Yaliyojiri kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 16, Nov 2021

Salaam Wakuu,


Leo tarehe 15/11/2021 shahidi wa 'Diary' anaendelea ikitarajiwa maamuzi kwenye kesi ndogo katika muendelezo wa kesi Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Kujua kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 15, Nov 2021

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

==========

Wakili wa Serikali: Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa Kuna Uamuzi Mdogo Ulipangwa Kutolewa Tarehe ya Leo, Tupo tayari Kupokea

Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari Kupokea na Kuendelea na Shauri hilo

Jaji: Ijumaa Siku ya tarehe 13, nilihairisha Shauri hili na Kutoa mwelekeo Mahakama Itatoa Uamuzi Mdogo Leo, Katika Kesi Ya Trial Within Trial SHAHIDI namba 2 ambaye alijitambulisha Mwenye Namba H4323 DC Msemwa Akitoa Ushahidi Wake alisema akiwa Polisi Central Dar es Salaam alikuwa akifanya kazi kama General Duty, Katika Chumba cha Mashitaka, Wakiwa katika Chumba cha Mashtaka kazi yao ilikuwa Kupokea Malalamiko, Akasema Siku 07 August 2020 alimpokea Watu wawili ambao ni Adam Kasekwa Mohammed Ling'wenya.

Na Kwamba Baada Muda Mfupi ya Kuwakabidhi Washtakiwa hao na kuwahifadhi, Walirudi Afande Kingai na ASP Jumanne. Na Kwamba waliporudi aliwakabidhi Washtakiwa, Na Mshtakiwa namba 3 Akimkabidhi kwa Afande Jumanne, Na baada ya Kuwakabidhi hakushughulika na Jambo hilo zaidi ya Kuwatembelea Wakiwa Magereza (Mahabusu), Na wakati wote alipowatembelea Walikuwa Wazima wa Afya, Alipata Uhamisho Kwenda Kituo Kingine Cha kazi, ambapo alipata wito wa Kuja Kutolea Ushahidi. Na Kwamba alienda Polisi Central Kwenda Kuchukua Kielelezo Cha Kuja Kutolea Ushahidi Mahakamani, akapapewa. Na akaja Kutolea nacho Ushahidi Mahakamani Katika. KESI Ndogo Ya Mshtakiwa Namba Mbili. Alimpokea tena Wito wa Kuja Kutolea Ushahidi Mahakamani akaenda Tena Central Polisi Kuomba Kielelezo. Na Kwamba alipoenda akaambiwa aende Kuomba Kwa Msajili.

Jaji: Na Msajili alimpatia kwa Kusaini Kwenye Kitabu Kielelezo na Barua, Na baada ya hapo alikitambua Kielelezo, Na baada ya hapo akaomba Mahakama Ikipokee Jambo ambalo lilipingwa na Mawakili wa Utetezi, Mawakili wa Upande wa Utetezi walisema Kwamba Barua hiyo haikuwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka. Kielelezo kinaletwa Kwa Mujibu Wa Sheria. Jambo ambalo angeonyesha alipataje Kielelezo Kingesaidia Kuthibitisha Kielelezo hiko. Sawa ameonyesha baadhi ya Unique Features lakini alishindwa Kutaja Features zingine kama Kumbukumbu namba. Shahidi anatakiwa Kuwa Competent, Na Kwa sababu hiyo wakasema Kwamba Kielelezo kinakosa Sifa hizo mbili na Kwamba Mahakama ikatae Kupokea.

Jaji: Mashtaka Walipata nafasi Ya Kujibu. Wakaomba Mahakama itumie Kanuni ya Nyaraka Kujizungumzia yenyewe. Barua kwa Kuwa inaonyesha alipewa Nakala basi anaweza Kuiongelea Mahakamani. Na Kwamba Kwakuwa Barua hiyo imetolewa na Msajili Basi Hoja ya Dispatch imekosa Mashiko zimetajwa Katika Kesi ya DPP VS MIZIRAHI kesi namba 493 ya Mwaka 2016 Ukurasa wa Saba na Wa Nane.. Wakaendelea Kueleza Mahakama Kwa Mujibu wa Maelekezo Ya Maelezo Iliyotoka Kwamba wanaweza Kufanya Utaratibu wa Kiutawala na Kwamba wafanye hivyo baada ya Kuomba kwa Utawala Upande wa Utetezi umefanya Rejea Ya Kielelezo wakati Kielelezo Bado hakijapokelewa. Hivyo wakaomba Mahakama ione Kwenye kesi ya ROBISON MWANGISI Vs JAMHURI ya Waka 2018. Na Kwa sababu hiyo basi Kielelezo kinapaswa Kiangaliwe Chain Of Custody Kama Kielelezo Kimemfikiaje Shahidi..

Upande wa Utetezi umefanya Rejea Ya Kielelezo wakati Kielelezo Bado hakijapokelewa. Hivyo wakaomba Mahakama ione Kwenye kesi ya ROBISON MWANGISI Vs JAMHURI ya Waka 2018. Na Kwa sababu hiyo basi Kielelezo kinapaswa Kiangaliwe Chain Of Custody Kama Kielelezo Kimemfikiaje Shahidi..

