Yamenifika kooni, nimeshindwa kulea kiburi chake

Yamenifika kooni, nimeshindwa kulea kiburi chake

fundichupi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2015
Posts
382
Reaction score
238
Wasalaam,

Nitaenda katika mada moja kwa moja. Nimekuwa katika mahusiano na single mum kwa takribani mwaka na miezi sasa ila baada ya kumaliza nae nusu mwaka nimejikuta napitia mabidiliko makubwa ya kihisia na fikra. Mama huyu nilimkuta na mtoto mdogo wa miezi saba na alikuwa katelekezwa akiwa na ujauzito wa miezi mitatu.

Nilipomtongoza nlihoji majina ya ubini wa mtoto kama ni ya koo ya mama au baba, mawasiliano yake na mzazi mwenzake na kama mie ntalazimika kutoa huduma zote za mtoto. Akasema mtoto anatumia ubini wa koo ya mama, hana mawasiliano yeyote na mzazi mwenzake mana alipotelekezwa huyo mpenzi wake wa zamani alipotea kabisa na kuhusu mtoto sitolazimika kuhudumia asilimia zote.

Tulianza vizuri na huyu mama na aliweza kunifanya nimpende dhati hadi kufikia hatua ya kusema nitashikamana nae daima. Matatizo yalianza kuja baada ya kujua kuwa alinidanganya mengi mwanzoni, mtoto amebatizwa tayari na kadi la kliniki na uzazi mtoto ana jina la baba ake, mbaya zaidi mama huyu namhoji kwa nini aliniongopea ananjibu kuwa alisema vile kwa kuropoka tu ila atabadili jina na kuandikisha lake.

Tumevutana katika hili hadi akafikia kuniambia mie nimemkuta mtoto hvo nisimpelekeshe maana haoni tatzo mtoto kutumia jina la baba ake. Baba wa mtoto alikuwa anapigaga simu kuulizia hali ya mtoto, ila hachangii hata mia katika mahitaji ya mtoto. Nilimwambia huyu mama hali hio siipendi na abadili laini ya simu ili kusiwe na mawasiliano kati yao mana hata huyo mpenzi wako wazamani namba anayopigia ukiipiga baada ya yeye kukata simu huwa imefungiwa.

Mama huyu kubadili laini alikataa hata nilipomwambia tutaachana katika hili nikiona bado mpenzi wangu anampigia simu ambazo hazna msaada katika maisha yake wala ya mtoto ( huyu mpenzi wa niliwahi mpigia ili niongee nae kiutu uzima kwamba aniambie plan zake kwa mtoto tusaidiane ili abaki na haki zake kwa mtoto ila niliambulia matusi ya nguoni na mama huyu alishuhudia kila kitu mana nilitaka ajue malengo ya mwenzake tuwekeane makubaliano ili kuepuka mie kukaa na hasira kila nikijua wanawasiliana), mwezi baadae ikatokea akapigiwa na huyo nami nipo nyumbani.

Nikamwambia nimeshindwa mie kulea kiburi chake hivyo natamani tuachane tuu kama hali ni hii ndio akabadili laini. Jingine ni mama huyu tumevutana kuhusu mimi kutotaka kuona kitu chochote ambacho alipewa katika mahusiano yake ya zamani ila amekuwa na kiburi katika kuvigawa kwa nduguze ili tukae kwa amani mie nisiiwazie past yake nikiona vitu vya past na kuumia.

Vitu vyenyewe ni nguo hasa hasa na amekomaa kwamba kama sipendi nichome moto begi zima ila yeye hagawi nguo zake. Nimekwazika sana kuona najitoa kumhudumia yeye na mtoto ila hawezi kujali hisia zangu. Nimefikia hatua nimekuwa na uchungu sana ndani yangu na kna mda najikuta na mawazo mengi kama nikae nae au niachane nae nisije nikachukia kila mwanamke kwa sababu yake. Nalileta hili kwa wana MMU mnisaidie mawazo na ushauri, nimeyaweka yale nayoona ni makubwa kwangu ila kna mengi yameendelea hadi mie kufikia hatua ya kutaka kufanya maamuzi magumu.

Mwanamke huyu siwezi nikamwambia kitu ambacho kinaniumiza akafanyia kazi hapo hapo, ni lazma kichukue mda yeye kufanya na akifanya ni hadi hali iwe tete. Nimeichoka hali hii na upendo wangu kwake umepungua, namekuwa nawaza kuendelea na maisha yangu kwingine ila nafsi inasita kuwaacha mana wananitegemea kwa asilimia kubwa katika mahitaji yao ya kimaisha.

Hivo naombeni ushauri wenu wa kiutu uzima
 
Pole saaana ndugu yangu nimejikuta nimevaa viatu vyako kwa mpenzi wangu wa zamani ila ni hivyohivyo vitu vidogo mimi naumia kama nina kaa la moto moyoni mwenzangu kutwa na ma-ex zake nikaondoka na penzi langu zito juu yake.

