Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi Februari 01, 2022

Mkuu niaelewa na sababu ya msimamo wako. Uri kesha hojiwa. Mbowe alikataa kutoa maelezo polisi na akaahidi atafanya hivyo mahakamani. wakati wake hajafika. wache ufike ndipo tujadiliane.
Kuhusu simu- nina hakika taariifa za kuchunguzwa simu za Mbowe simu yake haiitajiki. Zipo tayari na zinamuunganisha na mashahidi na watuhumiwa wenzake
Comte acha mambo ya misimamo, mimi sina chama ila tu ukweli lazima usemwe kwa maslahi ya taifa letu maana huu ujinga wa Kingai, Urio na waliowatuma unatugharimu Sana sisi walipa kodi.

Ila ni vizuri sasa nawe unaanza kuona ukweli wa mwenendo wa kesi hasa ushahidi mfu wa upande wa washtaki Ndiyo maana unasema tumusubili Mbowe atoe maelezo yake, ila mpaka sasa kazi ya Mbowe ni ndogo Sana maana tayari Urio amekwisha imaliza kesi hii kwa kuonesha ushahidi wake usioaminika kutokana na kuwa na matobo mengi.

Naendelea kukumbusha kuwa kitendo cha Mbowe kuwasiliana au kutumiana hela au kukutana na Urio hakiwezi kuwa kiashiria cha nia ya kutenda kosa lolote, achilia mbali ugaidi Hadi hapo yatakapo patikana maneno au nyenzo yoyote ya kuthibitika kufafanua lengo la mawasiliano hayo.

Kama kwa hapa Urio ameshindwa kuthibitisha nani mwingine wa kuja kuthibitisha?
 
Kibatala: Tarehe 11 August 2020 kwa Ushahidi Wako Ndiyo Ulikwenda Kutoa Maelezo Ushahidi Wako Kwa Inspector Swila.. Inspector Swila alikufafanulia Kwanini alisubiri Mpaka Mwezi Mmoja Baadae?

Shahidi: Hakufafanulia

Kibatala: Tukisema Kuwa Mlitunga Kesi Mapema Kisha Baadae Ndiyo Makaanza Kutafuta Watuhumiwa, Nitakuwa Nakosea Kwa Fact hizo
 
Jambo la maana kuliko yote leo kutoka kwenye dodoso za Mh. Kibatala

Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3 Asubuhi.

Kibatala: Mhe Jaji Nauliza Swali la Mwisho halafu nitatoa hoja

Kibatala: Ulisema Bwire Alikwambia Wapo katika Utekelezaji Wa Mpango

Shahidi: Siyo Mpango, alisema Samahani Bro tumeshakengeuka, Tumeshawishiwa na Freeman Mbowe, Na Vijana Wapo Kilimanjaro Katika Utejelezaji
Wamekengeuka? Kukengeuka maana yake nini? Wameshawishiwa wakashawishika kwenda kufanya uhalifu, imekuwaje si wanaviapo hao? Imekuwaje? Walisahau kuwa wana viapo? Au askari wamekuwa raia na si makomandoo tena maana wameshawishika kilani mno! Basi haya! Nawaza peke yangu.
 
Kwa wakuu wahusika humu: heshima yenu! Hii kesi ni kubwa na muhimu sana, inafunua jinsi jamii na taasisi zetu zilivyooza....ninapendekeza/omba ikiwapendeza mlolongo wa hii kesi tangu ilipoanza uwekwe pamoja ili hata wale ambao hawakupata bahati ya kuanza nasi iwe rahisi kwao kupata mfululizo wa kesi hii kwa tarehe ambazo walipitwa.
Ngoja tuiweke kwenye Pdf moja itapendeza
 
Kinachoniuma kwanini awaingize akina Adamoo na khalifani kwenye dili za ugaidi bila wao kujua.Alafu yeye yupo nje anakula maisha.
Ugaidi unafadhiliwa kwa laki tano
 
Ulio yupo sawa na kibatara anatoa ushahidi mzr Sana anawasaidia upande wa jamhuri ku justify kuwa kulikuwa na mawasiliano, na komando anathibitisha, kimsingi mwisho wa ck anachokifanya ulio Ni mtego ambao kibatara anauingia bila kujua au kwa kujua,

Stay tuned..
Nyie akili zenu za kishetani kabisa.
Hamuwezi kuona hii ni kesi feki?
Shame on you Satans.
 
Yaani ni full kujichanganya...

Hebu fikiri hivi;

1. Simu zinakadhiwa na kushikiliwa polisi tangu tarehe 12/8/2020...

2. Shahidi anakutana nazo mahakamani Januari, 2022...!

3. Lakini cha ajabu simu hizo zinaonekana kutumika hapa katikati. Zimetokaje polisi? Wao wabumba kesi bila shaka wanajua..

4. After all kuna hili very interesting, kuwa, hakuna uthinitisho/risiti ya makabidhiano iliyopelekwa mahakamani kuonesha kuwa hizo ni mali za Urio na zilikuwa polisi kwa uchunguzi...

5. Tuwape kongole jamani mawakili wa upande Wa utetezi kwa sababu wanafanya kazi kubwa na ngumu sana kumwokoa M/Kiti toka ktk midomo ya hawa simba wala watu...

Wanaendelea kuthibitisha pasipo shaka kuwa, mashtaka hayana ukweli wa uhalisia kwa sababu ni ya uongo wa kutungwa na watu wakiwa wamekaa ofisini...!!
Tuwape kongole jamani mawakili wa upande Wa utetezi kwa sababu wanafanya kazi kubwa na ngumu sana kumwokoa M/Kiti toka ktk midomo ya hawa simba wala watu...
 
Back
Top Bottom