Jaji: Hapakuwa na Sababu ya Kiutawala kwa NPS Kunukuu Shahidi Kwa sababu Shahidi alikuwa na Nakala yake. Na Upande wa Utetezi walirudi kwa ajili ya Utetezi wao.. Na Kwamba Katika Utetezi Wao, Nyaraka haiwezi Kujizungumzia Yenyewe lazima awepo Mwingine wa Kuisemea

Na Ione kwamba Shahidi ajaonyesha Uelewa kuhusu Nyaraka hiyo. Na Nyaraka hiyo haiwezi Kupokelewa kwa sababu ni MSIMAMO WA SHERIA. Na Kwamba Mahakama isishawishiwe na Hoja iliyotoka. Kwamba Mahakama ilisema fanya Uamuzi na Maamuzi siyo Kwamba yalielekeza Utaratibu huu Bali Maamuzi yalikuwa Kuwakumbusha Kufuata Utaratibu. Kwa sababu hiyo basi Wakaomba Mahakama hii Ikikatae Kielelezo hicho, Na huo Ndiyo Mwisho wa Hoja za Pande zote Mbili

UAMUZI

JAJI
: Pingamizi hilo lilijengwa kwamba Shahidi Hakuweka Misingi Kwamba Shahidi Hakuweka Misingi wa kutoa Kielelezo na Misingi Wa Competence ya Kielelezo. Hayo ndiyo Mambo Mawili ya Kuangalia.

Kama Ndiyo Basi Sheria kesi ambazo zimerejewa Ambazo ni

SHARIF Vs DPP na CHARLES ABEL GEZILAHABO zinaonyesha namna gani ya Kupokea Kielelezo. Zinasema Kuangalia RELEVANCE, MATERIAL na COMPETENCE. Na Competence yenyewe ni Namna Kielelezo kilivyo fika Mahakamani. Na Competence kwa Ujumla ni Competence ya Shahidi Na Kielelezo Chenyewe

Sheria Kesi zinasema Kwamba Ili kupima Competence lazima kwa Kungalia AUTHENTICATION. Kwa Shahidi Kutambua Unique features, na Chain of Custody. Chain of Custody ni Kuonyesha Kwamba Kama Kielelezo Kipo Vilevile Kama alivyokiacha Mara ya Mwisho.

Jaji: Mahakama hii Inaona kwamba Pande zote Mbili wameziangalia kwa Kina, Kwa upande wa mashtaka wao wanasema Jambo hilo la Unique features na Unique Objects zilijitosheleza Wakati wa Kesi, Na Kwa namba hiyo basi tuache kutumia Unique Objects badala yake isomeke Features

Kwa Upande wa Utetezi wanasema Hakuna Unique features Kama Tarehe na Kumbukumbu namba.. Kwa Upande wa Mashtaka Wao wanasema kazitaja Ambazo ni Sahihi ya Msajili na Force Namba zake.

Jaji: Mahakamani hii Ili iweze Kupata Neno halisi ya Unique features kwenye kamusi ya Kingereza, Mahakama hii imeshindwa Kupata Tafsiri ya Moja Kwa Moja ya Unique features..

Hivyo mahakama ikaenda kwenye Kamusi ya Mtandao Kwa Kuangalia Htttps/Dictionary. Universally

Kwamba ni Kitu cha pekee.. Kwa namna ambavyo Upande wa Utetezi wamejenga Hoja zao, Sahihi ya Msajili haiwezi Kuwa kuwa ni Unique Features. Na Kwa namna hiyo pia Mahakama hii Inaona kwamba Jina na Force Namba ni Unique features..

Jaji: Kuhusiana na Issue ya Chain of Custody, Hoja ya Utetezi haikuwa Chain of Custody, Hoja yao ni kwamba Barua hiyo Imeelekezwa NPS na Kwamba Shahidi Siyo Muajiriwa wa NPS basi haimuhusu. Na Kwamba hajaonyesha ni Jinsi gani alipata Barua

Na Kwa Jinsi hiyo alipaswa kuonyesha Kwenye Dispatch Ambavyo Msajili Alimkabidhi Barua hiyo. Kwa kukosekana Kwa Mambo hayo Mawili, Basi Imekosekana Uthibitisho namna gani Shahidi alipata Barua hiyo Kuleta Mahakamani,

Kwa Upande wa Mashtaka suala la Barua tayari Shahidi kaonyesha namna gani alipata Barua Kutoka kwa Msajili, Maoni yao Kwamba Chain of Custody ya Kawaida haipaswi Kutumika, Na Kwa Maoni Yangu kama Ambavyo Upande wa Utetezi siyo Chain of Custody Siyo wa kawaida...

Jaji: Tunachopaswa kungalia Kama alipata Kielelezo Kwa Utaratibu, Ni kweli alipaswa kutoa Dispatch. Lakini tayari Shahidi amesha onyesha kwa Mdomo namna gani ambavyo amepata Ushahidi huo. Kwa Sheria ya Ushahidi inasema Shahidi anaeleza Ushahidi wake kwa Mdomo na ataweza Kuaminika

Jaji: Labda iamuliwe Vinginevyo, Kwa Kesi ya GOODLUCK GADO Vs JAMHURI 118/2013 na Kesi ya SANGA Vs JAMHURI 12/2018, Na Kwamba Shahidi atapaswa Kuaminika Kwamba Ushahidi wake Mkweli, Na Kwamba nafasi ya kuonyesha Kwamba Shahidi huyu si Mkweli ni Wakati wa Dodoso..

Jaji: Mahakama inashindwa Kuona Shahidi huyu siyo Mkweli. Upande wa Utetezi wanayo nafasi wakati wa Dodoso, Wanaweza Kumpima Shahidi huyu Kama Mkweli au siyo Mkweli. Kielelezo kinatakiwa Kisomwe lakini Ku' refer Content ili aweze Kutambua Nyaraka hiyo.

