Yaliyotokea mwaka 2009 Picha hizo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyotokea mwaka 2009 Picha hizo

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Jan 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  KIFO CHA PAKANJIA, MENGI YAIBUKA

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Na Waandishi Wetu

  Siku mbili baada ya kifo cha mfanyabiashara ‘The Big Name’, jijini Dar es Salaam, Mohamed Athuman Mpakanjia ‘Meddy’,37 Amani linaweza kuwa la kwanza kumwanika mke mpya wa marehemu, Zaitun Kessy Mpakanjia.

  Zaitun ambaye anaonekana ukurasa wa mbele wa gazeti hili, alifunga ndoa na Meddy Jumapili iliyopita na kuishi naye kwa saa kumi na saba kabla ya kifo cha mumewe.

  Hata hivyo, gazeti hili lina mengi ambayo yameibuka kufuatia kifo hicho kilichotokea ghafla, moja ya hayo ni kugundulika kuwa, marehemu alishaandika mirathi ya nyumba zake mbili, zilizoko Sinza na Mbezi, jijini Dar es Salaam.

  Habari zinasema kuwa, marehemu alimwandika mtoto wake wa mwisho, Abdulrahman Mohamed Mpakanjia a.k.a Rahmanino kurithi ule mjengo wa pale Sinza-Mori.

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Mbali na huyo, mtoto mwingine ambaye amepata nyumba kupitia mirathi hiyo ni Rahim Mohamed Mpakanjia ambaye anakuwa mmiliki wa nyumba ya Mbezi.

  Watoto wengine wa marehemu, Ibrahim na Karim Mohamed Mpakanjia, wote wamerithi nyumba mbili zilizopo, Tandika, wilayani Temeke, Dar kwa kila mmoja kuchukua ya kwake.

  Kauli ya marehemu aliyoiacha kwa mkewe mpya, Zaitun wakati akipelekwa Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo ni jambo lingine nyuma ya msiba huo. Habari zinasema, marehemu Mpakanjia alimwambia mkewe huyo kwamba, anapelekwa hospitali, lakini hatopona na hivyo ana uhakika kuwa, anamwacha katika eda.

  Zaitun alilithibitishia gazeti hili kuwa, kweli marehemu alitamka maneno hayo, licha ya kwamba awali hakuwa amejua alilenga nini. “Marehemu wakati anapelekwa hospitali aliniambia, mke wangu nakuhurumia, napelekwa hospitali lakini nakuacha eda,” alisema Zaitun.

  Aidha, mapya mengine ambayo yaliutikisa msiba wa Meddy ni ndogo ndogo ambazo zimelifikia gazeti hili kwamba baadhi ya ndugu wa marehemu wanamnyanyapaa Zaitun kwa maelezo kuwa yeye si mke halali.

  Ushakunaku wetu msibani umebaini kuwa mpaka juzi, Zaitun alikuwa hajavalishwa mavazi rasmi ya mwanamke mjane ambayo huvaliwa wakati wa eda.

  Katika hilo, Amani limebaini kwamba kulikuwa na mikakati ya chini kwa chini kutoka kwa baadhi ya ndugu wa marehemu, waliotaka ‘kutaifisha’ haki zote za mjane huyo.

  **********


  2. WASOMANI 8602:
  Kijiji cha ngono

  [​IMG]
  Na Waandishi Wetu

  Baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam linaloongozwa na Mheshimiwa William Lukuvi, yamekuwa katika mazingira hatarishi ya kuenea kwa kasi Ugonjwa wa Ukimwi kufuatia kushamiri kwa vitendo vya ngono vinavyofanyika nyakati za usiku, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili.

  Uchunguzi wa muda mrefu uliofanywa na timu ya waandishi wetu umebaini kuwa, miongoni mwa maeneo ya jiji yanayosifika kwa zinaa pamoja na vitendo vingine vichafu ni Buguruni Sheli jirani na Baa ya Kimboka ambapo biashara haramu ya kuuza miili bila kificho imekuwa ikifanyika kiasi cha kuigeuza sehemu hiyo kama kijiji cha ngono.

  Eneo hilo linaloonekana kuchangamka sana inapotimu mishale ya saa 3 usiku na kuendelea kufuatia kufanyika kwa biashara mbalimbali pamoja na burudani za muziki hasa wikiendi, limekuwa kivutio kikubwa kwa wasichana wenye umri mdogo wakiwemo wanafunzi ambao hujitokeza na kuinadi miili yao kwa wanaume wanaofika eneo hilo.
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Aidha, imebainika kuwa, mabinti wanaofika katika eneo hilo kujiuza wakitokea maeneo mbalimbali, hufanya hivyo kwa kushinikizwa na wazazi wao kutokana na hali ngumu ya maisha ambapo hutakiwa kutoka usiku na kurudi na ‘chochote kitu’ kwa ajili ya kujikimu kimaisha.

