Yamenifika kooni, nimeshindwa kulea kiburi chake

Yamenifika kooni, nimeshindwa kulea kiburi chake

mi naona mambo yafuatayo yanawezekana kuwa chanzo cha ugomvi:

1. Ulimkuta msichana akiwa na ujauzito wa miezi mitatu. Alikuwa ametelekezwa tu lakini huenda bado alikuwa anampenda mwenzie kwa hiyo ulitumika kama kipoozeo kwa hiyo msichana alikubali kuwa na wewe kwa sababu ulimfungulia mlango kama ulaya wanavyofungua milango kwa wakimbizi wa syria.

2. Inawezekana kweli alikupenda kama wewe ulivyompenda na mkiweza kujishusha mkasikilizana mnaweza kudumu.

3. kuna dalili kuwa wewe ni control freak. Kitendo cha kufatilia simu zake na kumtaka achome nguo, kutaka mzazi mwenzie akupigie wewe, kinaonyesha una kiwango cha juu cha wivu kwa hiyo huyo dada ana-suffocate. Hata asingekuwa na mtoto lakini alishakuwa na mahusiano kabla yako au ukahisi kuna mtu anammendea ungefanya hivi hivi. Punguza wivu ili uweze kukaribisha hekima kutatua hili swala.

4. unaona kama kuwa na uhusiano na huyo dada akiwa na mtoto umemsaidia sana na unataka alipe fadhila kwa kutii matakwa yako yanayoonekana ya kibabe. kwa upande wa msichana haoni kama umemsaidia. anaona umemchagua kwa vigezo vyako ambavyo hata angekuwa bila mtoto ungemchagua, na kwa mtazamo wangu yuko sahihi.

6. umesema unatilia mashaka mapenzi yake kwako kwa sababu ulipendekeza mzae mtoto wenu akakataa, akakwambia ukajitambulishe na kupeleka mahari, vinginevyo hatazaa. Ukazidi kumchokonoa na kumuuliza kama anakuruhusu ukazae na mtu mwingine akakwambia nenda, na kwa jinsi ulivyogubikwa na hisia hasi ukaona kuwa alimaanisha. Ni hivi, kosa moja halifanyi la pili kuwa sawa. Msichana keshazaa na kutelekezwa, ameshajua athari za kuzaa bila utaratibu na makubaliano. Atakuwa na akili ya kuku kama atakubali kurudia kosa lile lile ili kukulipa fadhila kwa "kumuokoa" kwenye janga la kwanza. Hata kama ulimkuta na mtoto bado ana haki ya kuchagua. Amekosea nini kukwambia kama unataka mzae uhalalishe ndoa. Unafikiri hivyo mnavyoishi kinyumba kunampa usalama wa kutosha? Na wee uvaage viatu vya mwenzio, usikimbilie tu kusema hakupendi.

7. ulikosea kuwasiliana na x wa mpenzi wako wakati bado mko kwenye "sintofahamu", tena unamwambia akitaka kujua kuhusu mtoto awasiliane na wewe. hata mimi ningekuwa huyo mwanaume ningekuuliza "kwani nimezaa na wewe?!!". Swala la mawasiliano ya mwenzio na x wake mngelijadili wewe na mwenzio mpaka mfikie muafaka kisha umuachie yeye jukumu la utekelezaji. Mwenzio akishindwa kutekeleza makubaliano ndo uchukue hatua mlizokubaliana - kama ni kuachana au nini mtajua wenyewe. Kutumiatumia nguvu kila mahali si sawa. ndo hivyo unaishia kutukanwa halafu unaona umeonewa.

8. kama unajisikia kumuacha huyo dada we muache ila kama hamtajifunza namna nzuri za kutatua migogoro hata ukioa bikra matatizo yatakuja. Hakuna mahusiano yasiyo na vimbwanga. huyo mtoto unayemfikiria sana muachie tu, fate itamuamulia vingine kama ilivyomleta kwako. kama unampenda sana unaweza kuendelea kumsaidia akiwa hukooo na mama yake. ila nahisi kuna kitu usichokijua kinachokusukuma kuwa kwenye hali uliyopo. hebu kumbuka kumbuka experience za utoto wako.

