Yahya Jammeh aongezewa miezi mitatu na bunge

Yahya Jammeh aongezewa miezi mitatu na bunge

ECOWAS watamtoa kama Tanzania ilivyomung'oa Mohamed Bacar kule Anjouan mwaka 2008.
 
Tatizo wapinzani kiherehere chao cha kusema watamshitaki, maana jamaa mwanzo alikubali vizuri ila baada ya maneno ya rais mteule kuwa watamfungulia mashtaka jamaa akaona isiwe kesi nakataa matokeo
 
Tatizo wapinzani kiherehere chao cha kusema watamshitaki, maana jamaa mwanzo alikubali vizuri ila baada ya maneno ya rais mteule kuwa watamfungulia mashtaka jamaa akaona isiwe kesi nakataa matokeo
Ni kweli, labda walioshinda wasingeherereka na kumhakikishia jamaa usalama asinge badili maamuzi. Hilo linaweza bakia kuwa funzo kwa nchi nyingine za Afrika. Lakini ili liwe funzo zuri zaidi yafaa Afrika imtoe kwa nguvu huyo jamaa maana wananchi walishaamua lakini kwa kuwa ana majenerali anaoweza kuwaamrisha wakamtii kaona hiyo ndio njia iliyobaki. Afrika isipofanya lolote napata wasiwasi kuwa wengi hataheshimu sheria na maamuzi ya kidemokrasia hapo baadaye.
 
Jamaa anajivunia ushawishi wake ndani ya jeshi la gambia, sema wakimtoa kimabavu itasababisha maafa makubwa na kujenga hali ya visasi ndani ya jamii.....
 
View attachment 461312

Bunge la Gambia limeongeza muhula wa Rais wa Gambia Yahya Jammeh ambao unakamilika siku ya Alhamisi kufuatia kushindwa kwake kwenye uchaguzi kwa siku 90.

Bunge pia limeidhinisha uamuzi wa Jammeh wa kutangaza hali ya tahadhari ya siku 90, katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi.

Viongozi wa kanda wametishia kutumia nguvu za kijeshi kumlazimisha bwana Jammeh kuondoka madarakani, ikiwa atakataa kusalimisha mamlaka kwa rais mteule Adama Barrow.

Maelfu ya watalii raia Uingereza na Uholanzi wanaondolewa kutoka Gambia.

Nchi hiyo ni maarufu kwa watalii kutokana na fukwe zake.

Jammeh atangaza hali ya tahadhari ya siku 90Nigeria kumpa hifadhi rais Yahya Jammeh iwapo atajiuzuluBuhari kuongoza mazungumzo kuhusu GambiaWaziri wa habari Gambia akimbilia SenegalWatalii waondolewa Gambia

Gambia ilitumbukia kwenye mzozo baada ya bwana Jammeh kukataa ushindi wa bwana Barrow kwenye uchaguzi wa tarehe mosi mwezi Disemba.

Viongozi wa kanda wameshindwa kumshawishi Bwana Jammeh kuwacha madaraka.

Nigeria imetuma meli ya kivita kumshinikiza bwana Jammeh kuondoka madarakani.

Muungano wa nchi za magharibi mwa Afrika Ecowas, umeandaa kikosi kinachoongozwa na Senegal lakini bado unasema kwa hatua za kijeshi ndizo zitakuwa za mwisho.

Source: Freedomnewspaper online
Mbabe Yahya
 
Africa ni bara giza kwa dizaini ya viongozi wa aina hii... Uroho, ulafi, kutojali wananchi, udikteta,.. Tuna safari ndefu sana, tena sana ya kujikomboa..
 
Back
Top Bottom