  Akiongea na Ijumaa Wikienda, mmoja wa wazee waishio katika eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Mwinyi alisema kuwa, hali katika kitongoji hicho ni mbaya hasa giza linapoingia na kwamba matendo mengi kinyume na maadili yamekuwa yakifanyika hadharani.
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  “Kwakweli hali ndiyo kama mnavyoona wenyewe maana mwenye macho siku zote haambiwi tazama, watoto wadogo wanajiuza tena kwa watu wazima bila aibu yoyote, wanapigana vikumbo na wakubwa wao kuingia na kutoka gesti, yaani biashara ya ngono inafanyika wazi wazi kana kwamba imekubalika kisheria.

  “Cha kusikitisha zaidi ni kwamba, licha ya kujiuza hadharani inafika wakati hata maeneo wanayokwenda kufanyia ufirauni wao ni ya wazi ikiwa ni pamoja na kwenye vibaraza vya nyumba za watu na uchochoroni tena bila tahadhari, hii ni hatari,” alisema mzee huyo.

  Mzee huyo aliongeza kuwa, ilifika wakati walishindwa kuvumilia na kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Buguruni kufuatia ufuska unaofanyika hapo lakini polisi wamekuwa wakiiachia hali hiyo ikiendelea kushamiri na kuifanya jamii izidi kuangamia.
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  “Kuna kipindi mimi na wazee wenzangu tuliamua kwenda kutoa taarifa juu ya yale yanayoendelea katika eneo hili nyakati za usiku, polisi wakawa wanakuja na kuwamata lakini sasa hivi hatuwaoni na kuifanya hali irudi kama ilivyokuwa zamani, haijulikani nani mtoto nani mkubwa, kwakweli tunaomba vyombo husika viingilie kati,” alinena mzee huyo.

  Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita liliweka kambi ya saa sita (Kuanzia saa 2-8 usiku) katika eneo hilo na kushuhudia ufirauni wa kutisha ukifanyika bila kificho huku biashara ya ngono ikizidi kunoga kadiri muda unavyosogea mbele.

  Katika kuthibitisha kile ambacho kilikuwa kikilalamikiwa na wakazi wa eneo hilo, waandishi wetu walilazimika kuzunguka eneo hilo mtaa kwa mtaa na kushuhudia vibinti vidogo vikiwa na wanaume gizani wakifanya mambo yasiyofaa.

  Aidha, wengine walionekana wakiwa wameshikana mikono kuelekea kwenye nyumba za kulala wageni zilizopo karibu na aneo hilo ambapo katika uchunguzi huo imebainika kuwa, gharama ya ngono ni kati ya shilingi 5,000 na 10,000 ikijumlishwa na malipo ya gesti.

  Ilifahamika pia kwamba wasichana hao hutoa huduma ya ngono kwa shilingi 3000 endapo mteja hatakuwa na pesa ya kwenda gesti ambapo hupelekwa kwenye vibaraza vya nyumba za watu au sehemu zenye giza na kuhudumiwa chapchap.
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Wakiongea na gazeti hili baadhi ya mabinti wanaofanya biashara hiyo haramu katika eneo hilo walisema kuwa, wanalazimika kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili.

  “Tunajua kwamba kujiingiza katika biashara hii ni hatari kwa maisha yetu lakini sasa tutafanyaje? Maisha yenyewe magumu na mwisho wa siku tunahitaji kuvaa na kula tutapata wapi pesa wakati hatuna kazi?” Alihoji binti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 16 na 20 huku akikataa kutaja jina lake.

  Gazeti hili linalaani vikali biashara hiyo haramu na linaziomba taasisi husika ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kuingilia kati na kuhakikisha kijiji hicho kinasambaratishwa ili kuiepusha jamii hiyo na madhara makubwa yanayoweza kujitokeza hapo baadaye.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi na Kamanda wa Kanda Maalum, Suleiman Kova mnaweza kulimaliza hili. MHARIRI.

  *************


  3. WASOMAJI 8155:

  GROUP SEX

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Na Waandishi Wetu

  Katika kile kinachoonekana kwamba maadili yameporomoka, wanawake watatu (pichani mbele), wakazi wa Msasani, jijini Dar es Salaam wamebainika kuwa wanaendesha maisha yao mjini kwa kufanya mapenzi kwa wakati mmoja na mwanaume mmoja (group sex).

  Awali gazeti hili lilitonywa na chanzo cha kuaminika, kuhusu kuwepo kwa akina dada hao ambapo lilipewa namba za simu za mmoja wao anayesadikiwa kuwa ndiye kiongozi wao.