Jaji: Kwa hiyo basi Kwa Kesi ya ROBINSON MWANGISI siyo Sahihi Kutumika Kwenye kesi hii. Mahakama Inaona kwamba. Tunapopewa Nakala ya Nyaraka, anamaanisha Mambo 2 Kwamba Mtu anayepewa Nakala kwa Mhusika basi anataka Mtu huyo ajue na Pia anataka awe na Haki ya Kuitumia Nyaraka hiyo

Jaji: Mahakama Inaona ni wazi Kwamba Kwa kutolewa Nakala kwa Shahidi Juu ya Nyaraka hiyo basi ni wazi Lengo lilikuwa ili Shahidi aweze kutumia Nyaraka hiyo. Mahakama hii Inaona Haina Sababu ya Kum' fault Shahidi huyo ambaye ameleta Nyaraka hiyo.

Jaji: Kupokea Nyaraka ni Jambo Moja lakini Kupima Uzito wa Nyaraka ni Jambo lingine. Katika Kupima Uzito wa Nyaraka hiyo ni Mahakama Inaona Kwamba ni wakati wa Cross examination.

Kwa Maana hiyo Mahakama Inaona Barua hiyo iliyokuwa inaenda NPS na Kwamba Shahidi alipewa Nakala. Basi Mahakama hii inaona ni Nyaraka Sahihi na Kwa sababu hiyo Mahakama Inapokea Barua.

Mawakili wote wa Pande zote Mbili wameamka na Kukubaliana na Maamuzi ya Jaji.

Jaji Shahidi Yupo wapi

Shahidi Anapanda kizimbani

Jaji Kwa Mujibu wa kesi ya ROBISON MWANGISI Nyaraka Inapokelewa baada ya Kusomwa, basi naelekeza Shahidi aweze Kusoma..

Mtobesya: OBJECTION Siku ya Ijumaa Mahakama ilitolea Ufafanuzi Kwamba Kuna Suala itatolea Maamuzi leo.

Mtobesya: Tunaona ni Muhimu kwa Mahakama ilitolee Maamuzi hilo suala Kabla hatujaendelea..

Jaji: Upande wa Mashtaka Mna Hoja yoyote??

Wakili wa Serikali- Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ulikuwa umeshaelekeza Kwamba Shahidi asome ili ile Process ya Admission iweze Kukamilika, Kwakuwa Tayari Kuna
Maelezo hayo sisi tunaona tuendelee na Kusoma

Jaji: Ni Kweli nilisha Sema hilo lakini Kuna Jambo nilishalitolea Mahakamani, Upande wa Utetezi Wa naona Kwamba Shahidi aliendelea Kusoma Kabla wakati wao wanapinga Uhalali wa Mahakama.

Wakili wa Serikali - Robert Kidando: Mheshimiwa basi walete hizo Hoja wakiruhusiwa

Mtobesya: Nitaanza Mimi halafu Kaka Yangu Kibatala atamalizia... Mheshimiwa Jaji Shauri hili ni Shauri la Uhujumu Uchumi kwa Mujibu wa.........

Jaji: Siku ya Ijumaa ilikuwa off record naomba Unikumbushe sasa

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Siku ya ijumaa 12 November 2021 Upande wa Utetezi kupitia Kibatala, Alisimama na Kusema Kwamba Shahidi akiwa kwenye Shauri Dogo Kizimbani Shahidi alionekana Akiwa na Diary, Kalamu na Simu, Wakati Kibatala anatoa Hoja hiyo Diary hiyo ilikuwa wazi.

Mtobesya: Kufutiwa na Hoja hiyo Mahakama ikaeleza Kwamba Viletwe Vitu hivyo Mbele ya Mahakamani.. Wakati wa kufunga Siku hiyo Mahakama ilielekeza kwamba ni Busara Shahidi arudishiwe Simu yake.. Na Suala likabakia kuwa ni Diary.

Mtobesya: Na Asubuhi ya Leo Sisi sasa tupo tayari kuelezea ni kwanini Shahidi huyu asiendelee Kutoa Ushahidi Wake na Kisha Wakili Peter Kibatala atamalizia..

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji hili ni suala ambalo limejotokeza Katika kati ya Mwenendo Wa Shauri. Kama tunavyojua Kuwa Shauri hili ni La Uhujumu Uchumi Kama ambavyo inaonekana katika Sura ya 200, Sheria ya Mwaka 2019. Tumepitia Sura ya 200 ya Sheria hii.

Kifungu cha 28 na Kanuni zake, Inasema Kwamba labda patakapotokea Jambo Kubwa basi Ndiyo Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai ndiyo itatumika. Ukienda Sura 20 ya Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai Kwenye Kifungu cha 264 kinaonyesha Nguvu ya Mahakama hii.

Mtobesya: Kwa Vifungu hivyo Viwili Vya Sheria hizo Mbili kama ambavyo zimefanyiwa Marekebisho Mwaka 2019, Kama nilivyosema Kwenye Utangalizi, Kwamba Kitendo cha Shahidi Kukutwa na Diary hasa Ikiwa wazi wakati Mahakama Inaendelea Shahidi aonekane Hafai na hakidhi Tutaeleza Mahakama Kwanini tunasema hivyo.. Mheshimiwa suala la Kutoa Ushahidi Linaongozwa na Sheria namba 06 ya Sheria zetu ambayo ni Sheria ya Ushahidi Kama ambavyo imefanyiwa marekebisho Mwaka 2016.. Ukisoma Sheria ya Ushahidi na PGO inaonyesha Shahidi ambaye atakuwa ni Polisi

Mtobesya: Kwa sasa tunzungumzia ambaye yupo kizimbani, Kwamba Shahidi huyo ambaye ni Polisi atakuwa na Nyaraka zozote endapo tu ataruhusiwa na Mahakama. Na Kama Ruhusa inatoka ni pale anapotakiwa Ku' refresh Memory tu.