*****Mahusiano yote yawe yanahusisha watoto, wenzi wa zamani, wenye watoto, wasio na watoto, wanadoa na wasio wanandoa yanaweza kuyumba na kukufa kabisa endapo misingi ya mahusiano itakuwa lege lege. Misingi hiyo ni kama: ukweli na uwazi, uaminifu, kuaminiana, kuheshimiana, kujuana madhaifu, utayari wa kudumisha mahusiano, mawasiliano bora n.k. Hata kama upendo utakuwa umekufa kama mambo ya msingi yapo mahusiano yanadumu.
 
Best kwanza pole sana.......mahusiano na wanawake wa namna hiyo ni changamoto......kwanza huyobi dada inaonyesha hajitambui hata kidogo........hapo ni unatumika anaishi na wewe kama msamaria mwema........hivyo hisia za mapenzi ya ndoa hazipo kwako. Si kila msichana anayetelekezwa na mwanaume ni anaonewa wengine ni wanastahili hayo mateso maana MUNGU alishawaona viburi vyao hata kabla havijaanza .......hivyo anawapa adhabu ya kusota shenzi type.........huyo msichana ----- hahitaji mtu mwenye roho ya huruma kama wewe ambaye hata kumuacha unaomba ridhaa yake bila kuamua kibinafsi pekee yako.........ila fuata ushauri wangu.......acha huyo mwanamke .......shinda hisia za moyo zinazotaka kuongoza maamuzi yako fuata hekima ya kiume.......huyo X-man wake anajua kuwa anaweza kuwa ana emotional advantage juu ya hilo janamke ----- tena ----........na ukikaa vibaya siku atakuumiza hisia marambili hata utatamani jiua........anaweza fanya yafuatayo......1.Kuanza tena kufanya ngono kwa siri na huyo bazazi wake..2.Ataweza kukugeuka siku huyo jamaa akija na gia ya kutaka kuirudia familia yake ailee.....amini siku hiyo utalia kama mtoto mdogo na huyo demu ---- hatafikiria mara mbili kukukana na kukuacha na kukimbilia kwa huyo ---- mwenzake3.Jiandae kumuona anamimba nyingine ya jamaa huyo huyo..........
So why don't you be a man and dump her before she dumps you........dalili ya mvua ni mawingu .....usisubiri kulowa ndio ujiaminishe kuwa mvua itanyesha........fanya maamuzi magumu mapema.....usisubiri hadi upatwe na majanga na huku ishara zinakupigia kelele sasa..........shetani sio hadi anapenda kujificha kwenye vitu vizuri ili atushambulie nafsi zetu kwa urahisi ili atufanye watu wabaya kama na tufananie na roho yake......hapo anataka akupandikize roho ya chuki ili usiwena imani tena na mahusiano....usijali tena mwanamke hata kama atakuja mwenye roho nzuri......anataka uje kuwa wakala wake wa kushawishi binadamu wengine wasiwe na moyo wa huruma wa kuwapokea wanawake waliotendwa na wanaume mabazazi.........
Piga moyo konde.......mpe kisogo huyo msaliti wa wajane wenzake.......songa mbele yupo anayekusubiria ambaye anakiu ya huruma yako ambaye anaka apate hifadhi yako na malazi yako(sio maradhi maana kuna mabwege wanajifanya wanajua kiswahili watajimix hapa), mwanaume hupenda kweli baada ya kukosea mara kadhaa......hii ni miongoni mwa mwara kadhaa.....songa mbele hadi moyo utakapo komaa na kufahamu namna ya kujua ni wapi pa kupenda.......

ONDOKA........MUACHE......HAKUHUSU........HANA HADHI YA KUWANA WEWE.....HUYO NI SADAKA YA WANAUME MABAZAZI ILI ATUMIKE KAMA MFANO......NI NG'OMBE WA SADAKA..........KATAFUTE MWANAMKE MSTAARABU ACHANA NA HUYO KIZAZI CHA NYOKA .......THAT BITCH.......WALK AWAY.

