Full 8
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 313
- 271
Wiki hii tunatarajia kushuhudia makutano wa wakuu wa nchi za shirikisho la nchi za mashariki mwa Afrika.
Kati ya masuala yanayotegemewa kushika hatamu ni:-
1. Mswada wa EPA(EU)
2. Uanachama wa Somalia
3. Zuio la uingizaji wa mitumba toka magharibi(USA) n.k
4. Ujenzi wa reli, barabara na bomba la mafuta ghafi katika nchi hizi.
kilichopelekea kuanzisha uzi huu ni shinikizo la USA na EU katika baadhi ya ajenda zenye maslahi kwao na kiduchu kwa EAC. Tumeshuhudia USA ikizionya nchi hizi kwa hatua watakayochukua kuhusu zuio la kuingiza mitumba toka Marekani kwani inaweza pelekea kuathiri biashara baina ya nchi husika ukizingatia kwamba kuna mkataba wa AGOA.
Pia katika hili tumeona baadhi ya nchi, ikiwemo Kenya ikijitoa na nyingine zikionesha nia ya kumfuata Kenya kwa uamuzi huo.
Ajenda ya EPA pia itakuwa na vuta nikuvute hasa kwa Tanzania ambayo inaona itapelekea kuua viwanda vyetu vya ndani kwani kutakua na uingizwaji mkubwa wa bidhaa kutoka EU nyingi zikiwa za kiwango hafifu.
Wakuu hebu tujadili matokeo ya matamko toka magharibi katika maamuzi ya viongozi wetu hawa.
Nawasilisha.