Yajue majengo yenye alama(symbol) za Freemason Tanzania

Hahaha haya mavitu mnayataka ya nini?! Mbona mungu hamumfahamu sijawahi sikia mtu akimuulizia amfahamu?! Mungu akija nani ayamfahamu au ndio kila mtu atatimua mbio?!
 
Hivi ni kuwa hawajui au imekuwaje ?
Screenshot_20190125-232401.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwann soko la samaki liko pale ferry karibu na ikulu alafu km hawalioni.
Si shombo zinamnukia rahisi wetu na makamo.
Hivi hawajui au imekuwaje?
 
Mkuu,kama ulikuwa hufahamu ni kwamba Freemason kwa Tz imesajiliwa kama taasisi huru inayojishughulisha na mambo mengi ya kijamii kama vile siasa,mazingira,elimu,afya na miundombinu
Pia,usisahau kuwa wakubwa wengi kwa ngazi za vyama na serikali ni wanachama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo watu hawako well informed kuhusu freemason,kuna freemason halisi na fake,freemason fake ni hao wanaojidai kutajirisha watu,freemason original ndo hawa wenye jengo karibu na ikulu,ni society ya kawaida haihusiani na mambo ya nguvu za giza
 
Sasa mkuu unataka viongozi wetu wapate shida kwenda kufanya ibada mbali?

Maendeleo hayana chama
 
Katika jamii ya Freemason alama ya jicho na alama ya pembe tatu ni miongoni mwa alama kuu za ibada katika jamii hiyo.

Alama ya jicho (All seeing eye ) ni alama ya jicho la muungu wa kifremason aitwaye Horus.
Na alama ya pembe tatu inamaanisha miungu mitatu ya freeamason ambayo ni muungu wa kike aitwaye Isis, muungu wa kiume osirus na muungu wa kuzalisha amabaye ni horus.

Sasa kiasili jamii hii ya freemason ni ya wajenzi huru wa majengo makubwa makubw ana madaraja .
Sasa ni kawaida yao kampuni za kifreemason zikijenga majengo kuacha alama (Symbol) katika majengo hayo .
Alama hizo (Symbol) ni alama ya jicho na alama pyramid.
Yafuatayo ni majengo yaliyojengwa na kampuni za kifreemason kutoka a na alama zao walizoziacha hapo.

1.Jengo la machinga complex Ilala .Ukiliangalia kwa juu lina alama ya pembe tatu na duara linaloashiria jicho.

2.Jengo la walimu Ilala Boma .Lina alama ya pembe tatu na duara la jicho.

3.jengo la bunge lina alama ya pembe tatu na jicho.
Hata katika meza za bungeni tazameni kwa makini kuna alama ya pembe tatu.
5.Jengo la mawasiliano kwa juu lina alama ya pembe tatu.

6.Majengo pacha ya bot yanaashiria Namba 11ambayo ni number ya kafara ya Freemason.(Mnakumbuka tukio la September eleven 11).
Pia alama za clock tower kuanzia za kule London hadi pale posta ni miongoni mwa ujanja ujanja wa Freemason katika kuweka alama zao katika miji mikubwa duniani na new world order.
Kazi kwenu wadau kuchunguza alama hizo katika majengo hayo na majengo mengine pia nchini
Uzi wako batili hauna teaching aids(picha)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom