Yajue Madhara ya Vipodozi vyenye Kemikali na Vipodozi Vilivyopigwa Marufuku

binadamu tunaangamia kwa kukosa maarifa.

mkorogo-1.jpg
 
Wanaume wa sikuhizi mnajipendezesha km wanawake...

Wanaume wa siku hizi mnatumia dawa za nywele..

Na si vipodozi tuu hata wapenzi wenye sumu mnatumia..tena sumu ya kuwaua taratibu sababu mnachepuka na kwenda kavu kavu...


Na si hayo tuu hata vyakula mnatumia vyenye sumu...Vinywaji vyenye sumu.....

poison poison poison full poison

Weka asilimia kutoka moyoni kama alivyoweka EMT, acha ile ya 90% maana sijui uliitoa wapi (au 90% ya mtaa unaoishi au nyumba unayokaa? maana kama ni nje kwenye jamii huku unaweza ukapishana na wanaume 50 ukakuta wawili ama watatu ndio wamejipiga kipodozi cha kufa mtu)
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
nimesikia inapelekea mimba nyingi sana kuharibika na wanawake wengi sahivi wanakumbwa na tatizo la kuharibikiwa mimba zao ..wanasema vipodozi,vyakula vya kisasa,mavazi kama viatu michuchumio vinavyowatoa vigimbi n.k ila najiuliza ni kwa faida ya nani kama serikali inalinda uhai wa watu inakuwaje isiweke wazi ili kuwasaidia dada zetu na mama zetu wasiendelee kuwapoteza watoto wao
 
Hali inatisha....hata sie tunaokula vya mashambani tunaambiwa vinalimwa kisasa mno...makemikali kibao. Dunia hii hakuna kwa kukimbilia

Jitahidi mboga mboga ulime mwenyewe mama.....

Ila kwenye michele humu sijui tufanyaje....
 
Lazima hawa watakuwa wanawapelekesha waume zao maana kwa wanaume wengi walivyo mtu ukijipaka vipodozi kwa design hii aisee lazima jamaa either usiongozane nae au mtaishia kubishana kuhusu kutopendeza, vipodozi vingine huwa tunavumilia tutafanyaje maana angalau mtu anaonekana lakini hawa utasema wamepaka unga usoni ule wa wacheza ngoma sasa umegoma kutoka baada ya kuufuta
 

Inasikitisha mkuu, sio jambo la kufurahi hata kidogo. Fikiria muda, pesa na morale waliyopoteza kwenye hayo makitu na bado wanaishia kuwa kituko hivyo. Mama yangu na umri wake wa miaka sitini hajawahi kutumia kipodozi lakini kawazidi mara elfu chache...
 
EMT unatakiwa pia uniambie ni vipodozi gani mwanamke anaweza akatumia na ngozi yake ina shine,ningependa kuwepo kwenye hiyo semina maana nina maswali mengi ya kuuloliza.
1.kwanini wanapenda kutoa leseni za maduka ya vipodozi wakiwa ofisini na hawakuambii kipi hakiruhusiwa hadi wanakuja dukani kumfilisi mtu mara hiki hakina sumu ila hakijasajiliwa....
2.kwanini nchi zote za east africa wanatumia hizo vipodozi kasoro tz tu maana kama ugada wameweka kwenye mashelfu kabisa hawaoni kuwa hiyo vita ni ngumu?
3.kwanini wasianze kuwakamata watumiaji tena waanzie mle bungeni maana kama yule sofia simba kajikomboa wakati alikuwa blk tu na mwingine NAPE?
4.
 
Last edited by a moderator:
Wanaume wa sikuhizi mnajipendezesha km wanawake...

Wanaume wa siku hizi mnatumia dawa za nywele..

Na si vipodozi tuu hata wapenzi wenye sumu mnatumia..tena sumu ya kuwaua taratibu sababu mnachepuka na kwenda kavu kavu...


Na si hayo tuu hata vyakula mnatumia vyenye sumu...Vinywaji vyenye sumu.....

poison poison poison full poison

Umesema kweli tupu!nimekupenda buree
 
EMT unatakiwa pia uniambie ni vipodozi gani mwanamke anaweza akatumia na ngozi yake ina shine,ningependa kuwepo kwenye hiyo semina maana nina maswali mengi ya kuuloliza.
1.kwanini wanapenda kutoa leseni za maduka ya vipodozi wakiwa ofisini na hawakuambii kipi hakiruhusiwa hadi wanakuja dukani kumfilisi mtu mara hiki hakina sumu ila hakijasajiliwa....
2.kwanini nchi zote za east africa wanatumia hizo vipodozi kasoro tz tu maana kama ugada wameweka kwenye mashelfu kabisa hawaoni kuwa hiyo vita ni ngumu?
3.kwanini wasianze kuwakamata watumiaji tena waanzie mle bungeni maana kama yule sofia simba kajikomboa wakati alikuwa blk tu na mwingine NAPE?
4.

