Infopaedia
JF-Expert Member
- Oct 28, 2011
- 1,231
- 1,487
Pia kama una AC, hapa panakuhusu.
Twende moja kwa moja kwenye mada. Watu wengi tunamiliki majokofu au friji lakini tunauelewa mdogo juu ya utendaji wa hichi kifaa. Kimsingi, kama mtumiaji hautakiwi kuwa na uelewa sana juu ya utendaji wa jokofu lako. Wataalamu au mafundi wanaohudumia jokofu lako wakati wa matatizo ndio wanatakiwa wawe na uelewa na wakupe miongozo mbalimbali juu ya kifaa chako. Kwa bahati mbaya sana, mafundi wengi wa majokofu hawana uelewa huo. Hapa ndipo tatizo linapoanzia na kukulazimu mmiliki wa jokofu uwe na ABC fulani juu ya kifaa chako, kitu ambacho si cha lazima sana. Na hapo ndipo nilipoona kuna haja ya kuleta kwenu uzi huu.
Kiini cha uzi huu ni kuhusu tatizo la ujazaji wa gesi kwenye majokofu yetu Pamoja na AC za majumbani kwetu.
Ili tuweze kuelewana vizuri, naomba nielezee jinsi mfumo wa upoozaji ndani ya jokofu unavyofanya kazi.
Kimsingi mfumo wa upoozaji kwenye jokofu lako una sehemu kuu kama tatu hivi. Yaani COMPRESSOR, CONDENSER, NA EVAPORATOR.
Compressor kazi yake ni kuisukuma gesi iweze kuzunguka kwenye mfumo wa upoozaji. Inaisukuma gesi kwenda kwenye EVAPORATOR, ikitoka kwenye EVAPORATOR inaenda kwenye CONDENSER na kurudi tena kwenye COMPRESSOR, mzunguko unaanza tena na kuendelea. CONDENSER na EVAPORATOR ni mirija au tube katika muundo wa zigizaga zilizotengenezwa kwa shaba au malighafi nyingine yoyote inayoweza kubadilishana jotoridi kwa wepesi kama kielelezo cha mchoro kinavyoonyesha hapo chini.
Wakati gesi inafanya mzunguko au inazungushwa kati ya CONDENSER na EVAPORATOR ndipo inapofanya upoozaji. EVAPORATOR huwa iko ndani ya jokofu, yaani mule kwenye kabati ya baridi. CONDENSOR huwa nje ya jokofu upande wa nyuma. Gesi wakati inazunguka, ikipita kwenye EVAPORATOR inachukua lile joto na kwenda nalo nje kwenye CONDENSOR. Ikifika kwenye CONDENSOR inaliachia lile joto na gesi kuwa imepoa, inarudi tena kwenda kukusanya joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Kwa gesi kufanya mzunguko huo na kazi ya kutoa joto ndani ya jokofu, ndani ya jokofu hubaki na ubaridi. Hapo chini kuna kielelezo cha picha
kikionyesha jinsi mpangilio wa COMPRESSOR, EVAPORATOR, na CONDENSER unavyokuwa kwenye jokofu.
GESI
Tumeona kwamba, gesi kwenye jokofu kazi yake ni kuzunguka, kuchukua joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Inasukumwa kurudi ndani kuchukua tena joto kupitia EVAPORATOR, inakujanalo nje na kuliachia kupitia CONDENSER.
TAMBUA
Katika hali ya kawaida, gesi katika jokofu lako haitakiwi kuisha. Tumeona hapo juu jinsi gesi inavyofanya kazi ndani ya jokofu lako. Haiungui kama mafuta ya gari tuseme kwamba inaisha. Gesi ipo kwenye mzunguko wa mduara ambao umefungwa na hufanya kazi kupitia mirija kama tulivyoelezana hapo juu. Yaani unaweza ukazaliwa mpaka unazeeka, jokofu lako likawa linapoza kama kawaida. Na bahati mbaya sana mafundi wengi wa mifumo ya kupooza hawajui kwamba gesi haitakiwi kuisha katika hali ya kawaida.
Sababu moja kubwa ya kuisha gesi kwenye jokofu ni kuvuja kwa gesi. Pale ambapo kunakuwa na tundu kwenye mfumo wa mzunguko wa gesi na gesi kuanza kuvuja.
Kwanza fundi anatakiwa atatue tatizo la kuvuja kwa gesi ndipo ajaze gesi kwenye kifaa chako. Tofauti na hapo anakupa suluhu ya muda mfupi tu kwa kujaza gesi bila kuzuia kuvuja. Baada ya muda mfupi utamtafuta akujazie tena gesi. Kisheria huu ni wizi. Yawezekana wanafanya makusudi, inawezekana pia hawajui kwamba lazima kutakuwa na tatizo la gesi kuvuja sababu katika hali ya kawaida gesi haitakiwi kuisha. Pia inawezekana fundi anajua ila hataki kujisumbu. Au anajua ila anauhakika hutamlipa gharama za kutafuta leakage au panapovuja.
Kama una jokofu lako ambalo unajaza gesi kila baada ya muda Fulani, sasa ni wakati wa kulitengeneza na kuzuia kuvuja ili kuepuka gharama zisizo za lazima. Fundi anatakiwa atafute gesi inapovujia, adhibiti hiyo sehemu. Baada ya hapo atafanya majaribio ya kuhakiki kama mfumo hauna sehemu inayovujisha gesi. Jaribio hilo atalifanya kabla ya kujaza gesi. Na jaribio hilo la kuhakiki afya ya mfumo linaitwa ‘pressure test’. Baada ya kufanya pressure test na kujiridhisha afya ya mfumo wa upoozaji, atafanya ‘vacuum’. Hapa ataondoa hewa iliyoingia kwenye mfumo wa upoozaji. Sababu baada ya gesi kuvuja na kuisha, hewa ya kawaida huchukua nafasi na kuingia kwenye mfumo. Hii hewa haitakiwi. Endapo gesi itajazwa bila kutoa hewa iliyoingia, ufanisi wa gesi kupooza utapungua na utashangaa kwamba jokofu langu sikuhizi halipoozi vizuri. Ni kama mafuta ya gari uchanganye na kimiminika kingine. Lazima ufanisi wa mafuta utapungua. Ndani ya mfumo wa kupooza inatakiwa iingie gesi peke yake ili ifanye kazi kwa ufanisi wa juu.
Katika pitapita yangu na kukutana na mafundi wa mifumo ya kupooza, sikumbuki kumuona fundi ana ‘vacuum pump’. Yaani pump au kifaa cha kuondolea hewa kwenye mfumo wa kupooza wa jokofu au AC.
Nawatakia upambanaji mwema.
Wakatabahu