Yaliyojiri kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 16, Nov 2021

Na kijiwe chetu kwa umoja wetu tumefika ktk wingi wetu kuendelea kufuatilia mwenendo wa kesi hii .

WAKATI JAJI AKIHAIRISHA KESI KWA MAPUMZIKO MAFUPI YA AFYA ILI IENDELEE BAADAYE, WANANCHI NAO WACHUKUA NAFASI HIYO KUPATA MLO WA MCHANA
 
Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Akisoma uamuzi huo leo Jumatatu Novemba 15, 2021 Jaji Joachim Tiganga amekubaliana na hoja za upande wa mashitaka na kukubali barua iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama itolewe kama kielezo na Shahidi namba mbili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.
Mawakili upande wa utetezi walipinga kuhusiana na barua ambayo upande wa mashtaka uliomba kuiwasilisha mahakamani kupitia kwa shahidi wa pili katika kesi hiyo ndogo.

Upande wa mashtaka Ijumaa iliyopita kupitia kwa shahidi huyo wa pili uliiomba mahakama iipokee barua hiyo ya msajili inayoonesha kuwa upande wa mashtaka umeomba kitabu cha kumbukumbu za Mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam cha mwaka 2020, ili shahidi huyo aweze kukiwasilisha mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi wake na kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.
Source:Mwananchi updates
Safi sana!
 
Kuna Malaika wa Mungu ndani ya chumba cha mahakama anawapiga kwa 'upofu' hawa mashahidi wa uongo walioandaliwa kudhulumu haki za mshatakiwa asie na hatia.
 
majamaaa ni weupe sana mpaka una jiuliza hawa nao wamesoma vyuo vyetu kweli ama walipita bangalore university kama yule wakili wa MIC
 
Salaam Wakuu,


Leo tarehe 15/11/2021 shahidi wa 'Diary' anaendelea ikitarajiwa maamuzi kwenye kesi ndogo katika muendelezo wa kesi Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Kujua kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 15, Nov 2021

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

==========

Wakili wa Serikali: Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa Kuna Uamuzi Mdogo Ulipangwa Kutolewa Tarehe ya Leo, Tupo tayari Kupokea

Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari Kupokea na Kuendelea na Shauri hilo

Jaji: Ijumaa Siku ya tarehe 13, nilihairisha Shauri hili na Kutoa mwelekeo Mahakama Itatoa Uamuzi Mdogo Leo, Katika Kesi Ya Trial Within Trial SHAHIDI namba 2 ambaye alijitambulisha Mwenye Namba H4323 DC Msemwa Akitoa Ushahidi Wake alisema akiwa Polisi Central Dar es Salaam alikuwa akifanya kazi kama General Duty, Katika Chumba cha Mashitaka, Wakiwa katika Chumba cha Mashtaka kazi yao ilikuwa Kupokea Malalamiko, Akasema Siku 07 August 2020 alimpokea Watu wawili ambao ni Adam Kasekwa Mohammed Ling'wenya.

Na Kwamba Baada Muda Mfupi ya Kuwakabidhi Washtakiwa hao na kuwahifadhi, Walirudi Afande Kingai na ASP Jumanne. Na Kwamba waliporudi aliwakabidhi Washtakiwa, Na Mshtakiwa namba 3 Akimkabidhi kwa Afande Jumanne, Na baada ya Kuwakabidhi hakushughulika na Jambo hilo zaidi ya Kuwatembelea Wakiwa Magereza (Mahabusu), Na wakati wote alipowatembelea Walikuwa Wazima wa Afya, Alipata Uhamisho Kwenda Kituo Kingine Cha kazi, ambapo alipata wito wa Kuja Kutolea Ushahidi. Na Kwamba alienda Polisi Central Kwenda Kuchukua Kielelezo Cha Kuja Kutolea Ushahidi Mahakamani, akapapewa. Na akaja Kutolea nacho Ushahidi Mahakamani Katika. KESI Ndogo Ya Mshtakiwa Namba Mbili. Alimpokea tena Wito wa Kuja Kutolea Ushahidi Mahakamani akaenda Tena Central Polisi Kuomba Kielelezo. Na Kwamba alipoenda akaambiwa aende Kuomba Kwa Msajili.