Kwa hiyo nafeel unavyokwazika. Wataalamu watakushauri,ila mimi sikutaka ushauri wa maelezo,maumivu nliyoyapata hakuna hata mmoja wa washauri anayoyajua. Kupenda kwa dhati ni adhabu!!
 
mmmh mi hata cjakuelewa kiukweli ila poole saana katika maisha ili usonge mbele lazim upitie majaribu
 
Duniani ni sehemu ya kupeana faraja na furaha,kama mwenzio vyote hivyo hana na unajitahidi kumweleza na habadiliki,
Achana nae fanya mambo yako mengine single mums na wadada wapo tele utapata atakae kufaa
 
Hiyo mimba ya miezi mitatu imeishiaje hujasema teh pole
kuzuia mawasiliano ya mtu na mzazi mwenzie ni kitu kisichowezekana especially huyo mtu wako akiwa hajawa tayari kuacha hayo mawasiliano
kubali tu kuwa wewe ni kama mme mwenza otherwise achana na maisha ya tabu
tafuta chombo kipya tena fresh ambacho unajua hakina usumbufu wa kupigiwa simu kuuliziwa mtoto
anza maisha yako.
 
Kuna kitu hujatuambia! Una mtoto au watoto naye? Kwa mtiririko wa maelezo yako inaonekana kama hauna, kama ndivyo na umesema upendo umepungua ni nini kingine kinachokufanya ung'ang'anie kwake?

Kama unaweza kuwahudumia unashindwa nini kwenda kuanza maisha ya uhuru na full of choices? By the way, siku hizi kama una senti za kubadili nguo na mboga hiyo tayari ni mtama kwa watoto...kwani unateseka na K iliyokwisha oteshwa sugu tangu zamani?
 
Tafuta mwanamke mwingine tena asiye na mtoto...
 
Asanteni kwa mawazo,ushauri na michango ya pole.
 
Ndiyo maana siku zote nasisitiza kuoa mwanamke asiye na mtoto
 
Ndio nachowaza dada angu, nikitoka kwake sitojihusisha na mwanamke mwenye mtoto hata awe mzuri kiasi gani. Changamoto nayoipata hapa na nikikumbuka ushauri niliopewa mwanzoni na mme wa dada angu najikuta naumia zaidi mana alinambia kudate mwanamke mwenye mtoto kunaleta na uchungu pia nikapuuza mana alinipa mfano wa namna navyompenda mwanae ambae ni mtoto wa dada angu na namna ntavyobidi nmpende mtoto wakufikia. Mtoto wa dada yangu hamna anaenikataza uhuru nae mana mjomba ni mama ila wa kufikia ndio inakuja nikijali sana naambiwa na mama ake kwani unauchungu kuzidi mie mama ake..!? Yaan naumia balaaa.
Joasi mie sijamwoa huyu dada, twaishi kimahusiano ya kama wachumba tuu

Hiyo mimba nyingine hajajifungua au mliipeleka kwa mjomba daktari
usiingie katika uhusiano na mtu mwenye mtoto, mara chache na kwa watu wachache ndo inakuaga poa
ila mara nyingi jiandae na migogoro ya kutosha
naona fundichupi, chupi inakutoa jasho pole
 
Last edited by a moderator:
...Huyu x niliwahi mpigia ili niongee nae kiutu uzima kwamba aniambie plan zake kwa mtoto tusaidiane ili abaki na haki zake kwa mtoto ila niliambulia matusi ya nguoni na mama huyu alishuhudia kila kitu mana nilitaka ajue malengo ya mwenzake tuwekeane makubaliano ili kuepuka mie kukaa nahasira kila nikijua wanawasiliana)

Nilijifunza jambo..kutoingilia mahusiano ya nyuma ya mpenzi wangu. Nilijaribu kufanya hicho ulichokifanya. Na response niliyopata ilikuwa hiyo hiyo, matusi ya nguoni!

Baadaye rafiki yangu mmoja akanishauri hiyo kazi hainihusu mimi; moja natakiwa kumkubali kama alivyo na hiyo kazi ya ku-break up ni ya kwake binti maana yeye ndo anajua waliishije, waliahidiana nini mpaka huyo mwanaume ajitie kuwa na machungu hivyo.

Nilielewa na kuweka misimamo yangu kwa binti...maamuzi niliyoyafanya sikuelezei. Ila cha maana deal na huyo mwanamke wako...weka vitu unavyotaka na usivyotaka mkubaliane kisha subiria utekelezaji wake....hapo utafanya maamuzi ambayo KAMWE hawezi kukulaumu!
 
MZEE wanawake wengi ndo walivyo.
vitabu vya dini vinatuambia wanaume waishi na wanawake kwa akili.
kama na wewe ndio mahusiano yako ya kwanza utaona kama ni sheeda, waelewe na utaishi naye tu vizuri.
hata utakayeangukia baada ya huyo utagundua kuwa bado ni hivyo hivyo.
fundichupi
 
Last edited by a moderator:
Unataka kupewa ushauri lakini bado huelezi ukweli, hapo sio kwamba unaogopa kumuacha kwasababu unamsaidia na wanakutegemea, ishu ni kwamba umeshikwa na uzuri wa huyo mwanamke, ulikosea mwanzoni kwasababu uliifuata mihemko yako ukaweka utashi nyuma. Ni msaada wa aina gani unaoutoa huku ukiwa na manung'uniko malalamiko kibao?
Hujiulizi kwanini huyo baba mtoto amemtelekeza mwanamke na analia timing tu aje achukue mtoto wake baadae? Ulikosea kuanza sasa angalia ustaarabu mbele
 
Yaani mtu hujamuoa halafu anakutendea hayo na wewe unang'ang'ana.

Daah mkuu katika hili swali ni wewe tu ndo utayelitatua .

Wanawake wapo wengi sana kwanini ung'ang'a na huyo aliezalishwa .

Anakutegemea kwa kila kitu kwani wewe babake.

Acha uzezeta moveeeeee!!!

Mapenzi hayalazimishwi.
 
Back
Top Bottom