Mtobesya: Tunayesema hayo Kwa kifungu cha 168 (1) ya sura ya 6 ya Sheria ya Ushahidi. Na PGO namba 282(7). Na AYA 7 Paragraph A,B na C. Aya ya 7 inasema Kwamba Afisa wa Polisi anaweza Kuwa na Nyaraka baada ya Kupata Ruhusa ya

Mtobesya: Ikitokea Sasa Kuna Umuhimu Wa Kiambatisho au Nyaraka Kuingia Mahakamani Basi Utaratibu Utafuatwa na Kwa Utaratibu Ambao umetaja hapa Katika Sheria ya Ushahidi na Katika PGO 282(7). Shahidi alipaswa Kuomba Ruhusa ya Mahakama na Kibaya zaidi Ikiwa wazi Mahakama Ikiendelea

Mtobesya: Tunasisitiza hizo tataratibu lazima zifuatwe Ili washtakiwa wapate Haki yao wakati wa Cross Examination. Na hiyo ni Kwa Mujibu wa Kifungu cha 172 cha Sheria ya Ushahidi..

Mtobesya anasoma kifungu.

Amemaliza kusoma hicho Kifungu.

Mtobesya: Ilitokea Shahidi anafanya Kwa Kificho inakuwa Inamnyima Haki Mshtakiwa Kujua Shahidi ana rejea kwenye nini. Angeomba wazi Ku' refresh Memory Kwa sababu Sheria inaruhusu.. Na kwakuwa hakuomba tu apatiwe hiyo Diary ni hisia zetu kwamba Alikuwa nayo tangu anaingia.

Mtobesya: Ni Msimamo wetu kwamba Shahidi huyu, Alikuwa anatoa Majibu kwenye Diary wakati anatoa Ushahidi wake, Na Kwa sababu amefanya hivyo kabla hajamaliza Kutoa Ushahidi Wake basi Kwa Kifungu cha 127(1) tunasema Shahidi huyu ni Incompetent.

Mtobesya: Sababu zilizoelezwa Kwenye Kifungu cha 127(1) ni Nyingi lakini kuna Moja inasema...

Mtobesya ANASOMA...

Kwamba alichokifanya Shahidi Ni Sababu ya kumfanya yeye aonekane HAFAI Kuwa shahidi, Na Kwamba Tangu alipoishia Siku ya Ijumaa, asiendelee tena.

Na Kwa sababu hiyo Ushahidi wake wote aliotoa Mahakama UFUTILIWE MBALI. Na Kwa Maana hiyo Shahidi Aondolewe.. Na Mheshimiwa Jaji Kwa Kusisitiza tu hata sasa Ushahidi ulioingia hivi Punde Kwa sababu Umeingia Kupitia shahidi huyu basi Viondoke.

Mtobesya: Mahakama ambayo ina uwezo wa Kumuondoa Shahidi Ni Mahakama Inayomsikiliza Shahidi, ambayo ni Mahakama hii... Kama ambavyo Imeelekezwa Kwenye Sheria Kesi ya EMANUEL A NANYARO Vs PENIEL SAITABAU Ukurasa wa 57.

Mtobesya: Jaji ambaye anasikiliza Shahidi Ndiye anayetakiwa Kufanya Maamuzi Juu ya Competence ya Shahidi.. Kwa Mawasilisho hayo Mheshimiwa Jaji na hivyo Vifungu Vya Sheria, Ni Kwamba Shahidi huyu asiendelee Kutoa Ushahidi Wake na Ushahidi Wake aliotoa UONDOLEWE Kwenye Mahakama.

Mtobesya: Na Kwamba Kwa sababu ya Nyaraka aliyokuwa nayo kwenye Kizimba cha Mahakama hii, hata Ushahidi wake wote aliotoa UONDOLEWE, Kwenye KUMBUKUMBU za Mahakama.. Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji..

Mtobesya amemaliza. Amesimama Peter Kibatala.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji, zifuatazo ndiyo misingi ya kisheria ya utoaji wa ushahidi na uwepo wa shahidi Kizimbani,

Kizimbani Siku zote Hakuruhusiwi Kuwa na Material (Nyaraka) Isipokuwa Kifaa Kazi cha Uapishwaji tu.

Kibatala: Kitu Kingine chochote Kinachoweza Kuingia Kwenye Kizimba lazima kuwepo na Ruhusa ya Mahakama... Pia Upande wa Pili wawe na Haki ya Kutumia Nyaraka Iliyopo kwenye Kizimba.

Kibatala: Kwenye Sheria Neno tunalotumia Kuwepo Kwa Shahidi Kizimbani ni EXAMINATION au EXAMINE, Na hiyo inaenda Mpaka Panapokuwa na Amri ya Kumruhusu au Kumuonya Kumrudisha, Wakati Unaandika Uamuzi Wako tunakualika Utafute Maana ya Neno EXAMINATION.

Kibatala: tumetafuta sisi OXFORD Online "a formal test of personal knowledge or efficient of knowledge or skills"..

Test ambayo tunaitaka Mahakama Itumie Ni Kwenye Chumba Cha Mitihani, iangalie Je unapopatikana na Nyaraka isiyoruhusiwa, Je umepatikana na An authorised Material?

