Yaliyojiri Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 30 wa Mashirika ya Utangazaji ya Umma Kusini mwa Afrika (SABA), Oktoba 10, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Fuatilia yanayojiri kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 30 wa Mashirika ya Utangazaji ya Umma Kusini mwa Afrika, leo Okotoba 10, 2023 ambapo Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ni mgeni Rasmi.


AYUB RIOBA, MKURUGENZI WA TBC
SABA (Southern Africa Broadcasting Association) tulianza kama vyombo vya utangazaji vya umma vilivyopo kusini mwa Afrika, lakini sasa huvi tunavyozungumza ni taasisi ambayo imeshakaribisha vyombo vingine kwasababu shughuli tunanzozifanya si mikutano tu au vikao vya bodi, ni pamoja na makongamano, warsha, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kupata mafunzo mbalimbali yanayotusaidia kuboresha kazi tunayoifanya.

Katika mkutano huu tutakuwa na mafunzo mbalimbali, tutabadilishana uzoefu na tutaangalia namna gani tuviwezeshe vyombo vyetu kuendelea kuwepo kwa sababu vyombo hivi ni muhimu. Kuna watu wanaweza kudhani kwamba vyombo vya habari vya umma, kwa mfano, havina maana au vimepitwa na wakati lakini ukweli ni kwamba hakuna wakati ambapo vyombo hivi vina umuhimu mkubwa, hasa kwetu sisi Waafrika, kama sasa ambapo teknolojia ya usafirishaji wa taarifa kwa njia ya kidijiti imekuwa sana na inafikia watu wengi.

STANLEY BENJAMIN SIMILO, RAIS WA SABA
Kama SABA, sisi ni sehemu muhimu sana katika biashara yetu kwa sababu tunajaribu kuhakikisha kwamba kusambazwa kwa habari katika eneo hili na Afrika kwa ujumla unashughulikiwa kwa njia ambayo itahakikisha kwamba tunatoa hadithi za Kiafrika za kweli. Pia, tunapanua hili hadi sehemu nyingine za Afrika, tunaye ndugu yetu Arthur Asiimwe - yeye anawakilisha Africa Union of Broadcasting (AUB) - ambayo ni taasisi ya bara la Afrika kuhusiana na kile tunachojaribu kufanya.

Kama SABA, tunaona kwamba hatuwezi kubaki nyuma katika suala la teknolojia inayotolewa leo. Kwa sababu leo simu za mkononi ni sehemu muhimu ya maisha ya kila mtu. Sasa, kama watoa matangazo wa umma, ikiwa hatufanyi mabadiliko katika kuelewa teknolojia hii inavyoleta, tunaweza kutengwa kwa kiasi kikubwa kati yetu na hadhira yetu. Kwa hiyo, ni muhimu kwamba tunajibu wito wa kusema tunakwenda wapi, tunafanya nini, na tunawezaje kufanya hivyo.

Kuhusu sisi watoa matangazo wa umma tukikutana chini ya SABA, tunasema kuna hadithi nzuri za kusimulia kuhusu Afrika. Lakini tunataka sisi wenyewe kuwa waandishi wa hadithi hizi, si vinginevyo. Kwa sababu ikiwa hilo halitotokea, basi hadithi zitakuwa na maana tofauti kabisa. Mpaka sasa, tumefanikiwa kuandaa programu ya habari inayoitwa "I'm SADC" ambayo inasambazwa katika eneo lote. Jambo muhimu sana, katika sehemu hii ya programu yetu, inaendeshwa kwa Kiswahili, na kwa hili nataka kumshukuru Dk. Chacha (Ayub Rioba).

Katika kipindi cha siku mbili zijazo, tutajadili mambo mbalimbali ambayo tungependa kujadili kama kikundi, kama watu. Hivi karibuni, habari za uwongo zimekuwa jambo kubwa sana. Kama warusha matangazo wa umma, tunahitaji kuelewa na kuwa na uwezo wa kutambua hii na kushughulikia whenever inapotokea.

Mwelekeo wetu ni wazi kwamba tunataka kuchangia kujenga Afrika bora kupitia huduma zetu za utangazaji.

KUNDO ANDREA MATTHEW, NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI
Sekta ya habari, mawasiliano na TEHAMA ni nyenzo muhimu katika uchumi wa kidigitali. Kwa kutambua hilo, sisi ni wasimamizi wa sekta tunasisistiza maendeleo ya amtumizi ya TEHAMA hasa kaytika kuhakikisha kuwa tunafikia malengo ya mapinduzi ya ukuaji wa uchumi. Vyombo vya habari vina jukumu la kusukuma ajenda hii ambayo imekuwa ikisisitizwa katika mikutano hii ya SABA kwa kipindi cha miaka saba.

Mh. Rais, Tasnia ya habari ni nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi, uhifadhi wa mila na utamaduni wa wananchi wa Afrika. Jitihada mahsusi lazima zifanyike kupitia vyombo vyetu vya utangazaji kwa umma, vyenye jukumu la kutekeleza hayo. Niwaombe washiriki wote kuwa maudhui yote yanayoandaliwa na vyombo vya habari vya umma yazingatie mtazamo wa kuijenga jamii uwezo wa kujitambua nan a kujivunia Uafrika wao.