  Mara baada ya kupata namba hizo, Ijumaa lilianza kufanya mawasiliano na kiongozi huyo ambaye alimhakikishia kuwepo kwa huduma hiyo tena katika ubora akisema ana wenzake wawili bomba endapo wangepewa ‘mpunga’ wa maana.

  Gazeti hili halikuwa na tabu katika upande huo, lilikubaliana na mrembo huyo, kupatiwa huduma hiyo kwa gharama ya shilingi elfu ishirini na tano kwa kila mmoja ambapo ni sawa na shilingi sabini na tano kwa wote watatu.

  Baada ya hapo, timu ya kufuatilia operesheni hiyo iliundwa, ambapo Mashushu Wetu waliendelea kufanya mawasiliano na mrembo huyo kwa niaba ya wenzake kabla ya kupanga miadi ya kukutana Alhamisi katika Gesti ya Grand View Inn, iliyopo Sinza ya Kwaremy, jijini Dar es Salaam.

  Baada ya kuwekana sawa, Timu ya Ijumaa ikishirikiana na Askari Polisi watatu kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, Oysterbay jijini Dar, ilikuwa ipo tayari kukamilisha operesheni hiyo ya kufichua maovu yanayotendeka kwenye jamii hasa kipindi hiki ambacho serikali inapiga kelele kuhusu maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

  Paparazi mmoja aliingia katika chumba namba 30 ndani ya gesti hiyo, kilichokuwa kimelipiwa tayari ambapo aliwasubiri ‘wageni’ hao.

  Muda mfupi baadaye, warembo hao walitimba wakiwa ndani ya taksi, ambapo Paparazi wetu aliyekuwa amejibanza kona, alifanikiwa kupata picha (kama inavyoonekana ukurasa wa mbele).
  ‘Shushushu’ aliyekuwa chumbani, alihabarisha kila hatua iliyokuwa ikiendelea ikiwa ni pamoja na kueleza kuwa warembo hao wameshachojoa nguo zote tayari kwa kuanza kazi.

  Bila kupoteza muda chumba hicho kilivamiwa na kuwakuta wote wakiwa katika hali ya aibu.
  Wasichana hao baada ya kugundua wameingiliwa na maaskari na waandishi walilia huku wakiomba wasipigwe picha wala kupelekwa Polisi kwa kile walichokieleza kwamba walipitiwa na shetani mbaya na kwamba hawatarudia tena utetezi ambao haukuzingatiwa.

  Habari zaidi juu ya tukio hilo chafu linaloporomosha maadili yetu, fuatilia Jumatatu katika gazeti la Ijumaa Wikienda.

  Gazeti hili linalaani vikali wanawake hao na wengine wenye tabia kama yao. – MHARIRI.

  **********


  4. WASOMAJI 7470:
  Irene Uwoya arudi kwao!

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Na Musa Mateja

  Julai mwaka huu, Kanisa la Mtakatifu Joseph, Posta Dar es Salaam ilifungwa ndoa ya rekodi na mtoto wa kike aliyeolewa, Irene Uwoya alipanda ndege siku mbili zilizofuata na kwenda kuanza maisha mapya ya ndoa barani Ulaya.

  Hata hivyo, ikiwa ni miezi mitatu tu tangu Irene alipofunga ndoa na mcheza soka wa kimataifa wa Rwanda kwa mashamshamu yaliyoweka rekodi, Risasi Jumamosi lina ÔeksiklusivÕ kwamba mwanadada huyo amerejea Bongo na sasa yupo nyumbani kwa wazazi wake, Mbezi Beach, Dar.

  Gazeti hili halijawa na Ôofisho ripotiÕ kuhusu hicho kilichomrudisha nyumbani Irene, lakini usiku wa kuamkia Alhamisi ya wiki hii, paparazi wetu alimbamba ÔmdadaÕ huyo kwenye klabu yenye jina kubwa Dar, Billicanas.

  Paparazi wetu akiwa amejichanganya ndani ya klabu hiyo, huku ÔakikopÕ na staa mmoja baada ya mwingine, ilibidi apekeche mara tatu, pale Irene aliposogea jirani yake na kusalimiana naye kwa kupeana mikono.

  Pamoja na kuonekana klabu, Irene hakuwa katika hali ya kawaida, kwani muda mwingi alionekana ni mwenye wasiwasi, huku akikwepa mwanga wa taa ambazo huwaka kwa mtindo wa kuzunguka.

  Kutokana na kumshuhudia akiwa katika sura hiyo, paparazi wetu alijipa jukumu la kumfuatilia mrembo huyo ambaye katika siku za hivi karibuni ametokea kuwa muigizaji nyota wa filamu Tanzania.

  Katika ufuatiliaji huo, paparazi wetu alimshuhudia Irene akihama hama kituo cha kucheza muziki kutokana na kukimbia taa za klabu.