Marire habari nimeiweka kama nilivyoikuta, hayo maswali sidhani kama nitaweza kuyajibu authoritatively.
 
mkorogo.jpg

"Tunafanya kampeni ya kupambana na vipodozi vyenye sumu kwa sababu tatizo ni kubwa nchini."Hadi sasa asilimia 52 ya Watanzania hutumia mkorogo. matokeo yake wengi wameathirika na wanashindwa kuacha." Euphrasia Shayo

KWA UFUPI
Kuna watu ambao hujitoa mhanga kwa vipodozi vilivyopigwa marufuku ilimradi wanaamini wakivitumia wanapendeza zaidi mbele ya macho ya watu na kupendwa.

Nuru Masoud, mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, amekuwa akijishughulisha na biashara za vipodozi vya asili, maarufu kama mkorogo.

Hata hivyo, biashara hiyo aliisitisha mwaka 2013 baada ya kupata madhara makubwa ya ngozi ambayo yaliambukiza pia familia yake.

"Nilianza kuwashwa ngozi mfululizo, nikadhani nimeathirika na Ukimwi," anasema akikumbuka jinsi ugonjwa huo ulivyomtesa.

"Niliamua kwenda Hospitali ya Muhimbili kwa daktari wa ngozi ambaye alichukua kipande cha ngozi yangu na kwenda kuipima na kubaini tatizo ni mkorogo."

Nuru anasema alipewa dawa aina ya scaboma ambayo ilimsaidia na inaendelea kumsaidia hadi sasa. Kwa sasa ameachana na biashara hiyo na badala yake anatoa ushuhuda wa madhara ya dawa hizi.

Akizungumzia biashara hiyo, Nuru anasema licha ya kusitisha biashara iliyokuwa ikimpa fedha za kujikimu kimaisha, sasa amekuwa balozi wa kueleza madhara ya mkorogo kwa jamii.

Alianza biashara hiyo mwaka 1998 baada ya kufanya majaribio ya kupaka losheni hizo na kuona zinampendeza na watu wanazipenda na hivyo akawa anachanganya na kuuza.

"Kwa kipimo kimoja nilikuwa nauza kati ya Sh25,000 hadi 30,000 na ningeweza kupata hadi Sh400,000 kwa mwezi," anasema.

Hata hivyo, mwaka 2013, mambo yalianza kwenda vibaya baada ya kujikuta akiwashwa ngozi na kuharibika ikawa kavu, yenye mikunjo na kubadilika rangi.

Licha ya Serikali kupambana na utengenezaji na matumizi ya vipodozi vyenye sumu, imeelezwa kuwa zaidi ya nusu ya Watanzania hutumia vipodozi hivyo kwa lengo la kuongeza urembo.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Evirocare ya Dar es Salaam mwaka 2013 umeonyesha bado tatizo hilo ni kubwa.

Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha mkoa mmoja katika kanda sita nchini. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam ukiwakilisha Kanda ya Mashariki, Mbeya (Kanda ya Nyanda za Juu Kusini), Tanga (Kanda ya Kaskazini) na Dodoma (Kanda ya Kati).

Katika utafiti huo ambao watu 785,000 walihojiwa, asilimia 46.77 (asilimia 66 kati yao ni wanawake) walikiri kumiliki maduka ya vipodozi huku asilimia 27.38 walikuwa waajiriwa kwenye maduka hayo.

Utafiti huo pia umeonyesha kuwa maduka mengi ya vipodozi yako kwenye wilaya za Tanga (maduka 28), Ilala–Dar es Salaam maduka 27, Dodoma 23, Mbeya 22 na Kondoa maduka 20.

"Wilaya za Kinondoni na Temeke za Dar es Salaam zina maduka mengi lakini hazikuweza kuifikia wilaya ya Kondoa. Uwepo wa maduka mengi humaanisha kuwa hata watumiaji pia ni wengi japo ubora wa vipodozi katika mgawanyo na upatikanaji unatofautiana kati ya mtumiaji mmoja hadi mwingine," inasema sehemu ya utafiti huo.

Kuhusu uelewa wa watumiaji ilionekana kuwa asilimia 57.4 wanatumia kujipodoa uso, asilimia 30 wanaona kama kitu cha kujipaka mwilini na asilimia 12.6 wanaona kuwa inaimarisha mwonekano wa ngozi.


