KOMBAJR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2011
- 5,827
- 1,271
wanabodi heshima mbele ....
Naomba niwaletee update za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi ambayo kitaifa yanafanyika katika uwanja wa Sokoine jiji Mbeya.
Watu wameshaanza kuingia na viongozi mbali mbali wameshaingia nimemuona Hawa Ghasia,Mama Kabaka,Kinana,Kawambwa,Makongoro na mabalozi mbali mbali.
UPDATES:
- Kwa ufupi uwanja uko mtupu wazo la kupeleka mbeya linaweza kuleta tafsiri mbaya ya jamaa kukubalika kazi kweli kweli wanafuta muda ili watu wajae jae isijekuwa aibu kwa Mgeni rasmi. Hivi watoto wa shule nao ni wafanyakazi?
- Mgeni Rasmi Rais Kikwete ndo anaingia uwanja wa sokoine tayari kuongea na wafanyakazi akifuatiwa na maandamano ya wafanyakazi yalioyoanzia nzomve!
- Rais ameingia ila hamasa kwa wahuzuriaji siyo nzuri mpaka mshereheshaji akiwalazimisha wananchi kumshangilia kitu ambacho akijakubaliaka zaidi ya matarumbeta.....anadai eti wananchi wa mbeya wana historia ya kupokea wageni wapi!
- Rais ameshashuka kwenye gari lake amelakiwa na viongozi mbali mbali na kuelekea jukwaani, kwa ufupi watu wapo Doro sana Mshereheshaji anakazi ya ziada kuamasisha watu kushangilia kitu ambacho hakipo.
- Makundi ya wafanyakazi yanaingia kwa maandamano katika uwanja wa sokoine kulingana na sekta zao, Mshehereshaji anasema eti kujitokeza kwa wingi kwa walimu kutaongeza ufaulu wa wanafunzi wanabodi vinahusiano hivi?
- Ninachokiona kwenye maandamano haya ya wafanyakazi wa taasisi na sekta mbali mbali ni matabaka ya kiuwezo wa taasisi husika kuanzia kwenye mavazi mpaka vikorombwezo.................
- Boda Boda na Bajaji naona nao ndani ya nyumba ndizo ajira ambazo JK amezitengeneza
- Kudos ofisi ya bunge mmewakilisha vyema ............
- Wimbo wa taifa na wimbo wa wafanyakazi unatendewa haki
................................
Mkuu wa Mkoa anawakaribisha wageni mbali mbali katika jiji la mbeya na katika maadhimisho ya mei 2013 tayari kabisa kuanza maadhimisho........
Mgaya anatambulisha wageni walioalikwa katika sherehe hizi...........kinachofuata ni salamu za mkoa wa mbeya na zinatolewa na Mkuu wa Mkoa Bw. Kandoro....... ameambiwa atoe salamu za mkoa yeye anatambulisha
Kujipendekeza (Ukada) kubaya sana mtu hayupo kwenye ratiba yeye anataka aongee anataka Mama Salma atoe salaam amepotezewa!
Katika salaam za ATE wanasema maslai ya wafanyakazi hayaboreki kwa kasi ya mabadiliko ya kiuchumi,wanamtaka raisi waweke mgawanyo mzuri katika rasilimali za nchi hii
Waziri Kabaka - Mwenye mamlaka na wafanyakazi
Kila lililozungumzwa serikali watalifanyia kazi ni wajibu wao kuwasikiliza na kutatua kero za wafanyakazi.
Wanabodi Asanteni kwa uvumilivu wenu katika kufuatilia updates, Mtaniwia Radhi kwa yale ambayo sijaweka ni mapungufu tu ya kibinadamu unaweza ongeza kwa faida ya wanabodi. Kazi kwenu sasa Je yote yaliyozungumzwa ya Tija? Picha zitawajia ASP.
Naomba Kuwasilisha

- Waziri kabaka mpaka sasa wameshindwa kutamka kima cha chini cha sekta binafsi changa la kwanza, amehahidi kabla ya mwezi huu kwisha watakuwa wametangaza kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi. Uanzishwaji wa mfuko wa wafanyakazi wanaoumia katika maeneo ya kazi upo kwenye mchakato na hatua za mwisho
- Katiba Mpya izingatike haki kwa tabaka la wafanyakazi, mishahara iwe agenda ya kitaifa.
- Serikali kukopa katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kutorudisha kunazidi kuwaongezea majonzi wastaafu
- Amezungumzia suala la udini pia
- Hali ya elimu katika nchi pia TUCTA wanatakujua serikali imechukua hatua gani kukabiliana na wimbi kubwa watoto wengi kufeli.
- Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi itakuwa na tija pale tu maagizo na makubaliano yatakapokuwa yanatekelezwa.
- Wameipokea hotuba ya Katibu wa TUCTA na wataifanyia kazi sababu imekamilika katika idara zote.
- Serikali kutokuongeza mishahara kwa wafanyakazi kwa muda husika hakutokani na mtimanyongo bali ni hali halisi ya kipato cha serikali
- serikali wataunda chombo cha kusimamia utekelezaji wa mambo mbali mbali kwa kuanza wataanza na sekta 6
- Ajira 168,000 zimezalishwa kufikia mwisho wa mwaka jana
- Kodi kwenye PAYE Kupunguzwa 13% mpaka.......... waziri wa fedha atatangaza kwenye bajeti
- waligundua kasaro nyingi katika Mamilioni ya JK, watu wengi walipewa pesa bila kupewa mafunzo ila kwasasa watazingatia hilo katika kutoa mikopo kwa Vijana na wanawake.
- Serikali wanaanzisha utaratibu wa kuwakopesha nyumba wafanyakazi ili kuwapunguzia ukali wa maisha
- Kiwanja cha mbeya cha songwe Umekamilika hii inafungua biashara na kukuza uchumi kwa mikoa ya iranga,Njombe na Mbeya
- Wanambeya wanapata fursa ya kupata historia ya Malkia wa Uholanzi na uhusiano na Tanzania.....Duh!
- fursa za kilimo cha maua kutokana na miundo mbinu zilizopo katika mikoa tajwa, makampuni ya kigeni yatakuwa ila ndiyo mambo ya eeh!this one eeh dont worry hakuna
- Mbeya kufikia mwaka 2018 hakutakuwa na tatizo la maji kabisa.
- Anazungumzia Udini watanzania wajiepushe na migogoro inayotokana na imani
- Turejee enzi za mababu za waislamu na wakiristo kushirikian
- JK amezindua Gazeti la Mfanyakazi