  Katika hilo, Irene ambaye ni Miss Tanzania namba tano 2006-07, alikuwa akitaka kucheza gizani tu na kila mara aliingia kwenye pembe moja mafichoni, ili kupisha taa zipite.

  Jitihada za mwandishi wetu kuongea na Irene ziligonga ukuta, baada ya mrembo huyo kutoka nje haraka kama aliyekuwa anakimbia kitu, ambapo aliingia kwenye gari na kutoweka.

  Gazeti hili, linafuatilia kwa kina sababu iliyomrudisha Irene nyumbani kwao, kwa staili ya kimya kimya.
  Irene baada ya kufunga ndoa na Kataut, hakuchukua muda jijini, kwani siku mbili zilizofuata alipanda ndege na kutua kwenye Jiji la Nicosia, Cyprus ambako mumewe anacheza soka la kulipwa kwenye Klabu ya AEL Limassol.

  Kataut, alisaini mkataba wa miaka mitatu na Limassol Julai 18, mwaka huu, hivyo bado ana maisha marefu kwenye kisiwa hicho cha Cyprus ambacho ni cha tatu kwa ukubwa kwenye Bahari ya Mediterranean.


  ******


  5. WASOMAJI 7312:

  JOYCE KIRIA: Nimekula uroda na wanaume wengi sana!

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->​

  Mtu mzima nishatia timu kwenye uwanja wangu wa kujidai, shwari lakini? Kama mtakumbuka vizuri, wiki iliyopita tulikuwa na Kalala Junior ambaye kama kawa tulimtwanga maswali yake kumi.
  Leo uwanjani tunaye Mtangazaji anayekuja kwa kasi ajabu katika fani hiyo anayekwenda kwa jina la Joyce Kiria. Nimezungumza naye kama mlivyonituma kwani siku zote huwa nafanya kazi hii kwa ajili yenu wasomaji wangu wapenzi.
  Unajua ilivyokuwa? Sebeza na interview kali hapa chini.

  TQ: Nipo hapa kwa niaba ya wasomaji wa gazeti la Ijumaa ambao wanataka kujua maisha yako ndani na nje ya kazi. Bila kupoteza muda anza kwa kutueleza ni kitu gani hasa kilikufanya ukaamua kuingia katika fani ya utangazaji hasa ya kuchambua filamu za kibongo?

  Joyce: (Akiwa makini) Napenda sanaa ya maigizo, lakini kila kukicha matatizo yamekuwa hayaishi kwenye filamu zetu, nikaona ni bora niingie niweze kuwakosoa na kuwapongeza waliofanya vizuri kama njia ya kuikuza.
  TQ: Kazi yako ya utangazaji umewahi kuifanya nje ya Bongo?

  Joyce: Zaidi ya Clouds Fm, Channel Ten na sasa EATV, sijavuka mipaka ya nchi yetu ingawa ni moja ya ndoto zangu za baadaye.
  TQ: Nini mafanikio yako katika kazi yako?

  Joyce: Mafanikio yapo ingawa siyo ya moja kwa moja. Kubwa zaidi ni kufahamiana na watu wa nyanja mbalimbali.
  TQ: Unaweza kukumbuka idadi ya wanaume uliokuwa nao kabla ya kukutana na mumeo Dj Nelly?

  Joyce: (Huku akicheka) Hapa lazima niseme ukweli...sikumbuki idadi kamili maana nimetembea na wanaume wengi sana! Uzuri wangu ndiyo unaowachanganya kwahiyo nikajikuta nikiwa na wanaume wengi sana, lakini baada ya kukutana na toto la Kihaya, Nelson Nkongo (Dj Nelly) nimetulia kwa raha zangu, maana ananipa kila ninachokihitaji.

  TQ: Mh! Hujatulia wewe, enhee nini kilisababisha ukachaana na wapenzi wako wa nyuma?
  Joyce: Unajua mimi nilikuwa natafuta mume wa kuishi naye, kwahiyo kila nilipogundua mtu ana nia ya kunitumia, niliachana naye haraka sana, ndiyo sababu nikawa na wanaume wengi.

  TQ: Sasa wanaume wote hao jamani, hukukanyaga miwaya kweli?
  Joyce: Nilikuwa makini sana, mara zote nilikuwa nikitumia kinga. Hata hivyo niliwahi kupima na kukuta nipo poa.

  TQ: Unataka kuniambia baada ya kukutana na Dj Nelly mlipima?
  Joyce: Kwakweli hapana, lakini najiamini maana sijawahi kutoka nje ya penzi letu, na hata yeye namuamini pia.

  TQ: Kuna nyepesi zinasema kwamba, Dj Nelly alikuwa mume wa mtu na wewe uliingilia ndoa ya watu. Hilo unalizungumziaje?
  Joyce: Hakuwa mume wa mtu bali alikuwa akiishi na mwanamke, lakini baada ya kuridhika na mimi ndiyo akaamua kunichukua jumla kwa ndoa halali ya Kanisani.

  TQ: Sasa naomba kukuuliza swali la chumbani zaidi. Ni kitu gani ukifanyiwa na mpenzi wako faragha unajisikia raha zaidi?
  Joyce: Mi’ napagawa zaidi na romance, hapo tu, ndipo panaponiacha hoi mtoto wa kike.

  TQ: Halafu kuna tetesi mjini kwamba huo weupe wako ni wa dukani, nikimaanisha kwamba unajichubua. Hiyo nayo imekaaje?
  Joyce: Naona maswali yamekuishia sasa...kifupi weupe wangu ni wa asili, kwaheri bro!


  *******


  6. WASOMAJI 7299:

  RAY C AMEFULIA

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Na Imelda Mtema
  Mwanamuziki wa kike ‘alwatani’ nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’ juzi (Jumatatu) alipatwa na aibu ya mwaka baada ya wifi yake kutinga dukani kwake na kumtupia mabegi yake yenye nguo, Risasi lilikuwepo.


  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->​

  Sakata hilo lililokusanya watu kibao, lilijiri majira ya saa kumi na moja jioni nje ya duka hilo lililopo maeneo ya Morocco, jijini Dar es Salaam.

  Wifi aliyemfanyia ‘undava’ huo Ray C ni mke wa kaka yake, Ton aliyejulikana kwa jina la Loveness kufuatia kuibuka kutokuelewana baina yao na mwanamuziki huyo kuanza kumtukana wifi yake kwa meseji za simu.

  Akiongea na kwa jazba na Risasi, wifi huyo alitoboa kuwa, awali aliyahifadhi mabegi yenye nguo ya mwanamuziki huyo nyumbani kwake kwa takribani miezi mitatu baada ya baba mwenye nyumba wa Ray C kumtimua kwa kushindwa kulipa kodi ya nyumba hivyo kuanza maisha ya ‘kumbonji’ gesti.

  Aliendelea kusema kuwa, mbali na mabegi ya nguo, pia Ray C alipeleka kwa wifi yake huyo, dishi lake kwa ajili ya channel za Tv.

  Akasema kuwa, kisa cha yote hayo ni Ray C kutaka kumpelekesha wifi yake kama ‘garibovu’ baada ya hivi karibuni kumtumia ujumbe kwenye simu akimtaka ampelekee dishi hilo dukani kwake wakati akienda kazini.

  “Alinitumia ujumbe wa simu, akasema ninapokwenda kazini nimpelekee dishi lake dukani, nikamjibu kuwa sitaweza kupita muda huo, aende akachukue mwenyewe nyumbani,” alisema Loveness.

  Aliendelea kuweka wazi kuwa, baada ya hapo, Ray C alianza kumtumia ujumbe wenye maneno makali na ya vitisho kitendo kilichomuumiza wifi yake huyo.

  Aliendelea kudai kuwa, ilifika mahali alishindwa kuvumilia kashfa za kwenye meseji ndipo alipoamua kumkusanyia virago vyake vyote na kumpelekea dukani kwake ili ‘wasijuane’ tena.

  “Sikupenda maneno yake ya kashfa kwenye simu, niliamua kubeba mabegi yake na kumpelekea dukani kwake maana hana sehemu maalumu pa kuishi,” alisema Loveness.

  Sakata zima la dukani lilianza baada ya Loveness ‘kutia timu’ na kuyabwaga nje mabegi yenye nguo kitendo kilichomfanya Ray C kudata kwa dakika kadhaa huku akiwaambia walinzi warudishe mabegi hayo, ambayo mengine hayana zipu, ndani ya gari la wifi yake.

  Sekeseke hilo lililodumu kwa takribani dakika kumi lilinoga zaidi baada ya kijana mmoja wa dukani hapo kuchukua begi moja na kuliweka nyuma ya gari kwa lengo la kulizuia lisitoke, kitendo kilichomfanya wifi mtu kushuka ndani ya gari na kulitupa begi hilo kwenye mtaro wa barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

  Baada ya kujiridhisha kwamba amemaliza zoezi salama, Loveness ‘alitimua vumbi’ na gari lake, lakini kabla hajafika mbali, alipokea ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa Ray C akimuonya kwamba asimkute nyumbani kwa kaka yake.

  Risasi lilifuatilia bega kwa bega sakata hilo ambapo lilifika nyumbani kwa wifi huyo, Mbezi jijini Dar majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni, dakika kumi baadaye Ray C naye alikanyaga akiwa ameongozana na askari wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay cha jijini Dar na kumzoa wifi huyo.

