Yaliyojiri Uganda kwenye Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na maazimio ya viongozi hawa

Full 8

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
302
250
Wiki hii tunatarajia kushuhudia makutano wa wakuu wa nchi za shirikisho la nchi za mashariki mwa Afrika.
Kati ya masuala yanayotegemewa kushika hatamu ni:-
1. Mswada wa EPA(EU)
2. Uanachama wa Somalia
3. Zuio la uingizaji wa mitumba toka magharibi(USA) n.k
4. Ujenzi wa reli, barabara na bomba la mafuta ghafi katika nchi hizi.

kilichopelekea kuanzisha uzi huu ni shinikizo la USA na EU katika baadhi ya ajenda zenye maslahi kwao na kiduchu kwa EAC. Tumeshuhudia USA ikizionya nchi hizi kwa hatua watakayochukua kuhusu zuio la kuingiza mitumba toka Marekani kwani inaweza pelekea kuathiri biashara baina ya nchi husika ukizingatia kwamba kuna mkataba wa AGOA.
Pia katika hili tumeona baadhi ya nchi, ikiwemo Kenya ikijitoa na nyingine zikionesha nia ya kumfuata Kenya kwa uamuzi huo.

Ajenda ya EPA pia itakuwa na vuta nikuvute hasa kwa Tanzania ambayo inaona itapelekea kuua viwanda vyetu vya ndani kwani kutakua na uingizwaji mkubwa wa bidhaa kutoka EU nyingi zikiwa za kiwango hafifu.

Wakuu hebu tujadili matokeo ya matamko toka magharibi katika maamuzi ya viongozi wetu hawa.

Nawasilisha.
 
Massanda OMtima Massanda

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
1,059
2,000

Nchi za Kenya, Tanzania na Uganda kwa muda mrefu zimekuwa na viwanda vya nguo (ingawa viwanda vya Tanzania vilihujumiwa), lakini bila sera maalum ya masoko ya ndani na nje! Kama zitakuwa na nia njema ya kulinda viwanda vyake vya nguo, sioni tishio lolote kutokana na kupiga marufuku mitumba na kujiunga na EPA!
 
Mkuu, kumbuka EPA wanatafuta soko la bidhaa zao, na pia kwa gharama za uzalishaji wao wanazalisha kwa gharama ndogo kulinganisha na sisi;hivyo bidhaa zao zitakuwa nafuu kuliko za ndani, hapo ndipo kiama cha viwanda vyetu kitakapowadia.
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
3,917
2,000
Yaani wao wanaona mitumba ya nguo tu.. Wanasahau kuna mitumba ya kila kitu kwa sasa.. Hadi viungo vya miili ya binadamu..!!
Wakiamua kupambana wapambane na mitumba yote..!!
 
Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,287
2,000
Mkuu, kumbuka EPA wanatafuta soko la bidhaa zao, na pia kwa gharama za uzalishaji wao wanazalisha kwa gharama ndogo kulinganisha na sisi;hivyo bidhaa zao zitakuwa nafuu kuliko za ndani, hapo ndipo kiama cha viwanda vyetu kitakapowadia.
Sisi tuna viwanda gani? Wacha vife tu kama hawawezi kushusha bei ya bidhaa zao!
 
Lekakui

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,448
1,225
Mkuu, kumbuka EPA wanatafuta soko la bidhaa zao, na pia kwa gharama za uzalishaji wao wanazalisha kwa gharama ndogo kulinganisha na sisi;hivyo bidhaa zao zitakuwa nafuu kuliko za ndani, hapo ndipo kiama cha viwanda vyetu kitakapowadia.
Kaka nadhani hapo haujaelewa kinachotakiwa,hapa ni kwamba kama watakubalina then kitakachofuata ni kusubsidize ili bei ziwe chini na quality iwe sawa na hizo zinazotoka huko kwa mabwenyenye,na sheria zinawekwa kwamba ni marufuku kununua nguo za nje,India walifanya hivyo wakati wa mahatma gadhi,na waliifanya hadharani walichukua nguo zote za mabwenyenye wakazichoma,na baada ya hapo ikapitishwa sheria ni marufuku kununua vitu vya nje,kuanzia nguo magari etc,leo hii India inasifika kwa kutengeneza nguo na wanauza nje kwa hao hao mabwenyewe,so ni strategy ya kuamua unachotaka,still we have time,na na uhakika huyu muheshimiwa wetu yuko serious akisema kitu ni kweli kinafanyika so wach this space,in the next 6 years utaniambia
 
Full 8

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
302
250
Sisi tuna viwanda gani? Wacha vife tu kama hawawezi kushusha bei ya bidhaa zao!
mkuu, kumbuka vyerehani viwili tayari ni kiwanda. ha ha haa japo tunabeza ila ukweli utabaki kuwa ni kiwanda maana nguo inashonwa na inavaliwa. kuna achali zinazalishwa na mikate pia, ukiingia super market zimejaa bidhaa kutoka nje ambazo zitazidi kujaa mara baada ya kusaini mkataba huu, sijui itakuwaje.
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
30,344
2,000
Wakuu, kama mnavyojua leo ni mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki.