Jaji: Na Msajili alimpatia kwa Kusaini Kwenye Kitabu Kielelezo na Barua, Na baada ya hapo alikitambua Kielelezo, Na baada ya hapo akaomba Mahakama Ikipokee Jambo ambalo lilipingwa na Mawakili wa Utetezi, Mawakili wa Upande wa Utetezi walisema Kwamba Barua hiyo haikuwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka. Kielelezo kinaletwa Kwa Mujibu Wa Sheria. Jambo ambalo angeonyesha alipataje Kielelezo Kingesaidia Kuthibitisha Kielelezo hiko. Sawa ameonyesha baadhi ya Unique Features lakini alishindwa Kutaja Features zingine kama Kumbukumbu namba. Shahidi anatakiwa Kuwa Competent, Na Kwa sababu hiyo wakasema Kwamba Kielelezo kinakosa Sifa hizo mbili na Kwamba Mahakama ikatae Kupokea.

Jaji: Mashtaka Walipata nafasi Ya Kujibu. Wakaomba Mahakama itumie Kanuni ya Nyaraka Kujizungumzia yenyewe. Barua kwa Kuwa inaonyesha alipewa Nakala basi anaweza Kuiongelea Mahakamani. Na Kwamba Kwakuwa Barua hiyo imetolewa na Msajili Basi Hoja ya Dispatch imekosa Mashiko zimetajwa Katika Kesi ya DPP VS MIZIRAHI kesi namba 493 ya Mwaka 2016 Ukurasa wa Saba na Wa Nane.. Wakaendelea Kueleza Mahakama Kwa Mujibu wa Maelekezo Ya Maelezo Iliyotoka Kwamba wanaweza Kufanya Utaratibu wa Kiutawala na Kwamba wafanye hivyo baada ya Kuomba kwa Utawala Upande wa Utetezi umefanya Rejea Ya Kielelezo wakati Kielelezo Bado hakijapokelewa. Hivyo wakaomba Mahakama ione Kwenye kesi ya ROBISON MWANGISI Vs JAMHURI ya Waka 2018. Na Kwa sababu hiyo basi Kielelezo kinapaswa Kiangaliwe Chain Of Custody Kama Kielelezo Kimemfikiaje Shahidi..

Upande wa Utetezi umefanya Rejea Ya Kielelezo wakati Kielelezo Bado hakijapokelewa. Hivyo wakaomba Mahakama ione Kwenye kesi ya ROBISON MWANGISI Vs JAMHURI ya Waka 2018. Na Kwa sababu hiyo basi Kielelezo kinapaswa Kiangaliwe Chain Of Custody Kama Kielelezo Kimemfikiaje Shahidi..

Jaji: Hapakuwa na Sababu ya Kiutawala kwa NPS Kunukuu Shahidi Kwa sababu Shahidi alikuwa na Nakala yake. Na Upande wa Utetezi walirudi kwa ajili ya Utetezi wao.. Na Kwamba Katika Utetezi Wao, Nyaraka haiwezi Kujizungumzia Yenyewe lazima awepo Mwingine wa Kuisemea

Na Ione kwamba Shahidi ajaonyesha Uelewa kuhusu Nyaraka hiyo. Na Nyaraka hiyo haiwezi Kupokelewa kwa sababu ni MSIMAMO WA SHERIA. Na Kwamba Mahakama isishawishiwe na Hoja iliyotoka. Kwamba Mahakama ilisema fanya Uamuzi na Maamuzi siyo Kwamba yalielekeza Utaratibu huu Bali Maamuzi yalikuwa Kuwakumbusha Kufuata Utaratibu. Kwa sababu hiyo basi Wakaomba Mahakama hii Ikikatae Kielelezo hicho, Na huo Ndiyo Mwisho wa Hoja za Pande zote Mbili

UAMUZI

JAJI
: Pingamizi hilo lilijengwa kwamba Shahidi Hakuweka Misingi Kwamba Shahidi Hakuweka Misingi wa kutoa Kielelezo na Misingi Wa Competence ya Kielelezo. Hayo ndiyo Mambo Mawili ya Kuangalia.

