Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,355
- 2,767
Google inaandaa maboresho makubwa kwenye Pixel HiLight ๐ก.
Pixel HiLight ni mfumo wa taa ndogo za LED zilizowekwa karibu na sehemu ya kamera ya nyuma. Simu ikiwa imegeuzwa chini juu (face down), taa inaweza kuwaka kukupa taarifa bila kulazimika kuangalia skrini. Google imeleta HiLight kwenye Pixel 11 Pro series.
Mfumo huu kwa sasa una rangi 5 lakini Google wataweza kuziongeza na kufikia 9 ambapo unaweza kufanya yafuatayo:
๐ Ukipigiwa simu toka kwenye Contacts unaweza kumpangia mtu rangi yake, hivyo ukiona mwanga fulani unajua nani anakupigia.
๐ค Gemini โ HiLight inaweza kuonyesha mwanga tofauti wakati Gemini inakusikiliza, inachakata ombi lako au inakujibu.
๐ฌ Bila kusahau inafanya kazi pia kwa simu kutoka kwa WhatsApp unapochagua favorites contact.
Hii inamaanisha unaweza kujua kuna taarifa mpya bila hata kuwasha skrini! ๐ฎโ๐จ