Yamenikuta...Mahindi yanaharibika shambani

Ty_Vigilante

JF-Expert Member
Jan 19, 2015
2,545
2,000
Tafadhali kwa wale wanaojua magonjwa ya mimea hasahasa mahindi,
(i)Naomba mnijuze huu ni ugonjwa gani kwenye hili hindi?
(ii) Nawezaje kujikinga ntakapopanda mahindi tena msimu ujao.
Naomba ushauri ili nsije nkapata hasara kama mkulima.
 
CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,667
2,000
Ugonjwa huo unaitwa "Common Smut" na unasababishwa na fungus aitwaye Ustilago maydis .
Huyu fungus anaishi kwenye udongo na anaweza kukaa kwenye udongo kwa miaka mingi.
Huwa anaingia kwenye mmea wa mahindi kupitia vidonda na mbegu zake hukua na kuwa mmea kamili. Huyu fungus hula sehemu za chembe za uhai (cells) za mmea na kuziua. Anashambulia sehemu yoyote ya mmea ikiwa ni shina, majani, masuke, na gunzi. Hutengeneza vinundu fulani ambavyo ukivipasua vinatoa unga mweusi. Unga huo punje zake ndio mbegu za Ustilago maydis.
Ugonjwa huu huenea kwa kusambazwa mbegu zake na upepo,maji,wanyama,nk.
KUDHIBITI COMMON SMUT
Ugonjwa huu wa common smut hauna dawa kwa hiyo njia ya kuudhibiti usitokee au usishambulie kwa kiwango kikubwa ni kama ifutavyo:
1.Tumia mbolea yenye uwiano mzuri wa nitrogen na phosphorus. Udongo wenye nitrogen nyingi hufanya mimea kuwa laini na kukua haraka. Mimea hii hushambuliwa kwa urahisi na ugonjwa huu. Lakini phosphorus ya kutosha huzuia mashambulizi kwa kuwa hufanya mmea kuwa imara na.mgumu. Epuka kutumia samadi nyingi.
2. Epuka kujeruhi mimea. Mimea yenye vidonda hushambuliwa kwa urahisi zaidi.
3.Dhibiti wadudu waharibifu. Wadudu hutoboa mmea na kuujeruhi kwa hiyo hufanya mmea ushambuliwe kwa urahisi.
4. Hali ya ukame hufanya mashambulizi kuongezeka kwa hiyo kama inawezekana epuka kipindi cha ukame kulima mahindi kama hutaweza kumwagilia maji.
5. Acha kupanda mahindi kwenye eneo lenye historia ya kutokeza ugonjwa huu mara kwa mara. Panda mazao mengine
6.Kulima kwa kugeuza udongo ili ule wa juu ufukiwe chini sana kunaweza kupunguza tatizo kwa huwa.huyu fungus huishi kwenye udongo wa juu.
7.Muhimu zaidi: Tumia mbegu zenye kustahimili ugonjwa hasa hybrids.
Ugonjwa wa comon smut hauna dawa ukishaingia shambani lakini hasara unayosababisha haizidi 5%. Ukizingatia njia hizo za kuzuia unaweza ukautokomeza shamnani mwako.
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
5,244
2,000
Tafadhali kwa wale wanaojua magonjwa ya mimea hasahasa mahindi,
(i)Naomba mnijuze huu ni ugonjwa gani kwenye hili hindi?
(ii) Nawezaje kujikinga ntakapopanda mahindi tena msimu ujao.
Naomba ushauri ili nsije nkapata hasara kama mkulima.
Kuna mdau hapo juu ameeleza vizuri kabisa kwamba hii ni "Head smut" ambao ni ugonjwa wa kuvu! Siku nyingine usitumie mbegu za kuokoteza maana ugonjwa huu unadhibitiwa kwa kuchanganya mbegu na fungicides. Inawezekana ulitumia mbegu ambazo tayari zilikuwa zimeathirika, hasa zinazouzwa na hawa wagawa pembejeo za voucher asilimia kubwa yao siyo waaminifu kabisa, huwa wanachakachua mbegu! Hivyo tumia mbegu zinazosambazwa na watu wa kuaminika. Pita kwenye shamba haraka ng'oa miche yote inayoonesha kuathirika na ukaichome mbali na shamba. Huwezi kupata hasara kubwa ya kukuumiza.
 
Asante sana Mkuu
 
Asante sana Mkuu, nmeupata huo ushauri na ntaufanyia kazi
 
y-n

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
1,995
2,000
Upo wapi?
Kama ruangwa,dodoma,maeneo kadhaa ya singida-manyoni,peramiho,nk acha tu yakukute.
 
Stanley Mitchell

JF-Expert Member
Jan 2, 2014
4,602
2,000
Tafadhali kwa wale wanaojua magonjwa ya mimea hasahasa mahindi,
(i)Naomba mnijuze huu ni ugonjwa gani kwenye hili hindi?
(ii) Nawezaje kujikinga ntakapopanda mahindi tena msimu ujao.
Naomba ushauri ili nsije nkapata hasara kama mkulima.
So hapo ndo Kisutu sio?
Yet you want to compete with me....
See nilivoattack yo fuckin credibilty??

Imagine umeingia kwenye 18 zangu nakucross...hakuna rangi utaacha kuona mpaka ule hao VIWAVI JESHI VAMIZI waliovamia ilo shamba.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom