Yaliyonikuta Ziwa Rukwa sitokaa niyasahau

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,759
Ilikuwa mwanzoni kabisa mwa mwaka 2000 nikiwa nyumbani pamoja na wazazi wangu katika mji mdogo wa tunduma karibu kabisa na shule ya msingi maporomoko.

Sitasahau wakati huo nilikuwa nikiishi na mama wa kambo baada ya kumpoteza mama yangu mzazi .maisha nyumbani yalibadilika ghafla na baba akawa ni mtu wa kulewa na kurudi usiku wa manane.

Ilikuwa akifika tu basi wote mtaamshwa kupigiwa makelele usiku kucha ,Mimi na wadogo zangu ambao wengine walikuwa wadogo kabisa, ilifika mahari tunalala njaa.

Yule mama wa kambo alibadilisha kabisa maisha na tabia za baba akawa ni mtu wa hovyo sana. Wanakula kilabuni wanarudi usiku Mimi nabaki napambana na wadogo wazangu na nilikuwa nataka kwenda chuo lakini Mzee kasema hawezi kupoteza pesa yake kunisomesha natakiwa nipambane mwenyewe.

Niliamua kujiongeza kufanya vibarua mchana jioni nikipata kitu napelekea wadogo zangu ndio hapo nilikutana na jamaa Mmoja anaitwa Alfred akanipa mchongo wa kwenda kuvua samaki ziwa rukwa.

Nilijichangachanga nikapata nauli nikawaaga wadogo zangu Kwa uchungu sana ilikuwa hakuna namna lazima nikapambane na Kwa vile jamaa alinipa matumaini ya kupata pesa nyingi Kwa muda mfupi nikaamini kabisa naenda kutoboa, tuliondoka Tunduma Kwa usafiri wa fuso kuelekea bonde la ziwa rukwa kupitia laela, Kalambanzite na usiku karibia Saa nne tukafanikiwa kufika Kijiji Cha Ilemba ambapo ndio mwisho wa gari.

Tukalala asubuhi mapema tukaanza kutembea Kwa mguu nakumbuka tuliamka Saa 12 mapema.

Kuendelea bonyeza kiungo hapo chini

Sehemu ya pili
Sehemu ya tatu
 
Ilikuwa mwanzoni kabisa mwa mwaka 2000 nikiwa nyumbani pamoja na wazazi wangu katika mji mdogo wa tunduma karibu kabisa na shule ya msingi maporomoko.

Sitasahau wakati huo nilikuwa nikiishi na mama wa kambo baada ya kumpoteza mama yangu mzazi .maisha nyumbani yalibadilika ghafla na baba akawa ni mtu wa kulewa na kurudi usiku wa manane.
Loh
 
Ilikuwa mwanzoni kabisa mwa mwaka 2000 nikiwa nyumbani pamoja na wazazi wangu katika mji mdogo wa tunduma karibu kabisa na shule ya msingi maporomoko.
Safari ya kuelekea ziwani ikaanza tukapita vijiji kadhaa ,.baada ya Saa nzima tukaingia nankanga Kijiji Cha mwisho kabla hujalifikia ziwa. Hiyo ilikuwa yapata Saa mbili hivi ,tulikatiza kwenye mapori yaliyoshona kweli kweli Kila muda nikawa nahisi tunakaribia kufika na jamaa ananipa Imani (mdogo wangu tunakaribia kufika .) Ilifika Saa Saba mchana jua limekuwa Kali Sana na lile bonde linajoto Kali Sana ,nikaanza kuhisi njaa Kali na kichefuchefu yule jamaa akanibebea mizigo yangu ,akaendelea kunihimiza kuwa karibia tunafika .mpaka inatimu Saa kumi na mbili ziwa silioni ni pori tu kiumweli nguvu ziliniisha nikaamua kukaa, jamaa kaanza kumaindi sana , ni hapo ndio nikagundua huyo jamaa ni mkali sana na anamaneno mabovu sana ,nikawa muwazi kwake kwamba hapa siwezi kuendelea .jamaa kaanza kufunguka huu msitu sio mzuri kwanza humu Kuna tembo hii ni hifadhi ya wanyama pori ,hatutaweza kutembea usiku tumekaribia sana we jikaze twende , du kusikia ni hifadhi Mzee nikanyanyuka msafari ukaendelea .

Kwa mbaali nikaanza kusikia sauti za watu na mziki ,ila jamaa alikuwa amenuna sana tukawa hatusemeshani Tena! Hofu ikaanza kuniingua juu ya mtu niliyesafiri nae kwenda nisikokujua. Baada ya dakika chache tukaingia Kambi Moja inaitwa lufufwe. Jamaa kaniambia bwana hapa hatujafika ila niombe chakura tule safari iendelee ! daa,! Nikamuuliza Kwani hatuwezi kulala tuondoke asubhui ?

