Yaliyojiri kikao cha CC ya CCM Jana usiku

Yaliyojiri kikao cha CC ya CCM Jana usiku

Wana JF,

Fununu toka magazetini ni kuwa kikao cha ghafla kilichoitishwa na mwenyekiti wa CCM mh. Jakaya M. Kikwete kimejadili kuhusu uwezekano wa kuvunja serikali ya umoja wa serikali ya Zanzibar kwani Maalim seif kaisaliti SUK na jambo jengine ni kuhusu kuangalia uwezekano wa kuvunja bunge maalum la katiba kwani uwezekano wa UKAWA kurudi ni mgumu na hivyo katiba haitaweza patikana.

Mwenye mpya zaidi atujuze wakati tunajadili hiki kilichopo .
utaufyata sasa ivi kijana
 
Nakumbuka kuna wakati CCM walimwita mtoto wa mmoja wa Waasisi wa Muungano ambaye pia ndiye aliyfanikisha kuwepo kwa SUK huko Zanzibara kuwa ni mlevi wa viroba. Sasa naona linawarudia kimya kimya
 
Attachments

  • Maalim Seif na Sheikh Karume.jpg
    Maalim Seif na Sheikh Karume.jpg
    26.1 KB · Views: 331
kwenye rasmu ccm walianza kuhoji juu ya maoni ya mabaraza ya kata, sasa wamepata majibu ya Warioba na Humprey Polepole wanaweweseka, watangaze wazi kuwa tujadili Rasmu na sio maoni ya ccm, UKAWA tutarudi, nje ya hilo wasahau, liwa lo na liwe
 
Kwanini ccm wana gh'agh'ania kubaki madarakani hata kwa njia za hila na propaganda?

wananchi tulio wengi ndio tumewachagua,sasa waondoke vipi nasi bado tunawapenda? na juzi juzi tumewaongeza wengine na Leo mapema asubuhi wameapishwa bungeni.
 
Mimi hua nawashangaa watu wanao kampeni GNU ivunjwe? Kisa ? Kukosoana na kudai serikali 3? Yaana wanafurahia enzi za uhasama na kubaguana na kuuana?
Jee hawa hawapendi utulivu uliopo?
Jee wanapenda watu wapigane.
Zaidi ya miaka 70 znz haijatulia kutokana na siasa hizi za vuta nikuvute leo Karume alivunja mwiko huo kwa kukaribisha mapatano na leo kunatokea mtu anasema turudi kwenye uhasama ! Huu ni uhayawani na ujinga mkubwa.
Ccm wanaogopa chini ya amani basi hawaiwezi CUF
hivo wanaona bora iwepo fujo walitumie jeshi janjaweed ma mbwa mwitu kuiba kura.
 
Rais wala asipate tabu aweke pending tu swala la katiba mpya mpaka Hapo waheshimiwa ukuwa watakapoamua kurudi bungeni kwa hiyari yao hata kama baada ya miaka 10,amwachie maagizo Rais anayekuja naye wala asiwe na pressure kwani katiba ya zamani ipo na ndio tunayoitumia sasa .
 
hayo magazeti ya udaku nini yanayoripoti fununu??!!!
 
Wazo la kuvunja bunge maalumu la katiba naliunga mkono 1000%. Kuhusu kuvunja serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar naona ni mwendelezo wa tanganyika kuingilia mambo ya zanzibar!
 
ImageUploadedByJamiiForums1399382907.496249.jpg

Tuko busy na kula ubwabwaaaa mtuache
 
Siamini kama ccm inaweza kuachana na mpango wa katiba mpya!!,huu utakuwa mwiba mchungu kwenye harakati za uchaguzi 2015,wataumia sana kisiasa wakifanya hivyo!!
Kuhusu kuvunja serikali ya umoja wa kitaifa tayari walishaanza kuropoka kwenye mikutano yao,nachoshindwa kuelewa je ilikuwa ni rushwa kwa seif ili asipige kelele??
Inashangaza kauli nyingi za ccm ni za ajabu na mtu yeyote makini ni lazima zitamshangaza!!
Wakati ukawa wameondoka dodoma waliambiwa warudishe posho!!swali la kujiuliza je hiyo posho ilikuwa rushwa wakubali kila kitu?na walipoambiwa posho ni kubwa walisema kuwa hazitoshi!!kama ndivyo hao ukawa si walishazitumia kwa siku walizokaa dodoma?ni posho zipi walitakiwa kurudisha?ccm wameshindwa kutenganisha mambo ya chama na serikali na ndiyo maana ilishangaza rais akijiuliza itakuwa vipi waziri asiwe mbunge eti kutakosekana muunganiko wa serikali na bunge wakati huo huo anashindwa kuelewa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali anaingia bungeni kwa wadhifa wake,tofauti itakuwa nini kwa mawaziri kama sheria itatamka hivyo!!!?
 
Wanavoiogopa zenji thubutu yake......Ku prove hyo kitu sheria ya mabadiliko y katiba ili provide kuwa tume maalum lazma iitambue SMZ katika aina yoyote ya muungano sasa jiulize kama moja ya kero za muungano ni pamoja na kuwamo kwa SMZ...je kulingana na sheria hyo tumesov tatizo? Kutokuwemo kwa option ya serikali moja ndani ya rasimu ni kunyima uwanja wa demokrasia na choice kw wananchi
 
wananchi tulio wengi ndio tumewachagua,sasa waondoke vipi nasi bado tunawapenda? na juzi juzi tumewaongeza wengine na Leo mapema asubuhi wameapishwa bungeni.
Mkuu hizi ni akili zako?Kuchaguliwa na wananchi walio wengi ndiyo sababu ya wao kuhangaika?Si kwamba wananchi ndio tulipaswa kuhangaika kwa ajiri yao kwa kuwa bado tunawapenda na kuwahitaji?
 
Rais wala asipate tabu aweke pending tu swala la katiba mpya mpaka Hapo waheshimiwa ukuwa watakapoamua kurudi bungeni kwa hiyari yao hata kama baada ya miaka 10,amwachie maagizo Rais anayekuja naye wala asiwe na pressure kwani katiba ya zamani ipo na ndio tunayoitumia sasa .
Hongera wewe inaonekana mambo yako safi-Heri yako
 
Back
Top Bottom