Mkutano unaoneshwa Live TBC1 ambapo wakuu wote wa nchi za A.Mashariki wamehudhuria.

Mkutano bado haujaanza lakini Rais John Pombe Magufuli pia amehudhuria.

Kwa sasa naona watoto wanatumbuiza hapa..

Namwona salva kiri wa sudan kusini, Paul kagame, museveni, uhuru kenyata, nkurunzinza pia..

Sijajua lugha gani itatumika katika mkutano huu.

[HASHTAG]#staytuned[/HASHTAG]
Umekaa kimajungu majungu mno!
 
Full 8

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
302
250
Kaka nadhani hapo haujaelewa kinachotakiwa,hapa ni kwamba kama watakubalina then kitakachofuata ni kusubsidize ili bei ziwe chini na quality iwe sawa na hizo zinazotoka huko kwa mabwenyenye,na sheria zinawekwa kwamba ni marufuku kununua nguo za nje,India walifanya hivyo wakati wa mahatma gadhi,na waliifanya hadharani walichukua nguo zote za mabwenyenye wakazichoma,na baada ya hapo ikapitishwa sheria ni marufuku kununua vitu vya nje,kuanzia nguo magari etc,leo hii India inasifika kwa kutengeneza nguo na wanauza nje kwa hao hao mabwenyewe,so ni strategy ya kuamua unachotaka,still we have time,na na uhakika huyu muheshimiwa wetu yuko serious akisema kitu ni kweli kinafanyika so wach this space,in the next 6 years utaniambia
Mkuu nakupata vyema kabisa, labda ungefafanua kidogo hili jambo.
1. Kwa uchumi wetu dhaifu sijui kama tunaweza subside wajasiliamali wetu ili waweze kuzalisha kwa bei nafuu ukizingatia gharama kubwa inatajwa kuwa ni UMEME(tunao wa mgao) na USAFIRISHAJI wa malighafi na bidhaa(miundombinu duni).
2. Nadhani mkataba utatutaka kununua kutoka katika soko la EU peke yake. hivyo ule wigo wa kutunga sheria kama hizo za India sijui kama upo.
Hivi majuzi USA wametoa pendekezo kuwa kuzuia mitumba toka USA si suluhu ya kulinda viwanda vya ndani, bali nchi ihimize watu wa kipato cha kati ndo wanunue zaidi nguo tunazozalisha ndani ili kuhakikisha soko la bidhaa hii.
 
likandambwasada

JF-Expert Member
May 27, 2015
5,424
2,000
johnthebaptist MAJUNGU KIVIP MKUU, NILITEGEMEA WATAONGEA KISWAHLI ILI NIWEZE KUUPDATE UZI, LAKN WANAONGEA INGLISHI

Maharo WHAT IS BAVICHA? NONSENSE

General Mangi WAMEWEKA KIZUNGU, NAOMBA Moderator HUU UZI UJE KUUPDATE KWA SABABU MIMI LUGHA YA MALIKIA HAIPANDI HATA KIDOGO, NAJUA KIMAKONDE, KINGONI, KIYAO NA KINYAMWEZI, BILA KUSAHAU KISWAHILI.
 
Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
9,925
2,000
Mkuu, kumbuka EPA wanatafuta soko la bidhaa zao, na pia kwa gharama za uzalishaji wao wanazalisha kwa gharama ndogo kulinganisha na sisi;hivyo bidhaa zao zitakuwa nafuu kuliko za ndani, hapo ndipo kiama cha viwanda vyetu kitakapowadia.
Si itakuwa heri kwa mtanzania masikini! Where you can get milk for cheap,there ain't no need to keep the cow! To hell with "Uzalendo"
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,799
2,000
Wakuu, kama mnavyojua leo ni mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki.

Mkutano unaoneshwa Live TBC1 ambapo wakuu wote wa nchi za A.Mashariki wamehudhuria.

Mkutano bado haujaanza lakini Rais John Pombe Magufuli pia amehudhuria.

Kwa sasa naona watoto wanatumbuiza hapa..

Namwona salva kiri wa sudan kusini, Paul kagame, museveni, uhuru kenyata, nkurunzinza pia..

Sijajua lugha gani itatumika katika mkutano huu.

[HASHTAG]#staytuned[/HASHTAG]
Madikteta wamekutana na Kenyatta
 
Top Bottom