Yaliyojiri bungeni: Serikali kupitia TISS inahusika na utekaji sio kwa CCM wala upinzani

5a52d836ab4ba480e3a265e456348d97.gif
taaaaaamuuuy
 
unaposema "Serikali kupitia TISS", Embu tufafanulie, "Serikali" ni nani?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kila mtu awe na ulinzi wake hujui saa wala dk atakapo kuja mwana wa sizonje kuja kukuteka
2EE3892500000578-3337885-image-a-4_1448754929117.jpg
 
Of all people, Zitto tunayemjua atakuwa natafuta headlines za kesho. Hana kitu anatafuta aambiwe kuleta ushahidi, akose ushahidi, kisha afukuzwe Bungeni kwa siku kadhaa apate recovery maana sasa akina Sugu, Mdee, Lissu na hata wabunge wengine kutoka CCM wanaonekana kumpita kwa mbali kwa viroja na hoja Bungeni. Haya kazana.
 
Hii serikali ya awamu hii imelewa madaraka, hasahasa Bashite na Sizonje!!! Hivi hatuna namna ya kuwafanya kitu hawa, wenzetu huko sumbawanga hamuwezi watumia radi mauti hawa jamaa, au kule bwagamoyo mlingotini hamuwezi watumi jini "Mkatakamba " hawa jamaa ili nchi itulie na tuishi kwa amani!!!!!
Huku koromije hata pembejeo hatuna , sukari nayo imepanda ila nchi nzima story ni bashite Na Ngosha!!!
twanogaga!!!!
 
Ee Mimi siyawezi kila MTU serikali hivi serikari ni nani? Kiongozi yeyote bila kupewa ushirikiano atajuaje?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Naamini sasa kwa kinachoedelea Bungeni kama mtu unajua kuchekecha mambo kamwe hautampuuza Roma Mkatoliki na kwamba ati "alijiteka".

Ulimboka katekwa kateswa katupwa Mabwepande mpaka leo hakuna uchunguzi wala majibu, Yeye mpaka leo hakusimulia nani kamfanyia hivyo.

Salma wa DW katekwa kateswa katupwa kati kati ya mji. Yeye mpaka leo hakusimulia kinagaubaga nani kamfanyia hivyo. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.

George Mgoba katekwa kateswa katupwa Magwepande, Yeye mpaka leo hakusimulia kinagaubaga nani kamfanyia hivyo. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.

Kibanda katekwa kateswa katobolewa jicho, Yeye mpaka leo hakusimulia kinagaubaga nani kamfanyia hivyo. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.

Yalinikuta mimi, wengi mpaka leo wanasema nilijiteka...na maneno kibaaaao....

Ben Saanane maarufu Ben-Rabiu Wa Saanane katekwa mpaka leo mwezi wa 4 huu, Hakuna yeyote mpaka leo anayeweza kusimulia kinagaubaga au hata kulisemea tu nani kamfanyia hivyo kijana huyu hazina ya taifa. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.

Roma na wenzake wametekwa wameteswa mnajipa moyo mnasubiri uchunguzi?

Ili wote tuamini kwamba Tanzania kuna utekaji na utesaji inabudi WOTE tuonje machungu haya ya kutekwa na kuteswa. Naamini wabunge hawa wasingeonjeshwe shubiri wasingefunguka hivi. Muda ukifika hatutaoishana hivi katika kuongea, WOTE tutaongea Lugha moja na hili limeanza huko Bungeni.

Nukuu za Wabunge leo ni jibu la haya mambo:

"Nipo tayari kuthibitisha kwamba waliovamia Clouds Tv ni Usalama wa Taifa kutoka kikosi cha Ulinzi wa Rais, Nipo tayari pia kuthibitisha aliyemtoloea bastola Nape ni Usalama wa Taifa"

Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo)

"Hivi Waziri wa Habari alikwenda kufanya nini katika Press ya Roma, mkiambiwa mlimteka mtakataa? Bora kusema ukweli kuliko kukaa kimya, najua mtasema kwa kuwa nilikosa uwaziri No!"

Juma Nkamia (CCM)

"Mimi nimekamatwa na kuteswa na Usalama wa Taifa. Nimenyanyaswa sana nchi hii. Ikibidi mnifukuze CCM (machozi)".

