Sugu za Mikono huweza kuwa Dalili ya Kuugua au Kukaribia Kuugua Kisukari

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Licha ya Sugu kujulikana kusababishwa na vinasaba vya kurithi, kushika kemikali au matumizi ya vipodozi vyenye kemikali kali zenye sumu, tafiti zimeonesha pia kuwa watu wanaougua au wanaokaribia kuugua, hupatwa na sugu za vidoleni

Sababu halisi ya Kisukari kusababisha sugu za vidoleni haijulikani ingawa kuna nadharia kwamba insulini nyingi inaweza kuathiri ukuaji wa seli ya ngozi

Ikiwa una kisukari cha aina ya 2 pia uko katika hatari kubwa ya kupatwa na hali ya 'acanthosis nigricans' ambapo ngozi hupatwa na mabaka meusi katika maeneo fulani, kwa kawaida nyuma ya shingo, kinena, au kwapa

Ngozi inaweza kuonekana kama mabaka meusi na pia kuwa na harufu mbaya

Ikiwa vifundo vyako vya vidole vimeanza kuwa na weusi usio wa kawaida ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi na ushauri zaidi
 
Duh
Nimejicheck chap mwendo wa chopa yan.
Hatarious!
TG Am safe.
 
Back
Top Bottom