illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Baada ya shughuli nzito za ujenzi wa taifa nikaona nitafute sehemu ya kujipongeza, dodoma ni mgeni kidogo hivyo nikatafuta tax nikamueleza dereva tax nikampa specifications ya sehemu nayo penda kupelekwa akaonekana amenielewa basi akanipeleka maisha club.
Binafsi situmii vileo ila napenda muziki kucheza na kujumuika kweli bwana nikafika nikakuta vijana kwa wazee wanafurahia maisha nami nikajumuika nao mpaka ilipofika mida ya usiku mkubwa nikaona niende kupumzika kwa muda nilookaa mule na kucheza mziki na lile giza giza la mule ndani ramani ikanipotea nikaanza kuutafuta mlango wa kutokea nikauona mlango karibu yangu wakati naukaribia ili nishike kitasa nikapigwa ngumi ya tumbo moja matata sana ni wale mabaunsa walinzi wa club nikamuuliza nini tena bila majibu akanichukua akanisukuma, pale aliponisukumia kulikuwa na mlango mwingine nikawa nashika kitasa ili niufungue pengine nitoke nje nikapigwa tena ngumi nyingine..
Sasa uvumilivu ukanishinda nikamwambia wewe una kichaa mbona unanipiga bila sababu halafu hutoi maelezo akaniambia samahani nilijua umelewa na ule mlango wa kwanza uliokuwa una ufungua ni ofisi na ule wa pili pia namshukuru Mungu nimepitia kidogo majugoruu pia nina uwelewa mkubwa wa temper management nikamwambia nimekusamehe ila mwambie bosi wenu aweke alama za maelekezo kama tuonavyo sehemu zingine mfano exit/ kutoka, nilikuwa na mpango wa kuchukua yale mambo yetu yaleee pale nje du lakini huyo baunsa akaniharibia mood kabisa.
Nimemaliza