Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5, Top 3 na Hatimaye Mgombea wa CCM!

Pasco We jamaa nimekukubali ni una akili sijui umesoma shule gani? dah!!! much respect kaka!!!
 
mkuu kimbunga, yes membe ni maarufu kuliko magufuli, ila magufuli ni mashuhuri kuliko membe!. Wengi wanashindwa kutofautisha kati ya umaarufu na umashuhuri!. Umaarufu ni popularity na umashuhuri ni prominence!.

Nikikuambia diamond platnum ni maarufu kuliko rais kikwete utakataa?!. Nimewashuhudia rais kikwete na diamond!.

Pasco

umeanza pumba sasa maana hujui unachokisimamia
 



Presidential Material ni sifa na uwezo, wakati ufisadi ni tabia!. Wana jf lazima tufike mahali tutenganishe sifa ambazo ni qualities na tabia ambazo ni human nature!.

Presidential material ni mtu mwenye sifa na uwezo wa urais, lani naweza kuwa na tabia na matendo ya ajabu, ambayo hayamuondolei sifa na uwezo wa urais. Tenganisha sifa na uwezo wa mtu wa kufanya jambo na tabia zake binafsi!.

Mfano kwa wale wa zamani, mtakuwa mnamfahamu Prof. Shaba wa Muhimbili Hospital, he was the best pathologist Tanzania had ever had, but alikuwa ni mlevi!, lakini pamoja na ulevi wake, bado kwenye kazi he was the best!.

Wenzetu wazungu ndio wanao oanisha sifa za uongozi na tabia ya mtu, mfano hata ukiwa na sifa njema na uwezo mkubwa kiasi gani, ukigundulika umekwepa kodi, au umetoka nje ya ndoa, kunakuondolea sifa za uongozi lakini huku kwetu Afrika, uongozi ni uongozi na tabia binafsi za mtu ni tabia, hii ni kitu inayoitwa 'the African Democracy'. Kwa watu wanaojua tabia binafsi za Jacob Zuma na ufisadi wake, umalaya wake, na ulevi wake, wasingeamini kama angeweza kuchaguliwa kuwa rais wa Afrika ya Kusini, tena alivyo mgonjwa wa 'chini', sio mara moja wala mbili, ametamani, akaomba na kukataliwa, anaamua kubaka!. Kwa mila yao ukibaka 'sealed' ukafungua wewe, unalipa 'lobola' unachukua jumla anakuwa mke wako!.

Bill Clinton akiwa rais wa Marekani, alipata 'denda' toka kwa kidemu Monica Lewinsky, kidema kikamuhadithia mwanamke mwingine Linda Tripp kuwa Clinton amekula 'denda' Oval Office!, ilikuwa issue!, hadi Bazaza la Senet likaanza process ya impeachment lakini mkewe Hilary akakomaa kubakia kwenye ndoa, ukiingia madarakani hata ukigombana tuu na mkeo akaomba talaka, uongozi basi!. Ukitembea nje ya ndoa ukajulikana, kazi basi!.

Zimbabwe rais Robert Mugabe, wakati mkewe Sally akiwa yungali hai, alikuwa akichepuka na mfagiaji na mleta chai wa Ikulu, sometimes game likirindima kwenye meza ya Ikulu!, mkewa alipofariki, mhudumu huyo akaolewa na mpaka sasa ndio first lady wa Zimbabwe!.

Jakaya ndie rais wetu, ni presodential material, ana sifa za urais ndio maana yuko ikulu yetu miaka 10 sasa, jee unazijua tabia binafsi za rais?. Officially anajulikana ana watoto 8, kati ya hao, unawajua wa mama Salma ni wangapi?, unawajua hao wengine mama zao ni nani?, jee waliolewa?, jee watoto wake ndio hao tuu?. Mambo yote hayo kwa demokrasia za kiafrika ni tabia binafsi za mtu, have nothing to do with his presidency!.

Kama kwa Lowassa hoja ni ufisadi, wangapi humu wanazijua mbinu za Mtandao wa Kikwete uliotumika kumuingiza madarakani?!, wangapi humu wanaijua Kampuni ya Kagoda ilichota kiasi gani na kilitumikaje?!. Kama hoja aganst Lowassa ni ufisadi wa Richmond tuu, hiyo sio issue, hilo ni zigo la watu, wenye akili zao wote wanajua!. Hivyo kama ni ufisadi, CCM ni chama cha kifisadi systematically, hivyo wato ni mafisadi!.

Kwa maelezo hayo natumaini watu humu mtatenganisa uwezo wa Edward Lowassa at the top of Presidential Material na kutofautisha na tabia zake binafsi za kuuchukia umasikini!.