Kibatala: Kama Jibu ndiyo basi Shahidi amekosa Sifa za Kuwa shahidi. Hiyo Diary aliyokuwa nayo ni Kwamba Ipo Katika Mahakama na Imetoka Kwenye Kizimba Moja kwa Moja Mpaka Kwenye Mikono ya Shahidi. Na haijapitia Kingine Kwamba inawaweza kuwa siyo.

Mtobesya: Na Kwamba nasema Muda ambao ilichukuliwa Diary alikuwa bado Kwenye Kizimba na Kesi ikiendelea,

Mheshimiwa Jaji Wakili Mtobesya amekurejesha kifungu cha 127 ambapo Inakuwa Nguvu ya Kumuondoa shahidi.

Ni kweli tunakili Mle hakuna Neno Shahidi, Isipokuwa BUNGE limeweka Maneno kwamba na Vingine Vinavyofanana na hivi.

Mheshimiwa Jaji Tunakurejeshe pia kwenye Kifungu cha 62, Kwamba Shahidi atoe Ushahidi Ndani yake yeye, Akitoa Kweingine Ushahidi Unakuwa siyo Direct Oral Evidence

Kibatala: Wenzetu wakija hapa na Kwamba Mahakama isizungumzie Mambo ya Presumption, Mahakama imetoka Kutoa Uamuzi kwa kutumia Presumption... Basi hata katika hili ni Presumption Kwamba Shahidi alikuwa anatumia Nyaraka Kwa nia Ovu bila Ruhusa ya Mahakama.

Kibatala: Naomba Nikupeleke Katika Sheria ya General Statute ya NOTH CAROLINA. Kwamba Kwa Shahidi ambaye ameingia na Nyaraka Isiyoruhusiwa siyo Shahidi Sahihi Kwanza Kwa Kuingia nayo na Pili Kwa Kushindwa Ku'

Kibatala: Wenzetu wanaweza Kuja na Suala Shahidi anaruhusiwa Kuwa na Notebook akiwa ni Polisi, Hakuna Open Check hapo hata Mwandishi wa PGO ameandika katika namna havurugi taratibu za Kizimbani. Lakini hiyo notebook ya Polisi ina masharti yake, inatakiwa iandikwe Kwa penseli.

Kibatala: Na Kwa Entry zilizopo Katika PGO namba 282(5) A Mpaka J, Na PGO 282(6), Aliyeandika alilemga Kwamba Shahidi asibebe Majibu Kizimbani, Na Hizo Entry zake ziingizwe kwa Penseli na siyo Kwa Pen Kama ambavyo Shahidi huyu alifanya juzi.

Kibatala: Suala linaweza Kuja kwamba hatakiwi mtu kuangalia notebook ya Polisi, basi ndiyo maana alitakiwa Ku' declare na ndiyo na sisi tungepewa nafasi ya

Kibatala: Na Kama Mheshimiwa Jaji, nasema Kama Utatafuta Sehemu Ukaona Hakuna Kifungu cha Sheria Moja kwa Moja. Basi Fikiria Kuhusu Mashahidi Millioni Wengine Watakao Ruhusiwa Kuingia na Diary Kizimbani.

Kibatala: Na kama ikibidi ukaona kumuondoa ni hatua kali sana basi turuhusiwe tuone Je aliandika nini humo, majina ya Askari aliokuwa anawataja?, Tarehe alizokuwa anazitaja? Information alizokuwa anazitoa? Ahsante Mheshimiwa Jaji.

Wakili wa Serikali-Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ataanza Mr Chavula..

Wakili wa Serikali-Abdallah Chavula, anasimama.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tumesikikiza Hoja za Wenzetu, Na siye ni Msimamo wetu kwamba Hatukubaliani na Misingi ya Hoja za Wenzetu, Lakini pili Hatukubaliani na Maombi Yaliyitolewa na Wenzetu

Wenzetu Wanadai Kwamba, Shahidi Wakati yupo kizimbani alionekana kuwa Vitu ambavyo wamesema ni Diary pamoja na Kalamu, na Simu, Kwa mujibu wao kwamba Vitu hivyo hairuhusiwi Kuwa katika miliki yake Katika Sehemu ya Kutolea Ushahidi.

Na Wakaielekeza Mahakama Kwenye Kifungu cha 168 Ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 kama Ilivyofanyiwa Marekebisho 2019.. Na PGO 282, Kwamba pia Malekezo ikaelekezwa zaidi, Kwamba Kuna Kanuni ya Kizimba.. Kwamba Kanuni hiyo ina piga Marufuku au Inakataza Kuwepo wa Kitu chochote kile Kwenye eneo la Ushahidi isipokuwa Vile Vitu ambavyo Vitamuwezesha Yeye Kwenye Kutoa Kiapo.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni Utaratibu ni Kanuni na ni Utamaduni unapoielekeza Mahakama Kwenye Kanuni yoyote ile walahu ielekeze Mahakama Kanuni ile unapoielekeza Mahakama Inatambulika Kisheria, ionyeshe Mahakama Kwenye Jurisdiction yetu Kanuni hii Inakubali Kama Inatambulika Bila Kuonyesha hayo, Inabakia kuwa tu ni Maneno yasiyoungwa Mkono na mamlaka za Kisheria. Mheshimiwa Jaji umealikwa Kwenye Kifungu cha 268(1) Cha Sheria ya Ushahidi na Ukaelezwa Kwamba Kifungu hiki kinamkataza Shahidi anapokuwa anatoa Ushahidi asiwe na Kitu chochote..

