Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi Februari 01, 2022

Huyu jamaa amekuwaje luteni wa jeshi kwa cheti cha form 4

Luteni kilaza sana

Amepita kweli TMA monduli huyu !?

Kasomea wapi huo uafisa.

Mbona analiabisha jeshi kuwa na afisa kilaza kama huyu!?

Aisee
Ndio anaenda mning'iniza Mbowe
 
Ulio yupo sawa na kibatara anatoa ushahidi mzr Sana anawasaidia upande wa jamhuri ku justify kuwa kulikuwa na mawasiliano, na komando anathibitisha, kimsingi mwisho wa ck anachokifanya ulio Ni mtego ambao kibatara anauingia bila kujua au kwa kujua,

Stay tuned..
Ok,let's wait and see what is going to happen DUDE!
 
ndg yangu asb nusu nindoshe laptop yangu nilicheka chekasana nikasema kweli dunia tambara bovu

Huyu jamaa nadhani kakata tamaa
Jamaa alisema last week eti parking ya staff ni "park at your own risk"

Huyu jamaa kwa kifupi ni anapewa script sasa anajikuta anasahau ndio maana hadi aliangua kicheko.
 
Nyie ni Nani Aliye Iba Sim Card Luteni?

Watu hawana Huruma Wanaiba Hadi Sim Card Ya Luteni.
Simu card hazikuibwa ila zimefichwa kimkakati. Si unaona hata calls wanaonyesha logs tu sauti zimeondolewa. Wao walichokuwa wanatafuta ni mambo ambayo yatasapoti tuhuma zao. Ktk hizo simu kulikuwa na mambo mengi tu ambayo yalikuwa yana crush vibaya sana tuhuma zao ndio maana wamezificha hizo simu card na kuondoa sauti kwenye calls
 
Nikweli haibadiliki kulingana na maelezo ya LT urio majibu ya maswali yaliyokushinda kuyajibu ni haya.

1. Mbowe alimtafuta LT urio kwajili ya kumtafutia vijana watakao ambatana nae (walinzi)

2. Mbowe alihitaji vijana mahili wa kufanya kazi ya ulinzi kwake ambao ndo hao alio watafuta Lt denis.

3. Mbowe alimtumia Lt urio pesa za nauli na kuwakusanya hao walinzi aliotafutiwa na urio.

4.;nikweli kabisa mpaka sasa hakuna shahidi hata mmoja aliedhibitisha mahali popote kwa evidence ya kuonekana kuwa mbowe na wenzake ni Magaidi zaidi ya kwenda kuongelea kizimbani baada ya kula makande nyumbani kwao.

Kama mimi ndo ningekuwa jaji ningeamuru Lt urio apigwe bakora 100 za mguvu hadharani kwa kosa la uongo na kuwauza makomando wasio kuwa na hatia kwa tamaa zake za pesa.

#Adamo, Bwire, Ling'wenya, Lijenje siyo magaidi bali ni makomando wazalendo walio uzwa na urio kwa watesi wake kina kingai kwa mgongo wa ugaidi.
Mkuu inauma sana makomandoo wetu walikua wanapambana na hali zao akawaita kuja kuwauza wakati anajua kabisa ameshaenda kuchoma kwa DCI dah....Kwa nn wasingetafuta maargent wwengine au hao hao kina adamoo wangewapa mchongo kua kamchunguzeni mbowe km anataka kuleta ugaidi ila wakauzwa mazima na kipigo juu tena kipigo heavy kilicho acha chuki ndani ya mioyo yao
 
Leo ndio nimetambua Urio Ni mpumbavu Sana. Yani aliwatoa wenzake kama chambo. Yani kumbe lingwenya alikuwa amepata shughulika ya kokoto kaenda kumtoa huko ili amtumie kwenye mpango wake. Halafu anaulizwa anajibu kwa jeuri. Tanzania Ina watu wakatili Sana, unapoteza Maisha ya wenzako kwa manufaa binafsi na haujari.
Huo ndio uhalisia wa ccm
 
Mkuu inauma sana makomandoo wetu walikua wanapambana na hali zao akawaita kuja kuwauza wakati anajua kabisa ameshaenda kuchoma kwa DCI dah....Kwa nn wasingetafuta maargent wwengine au hao hao kina adamoo wangewapa mchongo kua kamchunguzeni mbowe km anataka kuleta ugaidi ila wakauzwa mazima na kipigo juu tena kipigo heavy kilicho acha chuki ndani ya mioyo yao
Aisee dunia hii acha watu wapate laana. Kumsababishia mtu maumivu kiasi kile kwa manufaa binafsi. Hizi hela ukiona watu wanakula bata acha wale wanazipata kwa njia nyingi sana.
 
Kwanza ameulizwa:
Kibatala: Ulisema Kwamba Mohammed Ling'wenya baada ya Kufika Kwa Mbowe Tarehe 24 hujawahi Kuzungumza naye

Shahidi: Hapana, Nilimtafuta bila Mafanikio

Kibatala: Je unasema Kwamba Mbowe aliacha Kuwasiliana na wewe Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe 24 July 2020

Kibatala: Kwa hiyo Kwenye Kielelezo namba P 34 Kuna Meseji ambazo Ulimtumia Mbowe Hakujibu?

Shahidi: Zipo

Kibatala: Meseji hizo Ulimuonyesha Mheshimiwa Jaji ambazo hazikujibiwa na Mbowe Kwa Kuongozwa na Mawakili wa Serikali

Shahidi: Sikuonyesha


Kibatala: Vipi Kuhusu Calls, Ulimuonyesha Mheshimiwa Jaji

Halafu akaja kuuliwa kiujanja:
Kibatala: Ulipo surrender Simu zako zote toka Tarehe 12 August 2020, Ulifafanua Kwa Jaji Kuwa Ulikuwa unatumia Simu gani
Shahidi: Hapana Siku fafanua

Simu alikabidhi tarehe 12.8.2020 halafu akaendelea kuzitumia tena tarehe 24.8.2020. Huyu jamaa anastahili kuwa mshtakiwa wa kwanza halafu wenzake waliokuwa anashirikiana nao kuchonga mashtaka waunganishwe kama washtakiwa
24July ndio mwisho wa mawasiliano. 12 aug alikabidhi simu zake zote.
 
Hi
Watu mtakesha na kupoteza muda na rasilimali fedha mkifuatilia kesi hii huku muda wa maandalizi au hoja za kupata Time huru na Katiba Mpya ukipita. Kumbukeni muda wa mwanadamu haufidiwi. Ukipita hakuna kuurudisha. Mh Mbowe anapotezewa muda wake ambao angeutumia kukijenga Chama chake; CHADEMA, kuandaa mazingira ya Watanzania kutambua umuhimu wa Tume Huru ya uchaguzi na madai ya Katiba Mpya. Mara vuuup, uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu huu hapa
Hili linaendelea na kesi hii imekuwa chachu zaidi
 
Tuwape kongole jamani mawakili wa upande Wa utetezi kwa sababu wanafanya kazi kubwa na ngumu sana kumwokoa M/Kiti toka ktk midomo ya hawa simba wala watu...
Nasubir kwa hamu Uzi maalumu wa kuwachangia walau Kila Wakili laki 5 this. Wknd wanywe kamvinyo
 
Urio hayupo sawa,wampeleke kwa wanasaikolojia kabla hajaharibikiwa zaidi.

Wana Lumumba wanaona yupo fit kabisa...

Kuna sheria zamani walikuwa wanasema huruhusiwi mtu kucheka mahakamani,,, sijui ilikuwa kweli au stori za vijiweni
 
Back
Top Bottom