Kuhusu ufisadi wa Lowassa, mnaweza kosoma hapa
Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa


Ila pia kuna wengi wanadhani tunalazimisha lazima Lowassa awe rais!, no!, mnaweza kusoma hapa!.
Edward Lowassa sio lazima yeye tuu ndiye awe Rais wetu


Pasco.

Bado uko pale pale kama kawa unaspin, umejaribu kutengeneza haja lakin haina mashiko,tena mbaya sana UMEJUSTIFY kuonyesha kuwa CCM wote ni MAFISADI ili mtu wako AOGELEE kwenye bahari moja na IONEKANE wote wako hivyo....Nooooo bado uko chaka tu...nani asiyejua kuwa CCM ndani yake kuna watu WAADILIFU na wenye MAPENZI na NCHI yao, wapo kedekede.Uchafu wa kikundi cha watu fulani ndani ya society hauwekwi kuwa ndio tabia ya wote.Ulevi wa Wanaume wa Rombo haujustify kuwa Wanakilimanjaro wote ni wadhaifu kwenye nyumba zao mpaka kina mama wanaagiza Tarakea Kenya.Unachokipigania najua UNAMSALHI nacho uwe fair sio utumie karamu ya [keybord yako] kuhujumu AKILI ya wengine ...ukizingatia mihemuko ya mazingira yanayotengenezwa na mlio kwisha tengeneza miaka sita iliyopita kumbe wenzenu walianza miaka kumi iiyopita.Kuna kitu inaitwa USE and ABUSES ukiwa ni mtu wa KUFIKILIA jinsi KUFIKILI basi utajua STUDY CASE hiyo nawe pia waweza kuwa client pia kwa sababu.How Pasco wa JF awe client..kwa kuwa toka niko humu umeishi ukitetea kitu kile kile for number of years, kiasi kuwa Great Thinkers waioko humu ukitafuta walio kwenye msimamo mmoja na wewe kwenye kufikiria kuhsu kufikili utagundua your almost ALONE.Kwenye hoja hiyo acha wale wa kuja na ID za msimu nnooo nazungumza JF Member serious like you.

Sasa kiwango chako cha kuona katika kufikilia juu ya ufikili wetu naona UMESTUCK na sasa unachofanya ni kama mtu yuko kwenye ksima cha tope anastruggle kujinasua lakini kila anachokfanya katika kutafuta kujinasua na tope lile ndio anavyodhidi kudidimia.Sheria ya tope ni muhusika kukaa kimya ndani ya tope katika style ya UTULIVU hili wenye HURUMA wakikuona ulivyo basi watatafuta njia ya kukunasua kwenye TOPE.Lakini unasuaji huo unategemea USIJE ukawa ni KIBAKA umechomoa pochi ya Mama Mpeleka Mtoto Clinic kisha ukakimbilia kwenye Kisima cha Tope Ukitegemea Watu UJIFICHE na kuwa kiwingu cha watu kikisha sambaratika UTAIBUKA toka kwenye tope USEPE zako ukiwa HERO....No thubutu...Kwani ulijua ULEFU wa kina Cha Kisima cha Tope.

Kuna watu waliingia kwenye visima vya matope wakaonekana wana umuhimu wa kulushiwa kamba watoke kwenye rojorojo lile walitoka na sasa hivi kila wanakuzunguka wako free from stress za Public Image ..Sasa ukijiulza katika kufikiria iweje Juniors waibuliwe kwenye Matope Seniors waachwe na bado wewe Pasco uone hoja zako ziko sahhi...yani katika kuwaza na kufikiria uko kudogo tuuu bado una pata wapi muscles za kufurukuta kwanza unaweza kuwa Mike Tyson [undisputed Champion] kupigana na Lewis ebu tujikumbushe hapa:
''This was hard to believe. Lewis is enormous—six-five, two hundred and forty-odd pounds, and with the musculature of a tight end—and yet neither his fighting style nor his character suggests a tendency to rage. He is laid-back, meticulous in his training habits, a moralist. There is something high-minded about him, at least relative to Tyson. Lewis had been offended not merely by the nibble in New York but also by a meeting with some invited reporters which Tyson had conducted in his training camp in Hawaii just a few days earlier. It had been a vintage Tyson performance, full of contempt for his visitors and fury at the world; there is more nihilism in an hour with Tyson than in a chapter of “The Possessed.”

