Yaliyojiri kikao cha CC ya CCM Jana usiku

Yaliyojiri kikao cha CC ya CCM Jana usiku

sem2708

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,934
Reaction score
5,141
Wana JF,

Fununu toka magazetini ni kuwa kikao cha ghafla kilichoitishwa na mwenyekiti wa CCM mh. Jakaya M. Kikwete kimejadili kuhusu uwezekano wa kuvunja serikali ya umoja wa serikali ya Zanzibar kwani Maalim seif kaisaliti SUK na jambo jengine ni kuhusu kuangalia uwezekano wa kuvunja bunge maalum la katiba kwani uwezekano wa UKAWA kurudi ni mgumu na hivyo katiba haitaweza patikana.

Mwenye mpya zaidi atujuze wakati tunajadili hiki kilichopo .
 
Hapo hakuna solution, ni kwamba ameshaiingiza CCM na serikali yake matatizoni tayari.
 
Kuivunja Sirikali ya umoja wa kitaifa (SUK) ya Znz hiyo ni ndoto ya mchana kwa vyama vya siasa. Ikumbukwe kuwa SUK imewekwa pale kutokana na kura za wananchi wa Znz na sio wanasiasa. Na hata ombi lao likipelekwa barazani haliwezi kamwe kupata 2/3 ya kura ya maamuzi.

kama watakuwa wamejadili hilo basi imekula kwao. Msingi mkubwa tu ni KUHISHIMU MAONI YA WANANCHI KATIKA KATIBA MPYA YALIYOWASILISHWA NA JAJI WARIOBA.Ili kuinusuru nchi na khasara ya kukosa katiba mpya wakti wametumia pesa nyingi sana na kuikubali rasimu hiyo ya warioba na kuiboresha sio kuandika upya.
 
JK hana mawazo mgando kama ya mleta mada. JK angekuwa Dicteta, hata UKAWA wasingekuwepo.
 
muhimu wanapaswa kuweka uchama nyumba na kuangalia maslai ya taifa na so kuangalia nini kitawafanya watuwale kizembe
 
Kwa masharti ambayo UKAWA umetoa ili kurudi bungeni kamwe CCM/serikali haiwezi kuyatimiza! Hivyo ni bora bunge hilo likavunjwa rasmi!
 
Liwalo na liwe tu kwani tumechoka na porojo tunahitaji vitendo sasa.
 
Kwa masharti ambayo UKAWA umetoa ili kurudi bungeni kamwe CCM/serikali haiwezi kuyatimiza! Hivyo ni bora bunge hilo likavunjwa rasmi!

Mmmh, livunjwe kirahisi tu, mabilion yamepotea buree, lazima kwanza usuluhishi ufanyike! Watafutwe wazee ambao wana hekima kuweka mambo sawa! Shart gumu hapa msimamo wa kusadikika wa S2 ambao haumo kweny RASIMU II!
 
Back
Top Bottom