Kama Ndiyo Basi Sheria kesi ambazo zimerejewa Ambazo ni

SHARIF Vs DPP na CHARLES ABEL GEZILAHABO zinaonyesha namna gani ya Kupokea Kielelezo. Zinasema Kuangalia RELEVANCE, MATERIAL na COMPETENCE. Na Competence yenyewe ni Namna Kielelezo kilivyo fika Mahakamani. Na Competence kwa Ujumla ni Competence ya Shahidi Na Kielelezo Chenyewe

Sheria Kesi zinasema Kwamba Ili kupima Competence lazima kwa Kungalia AUTHENTICATION. Kwa Shahidi Kutambua Unique features, na Chain of Custody. Chain of Custody ni Kuonyesha Kwamba Kama Kielelezo Kipo Vilevile Kama alivyokiacha Mara ya Mwisho.

Jaji: Mahakama hii Inaona kwamba Pande zote Mbili wameziangalia kwa Kina, Kwa upande wa mashtaka wao wanasema Jambo hilo la Unique features na Unique Objects zilijitosheleza Wakati wa Kesi, Na Kwa namba hiyo basi tuache kutumia Unique Objects badala yake isomeke Features

Kwa Upande wa Utetezi wanasema Hakuna Unique features Kama Tarehe na Kumbukumbu namba.. Kwa Upande wa Mashtaka Wao wanasema kazitaja Ambazo ni Sahihi ya Msajili na Force Namba zake.

Jaji: Mahakamani hii Ili iweze Kupata Neno halisi ya Unique features kwenye kamusi ya Kingereza, Mahakama hii imeshindwa Kupata Tafsiri ya Moja Kwa Moja ya Unique features..

Hivyo mahakama ikaenda kwenye Kamusi ya Mtandao Kwa Kuangalia Htttps/Dictionary. Universally

Kwamba ni Kitu cha pekee.. Kwa namna ambavyo Upande wa Utetezi wamejenga Hoja zao, Sahihi ya Msajili haiwezi Kuwa kuwa ni Unique Features. Na Kwa namna hiyo pia Mahakama hii Inaona kwamba Jina na Force Namba ni Unique features..

Jaji: Kuhusiana na Issue ya Chain of Custody, Hoja ya Utetezi haikuwa Chain of Custody, Hoja yao ni kwamba Barua hiyo Imeelekezwa NPS na Kwamba Shahidi Siyo Muajiriwa wa NPS basi haimuhusu. Na Kwamba hajaonyesha ni Jinsi gani alipata Barua

Na Kwa Jinsi hiyo alipaswa kuonyesha Kwenye Dispatch Ambavyo Msajili Alimkabidhi Barua hiyo. Kwa kukosekana Kwa Mambo hayo Mawili, Basi Imekosekana Uthibitisho namna gani Shahidi alipata Barua hiyo Kuleta Mahakamani,

Kwa Upande wa Mashtaka suala la Barua tayari Shahidi kaonyesha namna gani alipata Barua Kutoka kwa Msajili, Maoni yao Kwamba Chain of Custody ya Kawaida haipaswi Kutumika, Na Kwa Maoni Yangu kama Ambavyo Upande wa Utetezi siyo Chain of Custody Siyo wa kawaida...

Jaji: Tunachopaswa kungalia Kama alipata Kielelezo Kwa Utaratibu, Ni kweli alipaswa kutoa Dispatch. Lakini tayari Shahidi amesha onyesha kwa Mdomo namna gani ambavyo amepata Ushahidi huo. Kwa Sheria ya Ushahidi inasema Shahidi anaeleza Ushahidi wake kwa Mdomo na ataweza Kuaminika

Jaji: Labda iamuliwe Vinginevyo, Kwa Kesi ya GOODLUCK GADO Vs JAMHURI 118/2013 na Kesi ya SANGA Vs JAMHURI 12/2018, Na Kwamba Shahidi atapaswa Kuaminika Kwamba Ushahidi wake Mkweli, Na Kwamba nafasi ya kuonyesha Kwamba Shahidi huyu si Mkweli ni Wakati wa Dodoso..

