Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru: Kuapishwa kwa Dr. Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania

wabungenjaa

wabungenjaa

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
1,783
1,225

Ndugu mtanzania. Leo ni siku ya kihistoria katika nchi yetu ambapo rais mteule John Joseph Magufuli ataapishwa na kukabidhiwa Nchi rasmi.

Maandalizi yote muhimu yamekamilika.

Fuatilia uzi huu kwa live updates mwanzo mwisho.
Tukio hili la aina yake litarushwa mubashara na Tbc1,star tv,channel ten,Azam tv na clouds tv pamoja radio mbalimbali ikiwemo tbc fm.

Stay updated. Stay tuned

*******updates********

- Wageni mbalimbali wanaendelea kuwasili hapa uwanjani.

- Wameingia marais wastaafu akiwemo Benjamin Mkapa,Ally Hassan Mwinyi na wake zao,mawaziri wakuu wastaafu Msuya na wengineo,Jaji Augustino Ramadhan na sasa jaji mkuu Othman Chande anaingia na ndio atamuapisha rais mteule.

- Marais saba wa nchi mbalimbali wanahudhuria tukio hili. Pia waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga yupo

- Wapo mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa jumuiya za kimataifa na mashiriki ya UN.

- Spika wa bunge Anne Makinda na naibu spika Job Ndugai wamo.

- Rais wa Zanzibar na delegation yote ya Zanzibar akiwemo Pandu Ameir Kificho wamehudhuria.

- Watu ni wengi kweli kweli.RAIS MTEULE KATIKA KILA TUKIO MUHIMU MVUA ILINYESHA IKIWEMO LEO. ISHARA YA BARAKA NA UTAWALA HALALI WA RIDHAA YA WANANCHI.

- Vikosi vya majeshi ya wananchi ya tanzania viko tayari kwa gwaride maalum.

- Wabunge wateule wa Jamhuri ya Muungano wameshaketi tayari.

- Jaji Mkuu Othman Chande ndio anawasili sasa hivi.

- Bendera ya Rais wa sasa itashushwa na kuashiria ukomo wa serikali ya awamu ya nne na Rais wa awamu ya tano atakapoapishwa bendera ya taifa itapandishwa.

- Anaingia mke wa Rais Mteule Mama Janet Magufuli

- Wapo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa

- Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amewasili hivi punde.

- Rais Jakob Zuma wa Afrika Kusini pia naye amefika.

-Maandamano rasmi ya kuelekea Jukwaa Maalum la Kuapishwa Rais mteule yataongozwa na Jaji Mkuu,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu Mkuu Kiongozi.

- Tukio linalofuata ataingia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

- Rais mteule Dr. Magufuli ameelekea jukwaa maalum la kiapo.

- Rais anakagua gwaride kwa mara ya mwisho kisha ataenda jukwaa la kuapisha na mizinga 21 inapigwa, kisha bendera ya serikali ya awamu ya nne itashushwa.

-Wimbo wa taifa unaimbwa.

Bendera ya serikali ya awamu ya nne inashushwa kuashiria mwisho wa utawala wa awamu ya nne.


TUKIO LA KUAPISHWA MAGUFULI LINAENDELEA.

- Rais anayemaliza muda wake akiwa na makamu wake wanasaini kukubali kwao kukaa benchi na kukabidhi nchi rasmi kwa Rais wa Awamu ya Tano.


***UPDATES***

- Rais wa awamu ya Tano na makamu wake wameshakula kiapo, sasa ni sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa dini.

****updates*****

Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mh. Magufuli anapigiwa mizinga 21 ya Utiifu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)

Rais John P Magufuli anakagua gwaride la Tanzania likiwa katika umbo la ALFA kuashiria mwanzo wa Serikali Mpya. Rais amemaliza kukagua gwaride na sasa amepanda jukwaa kuu


******Updates****

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli kwa ufupi

Anawashukuru wote waliojitokeza kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake,anashukuru tendo la kubadilishana madaraka kwa njia ya amani na anasema anatambua changamoto na majaribu yaliyopo katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Anawapongeza wapinzani walioonyesha ushindani na kuwaomba ushirikiano. Kwamba uchaguzi umepita sasa turudi katika umoja wetu tujenge taifa.

Sasa ni kazi tu.

Anaishukuru tume ya uchaguzi na wote waliofanikisha uchaguzi.

Anawapongeza jeshi kwa ukakamavu walioonesha kwenye gwaride na kwamba anafarijika na kuona ataongoza jeshi lenye afya.

Anawashukuru marais wastaafu mawaziri wakuu wastaafu na watanzania wote waliompa ushirikiano na kumuamini.