Vipodozi vinavyouzwa zaidi
Walipoulizwa kuhusu vipodozi vinavyouzwa zaidi, watu 118 walisema ni losheni, 44 walisema mafuta ya nywele, 38 vipodozi vinavyobadilisha nywele, 37 mafuta ya mwili, 26 walisema krimu na 19 walisema manukato.

Wakati matumizi ya losheni yakiwa juu kwa watu wengi hivyo kuwaweka hatarini watumiaji hao, uchanganyaji wa manukato nao unaelezwa kuwa na athari zaidi kwani huweza kuumba kemikali nyingine kutokana na zile zilizochanganywa jambo linaloweza kuzalisha usugu wa matibabu.

"Matumizi ya losheni pia yanaiweka ngozi kwenye nafasi kubwa ya kuathirika na kemikali hasa kama mtumiaji atapaka vipodozi vilivyopigwa marufuku vya Carolite na Extra light."


Waliopo hatarini zaidi
Kati ya idadi ya watu wanaotumia kwa wingi vipodozi sumu, imeonekana kuwa asilimia 67.6 ni wanawake.

"Kwa wanawake kutumia zaidi vipodozi hivyo, inamaanisha kuwa wengi wako kwenye hatari ya kuathirika.

"Kwa mfano kuna rangi za midomo, kama mwanamke atambusu au kugusana mara kwa mara na mwanaume, wote wawili wataathirika," unaeleza utafiti huo.

"Watoto wanaoathirika zaidi ni wale wanaonyonyeshwa na wanawake wanaotumia mkorogo."


Wengi hawajui madhara yake
Walipoulizwa kuhusu aina ya kemikali zilizomo kwenye vipodozi wanavyotumia, asilimia 62.4 ya watu 263 walisema hawajui huku asilimia 34 wakisema wanajua.

Unasema pia nusu ya wauzaji walisema hawajui kemikali zitumiwazo katika vipodozi wanavyouza, achilia mbali madhara yatokanayo na vipodozi, hivyo kipaumbele chao ni kupata faida kuliko afya za watumiaji.

Akizungumzia utafiti huo, meneja mradi wa kupambana na vipodozi vyenye sumu, Euphrasia Shayo anasema hali ni mbaya kwa Tanzania ndiyo maana Envirocare wameanzisha kampeni ya kupambana na vipodozi hivyo.

"Tunafanya kampeni ya kupambana na vipodozi vyenye sumu kwa sababu tatizo ni kubwa nchini. Hadi sasa asilimia 52 ya Watanzania hutumia kati ya Sh35,000 hadi 50,000 kwa mwezi kununua mkorogo. matokeo yake wengi wameathirika na wanashindwa kuacha," anasema Euphrasia na kuongeza:

"Kichocheo kikubwa ni wanaume ambao huwashawishi wanawake watumie ili wawapende. Tunatoa elimu kwa wanawake kujiamini na uzuri walionao na kutumia vipodozi visivyo na sumu."


Madhara ya vipodozi
Akizungumzia madhara ya vipodozi hivyo, Shayo anasema kwa kiasi kikubwa cha mikorogo husababisha saratani ya ngozi na kupunguza nguvu za kiume.

Madhara haya pia huwaathiri wale ambao wenzi wao wanatumia vipodozi vyenye viambata vya sumu.

"Kwa mtu aliyeathirika na matumizi ya mkorogo inabidi atumie dawa kwa miaka mitatu mfululizo huku akipewa ushauri wa kitaalamu.

Siyo rahisi kuacha kwani kwa siku mtu hutumia hadi dawa tisa, hivyo itabidi kuacha moja baada ya nyingine, vinginevyo ataharibika kabisa mwili wake," anasema.

Ofisa Habari wa Taasisi ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudencia Simwanza anasema wamekuwa wakishirikiana na wadau kama Envirocare kupambana na tatizo la matumizi ya vipodozi vyenye sumu.

Anasema TFDA vile viel, imekuwa ikifuatilia na kukamata vipodozi vyenye sumu vinavyoingizwa nchini mbali na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari zake.

Ametaja baadhi ya viambata vya sumu vinavyotumika katika miongopni mwa vipodozi walivyovipiga marufuku ni pamoja na Bithionol, Hexachlorophene, zebaki, Vinylchloride, Zirconium, Halogenated salicylanilides (di-,tri-metabromsalan na tetrachlorosalicynilide), Chloroquinone na viambata vyake, Steroid, Chlofluorocarbon za kupuliza na Methyelene chloride.