Jaji: Mahakama inashindwa Kuona Shahidi huyu siyo Mkweli. Upande wa Utetezi wanayo nafasi wakati wa Dodoso, Wanaweza Kumpima Shahidi huyu Kama Mkweli au siyo Mkweli. Kielelezo kinatakiwa Kisomwe lakini Ku' refer Content ili aweze Kutambua Nyaraka hiyo.

Jaji: Kwa hiyo basi Kwa Kesi ya ROBINSON MWANGISI siyo Sahihi Kutumika Kwenye kesi hii. Mahakama Inaona kwamba. Tunapopewa Nakala ya Nyaraka, anamaanisha Mambo 2 Kwamba Mtu anayepewa Nakala kwa Mhusika basi anataka Mtu huyo ajue na Pia anataka awe na Haki ya Kuitumia Nyaraka hiyo

Jaji: Mahakama Inaona ni wazi Kwamba Kwa kutolewa Nakala kwa Shahidi Juu ya Nyaraka hiyo basi ni wazi Lengo lilikuwa ili Shahidi aweze kutumia Nyaraka hiyo. Mahakama hii Inaona Haina Sababu ya Kum' fault Shahidi huyo ambaye ameleta Nyaraka hiyo.

Jaji: Kupokea Nyaraka ni Jambo Moja lakini Kupima Uzito wa Nyaraka ni Jambo lingine. Katika Kupima Uzito wa Nyaraka hiyo ni Mahakama Inaona Kwamba ni wakati wa Cross examination.

Kwa Maana hiyo Mahakama Inaona Barua hiyo iliyokuwa inaenda NPS na Kwamba Shahidi alipewa Nakala. Basi Mahakama hii inaona ni Nyaraka Sahihi na Kwa sababu hiyo Mahakama Inapokea Barua.

Mawakili wote wa Pande zote Mbili wameamka na Kukubaliana na Maamuzi ya Jaji.

Jaji Shahidi Yupo wapi

Shahidi Anapanda kizimbani

Jaji Kwa Mujibu wa kesi ya ROBISON MWANGISI Nyaraka Inapokelewa baada ya Kusomwa, basi naelekeza Shahidi aweze Kusoma..

Mtobesya: OBJECTION Siku ya Ijumaa Mahakama ilitolea Ufafanuzi Kwamba Kuna Suala itatolea Maamuzi leo.

Mtobesya: Tunaona ni Muhimu kwa Mahakama ilitolee Maamuzi hilo suala Kabla hatujaendelea..

Jaji: Upande wa Mashtaka Mna Hoja yoyote??

Wakili wa Serikali- Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ulikuwa umeshaelekeza Kwamba Shahidi asome ili ile Process ya Admission iweze Kukamilika, Kwakuwa Tayari Kuna
Maelezo hayo sisi tunaona tuendelee na Kusoma

Jaji: Ni Kweli nilisha Sema hilo lakini Kuna Jambo nilishalitolea Mahakamani, Upande wa Utetezi Wa naona Kwamba Shahidi aliendelea Kusoma Kabla wakati wao wanapinga Uhalali wa Mahakama.

Wakili wa Serikali - Robert Kidando: Mheshimiwa basi walete hizo Hoja wakiruhusiwa

Mtobesya: Nitaanza Mimi halafu Kaka Yangu Kibatala atamalizia... Mheshimiwa Jaji Shauri hili ni Shauri la Uhujumu Uchumi kwa Mujibu wa.........

Jaji: Siku ya Ijumaa ilikuwa off record naomba Unikumbushe sasa

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Siku ya ijumaa 12 November 2021 Upande wa Utetezi kupitia Kibatala, Alisimama na Kusema Kwamba Shahidi akiwa kwenye Shauri Dogo Kizimbani Shahidi alionekana Akiwa na Diary, Kalamu na Simu, Wakati Kibatala anatoa Hoja hiyo Diary hiyo ilikuwa wazi.

Mtobesya: Kufutiwa na Hoja hiyo Mahakama ikaeleza Kwamba Viletwe Vitu hivyo Mbele ya Mahakamani.. Wakati wa kufunga Siku hiyo Mahakama ilielekeza kwamba ni Busara Shahidi arudishiwe Simu yake.. Na Suala likabakia kuwa ni Diary.