Mabwaku! so much rage! Ni nani huyo jamani? Let it go.
 
mi naona mambo yafuatayo yanawezekana kuwa chanzo cha ugomvi:

3. kuna dalili kuwa wewe ni control freak. Kitendo cha kufatilia simu zake na kumtaka achome nguo, kutaka mzazi mwenzie akupigie wewe, kinaonyesha una kiwango cha juu cha wivu kwa hiyo huyo dada ana-suffocate. Hata asingekuwa na mtoto lakini alishakuwa na mahusiano kabla yako au ukahisi kuna mtu anammendea ungefanya hivi hivi. Punguza wivu ili uweze kukaribisha hekima kutatua hili swala.

4. unaona kama kuwa na uhusiano na huyo dada akiwa na mtoto umemsaidia sana na unataka alipe fadhila kwa kutii matakwa yako yanayoonekana ya kibabe. kwa upande wa msichana haoni kama umemsaidia. anaona umemchagua kwa vigezo vyako ambavyo hata angekuwa bila mtoto ungemchagua, na kwa mtazamo wangu yuko sahihi.

7. ulikosea kuwasiliana na x wa mpenzi wako wakati bado mko kwenye "sintofahamu", tena unamwambia akitaka kujua kuhusu mtoto awasiliane na wewe. hata mimi ningekuwa huyo mwanaume ningekuuliza "kwani nimezaa na wewe?!!". Swala la mawasiliano ya mwenzio na x wake mngelijadili wewe na mwenzio mpaka mfikie muafaka kisha umuachie yeye jukumu la utekelezaji. Mwenzio akishindwa kutekeleza makubaliano ndo uchukue hatua mlizokubaliana - kama ni kuachana au nini mtajua wenyewe. Kutumiatumia nguvu kila mahali si sawa. ndo hivyo unaishia kutukanwa halafu unaona umeonewa.

*****Mahusiano yote yawe yanahusisha watoto, wenzi wa zamani, wenye watoto, wasio na watoto, wanadoa na wasio wanandoa yanaweza kuyumba na kukufa kabisa endapo misingi ya mahusiano itakuwa lege lege. Misingi hiyo ni kama: ukweli na uwazi, uaminifu, kuaminiana, kuheshimiana, kujuana madhaifu, utayari wa kudumisha mahusiano, mawasiliano bora n.k. Hata kama upendo utakuwa umekufa kama mambo ya msingi yapo mahusiano yanadumu.

mkuu ktk namba 3 mambo ni hv, nilibd nmipigie huyo X wake simu baada ya huyu mama kukataa kubadili laini yake ya simu. Mie sifuatiliagi simu yake ila kama kuhusu swala la kupigiwa simu ni kwamba yy ndio alinijuza na kusema anakereka nazo. Nikamwambia badili namba tukae kwa aman akawa mbishi kwamba kubadili namba ni kumwogopa huyo X ikabd mie sasa ndio nmtafte huyo X nijue shida yake nn hasa kukaa anapiga simu kama hana msaada wowote.

ktk namba 4 naomba nikwambie katika kila jambo nalomwambia huyu mwanamke huwa nampa na yeye nafasi ya maamuzi yake. Sijawahi mfosi kufanya kitu na hili nadhan ndio limeleta na haya mengine maana naona akaanza kuona kuwa si kawaida tuu nasemaga hafu sichukui hatua.

ktk namba 7 ntarudia nililosema ktk namba 3 yako. Nlipomtafta huyo X ni ilikuwa nmwambie kama hana plans na aliowatelekeza basi asikae kubugudhi watu. Ndio kuanza matusi kwamba atafanya analojisikia yy nisimpangie, nia yangu ni ilikuwa kwamba kama hana shida na mama mtoto na anataka kujua tuu hali ya mtoto basi afanye kupitia kwangu mie ili nijue kama namuasili mwanae au laa.

mkuu its a long story ila naloweza kusema ni kwamba kiburi cha huyu mtu ndio kimeleta hayo unayohisi ww kwamba mie ni control freak na mbabe. Nmepitia mahusiano mengi ila hapa nmejikuta nakuwa mtu ambaye sikutegemea mana nakaa nae huku inakuwa ni kama nashindana na yy pamoja na her past. Nacompete na vivuli, na nikimwambia yy ndio kwanza anakuwa don't care.
 
mkuu naona kama unalazimisha vitu ambavyo haviwezikuwa poa...siusepe tuu na yako...au unatak ubamizwe sanauanze kusema wanawake hawafai....we ujui kusoma alama za nyakati aisee
 
Ninachokiona ni kuwa unajaribu kulazimisha usiku kuwa mchana.....kuna mambo katika maisha hayawezekani mojawapo nikujaribu kwa namna yeyote kutenganisha damu ya mtu....
 