Jamaa Kawa mkali ananijibu Kwa mkato tu lazima safari iendelee! !ashukuriwe mungu wavuvi hawana tabia za unyimi Kwa wageni walitukalimu sana Kwa kutupa unga na samaki wakutosha kabisa ,msosi ulikuwa tayari baada ya kumaliza kula tu hapo ilikuwa ni mwendo wa Saa nne usiku ,jamaa kaniambia pumzika kidogo nitakuja kukuamsha .kiukweli lile Kambi kulikuwa na watu wengi sana na starehe nyingi mno ,wanaishi nyumba za majani kuanzia chini mpaka juu lakini Kuna bar kubwa tu na wanakesha mpaka asubuhi .pale kulikuwa na wachaga kibao ,wangoni wasukuma yaani Kila kabila lilikuwa pale .kulikuwa machangudoa wakutosha kabisa Kuna jamaa kaniambia bhn Huku ni makimbilio usione umati huu .

Huku watu kuuana ni kawaida na hamna Cha kufanya ,walio wengi Huku ni wale wamekimbia Soo walikotoka ,wengi hapa ni majambazi wakubwa sana na walikotoka wanamakesi kibao ,machangudoa unao waona hapa ni wale wamechoka mjini ndio wanaokuja kumalizia mhula wao Huku! Kiukweli kule Mahali hakuna anayejari! nililala kidogo tu ilipofika Saa nane usiku jamaa kaja kalewa kinoma kaanza kunikurupusha oyaaaa tutambae ! Kuangalia muda ni Saa nane za usiku , nikagoma maana nilianza kuhisi dalili za hatari sana. Kaninong'oneza pale hatutembei Kwa mguu nimepata mtumbwi tunapita ziwani ! Nikamwambia Sasa mbona usiku !

Jamaa kaanza kunyanyua mizigo anapeleka ufukweni ambako kulikuwa na mitumbwi mingi Sana ya watu! Kilichonishangaza alikuwa ananyata kutembea kama mtu asiyetaka mtu amuone! Akaja mara ya pili kunifuata oyaaaa amka ! Kwa sauti ya chini sana nilivyoamka kanipa ishara ya kunyata !! Nikawa na Mimi nanyata kuelekea ufukweni bila kujua Kwanini !nikaona mtumbwi mkubwa jamaa kashapakia mizigo kausumia majini na kuniamuru niingie safari ianze ! Nikaogopa sana Kwa sababu jamaa alikuwa kalewa na ziwa lilikuwa na mawimbi ya wastani ila sio ya kuyapuuza! Nikawaza moyoni tunaenda wapi ?

Tutafika mtu kalewa namna hii? Mimi sijui kogelea vipi tukiangukia majini hofu ikazidi kuniingia! Jamaa alipiga Kasia mwendo wa nusu akaamua kunichana (oyaa mwanangu Huku wanaokuja ni wagumu nakuona kama mtoto wa mama vile ,sikia nikwambie huu mtumbwi Mimi nimeiba Ili tukafanyie kazi huko tunakoenda hata sijui ni wanani.hapo kichwa kikaanza kuwaka moto na tayari kulishaanza kupambazuka .Kila tunaposegea naona viboko wametapakaa Kila sehemu lakini jamaa anapiga makasia tu hajali Wala nini ! Nilipata hofu sana nikajua kumbe huyu jamaa ni mwizi ,sa itakuwaje tukikamatwa ?

Kadiri tulivyokuwa tunaendelea kwenda mbele nikawa nayazoea maji hofu ikawa inapungua .nilishangaa kuona tunapishana na mamba kama kambale tu ! Lile ziwa nadhani litakuwa linaongoza afrika Kwa mamba wengi. Tulifika sehemu tulikotoka hakuonekani tunakoenda pia hakuonekani ,na jamaa alikuwa anabadilika Kila dakika anakuwa mkali mkali sana ! Na Mimi nilikuwa simjui vizuri kiviile ! Ndani ya mtumbwi jamaa alikuwa anavuta kitu ambacho nilihisi ni tumbaku lakini kumbe hapana ilikuwa bangi .,nakwavile Mimi nilikuwa mdogo nikiri kwamba nilikuwa sijawahi kuiona bangi live.

Kwa hiyo nilikuwa siijui, nilipogeuka nyuma nikaona mitumbwi mitatu inakuja Kwa Kasi sana .tukajua ni wavuvi muda huu ndio wanaingia kutafuta mtumbwi . Badae nikaona boti inakuja Kwa Kasi ajabu .dakika jamaa Hawa hapa ,hakuna kuuliza wakaanza kutushushia kipigo Cha mbwa na tuko katikati ya ziwa, tulipigwa sana na wakawa wanatulazimisha tushuke wachukue mtumbwi wao , oyaaaa shukeni mamba wananjaa hawajala mda mrefu shukaaa, Kuna jamaa alikuwa na sauti nzito na alikuwa mkali sana .

Akiwa amenikunja akawa ananinyanyua Ili anitupe kwenye maji, mwili mzima navuja damu wanatumia maKasia kupiga kichwani nikamtazama yule jamaa tulikuwa nae kashapasuliwa na kisu kichwani amekatwa kidole gumba analia kama mtoto , nyinyi ni !wezi mnatuibia Kila siku lakini Leo arobain zimefika ! Kwa jinsi nilivyopigwa fahamu nilikuwa Sina kabisa nikahisi hapa tayari nakufa, na wale jamaa walikuwa na roho mbaya sana! Oyaa tunawachewesha ,,Hawa tuwavue nguo tuwatupe mbona mnawalegezea haya vueni nguo na Kila asali Sala ya mwisho, alifoka jamaa Mmoja Kwa sauti nzito sana.....
 
Back
Top Bottom