Yajue mambo manne yanayomaliza sana hela katika haya maisha

hata mimi

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
930
1,000
Habari...

Kumradhi, ninaandika kwa kifupi sana

Kuna mambo mengi yanayomaliza pesa katika maisha haya ila manne kati yao ni kiboko. Mbaya zaidi ni kwamba mtu hawezi kuyakwepa

1.Ujenzi
Achilia mbali nyumba, Kitasa cha mlango tu elfu sabini! Fikiria kuhusu mlango wenyewe

2.Maradhi
Nadhani wenyewe mashahidi operesheni kwa jk institute ni milioni zake na hela, halafu wanakuwekea na neno tu!

3.Elimu
Waulizeni wanaosomesha; ada ya chuo cha urubani tu ni pension ya mzee halafu mnakuja kushangaa kwanini unesi au ualimu unakuwa na wahitimu wengi (umekuwa kimbilio la wengi) licha ya kuonekana kama sekta dhalili

4.Kesi
Dhamana tu milioni tano, kesi haijaanza kuunguruma hapo. Japo napo panategemea aina ya kesi na kesi/mahakama ila ilimradi tu imeitwa kesi basi ni kisa hasa

Tumwombe MwenyeziMungu huku tukiendelea kujipinda ili tuepukane na madhara ya mambo hayo (mfano kesi na maradhi) na tufaidi mazuri yake (mfano elimu na ujenzi)
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
23,266
2,000
vinavyomaliza pesa hapo ni viwili tu.

maradhi na kesi.

ujenzi na elimu haviji kama ajali.unajua kabisa ni jukumu linalokuhusu,ndio maana huwezi kudata sababu yake,labda kama umeparamia ukuta mrefu usio size yako.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
23,266
2,000
Kuna gharama zinakwepeka kwa kuishi maisha yanayofanana na wewe,mfano ujenzi: umetoa mfano wa kitasa cha sh 70,0000. lakini kuna kitasa cha sh 30,000.kinaweza kudumu hata miaka10 .
hii ni sawa kabisa na kufunga nyumba na kufuli ya elfu 6,ndani kuna tv ya laki 8.

kitasa cha elfu 30 ni kizuri ila labda milango ya ndani huko,nje pale gate kuu lazima ukaze matako,no way.
 
Craig

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
1,071
2,000
Pesa inamalizika kwenye matumizi yanayojirudia kila siku, hayo uliyoyaandika yanatumika kimazoea tu ili kufarijiana.

1Chakula
2Umeme/Nishati
3Maji
4Mafuta/Usafiri/Nauli
5Kuhonga
6 Vilevi/Pombe/Unga/Casino.
7Mavazi/Malazi
8Watoto
9Wakwe
10Wazazi/Ndugu/ Wategemezi.
 
Ujue mambo ya kila siku yanakula hela sawa ila ile ni papo kwa hapo you spend as you earn ila izo ngoma hapo juu ni hela ya mkupuo ambayo huwa ndo inaonekana zaidi (pengo lake)
 
hata mimi

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
930
1,000
vinavyomaliza pesa hapo ni viwili tu.

maradhi na kesi.

ujenzi na elimu haviji kama ajali.unajua kabisa ni jukumu linalokuhusu,ndio maana huwezi kudata sababu yake,labda kama umeparamia ukuta mrefu usio size yako.
Hata kama haviji kama ajali ila unavifanya huku unavisifu bosi (kwamba vinakufilisi)
 
Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
482
1,000
Habari...

Kumradhi, ninaandika kwa kifupi sana

Kuna mambo mengi yanayomaliza pesa katika maisha haya ila manne kati yao ni kiboko. Mbaya zaidi ni kwamba mtu hawezi kuyakwepa

1.Ujenzi
Achilia mbali nyumba, Kitasa cha mlango tu elfu sabini! Fikiria kuhusu mlango wenyewe

2.Maradhi
Nadhani wenyewe mashahidi operesheni kwa jk institute ni milioni zake na hela, halafu wanakuwekea na neno tu!

3.Elimu
Waulizeni wanaosomesha; ada ya chuo cha urubani tu ni pension ya mzee halafu mnakuja kushangaa kwanini unesi au ualimu unakuwa na wahitimu wengi (umekuwa kimbilio la wengi) licha ya kuonekana kama sekta dhalili

4.Kesi
Dhamana tu milioni tano, kesi haijaanza kuunguruma hapo. Japo napo panategemea aina ya kesi na kesi/mahakama ila ilimradi tu imeitwa kesi basi ni kisa hasa

Tumwombe MwenyeziMungu huku tukiendelea kujipinda ili tuepukane na madhara ya mambo hayo (mfano kesi na maradhi) na tufaidi mazuri yake (mfano elimu na ujenzi)
5. Mapenzi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom