Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,951
- 146,217
Huyo jamaa kakutana na baunsa,kwahiyo hapo hata ukiwa na gang haisaidii maana wale mabaunsa kama Maisha club wapo wengi sana.Kama unaenda na gang lako labda kujilinda na gang zingine.
Gang langu lina ma baunsa pia.
Naweza kuingia sehemu Dar na Chuche or a Chuche type mabaunsa wote wanamzimikia kama wamemuona Schwarzenneger, na kama humjui unataka kuleta fujo hapo ndipo utakapojua ladha ya nyongo yako mwenyewe.
Tusha roll na wabeba vyuma wa Upanga tangu enzi za Bonny Luv anadandia mabasi.
Au kama vipi naenda boogie letu wenyewe, mabaunsa wa mlangoni mabaunsa wetu wanaonyeshwa kabisa huyu mtu wetu, mstaarabu, kashuka, hajazoea tabu za kifala.
Hao mabaunsa wa hapo Shoppers tu unaambiwa baada ya kuni pat down wakati naingia, nilivyotoka mmoja ananitangazia shida (jamaa sijui kanusa cologne kajua mchizi kashuka au vipi).
Ananitangazia shida, huku wenzake wanamuua.
Basi na mie kwa kuwa zungu la roho, halafu hela za madafu zilikuwa zinanichafulia mfuko wangu, halafu kuanzia kiingilio mpaka vinywaji madogo wamenikataza kutumia hela (wenyewe wanasema "your money is not good here") nikatoa 10,000 na kumuachia.
Sasa baunsa kama huyo ukija siku nyingine tena unafikiri anaweza kukufanyia fujo? Ndiyo kwanza atakuelekeza mlango wa VIP.