Ukiludi kwenye hoja ya tabia ambazo zinashadadiwa na Waafrika na kufanywa ni Afrikan democracy ukweli tabia hizo ambazo ni personal ni mbili tu...moja ni Mapenzi [Wakina Mama] ambayo pia ni aina ya kilevi [opium] na tabiia ya pili ni Ulevi wa Pombe.Tabia nyingine uliyoisema UFISADI ikiwa mixed na RUSHWA noo hiyo siyo tabia ambayo Waafrika wa Makabila yoyote wanaweza kuikumbatia hata kidogo na kusema jamani huyu Mwenzetu ni fisadi ngoja twende nae hivyo hivyo ana jambo zuri litatusaidia mbele ya Safari.Hapana Pasco usifanye spinning za hivyo UNACHANGIA KUUA TAIFA ..uwezi kuwa na watu ambao kupitia UFISADI wana UWEZO wa kuuza TAIFA useme tabia hiyo ni sehemu ya UTAMADUNI wa Mwafrika,usidharau TAIFA kiasi hicho as if hakuna watu ambao ni CRTICAL THINKERS.

Ninavyotambua mimi tabia ambayo waafrika wote wanaweza kuivmilia ni KUPIGA MAJI -yani kunywa Pombe, hiyo fanya yote hata kama kiongozi wao ni cha pombe kama Profesa Shaba walikuwa wako tayari kumvumilia na kumfuata IFM akiwa chakali ili akapige kazi...Na watu wa aina ya Pro Shaba sekta za Enginering, Health na Geology ni wengi mno na wanachapa kazi ni balaa.Lakini ule ugonjwa wa kina Mama Waafrika Watanzania wana umakini nao pia sio kila mzunguka kwa kina Mama nae anapokelewa kwa kwa mikono miwili ukizingatia ni ka mchezo ka kujificha ambako ushahidi na uthibitisho wahitaji Evidence za kutosha.Kama muhusika ni mpita pita na wake na wachumba za watu hakika utamaduni wa Mwafrika HAUMKUBALIMTU HUYO HTA KIDOGO na watu walishasema Mke wa Mtu ni sumu na jamii nzima ipo tayari kumtafutia TIBA mujarabu dhidi ya ugonjwa wake huo, kama uwa anabanjuka na wake za watu.Na daima TIBa hiyo huwa chungu na ya sumu kisaikolojia zaidi ambayo inaua AKILI na MWILI taraatibuuu .natumai Pasco Unaifahamu vyema.Wabongo ukiwa sekta ya kinamama na magauni wewe ruka na kina dada mitaani huko wasio na waume, ukibahatisha mabinti wasomi wa level yoyote uwezevyo ilimradi usikamatwe basi wewe kazi na dawa wewe kuwa SUKARI YA WAREMBO si walishasema KAZI NA DAWA.

Kwa yote hayo Pasco nimejaribu kusema kile ambacho kiafrika kila Mtanzania anakifahamu katika uhalisia yani MITUNGI na MIKASI ...aka Mimi aka marehemu mangweah alipata kuimba kwenye wimbo wake wa MIKASI....Lakini ili lako la kutaka KUJUSTIFY UFISAID [ambao kwa lugha nyepesi NI WIZI WA MALI YA UMMA KWA TIKETI YA MAMLAKA VESTED to THE PERSON WHOM has An Authority Kwenye Jambo husika].

Hapana Tunga upya Pasco UFISADI SIO HAIBA .ufisadi ni IMMORAL [ reflections of behaviour against society]

 
swali langu,namba hizi ktk @ kundi zinaendana na umuhimu wake? i.e uliyemwandika namba moja n.k ktk kila kundi ndo namba moja n.k pia ki umuhimu,yaani anaongoza kwa umuhimu ktk kundi tajwa?ukitoka wiki ya utumishi wa umma tunasubiria majibu
 
Mashuhuri ndio wale Presidential Materials, ukumbuke hata Stalin na Hitler walikuwa ni ma populist leaders waliopendwa na watu!. Hata Amin alipendwa!.

Pasco
huko unakoenda siko! Hata JK pia alipendwa sana na watu lakini ana tofauti kubwa sana na hao uliowataja.
 
Sasa ukijiulza katika kufikiria iweje Juniors waibuliwe kwenye Matope Seniors waachwe na bado wewe Pasco uone hoja zako ziko sahhi...

Hapana Pasco usifanye spinning za hivyo UNACHANGIA KUUA TAIFA ..uwezi kuwa na watu ambao kupitia UFISADI wana UWEZO wa kuuza TAIFA useme tabia hiyo ni sehemu ya UTAMADUNI wa Mwafrika,usidharau TAIFA kiasi hicho as if hakuna watu ambao ni CRTICAL THINKERS.

natumai Pasco Unaifahamu vyema.Wabongo ukiwa sekta ya kinamama na magauni wewe ruka na kina dada mitaani huko wasio na waume, ukibahatisha mabinti wasomi wa level yoyote uwezevyo ilimradi usikamatwe basi wewe kazi na dawa wewe kuwa SUKARI YA WAREMBO si walishasema KAZI NA DAWA.

