Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru: Kuapishwa kwa Dr. Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania

Katka tizama tizama yangu nimeona uwanja wa taifa umejaa nguo zenye nembo ya ccm badala ya taifa
Hii inaashiria nn ,
anaye apishwa ni kipenz cha wana ccm .
Wananchi wanaipenda sana ccm kuliko taifa
Au huyu ni raisi wa ccm???
 
Kuanzia saa tano kasoro kumi na tatu mpaka saa tano kasoro kumi, nchi ilikuwa haina rais. Hii ni baada ya bendera ya rais kushushwa mpaka Magufuli alipomaliza kuapa na kusaini kiapo chake cha urais.
 
Bado yale majimbo mawili ya upaleni, Ndesamburo ana kazi na nyinyi asipowata mahakamani mjiandae 2020 ccm inafutwa rasmi mkoa wa Kilimanjaro maana hampaswi kuwa hata na mbunge mmoja kule kwa jinsi msivyo na adabu kwa wakaskazini.

Huo ndio ukabila sasa, kwa nini ccm ifutwe Kilimanjaro!! Nyie hamkuwa na nia nzuri na nchi hii.
 
Jana katika kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na BBC, msemaji wa CUF - Jussa alikaririwa akisema Maalim Seif hajapokea mwaliko wa kuhidhuria kuapishwa kwa Dr. Magufuli. Hii ilikuwa baada ya Mallim kukutana na JK huko ikulu. Kama kweli Maalim ambaye ni Makamu wa Rais wa ZNZ hajakaribishwa, CCM imechemsha. Haijengi bali inazidi kuchochea moto ambao unafukuta huko visiwani.
 
Kuna memo Jk amemwandikia Magufuli hlf akampa bodygurd ampe, sasa sijui huyu kamwambia nini. Isije kuwa anamdrive
 
Haaaaa walisema ni ICJ mkuu
Kwamba na wewe unaamini kitu ambacho hata mimi goigoi wa sheria najuwa Tume ikishatangaza matokeo ya Urais hayahojiwi popote pale, je mabingwa wa sheria kama kina Kibatala na Tundu Lisu wawe hawalijui hili? Watanzania tuna tatizo kubwa sana ni serious tunahitaji consultant kutoka nje.
 
Mkuu, Maalim Seif ana kofia mbili. Ni makamu wa kwanza wa Rais kule Zanzibar lakini pia ni kiongozi wa UKAWA. UKAWA wameweka msimamo wa kutoshiriki sherehe hizi za kuapishwa Magufuli. Ulitaka Maalim Seif apingane nao?
 
Back
Top Bottom