Comi
JF-Expert Member
- Oct 2, 2011
- 3,328
- 958
Baada ya wabunge kukutana tena jioni hii,spika wa Bunge Bi Anna Makinda ameahilisha tena shughuri za bunge mpaka kesho asubuhi.Ikumbukwe kwamba leo ndio ilikuwa ni uwasilishwaji wa taarifa za kamati.
Bunge limeahilishwa lakini malipo na posho kwa wabunge ziko palepale,kama majadiliano yalikuwa ya wiki mbili yaani 14,basi engeza siku moja tena,hivyo basi ni siku 15 badala ya siku 14.Kama malipo na posha kwa siku moja ni jumla ya pesa za kitanzania Milioni 85,basi zongezwe tena milioni 85 za siku moja iliyoongezeka.Ni hasala kubwa sana kwa Taifa letu,lakini hasara hii ya m85 za siku moja imesababishwa na nani kati ya hawa.
Mtoa taarifa Mh James Mbatia,waliofanya maandamano jana,Jeshi la Polisi au Bi Anna Makinda?
Vilevile ikumbukwe kwamba,wanaoumia zaidi na hasara ya pesa hizo ni tabaka la chini (lower class) ambao ni Waalimu,Machinga,wachoma mikaa,wauzaji wa kuku mjini na vijijini,wauza vitumbua,wapepetaji wa chenga za mpunga mashineni.
Huku Tabaka la juu (Higher class) likizidi kufaidika,lakini wakumbuke kwamba hawa tabaka la juu wenye majumba na magari ya kifahari,siku ikifika majumba na magari hayo yatakuwa ni magofu ambayo mavi ya kila aina ya wanyama kama vile fisi,Pimbi na ndege kama popo,bundi yatakuwa yamejaa,yaani yatakuwa makazi ya viumbe na sio wao tena. Tuchukueni maamuzi magumu sana katika uchaguzi wa okutoba 2015.
Anayecheka leo si yule atakayecheka kesho. The life of human bieng in the universe is like the shape of the World/Earth.Tafakari.
Wilbert Pm's Mandago.Katibu chadema (W) Kwimba.
Mshululu@yahoo.com.0765183733
katika makundi yanayoumia watoe waalimu maana wao wanaikumbatia hii serikali. pia naomba nikurekebishe hakuna aliyeandamana bali walikuwa katika maandalizi wakazuiwa. hata ukiangalia maelezo ya akina. lipumba walikuwa wanaenda zakiem kuwatawanya watu waliokuwa wametangulia kule.