Siamini kama anakutegemea kwa kila kitu,kama ni hivyo asingekuwa na kiburi hivyo ili hali akijua unamtunzia mtoto wake.Wanawake wengine matapeli yawezekana hela ya baba mtoto anaichukua na kukudanaganya wewe ili aendelee kuwakwangua wote kama vocha.Kma malalamiko yako ni ya kweli (kesi ya upande mmoja) na haujafunga nae ndoa mpe masharti yako akiyashindwa achana nae akahangaike na dunia,ya nini kujiweka kwenye msongo wa mawazo wakati maisha yenyewe mafupi? Mapenzi sio adhabu kama hataki kuimba wimbo mmoja na wewe akajiunge na kwaya ngingine ili wewe uwe huru utafute wa kuimba nae wimbo mmoja.
 
Majuzi kwenye mkutano wa mwakasege pale viwanja vya udsm,aliita wadada ambao hawajaolewa na wanataka wachumba wakaombewe,duh walienda wengi balaaaa

Katika ilo suala lako mkuu,ni bora tu ukajiongeza,kama ni kumsaidia umemsaidia hata mungu kakuona

PACK AND GO BRO.........
 
Wasalaam,

Nitaenda katika mada moja kwa moja. Nimekuwa katika mahusiano na single mum kwa takribani mwaka na miezi sasa ila baada ya kumaliza nae nusu mwaka nimejikuta napitia mabidiliko makubwa ya kihisia na fikra. Mama huyu nilimkuta na mtoto mdogo wa miezi saba na alikuwa katelekezwa akiwa na ujauzito wa miezi mitatu.

Nilipomtongoza nlihoji majina ya ubini wa mtoto kama ni ya koo ya mama au baba, mawasiliano yake na mzazi mwenzake na kama mie ntalazimika kutoa huduma zote za mtoto. Akasema mtoto anatumia ubini wa koo ya mama, hana mawasiliano yeyote na mzazi mwenzake mana alipotelekezwa huyo mpenzi wake wa zamani alipotea kabisa na kuhusu mtoto sitolazimika kuhudumia asilimia zote.

Tulianza vizuri na huyu mama na aliweza kunifanya nimpende dhati hadi kufikia hatua ya kusema nitashikamana nae daima. Matatizo yalianza kuja baada ya kujua kuwa alinidanganya mengi mwanzoni, mtoto amebatizwa tayari na kadi la kliniki na uzazi mtoto ana jina la baba ake, mbaya zaidi mama huyu namhoji kwa nini aliniongopea ananjibu kuwa alisema vile kwa kuropoka tu ila atabadili jina na kuandikisha lake.

Tumevutana katika hili hadi akafikia kuniambia mie nimemkuta mtoto hvo nisimpelekeshe maana haoni tatzo mtoto kutumia jina la baba ake. Baba wa mtoto alikuwa anapigaga simu kuulizia hali ya mtoto, ila hachangii hata mia katika mahitaji ya mtoto. Nilimwambia huyu mama hali hio siipendi na abadili laini ya simu ili kusiwe na mawasiliano kati yao mana hata huyo mpenzi wako wazamani namba anayopigia ukiipiga baada ya yeye kukata simu huwa imefungiwa.

Mama huyu kubadili laini alikataa hata nilipomwambia tutaachana katika hili nikiona bado mpenzi wangu anampigia simu ambazo hazna msaada katika maisha yake wala ya mtoto ( huyu mpenzi wa niliwahi mpigia ili niongee nae kiutu uzima kwamba aniambie plan zake kwa mtoto tusaidiane ili abaki na haki zake kwa mtoto ila niliambulia matusi ya nguoni na mama huyu alishuhudia kila kitu mana nilitaka ajue malengo ya mwenzake tuwekeane makubaliano ili kuepuka mie kukaa na hasira kila nikijua wanawasiliana), mwezi baadae ikatokea akapigiwa na huyo nami nipo nyumbani.