Kwa yote hayo Pasco nimejaribu kusema kile ambacho kiafrika kila Mtanzania anakifahamu katika uhalisia yani MITUNGI na MIKASI ...aka Mimi aka marehemu mangweah alipata kuimba kwenye wimbo wake wa MIKASI....Lakini ili lako la kutaka KUJUSTIFY UFISAID [ambao kwa lugha nyepesi NI WIZI WA MALI YA UMMA KWA TIKETI YA MAMLAKA VESTED to THE PERSON WHOM has An Authority Kwenye Jambo husika].

Hapana Tunga upya Pasco UFISADI SIO HAIBA .ufisadi ni IMMORAL [ reflections of behaviour against society]

Mkuu asante, nimekusikia na nimekuelewa!.
Pasco
 
  • Thanks
Reactions: DSN
swali langu,namba hizi ktk @ kundi zinaendana na umuhimu wake? i.e uliyemwandika namba moja n.k ktk kila kundi ndo namba moja n.k pia ki umuhimu,yaani anaongoza kwa umuhimu ktk kundi tajwa?ukitoka wiki ya utumishi wa umma tunasubiria majibu
Mkuu, kwenye list yoyote inayoitwa top, unaanzia juu, yaani kwenye top ten, tunahesabu kuanzia juu!.

Pasco
 
Mkuu umejitaidi kupanga hayo makundi lkn nimeona kama haukua free. Imean hisia zako zipo kwa watia nia fulan. Maana kuna ulowapanga mahari sipo kabisaaa.
 
Mkuu Majimojaumejitaidi kupanga hayo makundi lkn nimeona kama haukua free. Imean hisia zako zipo kwa watia nia fulan. Maana kuna ulowapanga mahari sipo kabisaaa.
Mkuu , ruksa kupangua na kupanga upya!, pia kupachua mahali asiyehusika na kupachika anayehusika, mfano ukiona fulani kapangwa mahali sipo, ruksa kumbandua na kumpanga mahali panapomstahili!.

Pasco
 
Mwisho wa siku kuongoza ni kipaji anachopewa mtu, kuweza kuwafanya watu wakukubali na ukawatumikia ni kipaji. Wenye elimu kubwa na mapesa wamekuwa wanahangaika sana ili kuhararisha elimu zao kubwa walizonazo na mapesa yao ila walishindwa, haimaanishi kwamba mvuta sigara hawezi kuwa kiongozi kwasababu anavuta sana sigara wala kwamba kama hana makampuni ya biashara basi hawezi kuwa kiongozi ...charisma ndo asiri ya uongozi na mfano mzuri ni Mwalimu Nyerere wakati anatoka Butiama na kuamua kuja Dar hakuwa amewahi kuongoza popote zaidi ya kufundisha akitokea Makerere, wala hakuwa na pesa lakini waliomsikiliza mawazo yake walimwelewa na wakamkubali awaongoze, hiyo ndo nafasi ya uongozi sema tatizo sahivi mabepari wameamua kuunganisha uongozi na vitu, formalities zimekuwa nyingi ili kupunguza wenye uwezo wa asiri, kuwazuia wenye charisma ndo maana mara uwe hivi, uwe vile kitu ambacho wengi wenye asiri wanashindwa kwasababu hivi vigezo hawana, tunaishia kuwapata wenye hivyo vigezo lakini kimsingi si viongoI kwa asiri zao. Na kiongozi atakuwa kiongozi baada ya kwamba amepata nafasi na watu wakamwona ni kiongozi, mara nyingi usipopata nafasi ama ukawa kwenye mfumo ambao haukuruhusu kupewa nafasi kwa vile tu labda wewe si tajiri sana ama haukusoma maelimu makubwa basi utakufa na tarent yako hata kama ulikuwa na charisma by nature.
 
Majina saba yanayoumiza vichwa kamati kuu ya CCM
1) Augustino Ramadhan
2) John Magufuli
3)Mizengo Pinda
4)January Makamba
5)Benard Membe
6)Makongoro Nyerere
7)Mark Mwandosya

TOP FIVE ITATOKA HAPO ILA SHIDA NI HAO WAWILI WA KUTOA! NANI ATOKE?
Hayo mengine ni predictions zako mkuu ila list ni hiyo hapo!