Mtobesya: Na Asubuhi ya Leo Sisi sasa tupo tayari kuelezea ni kwanini Shahidi huyu asiendelee Kutoa Ushahidi Wake na Kisha Wakili Peter Kibatala atamalizia..

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji hili ni suala ambalo limejotokeza Katika kati ya Mwenendo Wa Shauri. Kama tunavyojua Kuwa Shauri hili ni La Uhujumu Uchumi Kama ambavyo inaonekana katika Sura ya 200, Sheria ya Mwaka 2019. Tumepitia Sura ya 200 ya Sheria hii.

Kifungu cha 28 na Kanuni zake, Inasema Kwamba labda patakapotokea Jambo Kubwa basi Ndiyo Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai ndiyo itatumika. Ukienda Sura 20 ya Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai Kwenye Kifungu cha 264 kinaonyesha Nguvu ya Mahakama hii.

Mtobesya: Kwa Vifungu hivyo Viwili Vya Sheria hizo Mbili kama ambavyo zimefanyiwa Marekebisho Mwaka 2019, Kama nilivyosema Kwenye Utangalizi, Kwamba Kitendo cha Shahidi Kukutwa na Diary hasa Ikiwa wazi wakati Mahakama Inaendelea Shahidi aonekane Hafai na hakidhi Tutaeleza Mahakama Kwanini tunasema hivyo.. Mheshimiwa suala la Kutoa Ushahidi Linaongozwa na Sheria namba 06 ya Sheria zetu ambayo ni Sheria ya Ushahidi Kama ambavyo imefanyiwa marekebisho Mwaka 2016.. Ukisoma Sheria ya Ushahidi na PGO inaonyesha Shahidi ambaye atakuwa ni Polisi

Mtobesya: Kwa sasa tunzungumzia ambaye yupo kizimbani, Kwamba Shahidi huyo ambaye ni Polisi atakuwa na Nyaraka zozote endapo tu ataruhusiwa na Mahakama. Na Kama Ruhusa inatoka ni pale anapotakiwa Ku' refresh Memory tu.

Mtobesya: Tunayesema hayo Kwa kifungu cha 168 (1) ya sura ya 6 ya Sheria ya Ushahidi. Na PGO namba 282(7). Na AYA 7 Paragraph A,B na C. Aya ya 7 inasema Kwamba Afisa wa Polisi anaweza Kuwa na Nyaraka baada ya Kupata Ruhusa ya

Mtobesya: Ikitokea Sasa Kuna Umuhimu Wa Kiambatisho au Nyaraka Kuingia Mahakamani Basi Utaratibu Utafuatwa na Kwa Utaratibu Ambao umetaja hapa Katika Sheria ya Ushahidi na Katika PGO 282(7). Shahidi alipaswa Kuomba Ruhusa ya Mahakama na Kibaya zaidi Ikiwa wazi Mahakama Ikiendelea

Mtobesya: Tunasisitiza hizo tataratibu lazima zifuatwe Ili washtakiwa wapate Haki yao wakati wa Cross Examination. Na hiyo ni Kwa Mujibu wa Kifungu cha 172 cha Sheria ya Ushahidi..

Mtobesya anasoma kifungu.

Amemaliza kusoma hicho Kifungu.

Mtobesya: Ilitokea Shahidi anafanya Kwa Kificho inakuwa Inamnyima Haki Mshtakiwa Kujua Shahidi ana rejea kwenye nini. Angeomba wazi Ku' refresh Memory Kwa sababu Sheria inaruhusu.. Na kwakuwa hakuomba tu apatiwe hiyo Diary ni hisia zetu kwamba Alikuwa nayo tangu anaingia.

Mtobesya: Ni Msimamo wetu kwamba Shahidi huyu, Alikuwa anatoa Majibu kwenye Diary wakati anatoa Ushahidi wake, Na Kwa sababu amefanya hivyo kabla hajamaliza Kutoa Ushahidi Wake basi Kwa Kifungu cha 127(1) tunasema Shahidi huyu ni Incompetent.

Mtobesya: Sababu zilizoelezwa Kwenye Kifungu cha 127(1) ni Nyingi lakini kuna Moja inasema...

Mtobesya ANASOMA...

Kwamba alichokifanya Shahidi Ni Sababu ya kumfanya yeye aonekane HAFAI Kuwa shahidi, Na Kwamba Tangu alipoishia Siku ya Ijumaa, asiendelee tena.

Na Kwa sababu hiyo Ushahidi wake wote aliotoa Mahakama UFUTILIWE MBALI. Na Kwa Maana hiyo Shahidi Aondolewe.. Na Mheshimiwa Jaji Kwa Kusisitiza tu hata sasa Ushahidi ulioingia hivi Punde Kwa sababu Umeingia Kupitia shahidi huyu basi Viondoke.

Mtobesya: Mahakama ambayo ina uwezo wa Kumuondoa Shahidi Ni Mahakama Inayomsikiliza Shahidi, ambayo ni Mahakama hii... Kama ambavyo Imeelekezwa Kwenye Sheria Kesi ya EMANUEL A NANYARO Vs PENIEL SAITABAU Ukurasa wa 57.

Mtobesya: Jaji ambaye anasikiliza Shahidi Ndiye anayetakiwa Kufanya Maamuzi Juu ya Competence ya Shahidi.. Kwa Mawasilisho hayo Mheshimiwa Jaji na hivyo Vifungu Vya Sheria, Ni Kwamba Shahidi huyu asiendelee Kutoa Ushahidi Wake na Ushahidi Wake aliotoa UONDOLEWE Kwenye Mahakama.

Mtobesya: Na Kwamba Kwa sababu ya Nyaraka aliyokuwa nayo kwenye Kizimba cha Mahakama hii, hata Ushahidi wake wote aliotoa UONDOLEWE, Kwenye KUMBUKUMBU za Mahakama.. Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji..

Mtobesya amemaliza. Amesimama Peter Kibatala.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji, zifuatazo ndiyo misingi ya kisheria ya utoaji wa ushahidi na uwepo wa shahidi Kizimbani,

Kizimbani Siku zote Hakuruhusiwi Kuwa na Material (Nyaraka) Isipokuwa Kifaa Kazi cha Uapishwaji tu.

Kibatala: Kitu Kingine chochote Kinachoweza Kuingia Kwenye Kizimba lazima kuwepo na Ruhusa ya Mahakama... Pia Upande wa Pili wawe na Haki ya Kutumia Nyaraka Iliyopo kwenye Kizimba.

Kibatala: Kwenye Sheria Neno tunalotumia Kuwepo Kwa Shahidi Kizimbani ni EXAMINATION au EXAMINE, Na hiyo inaenda Mpaka Panapokuwa na Amri ya Kumruhusu au Kumuonya Kumrudisha, Wakati Unaandika Uamuzi Wako tunakualika Utafute Maana ya Neno EXAMINATION.

Kibatala: tumetafuta sisi OXFORD Online "a formal test of personal knowledge or efficient of knowledge or skills"..

Test ambayo tunaitaka Mahakama Itumie Ni Kwenye Chumba Cha Mitihani, iangalie Je unapopatikana na Nyaraka isiyoruhusiwa, Je umepatikana na An authorised Material?

Kibatala: Kama Jibu ndiyo basi Shahidi amekosa Sifa za Kuwa shahidi. Hiyo Diary aliyokuwa nayo ni Kwamba Ipo Katika Mahakama na Imetoka Kwenye Kizimba Moja kwa Moja Mpaka Kwenye Mikono ya Shahidi. Na haijapitia Kingine Kwamba inawaweza kuwa siyo.

Mtobesya: Na Kwamba nasema Muda ambao ilichukuliwa Diary alikuwa bado Kwenye Kizimba na Kesi ikiendelea,

Mheshimiwa Jaji Wakili Mtobesya amekurejesha kifungu cha 127 ambapo Inakuwa Nguvu ya Kumuondoa shahidi.

Ni kweli tunakili Mle hakuna Neno Shahidi, Isipokuwa BUNGE limeweka Maneno kwamba na Vingine Vinavyofanana na hivi.