Wakili wa Serikali: NAOMBA nisome Kichwa Cha Habari, Inapatikana Kwenye Part 4, Sehemu hii tunapata Kumbukumbu ama Kurejea Kupata Kumbukumbu na la Pili Ni Production of Documents Na Kifungu Cha 168 (1)

ANAKISOMA... Mheshimiwa Jaji Lugha iliyotumika hapa haina Ukakasi, Ni Lugha iliyonyooka. Hakisemi Shahidi asiingie na Simu wala Karatasi. Kusema Kifungu Kinaweka Katazo Kubeba Kitu, Tunasema Hapana na Kwa Heshima zote hatukubaliani na wenzetu, Na Kingine ni PGO namba 282. Mahakama Imeelekezwa Katika PGO 282(7) na (8).

Wakili wa Serikali: PGO hii inatoa Maelekezo Kwamba Afisa wa Polisi anapokuwa anatoa Maelezo ya Ushahidi Wake lazima awe na Notebook.. Sharti la Pili anapopewa kwamba Kabla hajaenda Mahakamani arejee Kwenye Notebook yake, Kwa hiyo Kinachoonekana hapa haitegemewi Kwamba Kwenye Notebook ya Shahidi ambaye ni Askari kutakosekana Jambo au Taarifa ya Jambo anaenda kulitolea Ushahidi Mahakamani.. Isifanywe Maajabu sana kwa Afisa wa Polisi kukutwa na Notebook ya Jambo analokwenda Kulielezea

Wakili wa Serikali: Naomba niende Kifungu B PGO hiyo hiyo ya Saba, Kwa Ruhusa ya Jaji au Hakimu Mmiliki anaweza (ili kurejea Kumbukumbu pekee na Siyo Kwa Dhumuni la Kusoma au Kuelezea Kilicho andikwa).. hapa ipo wazi, Yaliyomo humu ama Yalipo hapa Kwa Ruhusa ya Mahakama ama Jaji au Hakimu Kwamba Mwenye Notebook "The Holder" Ikawa Kuna Haja ya Kujikumbusha na Kujikumbusha pekee na Siyo Kufanya Quotation, Na hajaruhusiwa Kufanya hivyo, Hivi Vifungu viwili ukivitazama Kwa pamoja, Havitoi katazo.

Wakili wa Serikali: Yeye Shahidi ambaye ni Afisa Wa Polisi Kuwa na Notebook, Vifungu Vipo wazi haihitaji Kufanya Presumption, Na Kama Pangekuwa na Katazo Pangewekwa wazi Kwamba ni Marufuku. Ndiyo Maana huko huko unaona "The Holder may refresh the Memory"


Mheshimiwa Jaji PGO 282 (8) ingetanguliwa na Kichwa ha Habari "INSPECTION OF NOTEBOOK", Hii Kanuni ya Nane inaongea Habari ya Inspection na Kuna Mazingira Matatu
A. OC. DISTRICT may examine the notebook........

Wanaruhusiwa Kufanya Ukaguzi Kama zinatunzwa Vizuri

Wakili wa Serikali: C. NOTEBOOKS may only be shown to...... Police Officer, Magistrate or Judge.. Hapa panatolewa Mpaka haswa wa Nani anapaswa Kuziona kwa ajili ya Ukaguzi.. Kama siyo Polisi Officer basi ni Polisi alikuwa gazetted, Wengine ni Mahakimu na Majaji Ni wale tu ambao Sheria imewatambua, Kwanini wanafanya hivyo,..? Ulielekea PGO Ndogo ya Saba Kifungu C, Kwamba Notebook Zinakuwa na Mambo ya Kesi Mbalimbali na Mengine ni Mambo ya Siri.. Ndiyo Maana Wanaweka Mpaka Kwamba ni akina nani wanaweza Kuonyeshwa.

Nahitimisha hoja yetu Kwamba PGO ya 282 sehemu ya Saba Haijaweka katazo Kwa Shahidi ambaye ni Polisi Kuwa na Notebook, Kichwa Cha Habari kinasema pale anapo fanya Rejea. Jaji hawezi kataza kwa Shahidi Kuwa na Notebook.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Hoja Nyingine iliyotolewa ni Hoja inayohusu Competence ya Shahidi Kwa Kile Kilichojotokeza, Mahakama ikaelekezwa Kwenye Kifungu cha 127(1), Na wakasema Kwamba Kwa Mujibu wa Kifungu hicho cha Sheria ya Ushahidi

Kwa Kile wanachokodai wao kwamba Mahakama Inauwezo wa Kutaka Maelezo ya Shahidi Yaondolewe, Mheshimiwa Jaji naomba nisome

Wakati wanatoa Hoja walisema Shahidi anaoekana ana vitu pale kwenye Kizimba na ana pen ananukuu.. Na wakasema ana simu.

Wakati hayo yanatokea Shahidi alikuwa hatoi Ushahidi Alikuwa amekaa anasikiliza Malumbano ya Hoja, Na hata hayo yanayoseemwa alikuwa Anaya fanya Alikuwa hayafanyi.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wakati Shahidi anaongozwa Kuanzia Maapisho Mpaka anatoa Ushahidi Wake, Mahakama ilikuwa ikimtizama, Hakuna hata Mmoja wetu alisimama kwamba Shahidi alikuwa anaongozwa na Kuna Vitu alikuwa anasoma kuvirejea, Hiyo hoja haikuletwa

Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima yote, Mahakama Yako Inaalikwa Kufanya Presumption, Je ni Kweli Inaalikwa kwenye FACTS?