CHANZO: Mwananchi
 
Aina nyingi ya vipodozi vya viwandani (synthetic beauty products) vimetengenezwa kwa viambato (ingredients) vyenye sumu (toxins) ndani yake. Sumu hizi huleta uharibifu kwenye ini na pia huleta saratani (liver-damaging and cancer causing toxins) vinapotumiwa kwa muda mrefu.

Kadhalika vipodozi vya viwandani hutengenezwa kwa viambata vinavyosaidia ufyonzaji wa vipodozi ndani kabisa ya ngozi kwa lengo la kuleta uzuri wa ngozi uliokusudiwa kwa mujibu wa kampuni husika ya vipodozi. Viambata hivi ambavyo kitalaam huitwa ‘penetration enhancers/sorption promoters/accellerants' ni pamoja na alcohol (ethanol), glycols (propylene glycol), sulfactants, nk.


Sasa mtumiaji wa vipodozi hivi anapopaka kwenye ngozi sumu hupenya ndani ya ngozi na kusafirishwa kwa njia ya damu kwenda kwenye viungo vya ndani (internal organs). Mwilini uchujaji hufanyika ambapo ini huusika na hutolewa nje (flushed out) ya mwili na figo. Hata hivyo baadhi ya sumu hubaki mwilini na huendelea kuongezeka kiwango chake kadiri tunavyoendelea kutumia vipodozi.

Kwa vile ngozi ndio kiungo kikubwa katika miili yetu sumu nyingi kukaa ndani ya ngozi. Ndani ya miili yetu sumu hizi kuchangamana na kemikali za asili za miili yetu na kusababisha mabdiriko ya ukuaji wa chembe chembe za miili yetu hali inayopelekea saratani. Madhara mengine ya kiafya yanayosababisha na vipodozi vya viwandani ni pamoja na mzio (allergies), kutokupata ujauzito (infertility), kuzeeka kabla ya wakati (aging prematurely), diabetes, na mengineyo ikiwa ni pamoja na wanawake kuota ndevu! Siku hizi kuna ongezeko kubwa la wanawake kuota ndevu…

Tuwe makini na utunzaji na kujali ngozi za miili yetu. Vipodozi vya viwandani ni hatari wandugu zangu. Ngozi ya binadamu kiasi cha ‘square inch' ina sweat glands 650, blood vessels 20, chembe chembe 60,000 zinazotengeneza rangi ya ngozi na zaidi ya 1,000,000 ya nerve endings. Ngozi ina midomo mingi (skin pores) iliyo tayari tayari kula chochote kinachogusana na ngozi kama vile vipodozi. Hapo ndo uone jinsi gani ngozi inapaswa kuangaliwa sana!

Katika zama zetu hizi zipo zaidi ya aina 100,000 za kemikali zinazotumika kutengeneza aina mbalimbali ya bidhaa tunazotumia kama vile rangi na vipodozi. Bahati mbaya sana ni asilimia 5 tu ya kemikali hizo zimefanyiwa majaribio ya kimaabara ili kujua madhara yake kwa afya ya binadamu. Hii ina maana asilimia 95 ya kemikali hizo bado hazijafanyiwa majaribio ya kitalaam na tunazitumia kupitia vitu kama vipodozi. Mathalani zebaki (mercury) ilikuwa ikitumika katika vipodozi kwa muda mrefu mpaka hivi karibuni ilipopigwa marufuku baada ya kufanyika utafiti kuhusu madhara yake.

Jambo jingine baya ni kwamba majaribio kuhusu athari za viambata vilivyomo katika vipodozi kufanywa kwa wanyama kama vile panya. Hakujawahi kufanywa majaribio hayo kwa binadamu ambaye ndiye mtumiaji! Halafu kuna makampuni mengine wanatufanyia hujuma za makusudi. Yanatengeneza vipodozi kwa viambata ambavyo havijafanyiwa majaribio halafu hawaanzi kuviuza huko kwao bali wanavileta Afrika.

Halafu wanafuatilia matokeo ya vipodozi vyao kwenye miili ya waafrika. Kwa nini wanatumia miili yetu? Kwanza wao ni wabaguzi wa rangi, pili sheria na kanuni zetu ama ni dhaifu au hazisimamiwi ipasavyo na mamlaka husika za Serikali.

Kwa leo na-stop hapa ndugu zangu, sasa mwenye sikio la kusikia asikie. Sifanyi kampeni ya kuzuia watu kutumia vipodozi vya viwandani au kuzuia biashara za watu au makampuni! Keep using at your own risk! Kwa yeyote atapenda kuelekezwa namna ya kutengeneza vipodozi uwasiliane kupitia


Email: alex.peter_75@yahoo.com

Mob: +255 688 308840

 
Back
Top Bottom