Yaliyojiri katika Maadhimisho ya Mei Mosi - Mbeya

Yaliyojiri katika Maadhimisho ya Mei Mosi - Mbeya

mkuu mimi nafuatilia kupitia tbc naona watu wamehamasika sijui wewe upo uwanja gani au upo uwanja wa jamhuri mkuu.
Achana na propaganda za TBC, mimi miko uwanjani, hakuna hamasa yeyote, watu sio wengi, halafu mvua inataka kuharibu.
 
hatuna habari na hizo sherehe, ambazo hazina tija , huyo jamaa si alitutukana sana wakati anaongea na wazee wa DAR , eti tuna akili za mabayuayu ohoo!!! Kong;ota,

sasa anataka nini leo??? mi nadhani akaazimishe siku ya wazee wa DAR ndo watamuelewa,

sisi atuache tuko huku mtaani tunapata Kinana Bariiiiiidi a.k.a Ndovu

Mgeni rasmi kwenye sherehe za mei mosi mjini Mbeya rais Kikwete akiwa anaingia uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine watu walikuwa wamekaa tu kama vile waliopoteza kabisa matumaini na kiongozi huyu wa serikali. Rais alionyesha uso wa furaha na kuwapungia mkono lakini wengi waliendelea kuketi bila kumpungia mkono mh. rais. Nadhani haya ni mambo rais anabidi asome alama za nyakati vizuri - naleta kwenu wanajf tujadili
 
Maisha bora kwa kila mtanzania yamegeuka bora maisha, na mtoa ahadi anachekacheka tu, mc asiwatibue zaidi wasije wakamzomea halafu mkulu akasingizia ni njama za Sugu yakaja ya Ar
 
Hao ni walimu, wapo hapo kwa sababu kuna rokoo iliyopitishwa pamoja na kuchimbwa mkwara "mwalimu asiyekuja atafukuzwa kazi"...

Kwahiyo unataka kutuambia kwamba waalimu wanawake ni waoga au wanajali? Je wanaume ni jasiri na hawajali au hawajielewi?
 
Mgeni rasmi kwenye
sherehe za mei mosi mjini Mbeya rais Kikwete akiwa anaingia uwanja wa
kumbukumbu ya Sokoine watu walikuwa wamekaa tu kama vile waliopoteza
kabisa matumaini na kiongozi huyu wa serikali. Rais alionyesha uso wa
furaha na kuwapungia mkono lakini wengi waliendelea kuketi bila
kumpungia mkono mh. rais. Nadhani haya ni mambo rais anabidi asome alama
za nyakati vizuri - naleta kwenu wanajf tujadili

Acha unafiki dogo! kwani we uko uwanjani au unaangalia kupitia ka tv kako ka duduproof? watu gani wamemnunia rais? we nani uwasemee watu mawazo yao?
 
Wafanyakazi wameimba wimbo wao 'Solidarity forever' lakini sura zao zinaonekana kukata tamaa na kutokuwa na matumaini yoyote ya kupata maisha bora.
 
Arusha Mambo inarusha moja kwa moja matangazo ya Sikukuu za Mei Mosi za nchi za Tanzania na Kenya na tutajitahidi uweze kusikiliza hotuma zote za Marais wa nchi Hizi, Uhuru Kenyata - Kenya na Jakaya Kikwete - Tanzania.

ili kusikiliza tembelea Arusha Mambo FM Radio - Home

Karibu kusikiliza.
 
Wengi hapo wamefuata posho tu...sijui hata wanapewa kiasi gani maskini...
 
mkuu hawezi kutatua matatizo ya wafanyakazi overnite,he needs time as matatizo ni mengi aliyoyakuta alipoingia madarakan pia some workers' demands are not realistic..
 
Namwona Mkuu wa mkoa wa Mbeya mhe.Abbas Kandoro anawakaribisha wageni.Pia anawataja baadhi ya wageni maalumu wakiwemo viongozi wa dini,wabunge n.k Naona ameanza kuzungumzia hali ya kilimo mkoani Mbeya huku akihusianisha wafanyakazi na wakulima.Amemaliza kuongea lakini hajapigiwa makofi.Mshereheshaji ameingilia kati, amewataka wafanyakazi kumpigia makofi matatu...kichekesho kwa kweli.Sasa anafuatia katibu wa TUCTA, naye pia anawatambulisha wageni maalumu walioalikwa akiwemo balozi wa China,Marekani,Italia,Msumbiji na wadau mbalimbali wa mashirika ya wafanyakazi. Mhe.Mgaya pia ametambua uwepo wa Mhe.Kinana,alisimama oa kupigiwa makofi kiduchu,huku Shukuru Kawambwa akipungiwa mkono na walimu wachache.
 
Hivi hata nchi nyingine siku ya Mei Mosi wananchi huwa wanajipitisha mbele ya Wakuu wa Nchi zao???
 
Nasikia wamenuna Msafara wa Raisi jana uliuwaa wananchi pale Nzovwe njia panda ya kwenda Itende wamejiapiza akaye na wafanyakazi wake ,sasa Kandoro anapiga mapambio ya eti watu wamejaa sana wakati uwanja unaonyesha mapengo kibao
 
Naangalia live TBC sherehe za mei mosi zinazofanyika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Siwaoni hawa wabunge wa majimbo mbalimbali ya mkoa huu ambao wanaheshimika na wana ushawishi mkubwa. Kulikoni?
 
Yupo Kinana hapo. Anatambulishwa kama mgeni mwalikwa na anatajwa na kila anayesimama kuongea ila sina hakika kama ni kimkakati zaidi.
 
Back
Top Bottom