Wakili wa Serikali: Sisi tunaona Hiki Kifungu 127(1) Cha Sheria ya Ushahidi haya Maneno "Any other Similar Course" ni Maoni yetu hayaingii hapa.. Similar Couse inayozungumzwa lazima iwe na Uhusiano na yale yanayotajwa.. Ugonjwa, Umri Mdogo, Ndiyo Cause zinazoweza Kufanya Mahakama Imkatae Shahidi

Ni lazima Shahidi huyo awe anashindwa Kuelewa Maswali na Lazima awe anatoa Majibu, Ili Cause Nyingine zije ni lazima kwanza Ipitie hii test kwanza, Shahidi aliyekuwa akiongozwa hapa, Alikuwa anauliza Maswali na alikuwa anatoa Majibu Kwenye Masuala aliyokuwa akiulizwa

Wakili wa Serikali: Hakuna Mahala Imeonyesha Kwamba Shahidi alikuwa haelewi na Majibu aliyokuwa anayatoa hayana Mahusiano Mbele ya Mahakama.. Hilo la Kwanza,

Pili, Hakuna Mahala Mahakama Yako imeelezwa Kwamba Wakati akiulizwa Maswali na Muendessja Mashitaka kwamba Shahidi alishindwa Kujibu na akawa anafungua Makabrasha kutoa majibu, Kwa sababu hayo hayapo na hatajajitoleza, Mahakama Yako haiwezi Kutumia hiki Kifungu Kumpoka Sifa Shahidi..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji, Mahakama yako imealikwa Kumkosesha/kumtengua Shahidi, Kifungu hiki hakikutajwa, Mheshimiwa Jaji tuna kesi hapa ya Mahakama Kuu ya Uganda tunaamini itakuisaidia ni Ya UGANDA.
UGANDA Vs OKUMU REGAN na Wenzake 5 Criminal Revison namba 003 ya Mwaka 2018 Ukurasa wa 12 kuanzia Paragraph ya 10,15, na 20, Naomba Kunukuu.

Wakili wa Serikali: Na Kama ni kweli Shahidi alionekana wakati wa Ushahidi wake anasoma, Basi kinaenda Kuathiri Uzito wa Ushahidi wake, Na ndiyo Maana Kwenye Kifungu cha 127(1) kwamba Alikuwa anasoma havikuonekana.. Kwa Kanuni hii ambayo tumeisoma Mahakama, Kwamba Itumie Mamlaka yake, Halipo

Wakili wa Serikali: Hakuna Nguvu ya Kisheria Kufanya Mahakama Yako iondoshe Shahidi Na Iondoshe Ushahidi Wake. Mheshimiwa Jaji nashukuru kwa kunisikiliza na Mimi na Komea hapa..Naomba Kumualika Mwenzangu Bw. PIUS HILA

Jaji: Bila Kurudia uliyoyaongea

Wakili wa Serikali - Pius Hilla: Nashukuru Mheshimiwa Jaji.. Nianze Kwa kusema kwamba Hoja ambazo Waleta ni Hoja ambazo hazipo sawasawa, Na Kwamba Mahakama Yako haijawa Moved Kwa Kujitosheleza. Vifungu Vilivyotumika Kui move Mahakama Kama Nilivyowasikia Wenzetu

Order walizoleta ni Kumkosesha, Kumtengua Shahidi ma Ushahidi wake Utupwe, Ni Kifungu cha 127 cha Sheria ya Ushahidi, Ni kweli waliongelea Kwa Hoja zao, Mheshimiwa kwa kuwa Maombi haya yapo Kwenye Jurisdiction of the Court Kwa Maana Order ambazo zilikuwa Moved, Maombi yalipaswa


Kuletwa kwa Vifungu ambavyo ni sahihi. Kutokuleta Kwa Vifungu hivyo Hakuifanyi Mahakama Kufanyia kazi.. Mheshimiwa Jaji niendelee Kuialika Mahakama, Wenzetu hawakatai Kwamba Kile kilichotokea hapo Kizimbani ni FACTUAL Issues hilo halina Ubishi

Wakili wa Serikali: Factual issues Zinakuwa Proved By Evidence In This Matter, Factual Issue Imetoka From the Back, Wote tuliopo kwenye Bar na Even From The Bench kama Hakuna aliyeona, Jaji Nikukumbushe Submission ya Leo hajasema ilikuwa From the Back.

Aliyeseoma hayo Hakusema Mahakamani ni swali lipi na Majibu yapi Aliyatafuta from where. Hajaeleza Kwamba Material Yaliyopo Kizimbani yalikuwa yamefunguliwa. Hakuna Namna Motion hiyo inaweza kuzingatiwa Mpaka Pale huyu anayeleta Motion kuyazingatia hayo

Wakili wa Serikali: Tunayaeleza haya Kwa sababu wote tulikuwepo Mahakamani Wakati Namuongoza Shahidi Mimi ndiye nilikuwa karibu na Shahidi Kuliko Mtu Mwingine, Mheshimiwa Jaji nizungumzie Kuhusu Presumption.. Hukuona Shahidi anasoma wakati ana Testify.

Wala Mheshimiwa hiyo haiwezi Ku Qualify kuwa hiyo ni Presumption, Tunawasilisha Alichokuwa akikitolea Ushahidi Shahidi ni Majibu Kutoka Kwenye Knowledge yake na Sio vinginevyo. Mheshimiwa Jaji Mahakama Yako imealikwa Kutumia Examination Room test, Sisi tunasema Siyo sawasawa.