Wakati TEHAMA inaingia nchini, watu wengi sana walihofia kupoteza kazi. Na hata sasa, kutokana na emerging technology, tunafikiria kwama AI itakuja kuchukuwa kazi za watu… lakini tunasema kwamba katika mawanda haya na katika kipindi cha digital transformation, imefikia wakati ambapo teknolojia hatuwezi kuikwepa. Imefikia kipindi ambacho uwe unataka au hutaki, teknolojia ipo tu. Kwhiyo, tunachotakiwa kufanya kama taifa na kama Afrika, it’s time for Africa to leapfrog.

Kitu tunachotaiwa kufanya ni ku-unlock mindset ili tukubali kuendana na hali halisi. Lakini pia it’s time to make sure kwamba hakuna anayeachwa nyuma katika zama hizi. Ni kipindi ambacho kupitia mikutano na makongamano haya, tunaweza kuwa na lugha moja, tunaweza kukaa pamoja na kufanya benchmarking. Itatusaidia sana kutembea kama taifa na kama Afrika kwa umoja wetu bila kufikiria kwamba tuwe tunatembea mmoja mmoja.

DKT. HUSSEIN ALI MWINYI, RAIS WA ZANZIBAR
Mada mlioichagua mmeileta wakati muafaka ambako dunia ipo katika mapinduzi ya nne ya viwanda inayochagizwa na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Katika muktadha hiuu, ili kwenda sambamba na mabadiliko haya, mashirika ya umma ya utangazaji ya nchi wanachama wa SABA na Afrika kwa ujumla hayana budi kubuni, kusimamia na kutekeleza mikakati Madhubuti inayopimka ya kuwezesha mashirika hayo kwenda sambamba na mabadiliko yanayojitokeza.

Tusipojipanga na kwenda na mabadiliko, wakati utatulazimisha kubadilika. Athari ya kusubiri kubadilishwa na wakati zinaweza kuwa hasi na pengine kufanya mashirika ya utangazaji ya umma kupoteza mvuto wa umma. Hivyo, napenda kutoa rai ya kuendelea kufanya uwekezaji katika mashirika yetu ya utangazaji kwa kuyawezesha kuwa na vitenfdea kazi vya kisasa vinavyoendana na maendeleo na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani.

Miongoni mwa wajibu wa serikali ni kuhakikisha uwepo wa huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa watu wake pamoja na kukuza uchumi endelevu na kupambana na umasikini. Kama nchi tumeweka dira ya kuweka mazingira wezeshi ambayo yatachochea na kukuza uchumi kwa kasi kwa kuwa na ushirikiano nan chi nyingine, kushirikisha sekta binafsi, pamoja na kuhakikisha uwekezaji katika sekta ya TEHAMA unaongezeka.

Msisitizo wa kukuza uchumi wa kidigitali na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano hautoiacha nyuma sekta ya utangazaji, hivyo mashirika yetu ya utangazaji TBC na ZBC nayo pia yanashirikishwa katika mpango huo wa nchi kwenye maendeleo ya TEHAMA na mchango wake katika ukuaji wa uchumi nchini kwetu kwa maendeleo endelevu.

Natumia fursa hii kuwakumbusha nafasi ya vyombo vya habari ikiwemo redio, televisheni na mitandao ya kijamii katika ukuaji wa kiuchumi, utengamano wa kitaifa pamoja na ustawi wa kiuchumi wan chi zetu hususan zilizopo kusini mwa bara la Afrika. Hivyo, hamna budi kuwa wabunifu na kuhakikisha kuwa sekta ya habari na utangazaji zinakuwa nyenzo za kutoa taarifa sahihi kwa wananchi kwani itasababisha utulivu na amani, na hivyo kuimarisha ushirikiano wa serikali na wananchi wake.

Sote ni mashahidi wan a namna vyombo vya utangazaji na habati, vikiwemo vyombo vya umma vya utangazaji vya nchi zetu za Afrika, vilivyo na umuhimu mkubwa katika kutoa taarifa zinazochangia maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kujenga amani, utulivu, usalama na utengamano wa nchi zetu.

Pia nimejulishwa kuwa mtajadili mambo mengi, napenda kuwasihi mshiriki mijadala hiyo kwa hoja zitakazosaidia kuweka mbele maslahi ya watu na nafasi ya bara la Afrika katika kuandaa na kutangaza zinazolenga kuleta maendeleo kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kiutengamano wa jamii. Huu ni wajibu wetu sote na kwenu vyombo vya habari vya utangazaji wa umma mnapaswa kusimamia mijandala yenye mawanda hayo.

Tambueni kwamba harakati za maendeleo zinazofungamanishwa na elimu sahihi kuhusu kujitambua kama Waafrika, kujenga taswira ya Kiafrika katika yale ambayo vyombo vyetu vinatangaza ndani na nje ya bara hili.

Sisi Tanzania na nchi nyingine wanachama wa SABA na nchi nyingine za Afrika tumekubaliana kwa dhati kwamba sasa ni wakati sahihi katika kuhakikisha kuwa vyombo vyetu vya utangazaji vya umma vinakuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato ili viweze kuhimili changamoto za kifedha na hivyo kutimiza ipasavyo dhana ya kukuza, kulinda nan a kutangaza utamaduni wa Mwafrika.

Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia TBC imeanza maandalizi ya kutunga sheria mahsusi itakayobainisha majukumu ya TBC pamoja na masuala mbalimbali yatakayowezesha TBC kutekeleza majukumu yake kwa tija iliyokusudiwa.
 
Back
Top Bottom