Hussein Bashe (CCM)

"Hakuna sababu ya Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi wanaishi kwa wasiwasi juu ya usalama wao. Kutoa kauli kunasaidia kutoa hofu"

Ridhiwani Kikwete (CCM)

"Mimi ni miongoni mwa wabunge niliotishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar, na mpaka sasa mimi sikanyagi Dar licha ya kuimisi sana"

Hillary Aeshi (CCM)

Tafakari, Chukua hatua

Na Yericko Nyerere
Usalama wa taifa ni idara ya serikali hata tukipiga kelele nani atatusaidia wakati wote watoto WA baba mmoja. Ndo maana hata hizi habar police hawaliingilii kabisa na hutaweza kumsikia sirro akitia maguuu bora kukaa kimya.
 
Kama unataka kuamini tz ni nchi ya amani, nenda Congo, bulundi, Kenya, somaria, Sudan. Nk, hebu tuongelee uchumi amani. Tz mtu anatembea na pesa nyingi tena wazi bila wasiwasi KWA wenzetu weee!
 
Bora wote wanasomeshwa Namba siyo CCM siyo wapinzani wasiokuwa na vyama namba ni zilezile labda hapo itatusaidia watanzania kujitambua,kwani tunapoambiwa usifanye hivi hatuelewi labda hizo namba zinaweza kutusaidia kujitambua na kuiona kuwa CCM hawana rafiki wa kudumu.
Wakati wa kampeni tuliwaambia kwamba huyo bwana hafai, hawakutuelewa. Hata jamaa akawaona hawana akili, akawaambia atawapatia elimu bure mpaka form four maana alishaona kwamba kwa mwenye elimu japo ya Form Four hawezi kuwa bwege. Sasa hii ndio Elimu ya bure anayowagawia. Ikifika 2020, kila mtu atakuwa ameelimika japo kwa kiwango cha Form Four, tena bure na atakuwa amejitambua na atapiga kura yake kwa akili.
 
Kama unataka kuamini tz ni nchi ya amani, nenda Congo, bulundi, Kenya, somaria, Sudan. Nk, hebu tuongelee uchumi amani. Tz mtu anatembea na pesa nyingi tena wazi bila wasiwasi KWA wenzetu weee!
Utaongelea uchumi upi wakati mtu anaogopa hata akienda shambani anaweza kutekwa. Bajeti ya kilimo ambao ndio uti wa mgongo ni asilimia 2%. Unazungumzia uchumi au uchimi?
 
Utasemaje serikali inahusika kupitia TISS lakini si chama cha CCM wakati kiongozi wa serikali ndiye yule yule kiongozi wa CCM?
 
Wakati wa kampeni tuliwaambia kwamba huyo bwana hafai, hawakutuelewa. Hata jamaa akawaona hawana akili, akawaambia atawapatia elimu bure mpaka form four maana alishaona kwamba kwa mwenye elimu japo ya Form Four hawezi kuwa bwege. Sasa hii ndio Elimu ya bure anayowagawia. Ikifika 2020, kila mtu atakuwa ameelimika japo kwa kiwango cha Form Four, tena bure na atakuwa amejitambua na atapiga kura yake kwa akili.
 
Unapokuwa na Vyama vya siasa vyenye makundi ya ulinzi/usalama ni hatari. na hasa makundi hayo yanapokuwa ndani ya vyombo vya dola vya usalama.
 
Ni kweli ila tumwogope hats mungu, utekaji unaousema si WA sisi walala hoi hao wana sababu zao wala hawanyang'anyi MTU pesa baadae MTU anaonekana hiyo tu inasababisha nchi nzima kukosa amani? Je wakiingia alshababu humu utasemaje?. Tupambane na wale wanaotubia Mali zetu za nchi tunakosa maendeleo, hebu fikiria watu 10 tu wanachukua bilioni mia tatu na watanzania tunaishi kwa shida hats mikopo tunayoletewa inatufanya tuendelee kuwa watumwa kwenye nchi yetu. Hebu tuachane na Habari za nape, makonda, gwajima. Hao wanaishi vizuri wanatutumia sisi walalahoi kukuza majina yao.
 
Saa hizi biashara inayolipa ni kuanzisha private security contracter,
maana kila mtu naona anahitaji ulinzi,
na hali ikiiendelea kila mwenye pesa zake anakuwa na mabodyguard wa kumlinda,
maana yake ni kuwa sasa wale polisi wastaafu ,wanajeshi,shushu msitaafu etc naona mlango wa ajira unafunguka huo
 
Back
Top Bottom