithi bana haifurahishi, haifundishi, wala haichekeshi hongera kwa kujipa nafasi ya mt. Yoseph baba mlishi wa YESU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom