Nifunge AC ipi kwenye nyumba yangu?

Mjuzi Wenu

Senior Member
Nov 18, 2017
108
100
Habari, kutokana na mada za watu tofauti wakiomba kufahamishwa kuusu aina gani ya AC wafunge nimeona nije na hii mada itakayo weza kutoa muongozo kwa yule mtu ambaye anahitaji kufunga AC kwenye ofisi au nyumba yake.

Kwanza tunajua kuwa kuna aina za ac hushauliwa kufungwa maofisini na kuna zile ambazo hufungwa majumbani hii ni kutoka na wingi wa watu wanaoweza kuwepo katika sehem husika mfano kwenye mabenk unawez kukuta watu zaidi ya 20 hii inaongezea kuongezeka kwa humidity katika hilo eneo na kupeleke AC kutoweza kufanya kaza kwa ufasaha.

1.Ukubwa wa eneo
Ushauriwa kuwa kabla ya kufunga AC inabidi ujue ukubwa wa eneo unalohitaji kufunga AC pia ujue wastani wa idadi ya watu wanaotazamiwa kukaa katika eneo hilo kwa mfano wastani wa watu wanaoweza kukaa bedroom ni tofauti na sitting room hii ni kutokana humidity inaongezeka kulingana na idadi ya watu hivyo hupelekea AC kutokufanya kazi kwa ufasaha na kuwai kualibika mapema.

2. Matumizi ya Umeme
Baada ya kujua ukubwa wa eneo lako unalotaka kufunga AC, unatakiwa ujue pia matumizi ya umeme utakao tumika ili iwe rahisi kujua gharama za umeme pia kujua ufanyaji kazi wa kifaa chako pale tu kitakapo fungwa. Mfano; kwa chumba chenye ukubwa wa 25-35 mita za mraba kinawez kikatumia umeme wa 3.5 KW kwa saa.

3.Eneo sahihi la kufunga AC
Eneo pia linaweza likawa kikwazo kwenye matumizi ya AC kwasababu linaweza kupelekea matumizi makubwa ya umeme au kufanya kifaa kisiweze kudumu kwa muda mrefu.
Mfano; inashauliwa outdoor unit isifungwe upande wenye jua au seheme iliyo bana ili kupunguza matumizi ya umeme yasiyo ya lazima kutokan n kifaa kutumia nguvu kubwa kwenye kupooza refrigerant

kwa nini tunazingatia haya
  • Kupunguza gharama ya matumizi ya umeme
  • Kupata ufanisi mzuri wa AC zetu pale tunapo zitumia
  • kupunguza gharama za matengenezo
  • kufanya kifaa kidumu kwa muda mrefu
MUANDAAJI
ENG. Mjuzi Wenu
AC distributor and Installer
Contact 0692235221
 
WaTz wengi wanajikuta wana matumiz makubwa sana ya umeme kwasabab ya kutozingatia utaalam ktk kufunga AC...
Kuna jamaa nyumba yake ina AC sitting room, bedroom na chumba kimoja cha watoto. Kwa mwezi anatumia umeme wa 260,000
 
WaTz wengi wanajikuta wana matumiz makubwa sana ya umeme kwasabab ya kutozingatia utaalam ktk kufunga AC...
Kuna jamaa nyumba yake ina AC sitting room, bedroom na chumba kimoja cha watoto. Kwa mwezi anatumia umeme wa 260,000

Utaalam huo ni upi?
Size ya AC na size ya eneo husika?
Power consumption ya appliance?
Matumizi ya AC?

Kipi kinapokosewa kwenye installation ya AC kinapelekea matumizi makubwa ya umeme?
 
Maana yake mtu ajiandae na 10000 ya umeme kwa masaa 12
inategemea na ufungaji wa fundi pia ushauli kutoka kwa mtaalamu jinsi ya kuilindi na kuitunza ili ifanye kazi kwa ufanisi na kwa gharama iliyo kusudiwa
 
Utaalam huo ni upi?
Size ya AC na size ya eneo husika?
Power consumption ya appliance?
Matumizi ya AC?

Kipi kinapokosewa kwenye installation ya AC kinapelekea matumizi makubwa ya umeme?
kwanza kabisa vitu vinavyo weza kupelekea AC kutumia umeme kupita kiasi ni
-uchafu katika chujio
-kufeli kwa baadhi ya vifaa vya AC mfano capacitor au motor
-AC ya kizaman au iliyo pita mda wake
-ufungaji mbovu
-kiasi kidogo cha refregerant

Ufungaji mbovu
Mfano fundi akifunga ac katika eneo kubwa kupita uwezo wa AC yaan over sized itapeleke mzunguko wa mfumo wa AC kuwa mfupi na hii itapelekea AC kujizima baada ya kupooza na kujiwasha muda mfupi tuu baadae hii ni kutokan na ukubwa wa eneo
pia tunajua kuwa AC huwa inatumia umeme mwingi pale inapowaka kuliko inapokuwa katika muwako huwa ina maintain hivyo basi kulingan na kujizima na kujiwasha kwa AC mara kwa mara hupelekea ongezeko kubwa la matumizi ya umeme kuliko AC inayo kuwa katika mfululizo wa kuwaka kwa muda mrefu
 
Back
Top Bottom