Wakili wa Serikali: Examination Room Ina kanuni zake na Sheria Zake. Test ya Kisheria ni Ile iliyopo Kwenye Section 1 ya Sheria ya Ushahidi. Wamesema Kwamba Shahidi amekutwa na unauthorised Material, Lakini hilo pekee hakutoshi Kumuondoa au Kumtengua Shahidi.

Haya ni Masuala Ya Kisheria na yanapaswa KUFANYIKA Kisheria. Kwa kuwa Material Yaliyopo Hayajaonekana popote kama yalikuwa yanatumika Kujibu Majibu. Ushahidi Wake ulikuwa ni Moja kwa Moja kutoka Mdomoni Mwake.

Wakili wa Serikali: Mahakama Yako ikaambiwa Shahidi Wako Haja Declare, Kesi ya GOODLUCK KYANDO imesema hayo. Je Mtu kutoka Nyuma anaweza Kuwa na Bad faith? Baada ya hayo naomba Mwenzangu Robert Kidando amalizie kuwasilisha
Ninaanza kukosa imani na Jaji. Hili swala la shahidi kukutwa na kibomu kizimbani alikuwa anataka lipitwe hivi hivi bila kulitolea maamuzi. Inamaana Mtobesya asingelikumbusha ndio ingekuwa imetoka hiyo
 
Mbowe sio Gaidi.. Mbowe ni MWAMBA..
Mbowe ni Mzalendo namba moja Tanzania..
Mbowe ni SHUJAA. Mbowe SIO GAIDI
Lazima mtage safari hii
JamiiForums430303985.jpg
 
Jaji kasoma projo zake haraharaka akataka kuruka mambo yaliyopangwa siku ya leo. Anasema Ijumaa ilikuwa off record akumbushwe.
Jaji mzito kwenye maamuzi kila penye mvutano anaweka break na kufanya kesi hii ichukue muda mwingi huku muda uliotumika kortini ni mchache badala ya kuangalia sheria inasemaje juu ya hilo afanye maamuzi sahihi

Hawa mawakili wa serikali wanasema tu kua sheria hazipingi shahidi kumiliki material akiwa kizimbani halafu wanaishia hapo wakati sheria halisi inadai hizo material zinaruhusiwa kwa idhini maalumu, mean while kama hujapewa idhini ni ilegal endapo utaonekana ume-hold hizo material kizimbani
 
Jaji mzito kwenye maamuzi kila penye mvutano anaweka break na kufanya kesi hii ichukue muda mwingi huku muda uliotumika kortini ni mchache badala ya kuangalia sheria inasemaje juu ya hilo afanye maamuzi sahihi

Hawa mawakili wa serikali wanasema tu kua sheria hazipingi shahidi kumiliki material akiwa kizimbani halafu wanaishia hapo wakati sheria halisi inadai hizo material zinaruhusiwa kwa idhini fulani, mean while kama hujapewa idhini ni ilegal endapo utaonekana ume-hold hizo material kizimbani
Mawakili wa serikali ni watu wa ajabu sana tena sana.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Jaji mzito kwenye maamuzi kila penye mvutano anaweka break na kufanya kesi hii ichukue muda mwingi huku muda uliotumika kortini ni mchache badala ya kuangalia sheria inasemaje juu ya hilo afanye maamuzi sahihi

Hawa mawakili wa serikali wanasema tu kua sheria hazipingi shahidi kumiliki material akiwa kizimbani halafu wanaishia hapo wakati sheria halisi inadai hizo material zinaruhusiwa kwa idhini fulani, mean while kama hujapewa idhini ni ilegal endapo utaonekana ume-hold hizo material kizimbani
Jaji ana wakati mgumu sanaa, ni ukweli vs uteuzi wake,
 
Mbowe sio Gaidi.. Mbowe ni MWAMBA..
Mbowe ni Mzalendo namba moja Tanzania..
Mbowe ni SHUJAA. Mbowe SIO GAIDI
MBOWE NI GAIDI
MBOWE NI MWIZI WA HELA MPAKA ZA OFISI KALA ZA SABODO KALA
MBOWE ANALAZIMISHA KUWA MWENYEKITI NDIY MAANA LISSU KAMSUSA
KIBATALA ANAMFUNGISHA MAKUSUDI
MBOWE GAIDI TU
 
Tuko pamoja, Leo tutafahamu Jamaa alikuwa anasoma Nini, ikibainika alikuwa anasoma notes za ushahidi basi ushahidi wake uwe void.
Umesikia lakini wanasheria wasomi wa serikali wanatoa material?yaani kibatala na wenzake hawajui sheria wanabwagwa kila siku hata hivyo vitu alivyokuwa navyo havikatazwi kuwa navyo
 
MBOWE NI GAIDI
MBOWE NI MWIZI WA HELA MPAKA ZA OFISI KALA ZA SABODO KALA
MBOWE ANALAZIMISHA KUWA MWENYEKITI NDIY MAANA LISSU KAMSUSA
KIBATALA ANAMFUNGISHA MAKUSUDI
MBOWE GAIDI TU
Ukajua kufungwa ni rahisi kama unavyonywa mkuuundru!
 
Umesikia lakini wanasheria wasomi wa serikali wanatoa material?yaani kibatala na wenzake hawajui sheria wanabwagwa kila siku hata hivyo vitu alivyokuwa navyo havikatazwi kuwa navyo
Iimesoma need kafuka njiani nikasahau nilikoanzia. Wanachoeoeza hakieleweki. Hiyo hotuba siielewi ya mawakili wa mashtaka.
 
Back
Top Bottom