Anasema sio siku ya kutoa hotuba. Uchaguzi umekwisha. Rais ni John Magufuli. Wapinzani tufanye kazi sasa. Naenda kufanya kazi. Tunaenda kufanya kazi. Tupeni ushirikiano
 
Last edited by a moderator:
Chachu Ombara

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,321
2,000
Picha na video kutoka Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Tanzania


 

Attachments

 • File size
  75.4 KB
  Views
  11,546
 • File size
  65.3 KB
  Views
  11,411
 • File size
  66.3 KB
  Views
  11,271
 • File size
  62.4 KB
  Views
  11,185
 • File size
  101.7 KB
  Views
  11,187
 • File size
  97.9 KB
  Views
  10,987
 • File size
  86.8 KB
  Views
  10,947
 • File size
  90.4 KB
  Views
  1,118
 • File size
  79.2 KB
  Views
  10,791
 • File size
  72.7 KB
  Views
  11,544
 • File size
  82.4 KB
  Views
  11,526
 • File size
  77.5 KB
  Views
  11,408
 • File size
  74.2 KB
  Views
  10,584
 • File size
  40.6 KB
  Views
  11,443
 • File size
  72.8 KB
  Views
  10,374
 • File size
  75.9 KB
  Views
  11,158
 • File size
  80.3 KB
  Views
  11,121
 • File size
  56.7 KB
  Views
  10,281
 • File size
  81.4 KB
  Views
  11,153
 • File size
  79.5 KB
  Views
  10,268
 • File size
  92.7 KB
  Views
  11,105
 • File size
  89.3 KB
  Views
  10,222
 • File size
  98.3 KB
  Views
  10,200
Last edited by a moderator:
Chachu Ombara

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,321
2,000
Picha na video kutoka Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Tanzania

 

Attachments

 • File size
  97.2 KB
  Views
  10,595
 • File size
  100 KB
  Views
  9,811
 • File size
  89.2 KB
  Views
  10,533
 • File size
  68.8 KB
  Views
  9,704
 • File size
  86.6 KB
  Views
  10,603
 • File size
  57.3 KB
  Views
  9,634
 • File size
  91.5 KB
  Views
  10,496
 • File size
  87.7 KB
  Views
  9,564
 • File size
  66.3 KB
  Views
  9,593
 • File size
  29.8 KB
  Views
  9,613
 • File size
  60.9 KB
  Views
  9,738
 • File size
  63.7 KB
  Views
  9,541
 • File size
  54 KB
  Views
  9,530
 • File size
  61.7 KB
  Views
  9,400
 • File size
  69 KB
  Views
  9,624
 • File size
  71.3 KB
  Views
  10,024
 • File size
  72.1 KB
  Views
  11,594
 • File size
  64.6 KB
  Views
  10,216
 • File size
  70.4 KB
  Views
  9,926
 • File size
  69.2 KB
  Views
  9,707
 • File size
  66.9 KB
  Views
  11,297
C

Chupaku

JF-Expert Member
Oct 15, 2008
1,092
1,500
Wakuu,imechelewa sana kuanzisha uzi huu. Where's the excitement?
 
luqmand

luqmand

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
219
0
Nimekupata mkuu wabungenjaa
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,268
2,000
Haimaanishi chochote.

Mvua kila mwaka zinanyesha na zina msimu wake.

Na sasa hivi ni msimu wa mvua za vuli.

Hivyo siku ya leo kunyesha mvua hakuashirii chochote kile kuhusu huyo jamaa.

Bali kunyesha kwake kuna uhusiano wa moja kwa moja na msimu uliopo.
 
M

mangola

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
681
195
Vile hisia zako zitakutuma ndo hivyo hivyo inaweza kuwa.
 
Naibili

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,683
1,225
Mfyuuu sherehe za CCM
 
JAPUONY

JAPUONY

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
378
195
Kwa Mila na Desturi za Kiafrika, kunyesha kwa mvua wakati wa shughuli kama hii ya leo ya kumuapisha Mhe. John P. Magufuli, ni ishara na dalili njema kwa kiongozi huyo.

Wenye hisia za kisiasa na wale wenye MAHABA hawatokubaliana na hili.
 
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,457
2,000
Leo ndio ile siku ya waliovimba kupasuka
 
 • Thanks
Reactions: nao
wabungenjaa

wabungenjaa

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
1,783
1,225
Duh .. wabungenjaa ...hizi ID za JF bana ....
Ilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa wabunge wa bunge maalum la katiba ambao siku ya kwanza tu kuingia mjengoni walianza na hoja ya kudai kuongezewa posho
 
Last edited by a moderator:
Kingmairo

Kingmairo

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
4,948
2,000
Ukiruhusu hisia ziendeshe mwili, akili huganda.
 
yaramazlik

yaramazlik

Member
Apr 7, 2012
86
225
Rekebisha heading....sema rais wa ccm...nenda taifa ndio utakubali ninayoyasema ...maana utakutana na kijani na njano uwanja mzima
Bendera ya taifa unaijua vizuri?
 
wabungenjaa

wabungenjaa

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
1,783
1,225
Rekebisha heading....sema rais wa ccm...nenda taifa ndio utakubali ninayoyasema ...maana utakutana na kijani na njano uwanja mzima
Moja ya walionuna kumbe mko hapa
 
GAUTAMA

GAUTAMA

JF-Expert Member
Aug 5, 2014
1,094
1,500
Duuh, WaAfrika wanapenda ulozi
 
Top Bottom