  Baada ya wote wawili kutinga kituoni hapo, Loveness aliwekwa lupango kwa madai ya kufanya fujo dukani kwa Ray C na kuamriwa kulala hadi jana (Jumanne).

  Mpaka mwandishi wetu anaondoka kituoni hapo, majira ya saa tano na nusu usiku, wifi wa mwanamuziki huyo alikuwa bado yupo mahabusu ‘akichengana’ na mbu.

  Hata hivyo, baadhi ya watu walioshuhudia timbwili hilo nje ya duka la Ray C walisema kuwa, msanii huyo amefulia (ametumia pesa vibaya, sasa hana kitu) ndiyo maana amefikia mahali hana sehemu maalum ya kuweka ubavu wake.

  Walisema kuwa, wanaamini pesa aliyoikamata Ray C enzi hizo kama angeipangilia vizuri, hata duka alilonalo Morocco lingekuwa mitaa ya Samora (katikati ya jiji) tena kubwa na lenye mtaji ulioshiba.

  “Ray C hakuwa wa hivi, mpaka nguo zake zinakaa kwa mtu, maisha bwana. Inaonekana ‘alifulia’ ndiyo maana anapata tabu leo, sasa hii aibu gani,” alisema shuhuda mmoja.

  ******


  7. WASOMAJI 7309:
  WEMA: Najuta kumfahamu Kanumba

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Musa Mateja na Edna Katabalo

  MTIKISIKO uliomkumba Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu baada ya kuburuzwa kwenye Mahakama ya Kinondoni juzi kisha kuswekwa mahabusu katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam umemfanya mnyange huyo ‘amkinai’ aliyekuwa mpenzi wake, Steven Charles Kanumba.

  Habari ‘zilizonyunyizwa’ na vyanzo vyetu ndani ya Segerea, zinapasha ya kwamba akiwa nyuma ya nondo nono na kuta zenye dirisha dogo, Wema mara kwa mara alikuwa akisema kuwa anajuta kumfahamu Kanumba kwa sababu bila yeye asingepata masahibu hayo.

  Wema akiwa na wifi yake, Aisha Jumbe walifikishwa kortini kwa kosa la kuharibu mali, baada ya kuvunja kioo cha gari la Kanumba katika ugomvi wa mapenzi. Wawili hao, waliwekwa rumande kutokana na wadhamini wao kuchelewa kukamilisha masharti ya dhamana.

  Chanzo chetu kimoja kilisema juzi: “Wema hana raha, akikaa anasema haamini kama ugomvi wa mapenzi ungeweza kumfanya alale Segerea. Anasema alimkubali Kanumba kwa moyo wake wote, akampa penzi lake, alipomchefua ndiyo alimuacha lakini haamini kilichotokea mpaka akalazwa Segerea.”

  Siku chache kabla ya Wema kuburuzwa mahakamani, mwandishi wetu aliongea na Kanumba walipokutana kwenye Hoteli ya Lamada, Dar es Salaam ambapo staa huyo alisema kwamba atahakikisha Miss Tanzania huyo analijua jiji ikiwezekana mpaka apigwe mvua jela.

  Juzi mchana, Ijumaa liliongea na mchumba wa sasa wa Wema, Jumbe Yusuf Jumbe ambaye alisema kwamba alikuwa tayari amekamilisha taratibu za dhamana na kuahidi kuwa jana kwenye majira ya saa nne asubuhi, ‘misezi’ wake angekuwa huru.

  **********


  8. WASOMAJI 6529:
  NDOA YA MSANII ALIYEKATWA MGUU: NI VILIO

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Na Imelda Mtema
  Hatimaye wasanii mahiri wa filamu nchini, Wastara Juma ‘Wastara’ na Juma Kihowolo ‘Sajuki’ wamefunga pingu za maisha licha ya Bibi harusi huyo kukatwa mguu wa kulia miezi miwili iliyopita kufuatia ajali ya pikipiki. Ndoa hiyo iliyofuatiwa na sherehe za harusi ilifanyika nyumbani kwa wazazi wa Bibi harusi, Tabata Segerea jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali wa Bongo ambao walitoa kampani vilivyo. Hata hivyo, sehemu kubwa ya
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->


  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  sherehe hiyo ilitawaliwa na vilio na majonzi, hasa pale Bibi harusi alipoingia kwenye eneo la wazi lililoandaliwa kwa shughuli hiyo akiwa amekaa kwenye baiskeli ya gurudumu (Wheel Chair).

  Aidha, vilio vilisita baada ya kukaa kwenye kiti kilichoandaliwa ‘spesho’ kwa Bibi harusi, lakini vilianza tena baada ya maharusi hao kuimba wimbo kwa pamoja unaoelezea mapenzi yalivyo.