CC Pasco

Haahaaa
Sipati picha...
Ngoja niulizie km kweli
 
Last edited by a moderator:
Sijaelewa kwa nini uweke mafisadi wenye sifa kubwa kabisa katika ufisadi wao eti kuwa mostpopular, au most prominent, au most popular. Mbona tunakuwa wepesi sana kusahau namna tulivyoumizwa na huyo mtu unayempigia debe?

Hata kama umelipwa kupiga promo ningeshauri uzingatie ukweli wa matendo yake na mbinu anayoitumia ya kujificha katika taasisi za kidini.
Mkuu , uwezo wa urais, (presidential material), umaarufu (popularity), na umashuhuri,( prominency) has nothing to do with ufisadi.

Mtu anaweza kuwa na uwezo mkubwa wa urais na bado akawa fisadi, dictator au fuska, hakumuondolei uwezo wake wa urais!.

Unaweza ukaoa, mke, ukampenda kwa moyo wako wote, na akakuzalia watoto wawili, hivyo kuwa ni mama watoto wako!.

Mke huyu anaweza kuwa malaya, kiruka njia, chawote, na kila sifa mbaya!, sifa zote hizi hazimuondolei sifa yake kuu kuwa ni mkeo na ndie mama wa watoto wako!, na hata ukiamua kumpa talaka asiwe tena mke wako, bado atakuhusu kama mtalaka wako na mama wa watoto wako forever!.

Pasco
 
Mkuu , uwezo wa urais, (presidential material), umaarufu (popularity), na umashuhuri,( prominency) has nothing to do with ufisadi.

Mtu anaweza kuwa na uwezo mkubwa wa urais na bado akawa fisadi, dictator au fuska, hakumuondolei uwezo wake wa urais!.

Unaweza ukaoa, mke, ukampenda kwa moyo wako wote, na akakuzalia watoto wawili, hivyo kuwa ni mama watoto wako!.

Mke huyu anaweza kuwa malaya, kiruka njia, chawote, na kila sifa mbaya!, sifa zote hizi hazimuondolei sifa yake kuu kuwa ni mkeo na ndie mama wa watoto wako!, na hata ukiamua kumpa talaka asiwe tena mke wako, bado atakuhusu kama mtalaka wako na mama wa watoto wako forever!.

Pasco

Sorry
Leo nimemuona Paschal Mayalla , star TV ,anachambua siasa kama mwana habari je n wewe au siye ? Nina jambo la kusema
 
Mkuu , uwezo wa urais, (presidential material), umaarufu (popularity), na umashuhuri,( prominency) has nothing to do with ufisadi.

Mtu anaweza kuwa na uwezo mkubwa wa urais na bado akawa fisadi, dictator au fuska, hakumuondolei uwezo wake wa urais!.

Unaweza ukaoa, mke, ukampenda kwa moyo wako wote, na akakuzalia watoto wawili, hivyo kuwa ni mama watoto wako!.

Mke huyu anaweza kuwa malaya, kiruka njia, chawote, na kila sifa mbaya!, sifa zote hizi hazimuondolei sifa yake kuu kuwa ni mkeo na ndie mama wa watoto wako!, na hata ukiamua kumpa talaka asiwe tena mke wako, bado atakuhusu kama mtalaka wako na mama wa watoto wako forever!.

Pasco

I usually rank you mediocre. But this is the lowest you could get. I'm sorry to use those words. Hunijui, sikujui!!
 
Sorry
Leo nimemuona Paschal Mayalla , star TV ,anachambua siasa kama mwana habari je n wewe au siye ? Nina jambo la kusema
Mkuu baro, don't be sorry, wengi wanatuchanganya hadi sisi wenyewe mimi Pasco na yeye Pascal pia tunajichanganya, ila sisi ni watu wawili tofauti, mimi ni Pasco wa jf, hili jina la Pasco ni just a pen name, yeye ni Pascal Mayala, pia ni member humu na ni verified. Kwa bahati nzuri tunafahamiana na sometimes tunakutana humu jf, kama unakitu unataka kusema kinamhusu, ukiniambia mimi kitamfikia, na kuna vitu vyangu kibao, akiambiwa vunanifikia, hivyo be free to say or ask anything, nikiweza kumjibia nitamjibia nikishindwa nitamtag atakuja kujibu mwenyewe!.

Pasco
 
I usually rank you mediocre. But this is the lowest you could get. I'm sorry to use those words. Hunijui, sikujui!!
Mkuu humu jf, tunatofautiana uwezo wa uchambuzi, ung'amuzi na uelewa, hivyo unapokutana na watu wenye level fulani ya uelewa, wanapokuita wewe ni mediocre, the best way kuwajibu ni "thank you!".

Pasco.
 
Back
Top Bottom