Yaliyojiri bungeni: Serikali kupitia TISS inahusika na utekaji sio kwa CCM wala upinzani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Messages
4,105
Points
2,000

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2012
4,105 2,000
Naamini sasa kwa kinachoedelea Bungeni kama mtu unajua kuchekecha mambo kamwe hautampuuza Roma Mkatoliki na kwamba ati "alijiteka".

Ulimboka katekwa kateswa katupwa Mabwepande mpaka leo hakuna uchunguzi wala majibu, Yeye mpaka leo hakusimulia nani kamfanyia hivyo.

Salma wa DW katekwa kateswa katupwa kati kati ya mji. Yeye mpaka leo hakusimulia kinagaubaga nani kamfanyia hivyo. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.

George Mgoba katekwa kateswa katupwa Magwepande, Yeye mpaka leo hakusimulia kinagaubaga nani kamfanyia hivyo. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.

Kibanda katekwa kateswa katobolewa jicho, Yeye mpaka leo hakusimulia kinagaubaga nani kamfanyia hivyo. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.

Yalinikuta mimi, wengi mpaka leo wanasema nilijiteka...na maneno kibaaaao....

Ben Saanane maarufu Ben-Rabiu Wa Saanane katekwa mpaka leo mwezi wa 4 huu, Hakuna yeyote mpaka leo anayeweza kusimulia kinagaubaga au hata kulisemea tu nani kamfanyia hivyo kijana huyu hazina ya taifa. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.

Roma na wenzake wametekwa wameteswa mnajipa moyo mnasubiri uchunguzi?

Ili wote tuamini kwamba Tanzania kuna utekaji na utesaji inabudi WOTE tuonje machungu haya ya kutekwa na kuteswa. Naamini wabunge hawa wasingeonjeshwe shubiri wasingefunguka hivi. Muda ukifika hatutaoishana hivi katika kuongea, WOTE tutaongea Lugha moja na hili limeanza huko Bungeni.

Nukuu za Wabunge leo ni jibu la haya mambo:

"Nipo tayari kuthibitisha kwamba waliovamia Clouds Tv ni Usalama wa Taifa kutoka kikosi cha Ulinzi wa Rais, Nipo tayari pia kuthibitisha aliyemtoloea bastola Nape ni Usalama wa Taifa"

Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo)

"Hivi Waziri wa Habari alikwenda kufanya nini katika Press ya Roma, mkiambiwa mlimteka mtakataa? Bora kusema ukweli kuliko kukaa kimya, najua mtasema kwa kuwa nilikosa uwaziri No!"

Juma Nkamia (CCM)

"Mimi nimekamatwa na kuteswa na Usalama wa Taifa. Nimenyanyaswa sana nchi hii. Ikibidi mnifukuze CCM (machozi)".

Hussein Bashe (CCM)

"Hakuna sababu ya Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi wanaishi kwa wasiwasi juu ya usalama wao. Kutoa kauli kunasaidia kutoa hofu"

Ridhiwani Kikwete (CCM)

"Mimi ni miongoni mwa wabunge niliotishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar, na mpaka sasa mimi sikanyagi Dar licha ya kuimisi sana"

Hillary Aeshi (CCM)

Tafakari, Chukua hatua

Na Yericko Nyerere
 

kipumbwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Messages
2,306
Points
2,000

kipumbwi

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2015
2,306 2,000
Yericko Nyerere najua walikuteka,hujawahi funguka kiundani,upo tayari kutuelezea hapa haswa ulitekwa na kupelekwa safe house zilizopo wapi kabla ya hawajakupeleka central? Kwenye utekaji na utesaji wao walisema wametumwa na Ikulu ama na kina nani?!

Kuna mipumbavu fulani huwa inatuhubiria kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani,sijui wanamaanisha Tanzania iliyopo pluto ama hii ya mijegeje na kufokewa!!

2020 bila ya umma na viongozi wa dini kuamka,wengi tutauawa,nchi itadidimia!!
 

Mushi92

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Messages
3,922
Points
2,000

Mushi92

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2013
3,922 2,000
Tangu kutekwa kwa kibanda.... Hadi roma serikali imekiwa ikishutumiwa kuhusika.
Na hawa wabunge waloambiwa live na mkuu wa mkoa flan ambaye ni mtoto wa mfalme kuwa atashughulikiwa anaongeza ushahidi juu ya hili.
Kama serikali imefikia kuyafanya haya... Je sisi wadogo tunajifunza nn.
Kwa hali ilivyo mtu akisema akisema aunde kikundi cha revenge hakika atapata wafuasi wengi na hapo ndo mwanzo wa vikundi vya waasi
 

Kingo

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2009
Messages
838
Points
250

Kingo

JF-Expert Member
Joined May 12, 2009
838 250
Tuone Kidogo STATISM
Authoritarianism, view a strong, authoritative state as required to legislate or enforce morality and cultural practices. The ideology of statism espoused by fascism holds that sovereignty is not vested in the people but in the nation state, and that all individuals and associations exist only to enhance the power, prestige and well-being of the state. It repudiates individualism and the family and exalts the nation as an organic body headed by the Supreme Leader and nurtured by unity, force, and discipline. Fascism and some forms of corporatism extol the moral position that the corporate group, usually the state, is greater than the sum of its parts and that individuals have a moral obligation to serve the state.

Statism - Wikipedia
 

Forum statistics

Threads 1,392,604
Members 528,644
Posts 34,112,492
Top