  “Mke wangu sitakuacha, wewe ni mahabuba wangu, sitakuacha,” Sajuki aliimba wimbo huo. “Mume wangu unilinde, unipende, usiniache…,” Wastara naye alijibu na kusababisha vilio kutoka kwa wageni waalikwa. Aidha, yeye mwenyewe alishindwa kuendelea kuuimba wimbo huo na kujikuta akilia kwa uchungu mkubwa.

  Habari zinasema wimbo huo pia waliuimba kwenye filamu ya Mboni ya Jicho Langu ambayo iliwashirikisha wote. Msanii wa kike wa filamu nchini, Aunt Ezekiel ambaye alikuwa miongoni mwa waalikwa, alishindwa kuvumilia na kuporomosha machozi huku akisema: “Kwa kweli kwa namna hii huwezi kuvumilia hata uwe na roho ya aina gani ni uchungu mno, lakini Sajuki ameonesha upendo wa ujasiri.” Ukumbi huo ulizidi kutawaliwa na simanzi ingawa na makofi kwa mbali, pale bwana harusi aliposhika ‘maiki’ na kuwatangazia waalikwa kuwa, Wastara ni mkewe wa maisha, kamwe hatomwacha.

  “Nimesimama hapa kwa ajili ya kumhakikishia nyonga mkalia ini wangu (Wastara) kuwa mimi ni wake milele sitomuacha mpaka kifo,” alisikika Sajuki.
  Baada ya Shamrashamra hizo, Sajuki alimbeba Wastara huku akicheza naye wimbo wa mwanamuziki wa Sauzi, Yvonne Machaka ‘Chakachaka’ uitwao ‘Mkomboti’ huku akielekea naye kwenye gari kwa ajili ya kuondoka. Tukio hilo lilisindikizwa na wasanii kibao kwa nyuma huku wakicheza mpaka maharusi hao walipopanda gari na kwenda kwenye Fungate lao Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya watu waliohudhuria harusi hiyo walisema kuwa, hawakutegemea kama Sajuki angemuoa Wastara, hasa baada ya kukatwa mguu na kwamba kwa tukio hilo ameonesha upendo wa hali ya juu. Wasanii waliohudhuria sherehe hiyo ya ndoa ni Steven Kanumba ‘Kanumba’, Vincent Kigosi ‘Ray’, Aunt Ezekiel, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, na Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo.’ Wengine ni Hisan Muya ‘Tino’, Adam Kuambiana, William Mtitu ‘Mtitu’ na Hawa Mkama.

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->

  PICHA:IMELDA MTEMA


  *********


  9. WASOMAJI 6369:

  CHID AFANYA MALAVU NA VICK

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Na Mwandishi Wetu- Mbeya

  Hatimaye fununu za Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Rashid Abdallah ‘Chid Benz kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Miss Tanga 2007,Victoria Martin hivi karibuni zimepakuliwa kwenye sahani ya ukweli mjini hapa.

  Chid na Vick, wawili waliotajwa kuwa ni wapenzi kwa siri kwa miezi kadhaa sasa, walinaswa na mtandao wetu wa habari uliokuwa ukinyatia nyendo zao ndani ya Hoteli ya Rift Valley walimopanga pamoja kwa lengo la kupeana malavu usiku kucha.

  Ukurasa wa kwanza wa ishu hii ulianzia kwenye safari ya kimuziki iliyomhusisha msanii huyo wa kizazi kipya ambaye alikuwa safarini mitaa ya mji huu kwa lengo la kumpa kampani Maximilian Bushoke ‘Bushoke’ aliyekuwa akizindua Albamu yake ya Dunia Njia.

  Ilielezwa kwamba, ndani ya msafara wa wasanii kutoka bongo waliounda timu ya kumsapoti Bushoke, mwanadada huyo alikuwemo, ingawa haikufahamika alikuwa na kazi gani katika shoo hiyo licha ya kwamba kulikuwa na tetesi kuwa, yeye na mpenzi wake walipanga kwenda kula ‘malavi davi’ huko mbali na Jiji la Dar.

  Aidha, kundi hilo lilipotia timu mkoani hapa, Vick alionekana ubavuni mwa Chid huku akisafiri ndani ya gari la wasanii hao ambao baadhi yao walikuwa wakivuta bangi na kumfanya naye avute kimtindo moshi wa sigara hiyo kali.

  Baada ya shoo iliyofana iliyofanyika ndani ya Uwanja wa Nane Nane, vinasa matukio vyetu vilivyoangalia nyendo za wawili hao, ‘vilijimuvuzisha’ moja kwa moja ndani ya Hoteli ya Rift Valley ambako viliwashuhudia wawili hao wakiingia ndani ya chumba kimoja.