Nikamwambia nimeshindwa mie kulea kiburi chake hivyo natamani tuachane tuu kama hali ni hii ndio akabadili laini. Jingine ni mama huyu tumevutana kuhusu mimi kutotaka kuona kitu chochote ambacho alipewa katika mahusiano yake ya zamani ila amekuwa na kiburi katika kuvigawa kwa nduguze ili tukae kwa amani mie nisiiwazie past yake nikiona vitu vya past na kuumia.

Vitu vyenyewe ni nguo hasa hasa na amekomaa kwamba kama sipendi nichome moto begi zima ila yeye hagawi nguo zake. Nimekwazika sana kuona najitoa kumhudumia yeye na mtoto ila hawezi kujali hisia zangu. Nimefikia hatua nimekuwa na uchungu sana ndani yangu na kna mda najikuta na mawazo mengi kama nikae nae au niachane nae nisije nikachukia kila mwanamke kwa sababu yake. Nalileta hili kwa wana MMU mnisaidie mawazo na ushauri, nimeyaweka yale nayoona ni makubwa kwangu ila kna mengi yameendelea hadi mie kufikia hatua ya kutaka kufanya maamuzi magumu.

Mwanamke huyu siwezi nikamwambia kitu ambacho kinaniumiza akafanyia kazi hapo hapo, ni lazma kichukue mda yeye kufanya na akifanya ni hadi hali iwe tete. Nimeichoka hali hii na upendo wangu kwake umepungua, namekuwa nawaza kuendelea na maisha yangu kwingine ila nafsi inasita kuwaacha mana wananitegemea kwa asilimia kubwa katika mahitaji yao ya kimaisha.

Hivo naombeni ushauri wenu wa kiutu uzima

Hiyo ID yako tu,Hahaha
 
mkuu ktk namba 3 mambo ni hv, nilibd nmipigie huyo X wake simu baada ya huyu mama kukataa kubadili laini yake ya simu. Mie sifuatiliagi simu yake ila kama kuhusu swala la kupigiwa simu ni kwamba yy ndio alinijuza na kusema anakereka nazo. Nikamwambia badili namba tukae kwa aman akawa mbishi kwamba kubadili namba ni kumwogopa huyo X ikabd mie sasa ndio nmtafte huyo X nijue shida yake nn hasa kukaa anapiga simu kama hana msaada wowote.

ktk namba 4 naomba nikwambie katika kila jambo nalomwambia huyu mwanamke huwa nampa na yeye nafasi ya maamuzi yake. Sijawahi mfosi kufanya kitu na hili nadhan ndio limeleta na haya mengine maana naona akaanza kuona kuwa si kawaida tuu nasemaga hafu sichukui hatua.

ktk namba 7 ntarudia nililosema ktk namba 3 yako. Nlipomtafta huyo X ni ilikuwa nmwambie kama hana plans na aliowatelekeza basi asikae kubugudhi watu. Ndio kuanza matusi kwamba atafanya analojisikia yy nisimpangie, nia yangu ni ilikuwa kwamba kama hana shida na mama mtoto na anataka kujua tuu hali ya mtoto basi afanye kupitia kwangu mie ili nijue kama namuasili mwanae au laa.

mkuu its a long story ila naloweza kusema ni kwamba kiburi cha huyu mtu ndio kimeleta hayo unayohisi ww kwamba mie ni control freak na mbabe. Nmepitia mahusiano mengi ila hapa nmejikuta nakuwa mtu ambaye sikutegemea mana nakaa nae huku inakuwa ni kama nashindana na yy pamoja na her past. Nacompete na vivuli, na nikimwambia yy ndio kwanza anakuwa don't care.
basi chapa lapa. maumivu ni sehemu ya maisha. umesema umeshakuwa na mahusiano mengi basi jumlisha na haya ya sasa uendelee kujaribu tena, ilimradi ukae chini ufanye mahesabu ya kujitathmini kabla hujaanzisha mengine.
 
Si wanasemaga mtalaka hatongozwi , wakikutana vicheche vya mapenzi vianawaka wanalianzisha . be careful kaa nae chini ongea nae , mpe muda na kama bado utaona giza mbele kimbia tu.
 
Back
Top Bottom