Mheshimiwa Jaji Tunakurejeshe pia kwenye Kifungu cha 62, Kwamba Shahidi atoe Ushahidi Ndani yake yeye, Akitoa Kweingine Ushahidi Unakuwa siyo Direct Oral Evidence

Kibatala: Wenzetu wakija hapa na Kwamba Mahakama isizungumzie Mambo ya Presumption, Mahakama imetoka Kutoa Uamuzi kwa kutumia Presumption... Basi hata katika hili ni Presumption Kwamba Shahidi alikuwa anatumia Nyaraka Kwa nia Ovu bila Ruhusa ya Mahakama.

Kibatala: Naomba Nikupeleke Katika Sheria ya General Statute ya NOTH CAROLINA. Kwamba Kwa Shahidi ambaye ameingia na Nyaraka Isiyoruhusiwa siyo Shahidi Sahihi Kwanza Kwa Kuingia nayo na Pili Kwa Kushindwa Ku'

Kibatala: Wenzetu wanaweza Kuja na Suala Shahidi anaruhusiwa Kuwa na Notebook akiwa ni Polisi, Hakuna Open Check hapo hata Mwandishi wa PGO ameandika katika namna havurugi taratibu za Kizimbani. Lakini hiyo notebook ya Polisi ina masharti yake, inatakiwa iandikwe Kwa penseli.

Kibatala: Na Kwa Entry zilizopo Katika PGO namba 282(5) A Mpaka J, Na PGO 282(6), Aliyeandika alilemga Kwamba Shahidi asibebe Majibu Kizimbani, Na Hizo Entry zake ziingizwe kwa Penseli na siyo Kwa Pen Kama ambavyo Shahidi huyu alifanya juzi.

Kibatala: Suala linaweza Kuja kwamba hatakiwi mtu kuangalia notebook ya Polisi, basi ndiyo maana alitakiwa Ku' declare na ndiyo na sisi tungepewa nafasi ya

Kibatala: Na Kama Mheshimiwa Jaji, nasema Kama Utatafuta Sehemu Ukaona Hakuna Kifungu cha Sheria Moja kwa Moja. Basi Fikiria Kuhusu Mashahidi Millioni Wengine Watakao Ruhusiwa Kuingia na Diary Kizimbani.

Kibatala: Na kama ikibidi ukaona kumuondoa ni hatua kali sana basi turuhusiwe tuone Je aliandika nini humo, majina ya Askari aliokuwa anawataja?, Tarehe alizokuwa anazitaja? Information alizokuwa anazitoa? Ahsante Mheshimiwa Jaji.

Wakili wa Serikali-Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ataanza Mr Chavula..

Wakili wa Serikali-Abdallah Chavula, anasimama.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tumesikikiza Hoja za Wenzetu, Na siye ni Msimamo wetu kwamba Hatukubaliani na Misingi ya Hoja za Wenzetu, Lakini pili Hatukubaliani na Maombi Yaliyitolewa na Wenzetu

Wenzetu Wanadai Kwamba, Shahidi Wakati yupo kizimbani alionekana kuwa Vitu ambavyo wamesema ni Diary pamoja na Kalamu, na Simu, Kwa mujibu wao kwamba Vitu hivyo hairuhusiwi Kuwa katika miliki yake Katika Sehemu ya Kutolea Ushahidi.

Na Wakaielekeza Mahakama Kwenye Kifungu cha 168 Ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 kama Ilivyofanyiwa Marekebisho 2019.. Na PGO 282, Kwamba pia Malekezo ikaelekezwa zaidi, Kwamba Kuna Kanuni ya Kizimba.. Kwamba Kanuni hiyo ina piga Marufuku au Inakataza Kuwepo wa Kitu chochote kile Kwenye eneo la Ushahidi isipokuwa Vile Vitu ambavyo Vitamuwezesha Yeye Kwenye Kutoa Kiapo.
Aliingia na Desa Kizimbani
 
Jaji alitaka kupotezea habari za diary na simu eti anamruhusu shahidi aendelee kutoa ushahidi wakati ikithibitishika alikua anasoma kwenye diary mambo yanayo husiana na kesi anakua amekosa sifa ya kuwa shahidi

Kongole kwa mawakili wa utetezi kwa kumkumbusha jaji japo naona hajafurahia
Jaji kasoma projo zake haraharaka akataka kuruka mambo yaliyopangwa siku ya leo. Anasema Ijumaa ilikuwa off record akumbushwe.
 
Back
Top Bottom