  Mishale ya sekunde, dakika na saa ilizidi kutembea huku macho ya mapaparazi wetu yakiambulia patupu kutokana na mwanadada huyo kutotoka ndani ya chumba hicho cha msanii huyo anayetajwa kupenda ‘undava’.

  Hata hivyo, masikio ya wanasa matukio wetu pamoja na ya baadhi ya wapangaji ndani ya hoteli hiyo walibahatika kusikia sauti ya mwanadada huyo akilia kilio ambacho hakikufahamika kilitokana na nini na hadi kunapambazuka mrembo huyo hakuwa ametoka ndani ya chumba hicho.

  Chid na Vitoria walipotafutwa kwa njia ya simu baada ya uchunguzi huo kukamilika hawakupatikana, ingawa mmoja kati ya wahudumu wa hoteli hiyo (jina kapuni) alikiri wawili hao kulala chumba kimoja.

  Gazeti hili linaendelea kuwasaka wawili hao na mara watakapopatikana tutawaletea upande wa pili wa nyeti hizi.

  ******


  11. WASOMAJI 6118:

  Ndoa ya kufuru
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Hamida Hassan na Christopher Lissa
  Hatimaye msanii nyota wa filamu nchini, Irene Uwoya amekata ngebe za ‘wapinzani’ wake kwa kufunga pingu za maisha na msakata ndinga wa kimataifa toka nchini Rwanda, Ndikumana Katauti.
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->


  Tukio hilo la kihistoria lilifanyika kwenya Kanisa la Mtakatifu Joseph (ST.Joseph) jijini Dar es Salaam Julai 11,2009 na kushuhudiwa na watu kibao.

  Irene ambaye pia amewahi kuudaka u-Miss ‘Tizedi’ nambari 5, 2006-2007 amefunga ndoa na mcheza kabumbu huyo baada ya kuwa wachumba kwa muda wa miezi sita.

  Baadhi ya wanandugu waliohudhuria ibada ya ndoa ya wawili hao ndani ya kanisa hilo, waliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kufungwa kwa pingu hizo kumeiondolea familia aibu kwa vile baadhi ya ‘maadui’ wa Irene walijiapiza kuwa, asingeolewa maishani kutokana na ‘laifustaili’ aliyokuwa akiishi.

  “Kwa kweli familia ina furaha kubwa, maana wapo waliosema haolewi, lakini leo kaolewa. Walidhani Irene si mwanamke anayefaa kuwa mke wa mtu,” alisema ndugu mmoja huku akisema jina lake si muhimu zaidi ya tukio lenyewe.
  Katika hali iliyoonesha kuwa ndoa hiyo ni ‘kufuru’ ndoa nyingine ambazo zilitakiwa kufungwa siku hiyo zilipigwa ‘stop’kwa muda kuingia kanisani hapo.

  Baada ya ibada ya ndoa, ilifuatiwa na shamra shamra kubwa za vikundi vya ngoma ya asili ya Rwanda, Kabila la Kimasai pamoja na matarumbeta ambavyo vilitawala katika viwanja vya kanisa hilo.
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->[/center]

  Aidha, alitinga Ngamia ambaye alikuwa kivutio kikubwa kanisani hapo, ambapo Bwana harusi Ndikumana alimpanda na Irene akawa anamvuta kuzunguka maeneo ya katikati ya jiji, huku wakiongozwa na umati mkubwa wa watu.
  Hali hiyo ilisababisha wananchi wengi kuacha shughuli zao na kujipanga barabarani kushuhudia kufuru hiyo.

  Aidha, kama zilivyo sherehe za mastaa, vioja kibao vilifunika ndoa hiyo, ikiwa ni pamoja na Bwana harusi kutinga Kanisani akiwa amesuka nywele huku akiwa amevaa hereni suala ambalo lilizua minong’ono.

  Pia, Ndikumana alizua mtafaruku baada ya kushindwa kufuata maelekezo ikiwa ni pamoja na kupiga magoti wakati wa ibada na kutoshiriki kula chakula cha Bwana (Sakramenti takatifu).

  Katika vipengele vyote hivyo Irene tu ndiye aliyeonekana kutekeleza hivyo kuzua viulizo vingi kwa waumini huku wakihoji uhalali wa wawili hao kufunga ndoa kanisani wakati mmoja anashindwa kutekeleza baadhi ya taratibu muhimu.
  Majira ya saa 10:15 msafara mkubwa wa magari uliowabeba mastaa hao ndugu, jamaa, na marafiki uliondoka katika viunga vya kanisa hilo kuelekea katika Hoteli ya kisasa ya Giraffe iliyopo Mbezi kwa ajili ya sherehe.

  http://www.globalpublisherstz.com/habari_mbalimbali/
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  OOOHHH!
  Its a good flashback..
   
Loading...